Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni chama cha kiasiasa nchini Tanzania ambacho kilianzishwa tarehe 28 Mei 1992 na mwanasiasa mkongwe Edwin Mtei, aliyewahi kuwa Waziri wa Fedha katika miaka 1997 hadi 1979.
Mwaka 2000 CHADEMA hakikuwa na mgombea wa Urais. Mwaka 2005 mgombea wa CHADEMA Freeman Mbowe alikuwa namba tatu kati ya wagombea kumi akapata asilimia 5.88 za kura.
Mwaka 2010 CHADEMA ilipata asilimia 27.1% na mgombea Urais wa chama Wilbroad Peter Slaa na kura 4,627,923 kwa 31.75%.
Hata hivyo CHADEMA imekataa matokeo mengi kutokana na mchakato mzima kuwa mikononi mwa Tume ya Uchaguzi isiyo huru.
MJUMBE WA KAMATI KUU YA CCM ATUA IGUNGA, AONGEA NA WANACHAMA NA KUKAGUA UJENZI WA WODI YA MAMA NA MTOTO
"Katibu wa CHADEMA Jimbo la Igunga, aunga mkono juhudu za Mama Samia na kuhamia CCM"
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Mlezi wa Mkoa wa Tabora Ndg. Afadhal Taibu...
Ilikuwa kama utani vile mwaka wa kwanza toka aondoke Nyerere tukadhani 2000 lazima Chadema waingie ikulu lakini wapi.
2005 wakaja na helikoptaa lakini mipango ikagoma, 2010 ngoma ikakataa, 2015 gwiji la siasa za urais Lowassa lakini wapi. 2020 tukajaribu gwiji la siasa za Brussels likakutana na...
Kiukweli udhaifu wa CHADEMA ulianzia pale Balozi Wilbroad Slaa alipoamua kuachana na siasa za majukwaani.
Baadae Patrobas Katambi akaidhoofisha Bavicha kwa kuhamia chama dume CCM.
Halima James Mdee akapigilia msumari wa mwisho kwa kusepa na kijiji kizima cha Bawacha.
Mungu ibariki CHADEMA!
Kwa mtazamo wangu, kuchoma ofisi za CHADEMA, lengo ni kuwa-prove CHADEMA wapandwe na hasira walipize kisasi wapate sababu ya kuishughulikia CHADEMA.
Nasema hivi kwasababu, ikitokea ofisi za chama fulani zimechomwa moto, baai CHADEMA watashukiwa kama mwewe na wale walio kimya wakati ofisi za...
Jambo hili la kusikitisha limefanyika usiku wa kuamkia leo, ambapo watu wasiofahamika wamelipua ofisi hiyo na kisha kutokomea kusikofahamika, nyaraka kadhaa za Chama hicho zimeteketea na nyingine zenye thamani kubwa zimeibwa.
Ikumbukwe pia kwamba Viongozi wa Chadema zaidi ya 50 wa Tunduma...
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema hakitashiriki vikao vya majadiliano ya wadau wa vyama vya siasa, vilivyoitishwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, hadi mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, atakapoachwa huru bila masharti yoyote.
Sharti hilo limetajwa leo...
Taarifa yao iliyosambazwa hii hapa
=============================================
"Ili [CHADEMA] tuweze kushiriki kikao chochote cha Msajili [wa Vyama vya Siasa] lazima zuio la vyama kufanya mikutano ya hadhara liondolewe, ili tukienda kwenye vikao, twende kama vyama huru, tusiende kama...
Siyo siri kuwa hii nchi ni ngumu sana. Uwekezaji uliopo dhidi ya haki na usawa ni mkubwa sana.
Kwa makusudi demokrasia na uhuru wa watu vimeminywa vilivyo ili kufanikisha hayo.
Hali hii haitaondoka yenyewe bila ya makabiliano. Ni muhimu kufahamu watesi wetu hujipanga upya kwa kila hatua...
Nakumbuka chaguzi ndogo kuanzia Dr Lamwai enzi zile za Manzese hadi Dr Augustino Lyatonga Mrema nyakati za akina Cisco kule Temeke.
Lakini siku hizi chaguzi ndogo zimedorora sana, mfano jana.
Kwanini!....... Why?..........Ndauli?!!
Nawatakia Dominica yenye baraka!
