ccm

Chama Cha Mapinduzi (CCM) ndicho chama tawala nchini Tanzania na chama cha pili kwa muda mrefu zaidi barani Afrika, baada ya Chama cha True Whig cha Liberia. Kilianzishwa mwaka 1977, baada ya kuunganishwa kwa Tanganyika African National Union (TANU) na Afro-Shirazi Party (ASP) cha Zanzibar.
  1. T

    JamiiForums Tanzania Manyanyaso ya awamu hii yalinifanya nikaacha kazi. Wenzangu vipi mnaendeleaje na utumishi wa Umma? Mie siwapi kura CCM

    Na kilichoniumiza zaidi ni pale Mkuchika aliposaini kurekebisha Kanuni za Utumishi wa Umma - Januari 2018 ile iliyofuta Kanuni ya 107(2) iliyofuta baadhi ya haki muhimu za watumishi wa Umma. Ukweli kura siwapigii CCM! Labda wajirekebishe sana kwa muda huu mfupi uliobakia. Nyie wenzangu...
  2. Allen Kilewella

    JamiiForums Tanzania Kwanini CCM mambo rahisi hawayaelewi kirahisi?

    Tume ya Jaji Fransici Nyalali iliposema kwamba asilimia themani (80%) ya watanzania wanapendelea kubakia kwenye mfumo chama kimoja lakini wanapendekeza mabadiliko kadhaa yafanyike kwenye CCM, wana CCM wengi walitafsiri kwamba watanzania wamekataa mfumo wa vyama vingi. Kama si uelewa wa Mwalimu...
  3. J

    JamiiForums Tanzania Ukiwa Chadema brand ya chama inakubeba lakini ukija CCM lazima " Ufurukute" ndipo utasikika, wahamiaji wajipange!

    Natoa tu angalizo kwamba Nyerere aliijenga CCM katika uwezo wa mtu na baadaye ndio kikundi. Ndani ya CCM usipofurukuta utasahaulika ndio sababu hata akina Waitara na Mollel wameonekana mapema kwa sababu walijiongeza hata kama ni kwa unafiki. Chadema wao kwanza waliamua kuijenga brand yao ndio...
  4. Superbug

    JamiiForums Tanzania Wakopeshaji umiza kwa watumishi wa umma ni matokeo ya sera za CCM

    Mara kwa Mara ukiiangalia taarifa za habari utakutana na watu wanaoitwa wakopeshaji umiza. Hawa ni shylocks kwa lugha ya Kiingereza au ukipenda waite "mashailoki". Hawa jamaa wanawakopesha watumishi wa uma kwa masharti makali na ya aibu mno. Kwanza riba ni kubwa sana inaanzia 40%+ lakini pia...
  5. Erythrocyte

    JamiiForums Tanzania GE2020 Je, CCM itaruhusu wanachama wake wachukue fomu za kugombea Urais kama Katiba yao inavyoelekeza?

    Hili ni swali tu ndugu zangu na wala halina uhusiano na jambo lolote lile. Maana tumeanza kuona vyama vingine vya siasa vikiruhusu watia nia kujitokeza na kujitangaza. Je, CCM nayo itafuata misingi ya demokrasia kama dunia na katiba ya nchi inavyoelekeza?
  6. Q

    JamiiForums Tanzania CCM imezindua kituo cha kutoa taarifa za wala rushwa wakati wa uchaguzi. Hawaiamini TAKUKURU?

    Katibu wa Halmashauri Kuu Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole amesema kwamba Chama Cha Mapinduzi kimezindua kituo maalum cha wananchi kutoa taarifa za Uchaguzi kimaadili ili kuwabaini wala na watoa Rushwa, kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 2020.
  7. Environmental Security

    JamiiForums Tanzania CCM - Chama kinachotoa uwanja sawa kwa kila anayetaka kuwania nafasi za kuwakilisha wananchi

    Chama Cha Mapinduzi, ndicho chama ambacho kinatenda kwa usawa kabisa bila kubagua katika kuruhusu wanachama wake kuwania nafasi mbalimbali za kuwawakilisha wananchi katika vyombo mbalimbali vya maamuzi, hilo unaweza kuthibitisha hata kwa kupitia kwa Rais wetu mpendwa JPM ambaye aliingia katika...
  8. YEHODAYA

    JamiiForums Tanzania Vyama vya upinzani, uchaguzi huu ungeni mkono mgombea urais wa CCM hamna mgombea wa maana wa kushinda kwenu

    Vyama vya upinzani havina mgombea yeyote wa maana wa kushinda uchaguzi wa urais kupitia vyama vyao sababu vyote kwanza havina nguvu pande zote za muungano. Chadema ina nguvu Tanzania bara tu mkoa wa Kilimanjaro tu kidogo mji wa Arusha upande wa Zanzibar hamna kitu. Hivyo akiwekwa mgombea uraisi...
  9. Miss Zomboko

    JamiiForums Tanzania Prof. Safari: Vyama vya upinzani vinasumbuliwa na ubinafsi ndiyo maana vimeshindwa kumtoa CCM

    ALIYEKUWA Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Prof Abdallah Safari, amesema vyama vya upinzani vina ubinafsi na matokeo yake vimeshindwa kukiangusha Chama cha Mapinduzi (CCM). Akizungumza mapema leo kwenye kipindi cha Front Page kinachorushwa na +255GlobalRadio...
  10. VUTA-NKUVUTE

    JamiiForums Tanzania Hivi, CCM tunamtapeli na kumlaghai nani kuhusu kuichukia rushwa uchaguzini?

