Kwa matokeo haya ya waliounga juhudi kuangukia pua, mmeamini kuwa CCM ina wenyewe na wenyewe ndio hao?

Petro E. Mselewa

Verified Member
Dec 27, 2012
9,523
2,000
Mlihama CUF na CHADEMA kwa mbwembwe sana kuhamia CCM. Mkatupa karata zenu kuwania Ubunge. Sasa mmeshindwa kwenye kura za maoni ndani ya CCM. Tena mmepigwa 'kipigo cha mbwa koko'.

Sasa mmeamini kuwa CCM ina wenyewe na wenyewe ndio hao waliowapita kura za maoni na waliowakataa kupitia kura zao? Ndiyo mjifunze kuwa vyama vina wenyewe. Na tena, muwe mnaridhika na kuvitumikia vyama vyenu.
 

zigii

JF-Expert Member
Apr 28, 2017
516
250
Mimi hisia zangu zinanituma hawa watu Jpm hatawaacha nje ya mfumo mwakani 2021 serikalini kuna vyeo vingi bila shaka atawashika mkono tena.

Kama itakuwa hivyo basi uwezekamo wa kuamini ndani yao hamna watu wazuri wanaoweza kufanya kazi za serekali
 

LESIRIAMU

JF-Expert Member
Feb 12, 2008
6,384
2,000
Hilo swali pia lipeleke kwa Silinde Calisti Lazaro na Lijua likali. Waliambiwa wawe na akiba ya maneno Asante sana Bulaya uliona mbali. Wana takiwa wajue hawakuwa na umaarufu wowote bali Chama ndicho kiliwapa umaarufu. Tukutane kwenye kiti moto bar.
 

Nazgur

JF-Expert Member
Apr 19, 2020
2,475
2,000
Kwanza niwape pole wote waliotia nia na kushindwa katika nafasi walizoomba kwani hata ingekuwaje kila jimbo anahitajika mtu mmoja hivyo niwape pole wale waliokuwa na matumaini makubwa ya kupata nafasi kisha wameshindwa.

Pili niwape pole wale wateule wa Raisi kwa kuacha majukumu yao na kwenda kucheza kamali kitu ambacho ni cha kubahatisha.

Nipingane na wengi wenye mawazo kama ulivyotoa hapo kwenye kichwa cha habali,
Kama CCM ina wenyewe basi wale wote walio tia nia basi wote wangepitishwa kwa sababu ni wenye CCM,

Kuingia kwa wanachama kutoka upinzani hawawezi kuwa Special na kuabudiwa kuliko waliopo, jambao la msingi ni wewe kukubalika na wapiga kura.

Kwa sasa CCM hakuna special kama vyama vya upinzani amabavyo bado vinahitaji watu kutoka CCM.

Kosa walilofanya hawa wateule ambao walipata nafasi za uteuzi wakitokea upinzani, walikuwa na kipimo kimoja tu ili waaminike na wanachama halisi ni kutumikia nafasi zao kwa muda wa kutosha huku wakiweka mahusiano yasio na shaka na chama angalau kwa miaka 5 kisha ndo waje kujipima.

Uhalaka umewapa hasara ya kukosa vyote wakati wangekuwa bado wakipata mishahara ya serikari kitu ambacho hapo nyuma hawakuwa nacho.

Kuhusu mtulia mbunge, sioni sababu ya kkumshambulia kwani hata wabunge wengine wa CCM waliokuwa na na fasi wanawez kubaki na yakaja majina mapya, sasa hao matsema walitoka chama gani?

Na hata huko upinzani kuna watu watabaki wengi na wakapita wapya, pia unaweza ukapita kwenye chama lakini kura za wengi ukabaki uwe CCM Au Upinzani lolote linaweza kutokea.

Yangu ni hayo kwa leo kuhusu watia nia.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom