chadema

CHADEMA (Chama cha Demokrasia na Maendeleo)
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni chama cha kiasiasa nchini Tanzania ambacho kilianzishwa tarehe 28 Mei 1992 na mwanasiasa mkongwe Edwin Mtei, aliyewahi kuwa Waziri wa Fedha katika miaka 1997 hadi 1979.

Mwaka 2000 CHADEMA hakikuwa na mgombea wa Urais. Mwaka 2005 mgombea wa CHADEMA Freeman Mbowe alikuwa namba tatu kati ya wagombea kumi akapata asilimia 5.88 za kura.

Mwaka 2010 CHADEMA ilipata asilimia 27.1% na mgombea Urais wa chama Wilbroad Peter Slaa na kura 4,627,923 kwa 31.75%.

Hata hivyo CHADEMA imekataa matokeo mengi kutokana na mchakato mzima kuwa mikononi mwa Tume ya Uchaguzi isiyo huru.
  1. The Boss

    CHADEMA kwanini inacheza ngoma za Rais Magufuli?

    Kila mtu anajua mpango wa kuivuruga Chadema unavyokwenda. Sasa why Chadema Wana play na mchezo huo? Kwanini wasijifunze kucheza tofauti? Kama mpango ni kuwavuruga mfukuzane ..why msiamue 'hafukuzwi' mtu Kwa sasa? Muache anaetaka kutoka atoke Tu mwenyewe? Why kumjibu mtu kama Makonda...
  2. J

    Zamani CCM walisema Zidumu fikra " sahihi" za mwenyekiti Sasa Chadema wanasema ' Zidumu fikra za mwenyekiti'

    Najaribu kukumbuka tu kiapo changu cha uanachama na salamu zetu ndani ya chama wakati ule wa awamu ya kwanza. Kwanza tuliitana " ndugu" pili tuliamini katika uhai wa chama ndio tulisema " kidumu chama cha mapinduzi" na tatu tuliamini katika uwezo wa mwenyekiti wetu na tulifahamu kuwa yeye ni...
  3. mwanamwana

    RC Makonda atoa saa 24 kuwakamata Wabunge kama wazururaji endapo hawatarudi Bungeni. Wabunge wamjibu

    Mkuu wa Mkoa wa DSM, Paul Makonda ametoa saa 24 kwa Wabunge wote waliokimbia kushiriki vikao vya Bunge na kwenda Dar es Salaam kula bata, kuhakikisha wanarudi Bungeni tofauti na hapo, watakamatwa kwa kosa la uzururaji kama wanavyokamatwa machangudoa wanaozurura usiku. RC Makonda amesema kwa...
  4. T

    Udhaifu wa Chadema sio Uimara wa CCM!

    Nimeona mjadala mkali na wa kuvutia ukiendelea kuhusu uhai wa vyama vya upinzani hususan Chadema kuelekea 2020. Nikiri mapema kuwa, hatuna vyama vya siasa Bali tuna vikundi vinavyopambana na dola. Hata CCM yenyewe ilikwisha acha siku nyingi kuwa Chama cha siasa badala yake uhai wake unategemea...
  5. Erythrocyte

    Wabunge wa CHADEMA waliohudhuria Bungeni, watakiwa kujiuzulu nafasi za uongozi Bungeni

    Wabunge wa Chadema kwa kauli moja wamependekeza kwamba Wabunge wasaliti walioamua kuhudhuria bunge la corona na kupuuza msimamo wa chama chao wa kujitenga na bunge hilo kwa wiki mbili kama mwongozo wa WHO unavyoelekeza ili kuzuia maambukizi ya Virus hatari vya corona , wametakiwa kuachia nafasi...
  6. J

    Kwanini wabunge wanaotoka Chadema na kuhamia CCM wanakuwa na " chuki binafsi" na chama chao cha zamani?

