Uchaguzi 2020 Kumkata Paul Makonda kwenye Kura za Maoni CCM, siyo maamuzi yenye akili

ROBERT HERIEL

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
1,016
2,000
KUMKATA MAKONDA SI MAAMUZI YENYE AKILI

Na, Robert Heriel

Ikiwa CCM itaamua kumkata Mhe. Paul Makonda itakuwa imefanya maamuzi yasiyo na busara. Yatakuwa ni maamuzi yasiyo na akili. Makonda ni moja vijana wachache muhimu kwa zama hizi katika taifa hili. Taifa la Tanzania linahitaji vijana mia moja mfano wa Makonda ambao watakuwa nchi nzima kwa ajili ya kuleta mabadiliko ndani ya nchi hii.

Ni muhimu Makonda akipitishwa na CCM katika nafasi ya ubunge kisha baadaye apewe nafasi ya uwaziri katika wizara zinazowahusu vijana, burudani na michezo.

Kwa nini Makonda ni kete muhimu kwa siasa za sasa hapa nchini?
Hoja zifuatazi zitahusika;

1. UJASIRI
Makonda ni kijana jasiri asiye mwoga. Ni moja ya vijana wachache hapa nchini ambao wameonyesha uwezo mkubwa katika uongozi, Makonda matukio aliyojiingiza yanambeba licha ya kuwa hajafanikiwa sana lakini angalau tuliona nia yake. Kuna mambo kuyafuatilia lazima uwe na roho ya kikulungwa, roho ya simba. Kufuatilia Wauza Madawa ya kulevya ni moja ya mambo ambayo ni magumu sio hapa nchini hata duniani kwa ujumla.

Makonda ni jasiri kwani haogopi kusimamia kile anachokiamini. Watu waoga huwa hawana Msimamo. Kilichomwangusha Makonda ni mipaka ya mamlaka katika kazi yake.

2. MWANAJAMII
Makonda ni moja ya viongozi wasiojifungia ndani. Huchangamana na jamii. Sio wale viongozi ambao wakipewa nafasi hujifungia ndani muda wote maofisini, kumuona tuu utahangaika mpaka ukate tamaa. Hii ni tofauti na Makonda, yeye anapatikana muda wowote, ukifika ofisini kwake hakuna milolongo ya ajabu ajabu. Makonda ni kawaida kumuona kwenye matukio ya kijamii mathalani matamasha ya vijana ya burudani na michezo, matukio ya misiba, n.k. Hii ni tofauti na viongozi wengine. Kiongozi lazima achangamane na jamii.

3. USTAHIMILIVU
Kama kuna vijana wavumilivu kwenye hili taifa ni pamoja na Makonda. Moja ya vijana walioonja joto la jiwe awamu hii mitandaoni na kwenye vyombo vya habari ni pamoja na Makonda. Licha ya kashfa kibao kama vile Kufoji vyeti, ambapo mahasimu wake walidai alicharaza mswaki kidato cha nne kwa majina yake halisi Daudi Albert Bashite. Hilo akalivumilia, kashfa za kuwa anatabia za kishoga, nalo akavumilia, kashfa za kuwa hana uwezo wa kuzaa mtoto, yote alistahimili.

Pengine aliniudhi siku moja aliyolia kanisani, ile siku alijishushia credit. Mwanaume kulia lia mbele za watu sio jambo jema hasa wanaume shupavu. Hata hivyo halimuondolei sifa zingine lakini namuasa, siku nyingine asilie lie mbele za watu. Mwanaume kulia lia ni dalili ya udhaifu.

4. DHAMIRI YA DHATI YA KUISAIDIA JAMII
Makonda ni moja ya viongozi waliojipambanua katika kuisaidia jamii yake hasa kwenye Mkoa aliopewa auongoze. Makonda amesaidia vikundi vingi vya kina mama na vijana. Makonda ameonyesha nia za kuwasaidia watoto na kinamama waliotelekezwa na waume zao. Makonda ameonyesha nia ya kuwasaidia wale walioonewa kisheria kwa kuwawekea wanasheria, Makonda kajitahidi kupunguza uchafu wa jiji la Dar es Salaam, Makonda kajitahidi kurejesha usalama jijini Dsm kwa kupunguza vikundi vya Panya Road, sijui watoto wa Mbwa n.k.

Makonda anaweza asionekane ni kijana bora labda kutokana na tabia yake ya kujitukuza, na kutoa maneno ya shombo ambayo kwa sehemu kubwa nafahamu analenga kujifariji na kuwaumiza adui zake. Kwa kawaida kisaikolojia watu wanaotoa maneno ya shombo huyatamka kama njia ya kujifariji na kuondoa sonona, na kuwaumiza adui zao.

Wapo wakuu wa Mikoa wengi lakini waliofanya kama makonda hawafiki kumi. Hii ni dalili kuwa Makonda anafaa kupewa nafasi zaidi ya ukuu wa Mkoa.

5. MSAADA MKUBWA KWA MAGUFULI
Kama kuna watu waliomsaidia Mhe. Magufuli katika uongozi wake basi ni pamoja na Makonda. Imekuwa ngumu kumtenganisha Magufuli na Makonda katika siasa za awamu ya tano. Makonda amekuwa moja ya wabadilisha upepo katika masuala yanayotokea hapa nchini. Kwa namna hii amekuwa msaada mkubwa katika siasa za awamu hii. Makonda haoni shida kusemwa yeye kwa kupoteza mada fulani iliyokuwa inavuma ikiisakama Serikali.