    Kisiasa, unapoisha uchaguzi mmoja maandalizi ya uchaguzi mwingine huanza. Maandalizi ya uchaguzi wa mwaka huu 2020 (kuihusu CCM pekee) yalianza tangu mwaka 2015. Makada walijipanga kutetea majimbo na kata na wengine wakitamani kuzipoka kata na majimbo kutoka kwa wasasa. Maandalizi ya kiuchaguzi...
  11. J

    JamiiForums Tanzania Ni ujinga uliopitiliza kupanga foleni kumpigia kura mgombea wa CHADEMA/upinzani wakati msimamizi wa uchaguzi ni kada wa CCM

    Wananchi ni lazima tujue kwamba katiba ya JMT ndio inayobariki ushindi wa CCM. Na kiukweli ukiangalia maeneo ambayo upinzani huwa unashinda mara nyingi inakuwa ni ulegelege wa mkurugenzi ambaye ndiye msimamizi wa uchaguzi au huruma tu ya CCM yenyewe. Ni wale wananchi wapenda mageuzi mkaendelea...
  12. Mystery

    JamiiForums Tanzania GE2020 Serikali ya CCM imepoteza "credibility" ya kupambana na watoa rushwa

    Tulisikia "maigizo" ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Humphrey Polepole, akieleza kuwa safari hii kwenye uchaguzi wa mwaka huu wa 2020, hawataruhusu hata kidogo watoa rushwa wenye nia ya kutaka kupendekezwa na chama hicho kwa nia ya kuwa wagombea kwa nafasi yoyote katika uchaguzi ujao...
  13. Mudawote

    JamiiForums Tanzania Raha tuliyonayo wana CCM kuelekea 2020

    Great Thinkers, Kwa heshima ya jukwaa hili na weledi wa ma GTs’ JF, ninaomba tuungane kusherehekea ushindi mnono wa CCM kuelekea 2020 kwa sababu: 1. CCM imeweza kutekeleza ahadi zake zote za 2015 2. CCM inamgombea urais anayekubalika 100% na hana mpinzani ndani na nje ya chama.
  14. F

    JamiiForums Tanzania CCM Wapongezwe kwa Kuiogopa CHADEMA, Wasibezwe!

    Tangu mwaka 2010 Chadema kilipokuwa chama kikuu rasmi cha upinzani nchini, siasa za Tanzania hazijawahi kubaki za kawaida! Kwa wenye kumbukumbu nzuri, tangu mwaka 2010 chama kilipoanza kuongozwa na Freeman Mbowe, CHADEMA kimekuwa chama pekee cha upinzani nchini kinachokua mfululizo (both...
  15. Mikopo Chefuchefu

    JamiiForums Tanzania CCM, Tumeshampata Rais, sasa mtuwekee wazi gharama za kuchukua fomu za ubunge na udiwani nchi nzima watu wajipange!

    Maana kulijitokeza malalamiko ya gharama kubadilika badilika kama hali ya hewa kwenye uchaguzi uliopita. Wekeni standardized amount ili wa kudunduliza waanze kudunduliza kiasi kitachotakiwa!
  16. J

    JamiiForums Tanzania GE2020 Rais Magufuli: Wagombea watarajiwa wa CCM wajipime kwanza kama wanatosha, wasikurupuke tu na kwenda kukiumiza chama

    Rais Magufuli ambaye ndiye Mwenyekiti wa CCM amewataka wagombea watarajiwa katika uchaguzi mkuu wajipime kwanza kama wana ubavu badala ya kukurupuka. Amewataka wagombea kujipima uwezo wao na kulinganisha sifa walizonazo na zile za watia nia wengine kama huna unachowazidi ni heri ukakaa pembeni...
  17. Roving Journalist

    JamiiForums Tanzania Kinondoni, Dar: TAKUKURU inawashikilia viongozi wanne wa Jimbo la Ubungo(CCM) kwa tuhuma za rushwa

    Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) Wilaya ya Kinondoni, inawashikilia viongozi wanne wa Jimbo la Ubungo(CCM) kwa tuhuma za rushwa pamoja na kuanza kampeni za uchaguzi mkuu kabla ya muda.
  18. T

    JamiiForums Tanzania GE2020 Polisi iepuke kabisa kuwa Polisi ya USA dhidi George Floyd!

    USA ubaguzi wa rangi na matendo ya kinyanyasaji yalizidi sana. Mpaka leo bado kuna Miji inatangaza maandamano. Nimeona waandamanaji wanaokuwa tayari kugongwa hata na magari ili wafe kwa ajili ya uchungu wa manyanyaso hadi kifo ya mpendwa wao George Floyd. CCM yangu inaingia kwenye Uchaguzi...
  19. K

    JamiiForums Tanzania Hakuna siku CCM Zanzibar ilipata tabu kama tarehe 25 - 28 Oktoba, 2015

    Kama mtakunbuka hali ilikuwa tete Zanzibar kwenye kinyanganyiro cha uchaguzi wa 2015 Zanzibar. CCM ilikuwa na hali Mbaya katika Maeneo yote. Uwe po Wa GNU kilikuwa kikwazo cha kwanza. Kukataliwa kwa ccm na wazanzibari kilikuwa kikwazo cha pili. GNU kuliinyima CCM Zanzibar bar Uhuru...
  20. I

    JamiiForums Tanzania Vijana wa familia maskini tuungane kupambana na hawa wakoloni weusi wa CCM

    Wakuu. Tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu napenda kuwakumbusha vijana wa nchi hii, hasa wale wanaotoka familia masikini mijini na vijijini kuwa imewapasa kuelewa kuwa nchi hii inapelekeshwa na hawa wakoloni weusi wa CCM kwa sababu wao wana advantage moja ya kuwa na urahisi wa kuitafuna keki ya...
Back
Top Bottom