Chama Cha Mapinduzi (CCM) ndicho chama tawala nchini Tanzania na chama cha pili kwa muda mrefu zaidi barani Afrika, baada ya Chama cha True Whig cha Liberia. Kilianzishwa mwaka 1977, baada ya kuunganishwa kwa Tanganyika African National Union (TANU) na Afro-Shirazi Party (ASP) cha Zanzibar.
Moja kwa moja kwenye mada; kitendo cha Mwenyekiti wetu kusema kura zote ziwe za wazi na zote zitangazwe hadharani kweli kimetuumbua makada wengi mno.
Sasa mtaani hatuna amani kila ukipita unasikia 4 mara 2 mara zero. Kwa kweli Mwenyekiti wetu tunakupenda sana ila kwa hili umetuumbua sana sisi...
Inafahamika huu msimu wa uchaguzi ndo msimu wa rushwa kwenye siasa.
Wagombea wanaotoa rushwa ni wengi mno..na wajumbe wanaodai rushwa wengi zaidi...sasa cha kushangaza hakuna taarifa za kukamatwa wajumbe hata moja.
Zinakuwepo taarifa za kukamatwa wagombea lakini wajumbe hakuna...
Jana tarehe 21/07/2020, katika harakati za wajumbe kupiga kura Bukoba Vijijini kwa wajumbe waliotia nia Ubunge kupitia CCM, kulitokea utofauti asubuhi ambapo mbunge Rweikiza alituma vijana wake kutoa rushwa na kukamatwa jana ile ile Asubuhi.
Naamini TAKUKURU watalitolea taarifa sakata hili...
Wajumbe wa Kamati ya Uchaguzi wa CCM jimbo la Butiama, mmefanya kitendo kibaya sana. Katika kura za maoni mmeshindwa kumuenzi Baba wa Taifa Mwl. Nyerere kwa kumchagua mtoto mmoja wa Baba wa taifa kweli mmeshindwa?
Familia ya Baba wa Taifa imetoa wagombea wawili katika hao mmeona hakuna...
Kama GENTAMYCINE ningekuwa ni Mwenyekiti wa CCM Taifa baada ya huu 'Mchakato' mzima wa Kura za Maoni ambazo zimefanyika kwa Uwazi zaidi huku zikionyesha kabisa kuwa wana CCM ' wameamua ' bila ' Ngendembwe / Hila ' zozote katika Kikao cha Maamuzi cha mwisho cha ' Watia Nia ' kwa nafasi ya Ubunge...
Sipendi kabisa ushabiki wa vyama vya siasa, Wengi wameshangilia kushindwa kwake katika Chama cha Mapinduzi.
My behavioral psychanalysis is:-
Kwa kauli za Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi:
Makonda ana uwezo mkubwa wa kiuongozi na amekabiliana na tough times kuliko wakuu wote wa mikoa hapa...
Katika majimbo yote hapa Tanzania, kwa Bukoba mjini CCM mtachezea kichapo cha karne.
Hivi huyo diwani wa Ijuganyondo, kamala anawezaje kumshinda Chief kalumuna kwenye ubunge? Hapo CCM jiandaeni kulia tena uzuri sisi Bukoba mjini tunajitambua.
Ukifuatilia vizuri na kuhoji watu mbalimbali wanaonaje matokeo yanayoendelea kura za maoni za CCM jibu utakalopewa ni kuwa yale makundi yaliypshindwa kuchukua nchi 2015 yakiwemo mafisadi na vibaraka wao na waliohujumu CCM uchaguzi wa 2015 yameanza kujikusanya kwa kushinda kura za maoni maeneo...
Habari,
Naomba kupata Taarifa ya mshindi wa kura za Maoni Jimbo la Kawe ndugu Furaha Dominic ni nani haswa?
Imekuwaje akawashinda vigogo wengine kwenye kura za maoni ndani ya CCM katika Jimbo la Kawe?
Je, ni mpinzani sahihi kwa Halima Mdee kwenye uchaguzi wa Oktoba?
Kuna msemo usema mwenzio akinyolewa wewe tia maji
CHADEMA msichelee wabunge wenu waliohamia CCM kupigwa chini kura za maoni ndani ya CCM
Hao wenu Waliobaki huko wasijione kuwa salama watashinda na kuzomea wenzao wahamiaji walioshindwa kura za maoni !!! Hao waliobaki CHADEMA watakoshindana na...
Wanabodi,
Hili ni bandiko la ombi maalum kwa Wana JF wenzangu, nawaombeni sana mnipe pole na msinicheke, wala msinibeze, kujaribu kugombea ubunge wa Kawe kupitia CCM, nimeambulia kura 1!
Japo nimeshindwa kwa kupata kura moja, lakini sababu za mimi kugombea ni very valid na very genuine...
Habari wakuu!
Kila siku Kuna habari mpya nchi Tanzania kutokana na Taifa linaenda kuingia katika uchaguzi wa viongozi.
Mnamo 20/07/2020 uchaguzi kwa WATIA NIA ya kugombea upande wa chama Tawala ulianza na mpaka hivi Sasa unaendelea, lakin Jana mida ya saa 1 nimepata kuona kapost Fulani...
Huu Uzi hauna kejeli, matusi wala dhihaka. Huu uzi umebeba ukweli mchungu (a bitter truth) ambao wengi hawaupendi.
Kama Magufuli angesimamishwa na MwanaCCM yeyote imara kuwania tiketi ya kupeperusha bendera ya CCM 2020 katika ngazi ya Urais asingeshinda.
Mioyoni mwa wanaCCM kuna siri na ajenda...
Kuangushwa katika kura za maoni za CCM, katika jimbo la Kigamboni, kwa Paul Makonda na Faustine Ndugulile, kumepokelewa kwa shangwe kubwa sana na watanzania wa nchi nzima
Hivi hali hiyo inaweza ikawa inaashiria nini?
Hivi inawezekanaje kwa mkuu wa mkoa, ambaye mara kwa Mara amekuwa akisifiwa...
Siku mbili kuanzia Jana Tarehe 20 July 2020, CCM wamekuwa na Kura za Maoni ndani ya Chama chao, kitu pekee katika mchakato huu ni namna ulivovuta hisia za Watanzania bila kujali vyama vyao, Wote tumetega masikio na kufungua macho kuuona wana CCM wataamua nini
Binafasi nawafahamu washindi wa...
Mlihama CUF na CHADEMA kwa mbwembwe sana kuhamia CCM. Mkatupa karata zenu kuwania Ubunge. Sasa mmeshindwa kwenye kura za maoni ndani ya CCM. Tena mmepigwa 'kipigo cha mbwa koko'.
Sasa mmeamini kuwa CCM ina wenyewe na wenyewe ndio hao waliowapita kura za maoni na waliowakataa kupitia kura zao...
Juzi baada ya kushtukia mpango wa viongozi wa CCM Wilaya kumpatia kura Dkt. Mwigulu Nchemba mpango huo ulichezwa kwa namna ingine.
Pamoja na kuweka mazingira yote kuwa kura zitahesabiwa kwa uwazi na taratibu zingine zote kufuatwa bado Dkt. Mwigulu alikuwa kishawashawishi viongozi wote wa CCM...
KUMKATA MAKONDA SI MAAMUZI YENYE AKILI
Na, Robert Heriel
Ikiwa CCM itaamua kumkata Mhe. Paul Makonda itakuwa imefanya maamuzi yasiyo na busara. Yatakuwa ni maamuzi yasiyo na akili. Makonda ni moja vijana wachache muhimu kwa zama hizi katika taifa hili. Taifa la Tanzania linahitaji vijana mia...
Wilayani kwetu tangu nikiwa mdogo, kuna kiwanja kilichotengwa kwa ujenzi wa Ofis za Chama Wilaya, kiwanja hiki kilikuwa kwenye prime area kinatazama barabara kuu.
Wakubwa walifika bei na kumuuzia Mwarabu ambae amejenga Hotel. Mpaka sasa ofisi ya CCM ni ile ile iliyokuwa ya TANU. Kuna pesa za...
Kwa kweli yaliyofanyika kuanzia Uchaguzi wa kuwapata wagombea Urais kule Zanzibar kuanzia ile tarehe 8 mpaka leo nchi yetu imesimama kwa maana ya uwazi wa mchakato wa uchaguzi ulivyokuwa
Haijawahi kutokea popote Duniani kwa chama chochote tangu kuumbwa kwa Dunia kuwa na mvuto kama wa CCM mwaka...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.