Bon-CN

JF-Expert Member
Oct 14, 2020
1,338
2,753
Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni. Pamoja na yote lakini Edward Lowassa alijitahidi kuipambania CHADEMA kwenye uchguzi mkuu wa 2015 ingawaje alishindwa kuipigania baada ya uchaguzi kupita. Lakini hali kwa Lowassa ikiwa hivyo, Membe ndio sikumuelewa kabisa.

Kwanza ile anaingia tu ACT na kupewa fursa ya kuipeperusha bendera, muda mfupi anaingia kwenye malumbano na Maalim Seif. Hivi nyie wenzangu mnafahamu Membe alifanya kampeni kwenye mikoa ipi hapa Tanzania?

Upinzani hawana watu wenye USHAWISHI wa kukubalika na nchi nzima.

Ndio maana wanakiangalia CHUO KIKUU CHA SIASA TANZANIA, CCM.

CCM ndiko wanakopikwa makada nguli, wabobezi wanaoendana na SIASA ZA TAIFA HILI.

Siasa za CCM ni umbile safi linaloendana na TANGANYIKA NA ZANZIBAR iliyoleta TANZANIA.....nje ya hapo ni HISIA TU.....HISIA TU nje ya hapo hakuna UHALISIA.

#SiempreCCM
#CCMNiImaniHaswa
 
ACT ni CCM B mzee achana nayo
Lakini hata chama chetu pendwa na chenyewe, kilifanya hiyo mistake! Tena si afadhali ACT ambao sioni mtu yeyote ambae ange-fit lakini CHADEMA walikuwa na mtu imara kweli kweli, Dr. Slaa lakini tukaamua kumleta Lowassa!!
 
Upinzani hawana watu wenye USHAWISHI wa kukubalika na nchi nzima.

Ndio maana wanakiangalia CHUO KIKUU CHA SIASA TANZANIA....CCM.

CCM ndiko wanakopikwa makada nguli, wabobezi wanaoendana na SIASA ZA TAIFA HILI.

Siasa za CCM ni umbile safi linaloendana na TANGANYIKA NA ZANZIBAR iliyoleta TANZANIA.....nje ya hapo ni HISIA TU.....HISIA TU....nje ya hapo hakuna UHALISIA

#SiempreCCM
#CCMNiImaniHaswa
Kwahiyo mnakubalika halafu bado mnaiba kura, tena kwa fujo huku mkituma polisi kupiga virungu wale wote wenye mwelekeo wa upinzani?
 
Upinzani hawana watu wenye USHAWISHI wa kukubalika na nchi nzima.

Ndio maana wanakiangalia CHUO KIKUU CHA SIASA TANZANIA....CCM.

CCM ndiko wanakopikwa makada nguli ,wabobezi wanaoendana na SIASA ZA TAIFA HILI.

Siasa za CCM ni umbile safi linaloendana na TANGANYIKA NA ZANZIBAR iliyoleta TANZANIA.....nje ya hapo ni HISIA TU.....HISIA TU....nje ya hapo hakuna UHALISIA.

#SiempreCCM
#CCMNiImaniHaswa
Mbona CCM hiyo hiyo inafanya mikutano ya hadhara, kutumia polisi, kukamata wapinzani n.k, Kwanini msiruhusu tume huru ya uchaguzi na mikutano ya hadhara kama mnavyofanya nyie CCM?
 
Kwahiyo mnakubalika halafu bado mnaiba kura, tena kwa fujo huku mkituma polisi kupiga virungu wale wote wenye mwelekeo wa upinzani?
CCM ni zaidi ya chama cha siasa.

CCM ni IMANI na UMBILE la nchi hii.

Kalaghabaho
 
Kama ni imara kwanini alirudi CCM badala ya kuanzisha chama chake?
Tuache masihara mkuu!!! Yaani unaweza kutilia shaka uimara wa Slaa wa kabla ya Lowassa?! Karudi CCM kwa sababu Wanasiasa sio watu wa kuwaamini lakini hiyo haiondoi ukweli kwamba Slaa alipambana sana hadi siku ya mwisho alipowekwa pembeni kwa ajili ya mtu aliyeitumikia CCM kwa maisha yake yote!
 
Lakini hata chama chetu pendwa na chenyewe, kilifanya hiyo mistake! Tena si afadhali ACT ambao sioni mtu yeyote ambae ange-fit lakini CHADEMA walikuwa na mtu imara kweli kweli, Dr. Slaa lakini tukaamua kumleta Lowassa!!
Dr Slaa alikua Imara Kwa Nini?!!.. Wewe ndio unamjua Slaa huko Vijijini wanamjua?
 
Upinzani hawana watu wenye USHAWISHI wa kukubalika na nchi nzima.

Ndio maana wanakiangalia CHUO KIKUU CHA SIASA TANZANIA....CCM.

CCM ndiko wanakopikwa makada nguli ,wabobezi wanaoendana na SIASA ZA TAIFA HILI.

Siasa za CCM ni umbile safi linaloendana na TANGANYIKA NA ZANZIBAR iliyoleta TANZANIA.....nje ya hapo ni HISIA TU.....HISIA TU....nje ya hapo hakuna UHALISIA.

