Upinzani Tanzania una matatizo? Vyama havina Succession Plan hivyo vina Usultani! CHADEMA kuna Usultani? Usultani huu Utakiinua au Utakiangamiza?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,442
113,452
Wanabodi,
Hili ni bandiko la maswali yenye facts
  1. Jee kuna ubishi kuwa Upinzani Tanzania Unamatatizo?. Ni matatizo gani na usaidiweje?.
  2. Vyama vingi vya Upinzani Havina Succession Plan, kwanini vyama hivyo havina succession plan na sio tuu kwenye uongozi wa ndani, hata kwenye ubunge na udiwani, mfano tunaelekea uchaguzi wa 2020, Chadema ina wabunge wa majimbo ambao wengine wame deliver na wengine hawaja deliver, hivyo uchaguzi wa 2020, wengi wanakwenda kupigwa chini na CCM!. Kwanini hakuna succession plan ya ndani kuwapima kukubalika na kuwapiga chini kabla kwa kusimamisha more able candidates wanaokubalika zaidi?.
  3. Vingi ya Vyama vya Upinzani, Vina Uongozi wa Kisultani, na sio Chadema pekee, Mzee Cheyo wa UDP, Mrema wa TLP, Lipumba wa CUF, etc. Kwanini hakuna grooming mechanism to groom their future leaders?.
  4. Hivyo jee hata uongozi wa Mhe. Freeman Mbowe ndani ya Chadema, ni kama Usultani fulani?.
  5. Jee Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Chadema hiyo 18 Dec, ni uchaguzi kweli au ni uchaguzi kiini macho tuu?, kama utakavyokuwa Uchaguzi Mkuu wa 2020, tayari mshindi anajulikana!. Hivyo ni uchaguzi wa kukamilisha tuu taratibu kuonekane demokrasia amechukua mkondo wake? au ni uchaguzi kweli?.
  6. Kuna msemo, " no one is indispensable", no matter how good one is, huwa anafikia kiwango cha mwisho wa uwezo wake, ndio maana katiba unaweka ukomo wa uongozi, hata katiba ya Chadema ya 1992 ilikuwa na kipengele hicho, kwenye katiba ya 2006, kipengele hicho cha ukomo, kiliyeyuka, just vanish into thin air, bila kujadiliwa popote!. Jee kipengele hiki kiliyeyukaje?
  7. Waliokiweka kipengele hicho kwenye katiba ya Chadema, walikuwa na maana yao, kwa vile ile katiba ya 2006 kipengele hicho hakikuondolewa, bali kilijiondokea tuu chenyewe, kuondoka huku kwa kipengele hicho kuna maana gani kwa Chadema?.
  8. Je ni kwa kutokuwepo kwa kipengele hicho, cha ukomo ndiko kunatoa fursa ya usultani kwenye uongozi wa vyama vya siasa yenye Usultani, Jee Chadema nacho ni chama cha kisultani?, kuna Usultani?.
  9. Mkimfanyia Mhe. Mbowe a quick assessment tangu alipoitoa Chadema alipoingia kwenye uongozi mpaka hapa alipoifikisha Chadema, jee hakuna kweli wana Chadema wenye kuona mbali ambao wanao ona trends za Mhe. Mbowe kuwa japo amekifanyia mengi, makubwa na mazuri Chadema, lakini pia amefikia kiwango chake cha mwisho wa uwezo wake kwa Chadema kuhitaji kupata fresh blood?.
  10. Swali la mwisho na la msingi sana ni, jee kuendelea kwa Mhe. Mbowe kama Mwenyekiti wa Chadema, kwenye era hii ya changing political dynamism ya siasa za Tanzania chini ya JPM na CCM imara, Mwendelezo huu wa Uenyekiti wa Mhe. Mbowe, Jee Utakinua Zaidi Chadema kuliko hapo kilipofika, Au Utakiangamiza na sasa Chadema kinaelekea Kwishney?.
NB. Hili ni bandiko la maswali, kama una majibu ya maswali haya karibu, ukiwa huna, nakushauri jipitie tuu kimya kimya, sio lazima kuchangia kila thread.
Natanguliza shukrani.