    Tofauti na wabunge wa vyama vingine wanaohamia chama tawala CCM, wabunge wanaotoka Chadema huwa na chuki sana na chama chao cha zamani kana kwamba walifukuzwa. Wabunge wote wa Chadema waliotoka CCM labda ukimtoa Ole millya wakisimama tu bungeni jambo la kwanza ni kuikejeli Chadema. Hata huyu...
  7. J

    Dkt. Slaa: Bunge la bajeti ni takwa la kikatiba haliwezi kuahirishwa, Chadema wanatafuta huruma ya kisiasa lakini wamechelewa

    Balozi wetu huko Sweden amesema bunge la bajeti ni takwa la kikatiba hivyo haliwezi kuahirishwa kwa sababu zozote. Katiba inatamka wazi kuwa bunge la kbajeti litakaa kwa siku zisizozidi 45 ukiondoa week end na sikukuu hivyo hakuna namna unaweza kuahirisha na wabunge wanalijua hilo. Pili Dr...
  8. Roving Journalist

    Dodoma: Pamoja na katazo la Kiongozi wao, Wabunge kadhaa wa CHADEMA wakiwemo Silinde na Lijualikali wahudhuria bungeni

    Wabunge wawili wa Chadema, David Silende (Momba) na Peter Lijualikali (Kilombero) wamehudhuria bungeni leo licha ya chama chao kuwataka wabunge wake kutohudhuria vikao vya Bunge ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona Mbunge wa Kilombero (Chadema), Peter Lijualikali, Hivi karibuni...
  9. J

    Mbowe ameathirika na " Hofu" baada ya kijana wake kupambana na Corona lakini CHADEMA ni kubwa kuliko familia

    Binafsi nakubaliana kabisa na wabunge wa CHADEMA kujiweka katika karantini kwa sababu hiyo ni haki yao ya kikatiba ya kulinda uhai. Kilichonishangaza kidogo ni namna Chadema inavyofanya maamuzi bila vikao rasmi vya kikatiba kuketi. Kwa mfano wabunge wa chama kutoingia bungeni ni muhimu wakapata...
  10. J

    Mkurugenzi Manispaa Ubungo amfukuza Meya Jacob kwa kutumia katiba ya zamani ya CHADEMA ambayo haitumiki

    Meya Jacob wa manispaa ya ubungo amesema yeye bado ni mwanachama halali wa Chadema na kwamba mkurugenzi wa manispaa hiyo ametumia katiba ya zamani ya Chadema ambayo ilishafanyiwa marekebisho kumuengua. Bonny anasema aliletewa barua ya kufukuzwa umeya jana Jumapili saa 3 usiku nyumbani kwake...
  11. technically

    Inadaiwa kuna Wabunge wa CHADEMA wataenda bungeni kesho

    Nashauri Chadema iwapuuze maana ni wale walio kwe list ya kuunga mkono juhudi na kwenda Ccm kabla ya uchaguzi october. Chadema wapuuzeni waacheni waende wakapambane na Corona.
  12. J

    Askofu Gwajima: Chadema wana mapepo ndio maana wamesusia bunge na wanalazimisha makanisa yafungwe, Wameshindwa katika jina la Yesu!

    Mambo ni moto mambo ni fire ndani ya Kanisa la ufufuo na uzima. Askofu Gwajima amesema wabunge wa Chadema wamesusia vikao vya bunge kwa kisingizio cha Corona ila ukweli ni kwamba wabunge hao wamepagawa na mapepo. Askofu Gwajima amewaambia waumini wake ambao ni wapenzi wa Chadema kuwa chama...
  13. Nigrastratatract nerve

    CHADEMA wameachwa kwenye mataa

    Wamesalitiwa na vyama vingine ambavyo inaonesha dhahiri kuwa nia yao si nzuri ndani ya Tanzania Chadema wameonyesha ngozi yao halisi kwenye hili janga LA Corona wametoka hadharani na kuionyesha Dunia kuwa wanataka watanzania wengi waugue na wafe kwa Corona ili kwao uwe ni mtaji wa kisiasa...
  14. J