Pengine Makonda asiwe na ushauri wa maana kwa Magufuli lakini kiukweli anamchango mkubwa katika kubadili upepo wa mambo yanayovuma hapa nchini. Hili pekee linatosha kwa Magufuli kumkubali Makonda. Kumzima Makonda kwa wakati huu sio uamuzi wa akili. Nyota yake inang'aa lazima itumiwe kwa maslahi ya nchi.

6. KAFANIKIWA KULETA UTISHO
Makonda ni moja ya viongozi wachache waliofanikiwa kuleta utisho kwa watu wengi hapa nchini. Watu wa kawaida na viongozi wengi wanamuogopa Makonda. Kujenga hofu ni moja ya mambo ya muhimu katika utawala. Hofu hufanya utekelezaji uende kwa haraka. Makonda kwa cheo alichokuwa nacho cha ukuu wa Mkoa hakilingani na hofu aliyoijenga ndani ya jamii yake. Wengi humheshimu kupita cheo alichonacho.

7. BINGWA WA UHAMASISHAJI NA UCHANGISHAJI
Kiongozi sharti awe amebobea katika kuhamasisha watu. Makonda anajua kuhamasisha watu. Makonda anauwezo wa kuwachangisha matajiri, Akawaweka pamoja wafanyabiashara, wasanii na watu maarufu. Makonda anauwezo wa kuhamasisha vyombo vya habari vizungumzie jambo fulani. Tumeona mara kadhaa Makonda akikodisha kumbi za gharama kwa ajili ya tukio fulani mpaka wengine wanasema huyu Makonda anatoa pesa wapi. Makonda ni mhamasishaji na mchangishaji kwa wale atakaowaona wadau wa maendeleo.

Matajiri watachanga iwe kwa kumuogopa au kwa upendo. Hiyo haitamhusu Makonda ilimradi lengo limefikiwa.

Viongozi wengine katika hili walishindwa kabisa.

Magufuli anahitaji vijana kama hawa, watu kama Makonda, Tundu Lisu, Jokate, Anthony Mtaka, Prof jay, Ally Hapi, GJ Malisa, Ole Mushi, Ole Sebaya, Sugu, Profesa Mkandara, Ummy Mwalimu, Joyce Ndalichako, Suleiman Jafo, Bashe, Kassim Majaliwa, Bashiru, Ester Bulaya, miongoni mwa viongozi wengine wenye sifa.

Nafahamu kila mmoja ana mapungufu lakini kwenye mizani; ubora uzidi mapungufu.

Makonda apewe nafasi kwani ni mtu anayejirekebisha kila uchwao, sio mtu wa kutoa boko tena kama zamani alipokuwa mgeni wa kazi.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300.
 

ROBERT HERIEL

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
1,016
2,000
Angetaka “kumsaidia Magufuli” angebakia kwenue ukuu wa Mkoa. Vikao vya kuchuja watia nia vitafanya kazi yao na labda watampitisha na kuwaachia wanaCCM wa Kigamboni wafanye maamuzi yao
Umenena vyema kwa upande wako, sio kosa kwake kumuambia Mhe. Rais matamanio yake pia. Kazi ya Ukuu wa Mkoa kafanya vizuri, bila shaka hata kazi ya ubunge atamsaidia zaidi na zaidi.
 

ROBERT HERIEL

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
1,016
2,000
Mwana kulitaka, mwana kulipata. Mbona mapema mno tusubiri bhana!
Katika Siasa za vijana, Makonda kamsaidia sana Magufuli kwa sehemu kubwa. Makonda ameshiriki matusi, katukanwa na watu wa ndani na nje ya nchi. Sijaona mpaka sasa aliyeonja uchungu na utamu kwa awamu hii kama Makonda. Mhe. Rais mwenyewe analijua hilo.
 

Uttarra

JF-Expert Member
Jan 5, 2019
397
1,000
Si ndio mwenye jiji lake huyu, zile kauli mbio na matukio lukuki yataendelezwa au ilikua kiki? Madawa ya kulevya, wajane, usafi wa Jumamosi na vingine ni unclosed projects.

Atarudi lini humu jamvini jukwaa la siasa na uchaguzi tujadili?
 

Bana likasi

JF-Expert Member
Jan 7, 2020
6,970
2,000
ROBERT HERIEL,

We ni muhimu wa falsafa za kikomunisti umetumwa kumsafisha, Mshawishika wa propaganda na sio tija. Uongozi na uoga hizo ni falsafa za kikomunisti.

Kioo cha mtu ni mtu mwenyewe,huyu aliyekutuma yamfatayo ni kutokana na matendo yake, haikuwa Vita ya unga Bali kutumia unga kuwashughulikia wapinzani wao, wajua ni pesa ngapi wamepiga pale kwa kuwambambikia watu sakata lile, huyu ndugu yako hafai kabisa hata kupewa uongozi wa darasa, hana ethics za uongozi.

Kuombea taifa lipate watu wa aina yake ni kumkosea Mungu.

Bashite ni sawa na maliyamungu wa Amini au Abubakari wa Abacha.
 

ROBERT HERIEL

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
1,016
2,000
Bashite hata akiwa wa mwisho kwenye kura za maoni lazima mtukufu ataamuru apitishwe tu wala hakuna namna
Kwenye siasa lolote linaweza kutokea mkuu. Ndio maana usishange tukijitokeza kuonyesha umuhimu wake. Sio tusubiri akose ndio tujitokeze kuonyesha sifa zake.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom