CHADEMA waibua ufisadi kwenye tozo za mafuta ya petrol, diesel & kerosene. Bei badala ya kushuka ndiyo imepanda

The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
7,759
2,000


1. Hii serikali ni ya ajabu sana. Inasema uongo mchana kweupe.

2. Yaani kiongozi anatoka anasema tumepunguza tozo hii na ile ili kupunguza bei za nishati ya mafuta ya petrol, diesel na ya taa (kerosene).

3. Lakini cha ajabu, badala ya bei kupungua ndiyo zimeongezeka kwa wastani wa shilingi kati ya 12 hadi 50.

## Maswali ya kujiuliza ni:

å Hivi hii maana yake ni nini hasa?

å Je, kuna shida huko serikalini?

å Kwanini mambo yaende kinyume nyume? Yaani serikali inatamka hivi lakini practically inakuwa ni absolutely opposite kabisa.

å Je, serikali ya CCM imeamua kutufanya wana wa nchi hii wajinga na wapumbavu kiasi hiki?
 

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Sep 9, 2020
1,602
2,000
Propaganda uchwara hizi.. Bado 2025 kipigo kipo pale pale kama ilivyokuwa 2010, 2015 na 2020. Uzuri wa watanzania wa miaka hii hawadanganyiki na propaganda za hovyo hivi.

Wao wana macho wanaona na wana akili wanachanganua.

Hawangoji kuhadithiwa ujinga wa aina hii wakakimbilia kuuamini, kama wale walioamini enzi ya Lowasa.
 

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Sep 9, 2020
1,602
2,000
Kipigo au wizi kura na kukimbia na masanduku, ?!
Jibu kilichoulizwa sasa ehee mwana teuzi,
Mungu kakupa akili ya kuchanganua mambo, kwahiyo itumie ikukomboe. Umeshaona kabisa jamaa wanatumia ujinga wa wanachama wao kuwahadaa kisiasa sasa kwann usitumie hiyo akili yako kukwepa kuhadaiwa tena. Waswahili wanasema kufanya kosa sio kosa kosa ni kurudia kosa.

Shtuka ndugu yang wenzio wanakufanya daraja la kufikia mafanikio yao ya kisiasa. Najiuliza waongo hawa wanatumia mzizi gani hadi ww umeendelea kuwaamini?

images (7).jpeg


2878995_images_9.jpeg
 

mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
58,426
2,000
Eh mbona mnapenda sana kuoionea pombe
Kwani wazalishaji wa vinywaji aina ya pombe nao
Hawatumi nishati ya mafuta

Ova
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
8,228
2,000
Hayo matamko yanatolewa kisiasa ndio sababu kubwa, kiongozi anasema anachoona kitamuongezea sifa kwa wananchi lakini upande wa pili wa utekelezaji kitu hicho kinakuwa hakitekelezeki.

Pia kwa upande wa kiongozi tuliyenaye naona bado hajajitengenezea authority inayotakiwa kwa mtu wa aina yake awe wa kusema jambo then ufuatie utekelezaji instantly kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake.

Hii zaidi inasababishwa na kuweka watu kwenye ofisi za umma kwa kuangalia zaidi sura zaidi badala ya utendaji, na kurudia sura zile zile kila wakati pia kunakwamisha juhudi za kusonga mbele kwasababu wateule hawa wamesharidhika, wanajiona wana hati miliki ya kuwa viongozi serikalini hata kama utendaji wao ni mbovu walishaharibu siku zilizopita.
 

Gulwa

JF-Expert Member
Jun 16, 2008
6,329
2,000
Kumbuka rais halisi wa awamu hi ni mfanyabiashara wa mafuta. Ona sasa vituo vya lake oil vinavyo chipuka tena kwa kasi ya ajabu baada ya kudhoofika utawala wa mwendazake
 

Kilatha

JF-Expert Member
Nov 28, 2018
4,148
2,000
Siasa ni ngumu sana tofauti na watu wanavyochukulia na moja ya majukumu ya vyama vya siasa ni kuelimisha jamii sababu za kufanya maamuzi.

Ndio kama sakata la mafuta leo elimu iliyotokewa kipindi hiki ni hafifu. Ndio maana bado ni ngumu sana watu kuelewa kufutwa kwa hizo tozo kumesaidia vipi kupunguza kupanda kwa bei ya mafuta (more could have been done, but that’s a different story).

Labda serikali ingesubiri bei ya mafuta ipande sokoni kutokana na bei ya kununua, watu waone maumivi; halafu ndio wachukue hatua ya kushusha tozo.

It’s never easy in politics given that people vary in perception; unaweza chukua hatua njema before impact na watu wengi wasielewe, timing becomes important in decision making.

In short bila ya serikali kutoa tozo bei ya mafuta ingepanda zaidi; kutokana na ongezeko la bei ya kununua mafuta sokoni.
 

ndammu

JF-Expert Member
Apr 21, 2017
2,290
2,000
Propaganda uchwara hizi.. Bado 2025 kipigo kipo pale pale kama ilivyokuwa 2010, 2015 na 2020. Uzuri wa watanzania wa miaka hii hawadanganyiki na propaganda za hovyo hivi...
Kipigo chá kutegemea kuiba kwani bila ya kufanya ujinga was kutumia vyombo vya dola na tume ccm inaweza kushinda majimbo mangapi?

Sent from my SM-N9150 using JamiiForums mobile app
 

ndammu

JF-Expert Member
Apr 21, 2017
2,290
2,000
Mungu kakupa akili ya kuchanganua mambo, kwahiyo itumie ikukomboe. Umeshaona kabisa jamaa wanatumia ujinga wa wanachama wao kuwahadaa kisiasa sasa kwann usitumie hiyo akili yako kukwepa kuhadaiwa tena...
Hii ni hadithi na kila siku mnakuja nayo.

Swali CCM bila kutumia vyombo vya dola na tumeccm jee hiyo ccm yako inaweza ikashonda majimbo mangapi?

Mbona hamjiamini kama wananchi wako pamoja na ccm.

Sent from my SM-N9150 using JamiiForums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom