Uchaguzi 2020 Magufuli kama angesimama na mtu mwingine kwenye kura za maoni asingeshinda kama ilivyokuwa kwa Makonda

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,692
36,054
Huu Uzi hauna kejeli, matusi wala dhihaka. Huu uzi umebeba ukweli mchungu (a bitter truth) ambao wengi hawaupendi.

Kama Magufuli angesimamishwa na MwanaCCM yeyote imara kuwania tiketi ya kupeperusha bendera ya CCM 2020 katika ngazi ya Urais asingeshinda.

Mioyoni mwa wanaCCM kuna siri na ajenda nzito sema tu hawana pa kusemea.

Hasira za wachache wa Kigamboni wamezipeleka kwa Makonda, ambaye ni mtu wa karibu na Magufuli kwa kipindi kirefu katika utawala wake wa miaka takribani 5 sasa.
 
Sandali Ali,

Ya Makonda ni ya Makonda na ya Magufuli ni ya Magufuli. Tutampima Magufuli kwenye uchaguzi wa rais ambao unashirikisha watanzania wote ili tuone kama kama anakubalika ama la.

Hivi ingewezekanaje kwa wanakigamboni wamtupe mtoto wao ndugulile wakamchukue Makonda ambae anaonekana kama mhamiaji tu. Hata kwa hizo kura tu alizopata bado ni nyingi sana, na amezipata kutokana na influence aliyonayo.
 
Ya makonda ni ya makonda na ya Magufuli ni ya Magufuli. Tutampima magufuli kwenye uchaguzi wa rais ambao unashirikisha watanzania wote ili tuone kama kama anakubalika ama la.

Hivi ingewezekanaje kwa wanakigamboni wamtupe mtoto wao ndugulile wakamchukue makonda ambae anaonekana kama mhamiaji tu. Hata kwa hizo kura tu alizopata bado ni nyingi sana, na amezipata kutokana na influence aliyonayo.
Uko sahihi, margin haikuwa kubwa sana kama mtu ambavyo angelitgemea. Haikuwa mbaya sana! Kwangu mimi bado Kigamboni kuna "takataka" za watu maana haikupashwa kupata kura hizo Makonda!
 
Uko sahihi, margin haikuwa kubwa sana kama mtu ambavyo angelitgemea. Haikuwa mbaya sana! Kwangu mimi bado Kigamboni kuna "takataka" za watu maana haikupashwa kupata kura hizo Makonda!
Na hizo kura alizopata siyo ajabu ndo zikampa back up kubwa ya kurudishwa kwa jina lake. Alipaswa kupata kura 1 au zero kabisa. Hapo ingekua ngumu kwa Kamati Kuu kurudisha jina lake, maana ingeonekana amekataliwa kabisa na wanakigamboni.
 
Ya makonda ni ya makonda na ya Magufuli ni ya Magufuli. Tutampima magufuli kwenye uchaguzi wa rais ambao unashirikisha watanzania wote ili tuone kama kama anakubalika ama la.

Hivi ingewezekanaje kwa wanakigamboni wamtupe mtoto wao ndugulile wakamchukue makonda ambae anaonekana kama mhamiaji tu. Hata kwa hizo kura tu alizopata bado ni nyingi sana, na amezipata kutokana na influence aliyonayo.
Tunaomba katika uchaguzi mkuu kura zihesabiwe kama katika mchakato wa kura za maoni kuwe na media kila Jimbo kura zihesabiwa live. Halafu tuone what will happen.

Hizo kura alizopata Bashite ni kwa kuhonga tu pengine labda na kuwatisha baadhi ya wajumbe. Ila kiukweli watekaji, wapiga watu risasi mchana kweupe, wakandamizaji wa demokrasia nk wamechokwaaaaaaaaaa.
 
Na hizo kura alizopata siyo ajabu ndo zikampa back up kubwa ya kurudishwa kwa jina lake. Alipaswa kupata kura 1 au zero kabisa. Hapo ingekua ngumu kwa Kamati Kuu kurudisha jina lake, maana ingeonekana amekataliwa kabisa na wanakigamboni.
Uko sahihi to some extent, ingawa maamuzi ya wanachi yaheshimiwe! Sioni taatizo la Ndungulile mpaka wambadilishe na Makonda
 
Sandali Ali,

Ninakubaliana na dhana yako.

