Uchaguzi 2020 Wana JF, nipeni Pole. Msinicheke wala msinibeze; nimegombea ubunge Kawe kupitia CCM nimeambulia kura 1. Ama kweli CCM ina wenyewe!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,337
113,180
Wanabodi,

Hili ni bandiko la ombi maalum kwa Wana JF wenzangu, nawaombeni sana mnipe pole na msinicheke, wala msinibeze, kujaribu kugombea ubunge wa Kawe kupitia CCM, nimeambulia kura 1!

Japo nimeshindwa kwa kupata kura moja, lakini sababu za mimi kugombea ni very valid na very genuine

Kwanza ni kushukuru kwa yote, hiyo kura moja niliyoipata ni kitu kikubwa sana kwangu, asante sana kwa aliyenipigia kura.

Pili, nimekubali matokeo na kukubali kuwa ama kweli CCM Ina wenyewe!, na wenyewe wenyewe ndio sisi, mimi nikiwemo!. Asiyekubali kushindwa sio mshindani.

Despite the facts ni njia gani wenzangu walizotumia kushinda, the end justifies the means, nawapongeza kwa dhati washindi wote,

Na tatu hili nilisema kwa moyo wangu, sina kinyongo chochote kushindwa, naahidi ushirikiano, na ile ahadi ya kutoa TZS Milioni 100 kwa CCM, nitaitimiza kupitia fund raising na sio kutoka mfukoni kwangu, hivyo naahidi ushirikiano wa dhati na kuendelea kuwa mwanachama mtiifu wa CCM.

Nipeni tu pole!.
Kidumu Chama cha Mapinduzi.
CCM Oye!.

Paskali

Uchaguzi 2020 - Pascal Mayalla aomba kura Kawe, adai akipitishwa atagawa Tshs. Milioni 10 kwa kila Kata

Uchaguzi 2020 - Kawe kunani? Why is a hot cake? Wamejitokeza wagombea 176! What is so special ? Kuchinja watu 175 kubaki 1, is not a joke!.Je, atakuwa nani?

Uchaguzi 2020 - Wingi wa wagombea CCM ni uthibitisho kazi nzuri ya Rais Magufuli kwa taifa letu. Je, Oktoba ni kuchagua au kuthibitisha tu taratibu?
 
Tatizo ulificha unagombea wapi na chama gani. Ukaja na uzi wa kuponda walochuku fomu wakati nawe upo. Ungetangaza mapema naamini kuna wangekufahamu na kukupigia kura.

Wanaokujua wengi Bwana Pascal ni JF kwa kizazi cha sa hivi huko mtaani ni wachache sana.
 
Pole Sana kaka. Jipange Next Time. Nimekuona Hapa una angaika Tu.

Najiuliza Hapa. Inakuaje Kada Kama Wewe,katika Wajumbe 500 na Zaidi Unapata Kura Moja.kweli CCM Ya Sasa Baba Lao.

Hongera Mmepishana Kidogo sana na Mwijaku.
 
182 Reactions
Reply
Back
Top Bottom