Nawatakia Chadema maandalizi mema uchaguzi na wengine wote Jumapili Njema.

Paskali
Rejea


 
Huwa wanasema damu ni nzito kuliko maji, Mzee Mtei hawezi kupindua kwa kaka wa Hai hata kidogo.

Akitaka kuongea anakumbuka kwamba aliyesimama mbele yake ni mume wa binti yake aliyemletea wajukuu duniani.

Matokeo yake ile CHADEMA ambayo Marehemu Julius Nyerere alizikubali sera zake, sio hii ya sasa kwani kimaadili imeshapoteza muelekeo.
 
Upinzani bado saaana kwa sasa.

Vizazi vilivyoimba fikra za mwenyekiti zidumu na kula kiapo cha chipukizi wote wana damu ya kijani, majority wamezaliwa 1990 na kurudi nyuma, wakiondoka kwenye nguvu kazi na kuachia kizazi kipya, may be millenials waliozaliwa after baada ya 1995.

Vinginevyo upinzani utaendea kujifurahisha tu.
 
Vyama havina succession plan kwa sababu wanajifunza kutoka ccm, vyama havina demokrasia kwa sababu ccm haina demokrasia ndani yake.

Haya ni matatizo yaliyetwa na ccm.
Sio kweli mkuu, wenyeviti wote wa CCM wanakuwepo katika uongozi kwa miaka isiyozidi kumi. CCM inao uwezo wa kwenda na wakati kwani inaheshimu taratibu inazojiwekea.

CHADEMA kuna mambo mengi ya kuzungukana, mnaongea mkicheka pamoja lakini ukiwapa mgongo watu wanaanza masengenyo ndani ya muda huo huo.
 
Wanatakiwa kuwa makini sana, tahadhari kubwa zaidi kwa wimbi la kuunga juhudi.
Siasa za Tanzania kwa sasa zina wanasiasa wasioaminika kama kuku, punje mbili tu za nafaka wanaingia kwenye mtego.
Hii ni kwa vyama vyote, hata CCM asili inalijua hilo.
 
Ikiwa vyama vya upinzani vina matatizo kama unavyotaka kutuaminisha, Jiwe anaogopa nini kuweka mazingira sawa ya kisiasa nchini? Kila siku ni kukamata, kutishia, kuteka, kupiga, kununua, kunyanyasa wapinzani wake......! Ajaribu kuruhusu mazingira sawa ya kisiasa aone!
 
Kwanz nikushukuru kwa uchambuzi mzuri.

Pili hili ni Jukwa huru, ukiweka bandiko, waachie watu wasome na waweke comments zao.

Japokuwa ninakubaliana na uchambuzi wako, na ulisemalo lipo kweli kabisa, uongozi wa vyama pinzani ni wakiSultani. Lakini umeharibu kukisifia chama chetu na kiongozi wetu, hapo hapakustahili hata kidogo.

Ushauri wangu kwako, I love reading your articles, would have loved you to be unbiased, nor to want to seek being seen unaelemea upande mmoja.
 
Hii ni inconvenient truth!

Mbowe ni Kiongozi wa kimila, chadema ni zaidi ya Chama cha Siasa, hiyo iko kihistoria. Wachaga ( Machame + Marangu) wanasapoti chadema shauri ya Mbowe + Mtei ambao kwao ni Chief, Mbowe akitoka na chadema kwishney kwani Wachaga (karibia wote ) watatoka pia.

Ni kama ilivyokuwa CUF na Waislamu ndivyo ilivyo chadema na Wachaga, bila ya Waislamu hakuna CUF, huo ndio ukweli hata kama hamuutaki.
 
Ikiwa vyama vya upinzani vina matatizo kama unavyotaka kutuaminisha, Jiwe anaogopa nini kuweka mazingira sawa ya kisiasa nchini? Kila siku ni kukamata, kutishia, kuteka, kupiga, kununua, kunyanyasa wapinzani wake......! Ajaribu kuruhusu mazingira sawa ya kisiasa aone!
Kama mazingira ndani ya chadema hayako sawa je hao wa nje ya chama watawapa mazingira sawa

Sumaye

Mwambe

Wameonyesha njia

Na wame adhibiwa tayari
 
Back
Top Bottom