Hilo mwenyewe aliliona kungali mapema, kwa hiyo kaweka tahadhari.

Ni nani angepinga utaratibu aliotaka yeye kama mwenyekiti ufanyike katika nafasi hiyo!

Na kumbuka, alianza mapema kabisa kuwatia jamba jamba wale wote aliojua wangeleta rabsha wakati huu na kumvuruga kabisa.

Akina Membe, aliyekataa kabisa kwa njia zote zilizotumika kumweka kwenye mstari hadi akafukuzwa ndani ya chama.

Akina Kinana, kagoma kabisa, hadi dakika za majeruhi kawekwa mbele za wazee asalimu amri - ikabidi abwage manyanga kwa shingo upande. Huyu Kinana, angegoma, na akaamua kupinga, hali ingemuwia ngumu sana Magufuli. Hata hivyo sijui huko aliko kinyongo cha kuonewa kitakuwa kimekwisha kabisa.

Akina Makamba wote wawili na Nape, wakalazimishwa kuomba msamaha. Hawa wote wangechachamaa, na kukataa kuonewa walikofanyiwa, Magufuli angepata wakati mgumu sana.

Kwa hiyo, haya yote alikwishayaona, na hatari zote zilizokuwa zimkabili kaziwahi kuzilainisha, akina Makamba na wenzake, au kuziondoa njiani kabisa, kama yaliyomtokea Membe.

Je, huko ndani ya CCM pamesafishika na hakuna litakalotokea kuelekea Oktoba?

Wengi sasa hivi ndani ya chama wanaingia kwenye mstari, kujipanga tayari kwa ulaji katika ngwe inayofuata. Itakuwa vigumu sana sasa kutokee hali ngumu kwake, kwa sababu wengi wanajua ni lazima wajionyeshe kwake kwa utii wasije wakakosa ulaji.

Kwa hiyo ndani ya CCM hakuna uthubutu tena, mpaka itokee kwamba Upinzani uonyeshe nguvu kubwa yenye kutishia kumng'oa. Hapo ndipo utakapoona mizuka iliyoko CCM ikipandia hapo na kumwondoshea mbali.

Bila ya upinzani kuonyesha dalili za nguvu kubwa kuelekea kwenye uchaguzi, tuhesabu tu sasa kwamba Magufuli tunaye kwa muda mrefu sana.
 
Kama atawaachia wapinzani wafanye kampeni kwa Uhuru bila bughudha, Upinzani ukaweka mgombea mmoja, kura zinahesabiwa wazi wazi kama jana.

Basi CCM atashinda kwa 50.9%
Ya makonda ni ya makonda na ya Magufuli ni ya Magufuli. Tutampima magufuli kwenye uchaguzi wa rais ambao unashirikisha watanzania wote ili tuone kama kama anakubalika ama la.

Hivi ingewezekanaje kwa wanakigamboni wamtupe mtoto wao ndugulile wakamchukue makonda ambae anaonekana kama mhamiaji tu. Hata kwa hizo kura tu alizopata bado ni nyingi sana, na amezipata kutokana na influence aliyonayo.
 
Tunaomba katika uchaguzi mkuu kura zihesabiwe kama katika mchakato wa kura za maoni kuwe na media kila Jimbo kura zihesabiwa live. Halafu tuone what will happen. Hizo kura alizopata Bashite ni kwa kuhonga tu pengine labda na kuwatisha baadhi ya wajumbe. Ila kiukweli watekaji, wapiga watu risasi mchana kweupe, wakandamizaji wa demokrasia nk wamechokwaaa.
Zile kura alizopata siamini kuwa ni za watu waliompigia kwa moyo kunjufu kabisa kuakisi uwezo wake wa uongozi.
 
Unajaribu kuwa influence watanzania nn juu ya bandiko lako. Wenye akili zao wanakuelewa unachojaribu ku hadaa.

Maisha mliyokuwa mnaishi mwanzo kabla ya Maguful ndiyo mmeyamiss, maisha ya wizi serikalin, maisha ya kufanya anasa kwa kuwa pa kuchotea kupo wazi.

Msiteseke namna hyo, fanyen kaz mpate fedha za kula maisha kihalali, mtateseka mpka lini?
 
Maisha yale ya mzunguko wa pesa mtaani na Maisha ya Kununua ndege ambazo zinapaki tu Airport bora nini?

Back
Top Bottom