#SiempreCCM
#CCMNiImaniHaswa
Siasa za CCM ndio baba wa kufisidi nchi na mama wa kudumaza maendeleo... Usisahau hiyo mnyonge mwenzangu maana sisi wanyonge bado tunanyongeka huku wala nyama wakisifiwa utukufu na watupiwa mifupa!

CCM inawenyewe au sio?
 
Lakini hata chama chetu pendwa na chenyewe, kilifanya hiyo mistake! Tena si afadhali ACT ambao sioni mtu yeyote ambae ange-fit lakini CHADEMA walikuwa na mtu imara kweli kweli, Dr. Slaa lakini tukaamua kumleta Lowassa!!
Leo Dr Slaa yuko wapi ?!. Hili nalo mbona hulioni ?!

Kama Lowassa alitoka Ccm baada ya figisu. Dr Slaa naye alitoka Cdm baada ya figisu hizo hizo za uchaguzi. Na wote walikimbilia upande wa pili .
 
Siasa za CCM ndio baba wa kufisidi nchi na mama wa kudumaza maendeleo... Usisahau hiyo mnyonge mwenzangu maana sisi wanyonge bado tunanyongeka huku wala nyama wakisifiwa utukufu na watupiwa mifupa!!
CCM inawenyewe au sio??
Siasa kokote iliko....ina watu wake.

Usisahau SIASA ni ushawishi bwana "Ahmednejad"

Ndio maana hata huko kwenu "Iran" inaongozwa na KIKUNDI CHA WATU.

Sijapatapo kuona jambo linasimamiwa na kuendeshwa na MTU/WATU wasio na ushawishi kwa wengine....hili huanzia ngazi ya mtu binafsi,familia ,kikundi mpaka TAIFA.

Siwalaumu wanasiasa....hasa CCM ya Tanzania ....kwani kwa kuwa inanipa AMANI NA UTULIVU wa kutafuta RIZIKI yangu halali basi haina makosa makubwa....mengine ni ya kibinadamu tu

Kujitahidi kufuatilia SIASA ZA DUNIA sijapata kusikia nchi isiyowalaumu WANASIASA NA SIASA ZAO ZINAZOWATAWALA ...hiyo nchi haiko.....unaweza kunitajia?
 
Ni ujinga kusema eti chama changu kinapendwa wakati kinatumia vyombo vya dola kubaki madarakani

Kusema kweli CHADEMA inaogopwa ña CCM,, CHADEMA ni chama chenye nguvu na ushawishi sana
 
Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni. Pamoja na yote lakini Edward Lowassa alijitahidi kuipambania CHADEMA kwenye uchguzi mkuu wa 2015

Naunga mkono hoja, Edward Lowassa ameisaidia sana Chadema, ila ni watu tuu hawana shukrani. Tena alikuwa afanye haya
ila ndio hivyo tena!.
Kusaidia watu wanaojitambua, yataka moyo!.
P
 
Upinzani hawana watu wenye USHAWISHI wa kukubalika na nchi nzima.

Ndio maana wanakiangalia CHUO KIKUU CHA SIASA TANZANIA....CCM.

CCM ndiko wanakopikwa makada nguli ,wabobezi wanaoendana na SIASA ZA TAIFA HILI.

Siasa za CCM ni umbile safi linaloendana na TANGANYIKA NA ZANZIBAR iliyoleta TANZANIA.....nje ya hapo ni HISIA TU.....HISIA TU....nje ya hapo hakuna UHALISIA.

#SiempreCCM
#CCMNiImaniHaswa
CCM hii haina tofauti na Bokoharam,wanachoweza ni utekaji, utesaji, mauaji na wizi wa kura. CCM kama chama cha siasa ilishajifia siku nyingi sasa hivi ni genge la kihalifu linalotegemea mitutu ya bunduki.
 
Leo Dr Slaa yuko wapi ?!. Hili nalo mbona hulioni ?!

Kama Lowassa alitoka Ccm baada ya figisu. Dr Slaa naye alitoka Cdm baada ya figisu hizo hizo za uchaguzi. Na wote walikimbilia upande wa pili .
Tuache ushabiki!! Hivi tunaweza kulinganisha utokaji wa Dr. Slaa na Lowassa kwenda CCM? Isitoshe, nimesema mwaka 2015 CHADEMA kulikuwa na mtu imara! Kukataa ukweli ni kutaka kuleta ushabiki usio na maana. Tusijisahaulishe uchaguzi mkuu wa 2010 Dr. Slaa ndie alipeperusha bendera ya CHADEMA, na alipata zaidi ya kura 2M.

Baada ya uchaguzi wa mwaka 2010, Dr. Slaa hakukata tamaa. Aakaendelea kukipigania chama, na kuzunguka huku na huko hadi dakika ya mwisho tulipomuona HAFAI na akaletewa Lowassa! Kwa kinyongo, Dr. Slaa akamwaga manyanga na kujiendea zake ughaibuni. Lakini hata huyo Lowassa, nae alijitahidi kuipambania CHADEMA pamoja na kuwa na matatizo ya kiafya, lakini kwavile shida yake ilikuwa urais tu, ndo maana alipoukosa, akarejea CCM.

Uhuni zaidi umefanywa na Membe.
 
Back
Top Bottom