Pale Bungeni simuoni Mbunge wa kuichambua ripoti ya CAG baada ya kukosekana Zitto Kabwe na wabunge wa CHADEMA

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,924
141,891
Tukiweka itikadi pembeni, kiukweli pale bungeni simuoni mtu mwenye uwezo wa kuichambua ripoti ya CAG kama walivyokuwa Zitto Kabwe, J J Mnyika, James Mbatia na Tundu Lissu.

Kuwa mwanasiasa mzuri ni jambo moja lakini kuwa mwanasiasa " mahiri" ni jambo lingine kabisa.

Hao niliowataja unapofika wakati wa uchambuzi wa maswala ya kitaalamu iwe uchumi, sheria au fedha huwa na udadisi wa kitaaluma siyo kishabiki.

Ripoti ya CAG iliyowasilishwa kwa mh Rais Samia leo inahitaji hoja nyingi za kibobezi/ kidadisi lakini sidhani kama akina Babu Tale na Nusrat Henje wana viwango hivyo.

Itoshe tu kusema wabunge wengi wa sasa wana uwezo mdogo na ujasiri hafifu wa kujenga hoja.
 
Dogo, leo umeendelea vizuri na dose ya dawa ulizopewa Hospitali Ya Milembe. Keep it up, akili zitakaa sawa tu mdogo mdogo.

Na hata kwa wale wana CCM wenzio waliokua hawaelewei ile kauli ya Mama "ALIESIMAMA HAPA NI RAIS", somo ni gumu kidogo ila taratibu wataelewa tu, kama TPA leo walivyoeleweshwa wakaelewa.

Somo linaendelea muda si mrefu, subiri majibu yaletwe kuhusu amri aliopewa CAG kufanya ukaguzi wa hela zote zilizotoka Hazina kuanzia January 2021 - Mpaka mwezi huu. Hapa waliochota hela kwa advantage ya Rais kuumwa na kwa kisingizio cha matumizi ya msiba wa Rais - Wataelewa somo vizuri pia (Iwe kuna Waziri, Naibu Waziri, Katibu, Muweka Hazina au yoyote kama amehusika, basi ataelewa somo).

Mama amecheza karata zake vizuri sana, kama ikitokea kuna Mawaziri au Manaibu Waziri (Hasa waliokua hawamtii kipindi yeye ni Makamo Wa Rais, na waliokua wakidiriki hata kumchongea kwa Rais pindi alipokua akiwahoji na kuwauliza baadhi ya maamuzi wanayofanya) wamehusika kuchota hela katika kipindi hicho cha kuanzia January, basi Mama hatawafumbia macho na anapata sababu ya kulivunja Baraza La Mawaziri For Good.

#Mlimpeleka Askofu Gwajima bungeni mkategemea aende kuichambua "REPORT YA CAG" kweli. Wakati report ya michango ya kanisa lake hajui kuichambua kwa waumini wake.
 
Dogo, leo umeendelea vizuri na dose ya dawa ulizopewa Hospitali Ya Milembe. Keep it up, akili zitakaa sawa tu mdogo mdogo.

Na hata kwa wale wana CCM wenzio waliokua hawaelewei ile kauli ya Mama "ALIESIMAMA HAPA NI RAIS", somo ni gumu kidogo ila taratibu wataelewa tu, kama TPA leo walivyoeleweshwa wakaelewa.
Dogo asubiri mama achukue na uenyekiti wa chama ili aweze piga pote pote.
 
Tukiweka itikadi pembeni, kiukweli pale bungeni simuoni mtu mwenye uwezo wa kuichambua ripoti ya CAG kama walivyokuwa Zitto Kabwe, J J Mnyika, James Mbatia na Tundu Lissu..
Kwenye post zako huwa nikiingia na hasa pale unaponicot hupenda kuniita "Bwashee" ila sikuzote huwa nakupotezea sababu nakuona mnaa kama wengine.

Kwa leo wacha niseme.

Mambo vp Bwashwee, tumuunge mkono Madame President ili atuvushe
 
Back
Top Bottom