    Kumbe wabunge waliohamia CCM kutokea Chadema siyo " minesterial material" naona teuzi zinawapitia mbali hadi wengine wanarudia

    Nawaza tu kwamba hata yule Mwita Waitara ndio uwezo wake umeishia kwenye unaibu. Hawa akina Mollel PhD na yule Ole Milya wanafeli wapi mbona ni wasomi wazuri lakini hawaonekani? Anyway ya ngoswe mwachie ngoswe, naishia hapo. Maendeleo hayana vyama!
  15. Roving Journalist

    Meya wa Ubungo, Boniface Jacob adaiwa kufukuzwa uanachama CHADEMA. Aandikiwa barua ya kuvuliwa umeya... Yeye aongea

    Kuna barua zinasambaa zikidai Mayor Jacob amefukuzwa uanachama CHADEMA na hivyo kuvuliwa umeya. JamiiForums imemtafuta Meya Jacob ambaye amesema barua ya kufukuzwa kwake imechongwa na hata Katibu anayedaiwa kuandika barua ya kufukuzwa kwake hajaandika barua hiyo. Ameshangaa kuona barua...
  16. J

    Katika hili nakubaliana na Chadema, Ushujaa ni kufia vitani ukiwa Jeshini au mhudumu wa afya akiwa hospitali anatibu lakini siyo bungeni!

    Maisha ya mwanadamu ni mafupi hivyo tusimbeze yoyote anayeamua kuyalinda maisha yake na familia yake bila kuvunja sheria. Hakuna ujasiri wowote wa mtu kufia bungeni eti anawakilisha wananchi waliomchagua, hiyo Johnthebaptist nakataa kabisa. Kwa hili la Corona mashujaa ni wahudumu wa afya walio...
  17. Nigrastratatract nerve

    Kwakuwa haijulikani Corona itaisha lini, napendekeza CHADEMA wasiweke mgombea hata mmoja kwenye ubunge na udiwani ili kujikinga

    Binafsi nawapongeza sana Chadema kwa uoga waliouonesha wa hali ya juu sana, yaani wao wamejiona bora sana kuliko wananchi tuliowachagua na kuwatuma Bungeni wakatutetee katika hali zote. Uamuzi walioufanya nimeupongeza kuwa hawa jamaa wamedhihirisha kuwa tulikosea kuwachagua. Wametukimbia wakati...
  18. denooJ

    Wabunge wa CHADEMA wakubaliana kutohudhuria tena vikao vya Bunge kutokana na janga la COVID-9, Kujiweka Karantini kwa wiki 2

    Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya amesema "Hali ya Corona ni mbaya sana, wabunge kupitia Chadema, leo tumefikia makubaliano ya kutoingia Bungeni na kila mbunge kubaki nyumbani kwake Dodoma, niwatake wananchi huko mlipo mchukue tahadhari kubwa."
  19. Chagu wa Malunde

    Kwanini CHADEMA mnachukia tunapohamia NCCR Mageuzi?

    Tulipambana sana kukijenga chama lakini kwa fitina na tamaa mbaya mkakiharibu chama chetu. Hii ilikuwa mwaka 2015. Na namna mlivyokiharibu kila mtu anajua. Kujiunga na chama chochote kile ni haki ya kila mtu kama ilivyowekwa wazi katika ibara ya 20(1) ya Katiba ya JMT. Tunahamia NCCR Mageuzi...
  20. YEHODAYA

    Sababu ya CHADEMA kutokuwa na mvuto kwa wafadhili wa mataifa ya nje

    Chama chochote cha siasa huwa na agenda yake ambayo huwa ndio roho ya chama Chadema kipindi cha Dk Slaa kilikuwa na agenda tena nzito ambayo ilikubalika na ilitikisa ndani na nje ikipigiwa makofi ndani ya nchi na nje ya nchi.La kujifunza kwa Dk Slaa ni kuwa Dk Slaa hakutetea maslahi binafsi...
Back
Top Bottom