Katika misingi ya kujenga hoja naona kama vijana wa Chadema wako vizuri sana. Kwani vijana wa CCM hawasomi shule hizihizi wanazosoma vijana wa Chadema?
Kuna nini CCM mi sielewi, ni kweli chama kimekubali kuwa na mtazamo wa vijana wa kusifia tu.
Kila nikiwaangalia vijana wa CCM nahisi kuna...
Unamsema vipi mtu ambaye hawezi kujitetea Kama Hayati Magufuli, Mkapa au Nyerere? Mimi binafsi Hawa watu siwadai Kama Mungu kashafanya hukumu yake waachwe wapumzike!!
Natoa angalizo tu kwa chadema kuelekea uchaguzi 2025 hasa Tundu Lissu na Mbowe wajitaidi kuepuka Mambo yafuatayo.
1: Acheni...
Wakuu chama chetu Cha CCM ndo kulikuwa chama Cha kwanza kuzindua Mambo ya CCM digital.
Walikuja na App ya CCM kwenye play store, ili wanachama wajisajiri kidigitali. Ukweli CCM hatujafanya vizuri kwenye hili. Hata mitandaoni Mfano Tweeter, JF ni kama Chadema wameiweka hiyo Mitandao mfukoni...
Kwamoto huu wa CCM Jimbo la Ushetu-Kahama Chadema mlikuwa sahihi kusogeza magoli nyuma | Hapa Shaka kule Mizengo Pinda pale Katambi huku Ditopile ni "Utajua Hujui "
"Hakuna kama Samia "
Sitaki kuongeza neno,hebu fungua mwenyewe hiyo video ili uone mafuriko ya maelfu ya watu huko Ushetu ikiwa...
1. Hii serikali ni ya ajabu sana. Inasema uongo mchana kweupe.
2. Yaani kiongozi anatoka anasema tumepunguza tozo hii na ile ili kupunguza bei za nishati ya mafuta ya petrol, diesel na ya taa (kerosene).
3. Lakini cha ajabu, badala ya bei kupungua ndiyo zimeongezeka kwa wastani wa shilingi...
CCM ikiwa na bahati ya kukuza na kutumia magwiji ya mikakati ya ushindi wa kisiasa hali hiyo imekuwa kinyume kwa vyama vya upinzani ambavyo havina hazina hiyo na matokeo yake kujiua vyenyewe. Chama chenye nia ya kushinda dola hakiwezi kuwa na mtendaji mkuu ambayo hana mbinu wala mikakati ya...
Wanabodi,
Ni jambo la kawaida sana kwa wana CHADEMA "Kukiuka" utaratibu ulipo kwa kufanya shughuli mbalimbali za siasa. Mara nyingi huwa wanalalamika sana na kusema kwamba wana haki ya kufanya shughuli zao kama ilivyo elezwa kwenye katiba. Je wana CHADEMA wanahaki kikatiba kufanya shughuli zao...
Taarifa ya sasa inaeleza kwamba Chadema kupitia BAWACHA inawaomba wananchi wote kuchangia Familia za Makomandoo Adamoo na wenzake, walioshitakiwa kwa tuhuma za ugaidi, ambao inadawa ulifadhiliwa na mshitakiwa mwenzao Freeman Mbowe kwa kitita cha Tsh Laki 6.
Tayari mchakato wa kampeni hiyo...
Hiki chama ni kundi tu la watu wanaotaka madaraka. Ukiangalia ugomvi wao wote na dola, kelele zao zote karibu asilimia 90 vinahusu wao kuingia madarakani.
Huwezi kuta CHADEMA wanaingia matatani na vyombo vya dola kisa walikusanyika kutetea wakulima wanaonyonywa na vyama vya ushirika...
Ni hali ya kawaida kumantain status kwenye siasa ya kimataifa kuwa taifa lenu linazingatia misingi ya vyama vingi ni lazima chama tawala kiwe na vyama kinavyovilea kama vyama vya upinzani. Hii itaonyesha kuwa kweli multiparty system ina prevail.
Ndivyo vyama vingi vya siasa hapa Tanzania...
Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni. Pamoja na yote lakini Edward Lowassa alijitahidi kuipambania CHADEMA kwenye uchguzi mkuu wa 2015 ingawaje alishindwa kuipigania baada ya uchaguzi kupita. Lakini hali kwa Lowassa ikiwa hivyo, Membe ndio sikumuelewa kabisa.
Kwanza ile anaingia tu ACT na kupewa...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.