RockCarnegie
JF-Expert Member
- Jan 17, 2019
- 963
- 1,927
Habani wana JF
Toka enzi za TANu kabla na baada Uhuru wa Tanganyika hadi kuzaliwa kwa CCM, chama hiki kimekuwa kikijinasibu kuwa ni chama cha kutetea maslahi ya Wakulima na Wafanyakazi wa nchi hii!
Tangu Serikali ya awamu ya Rais Magufuli maarufu a.k.a Jiwe iingie madarakani Wakulima Tanzania wamakuwa wakilalamika jinsi serikali ilivyowafukarisha kwa kuharibu bei na masoko ya mazao yao! Mfano wakulima wa korosho, pamba, kahawa, ufuta, mbaazi, choroko na mazao mengine mengi yameanguka kwa kukosa masoko.
Hivi karibuni mawaziri wa kilimo na viwanda naa biashara wamesikika wakiwaambia wakulima kuuza mazao yao popote wanapotaka baada ya miaka mitano ya kuwalazimisha wakulima kuuza mazao yao kwenye vya ushirika walivyovifisilisi wao wenyewe kwa ufisadi!
Wanunuzi wa mazao wametaifishwa mali zao wakilazimishwa kutumia vyama vya ushirika kununua mazao ya wakulima. Sasa wakulima wanaambiwa wajijitafutie wanunuzi mazao yao baada ya wanunuzi kukimbia ukatili wa serikali ya Jiwe!
Jembe limegeuka kutoka kuwa alana ya ukombozi wa maisha ya wakulima hadi kuwa zana ya kuchimba kaburi la uchumi wao.
Wafanyakazi wa umma ni mwaka wa tano sasa hakuna nyongeza ya mishahara na Rais wakati kuvunja bunge alisisitiza waziwazi kuwa waendelee kufunga mikanda kwani SGR, Stigler na mandege yako njiani kuja kuwakomboa kiuchumi!
Nyundo iliyokuwa alama ya ushujaa na thamani ya wafanyakazi kulijenga taifa sasa inawatwanga wafanyakazi wa Tanganyika na Zamzibar na kuwazika kwenye kaburi umasikini na uoga uliokithiri!
Jembe na Nyundo ni alama mfilisi inayotumiwa na CCM kuwahadaa Wakulima na Wafanyakazi Tanzania! Ili kuendelea kuwanyonya!
Tunapoelekea uchaguzi mkuu 2020, ni wajibu wa Wakulima na Wafanyakazi kuukataa Ubeberu Jiwe. Vinginevyo mjiandae kumusujudia miaka mingine mitano ijayo!