Watanzania kushangilia kuangushwa kwa Makonda katika kura za maoni Jimbo la Kigamboni kunaashiria nini?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,479
30,144
Kuangushwa katika kura za maoni za CCM, katika jimbo la Kigamboni, kwa Paul Makonda na Faustine Ndugulile, kumepokelewa kwa shangwe kubwa sana na watanzania wa nchi nzima

Hivi hali hiyo inaweza ikawa inaashiria nini?

Hivi inawezekanaje kwa mkuu wa mkoa, ambaye mara kwa Mara amekuwa akisifiwa hadharani na Rais Magufuli aliyemteua na kumtaja kuwa ndiye mkuu wa mkoa bora kabisa hapa nchini na wakuu wa mikoa wengine, wanapaswa waige mfano wa uchapaji kazi wa huyo Paul Makonda, wanaccm wa Kigamboni waamue kumnyima kura?

Licha ya malalamiko mengi sana ya wananchi kuwa Mkuu huyo wa mkoa hafai na kumwomba Rais Magufuli atengue uteuzi wake................

Hata hivyo Rais Magufuli amekuwa akiweka pamba masikioni na kutotaka kabisa kusikiliza maoni hayo ya wananchi, hadi wakati fulani aliwahi sikika Rais Magufuli akimwambia Mkuu huyo wa mkoa aendelee kuchapa kazi na asisikilize hizo shutuma zinazotolewa na wananchi walio wengi na akaendelea kumsifia kuwa yeye Makonda ndiye RC bora kabisa hapa nchini, ambapo maRC wengine wanapaswa wamuige yeye Makonda kwa.uchapaji kazi wake!

Je ni kiburi hicho alichopewa na Mheshimiwa Rais, ndicho kilichompa kichwa hadi kuwadharau watanzania wote hadi wakuu wake wa kazi?

Bila shaka wananchi bado hawajasahau lile sakata la namna mkuu huyo wa mkoa, Paul Makonda, alivyoweza kutunushiana "msuli" na waziri wa Fedha, Mheshimiwa Philipo Mpango, kuhusu yale makontena yake ya "fanicha" aliyotaka kuyaingiiza nchini bila ya kuyalipia ushuru, hadi pale Mheshimiwa Rais alipoingilia kati na "kumwamuru" mkuu huyo wa mkoa ayalipie ushuru stahiki makontena hayo

Kutokana na kiburi chake kilichopitiliza wananchi walifikia hatua ya kumbatiza cheo kisichokuwepo cha "Naibu Rais" wa Tanzania!

Hata hivyo wananchi wote wa nchi nzima, hatuna budi kuwapa pongezi wajumbe wa mkutano wa kutoa mapendekezo kwa Jimbo la Kigamboni kwa kufanya kazi iliyotukuka ya "kulikata" jina la Paul Makonda!

Ni matumaini ya wananchi wote kuwa kwenye vikao vilivyosalia vya juu zaidi vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, vitatia "tiki" uamuzi wa wanakigamboni na kutolirejesha jina la Paul Makonda kuwa ndiye mpeperusha bendera za ubunge kwa tiketi ya CCM na kuunga mkono mapendekezo yaliyotolewa na wanaccm wa Kigamboni kuwa Faustine Ndugulile ndiye apeperushe bendera ya CCM kugombea ubunge huo baadaye mwaka huu kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika hapa nchini

Mungu ibariki Tanzania
 
Tuishi vizuri na watu...

Tuache majivuno....

Tusiwatese na kuwaonea wasio na uwezo...

Tutende haki.....

Dunia hii tunapita tu......
Yule Rais wa Iran Mohamed Abdinajad alimtanguliza Mungu katika utawala wake. Sasa hivi u Rais umekwisha amerudia kazi yake ya Ualimu Chuo Kikuu na ana panda treni kwenda kazini. Anasalimiama na watu kama kawaida.
 
Kura za maoni zisikupumbaze mimi naamini Makonda ndio mkuu wa mkoa bora kabisa kuwahi kutokea, ni kiongozi mwenye uthubutu na mwenye maono na anayependa kujaribu. Naamini kama Makonda akifanikiwa kuingia kwenye baraza la mawaziri na akapewa wizara ya kilimo ambayo imeajiri watu wengi basi kutakuwa na mapinduzi makubwa sana ya kilimo wakulima watanufaika sana

Nilichokigundua mimi ni kwamba kuna nguvu kubwa sana ya media hasa mitandao ya kijamii inatumika kuaminisha uma kuwa Makonda ni kiongozi mbaya, na hii ni kutokana na ujasiri wake uliochangia kuokoa vijana wengi wa Tanzania waliokuwa wakiteketea, sasa wanufaika wote wakahakikisha wanaelekeza nguvu zao kuhakikisha wanamchafua. Kiongozi mzuri hawezi pimwa kwa wingi wa kura pekee yawezekana wale wajumbe waliopiga kura za maoni wakawa sio wafuasi wake, lakini ikumbukwe wananchi hawapigi kura kwa kuangalia ufuasi, wao huangalia ni kipi kiongozi alichowafanyia au atachowafanyia, na kama hivi ndivyo ilivyo naamini Makonda anaweza shinda jimbo lolote lile ndani ya Tanzania kutokana na kazi kubwa aliyoifanya ya kuokoa kizazi chetu hasa vijana . Ni binadamu wachache sana wenye uthubutu hapa duniani na hawa huwa ni tunu.
 
Uzima ya waliofanyika kwa mfano wa Mungu unamlilia kwa uchungu.

Mateso na vyote waliyowafanyia naye laana ile i juu ya yule awaapuuzae waja wa mwenyezi Mungu.

Amani yao huchanua kama ua na kunyauka kama jani la nyika.

Waliomsulubu watasitawahi kama mti ukiyopandwa kwenye chemchem ya maji matamu na kuishi milele kama mlima Kilimanjaro.

Sauti hii ya wananchi ni sauti ya aliyewaumba.

Asubuhi njema!
 
Back
Top Bottom