Zitto: Ndio ninautaka urais

Zitto: Ndio ninautaka urais

Status
Not open for further replies.
Ndugu zangu. Naomba msome makala nzima kabla ya kuchangia. Msichangie kwa kusoma kichwa cha habari tu. Hii ni makala nimeandika kama majibu kwa makala ya mwanazuoni mmoja kuhusu umri wa Urais.

Nimesema wazi, kuutaka Urais na kuupata ni mambo mawili tofauti. Kwanza lazima chama changu kiniteue. Kama chama kikiona bado lazima nikubaliane na chama. Kama chama kikiona kuna mwanachama mwingine ana uwezo zaidi yangu lazima nimwunge mkono huyo. Hata kama chama kikiniteua lakini wananchi lazima wakubali. Kwa hiyo unaweza kuutaka Urais lakini usiupate!

Pili nimejibu hoja za ubaguzi, hatari na matabaka za mwanazuoni huyo. Ni vizuri MoD akachukua makala hiyo na kuiweka juu kabisa ili watu wachangie jambo walilolisoma.

Miye nitaweka makala hiyo kwenye blog yangu zittokabwe.com

Mkuu Zito, kwa jinsi unavyooneka unautaka urais, na nikikumbuka Maneno ya Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere
"Ikulu pana Biashara gani hadi Mtu atake kupakimbilia"

akaongeza zaidi
"Mkimuona mtu anautaka sana uraisi Huyo hatufai"

My Take:
Kimsingi Kwa hili Kaka umechemsha ama kwa kujua au kutojua unajikuta unaleta "Bad atmosphere" chamani, kauli zako zimekaa kibaguzi baguzi, ingetosha kama ungetetea issue ya Umri wa Kugombea urais, hilo watu mbona tuko pamaoja nawe sana tu, ila unapokuja tena kusema unautaka urais,hii inapoteza hata msingi wa point yako kwa kufanya watu kuelewa kuwa unajipigia debe, na uki recall maneno ya Julius hapo Juu, ndo kabisaaaa, i think its better some times kabla hujafunguka ukajaribu ku consult wazee (Sio wa Magamba kama unavyofanyaga).
Biliv me, reputation yako mbele ya Vijana inashuka kwa kasi ya ajabu, wengine wanadiriki kusema kuwa eti wewe ni Mgonjwa so unataka chance ya urais ili upate muda mzuri wa kutumia rasilimali za taifa kujitibu... take this.
 
Mimi naamini kila mtu anao uhuru wa kusema anautaka uraisi, hii ndio freedom yenyewe. Lakini timing ya kauli kama hizi ndio inayoleta maswali ya kujiuliza pengine wengi wetu tunaishia kukosa majibu. Hiki kijitabia cha mtu kuona watu wanamuandika andika kwenye magazeti kila siku akafikiri kila kitu anaweza ni hatari sana. Mh. Zito anakurupuka mambo mengi sana, siasa makini haziendi namna hiyo, mtu anajengwa kwenye chama na kuna wakati unafika unakuwa automatic choice, sio lazima ujitangaze bila taratibu.

Wakati ule anataka kugombea uenyekiti, ijapokuwa ni haki lakini mtu unajiuliza hivi kweli kwa umri wake wakati ule tuseme 33 hata ukiupata huo uenyekiti je unaweza kuvutia watu wa rika zote kujiunga na chama? je umekomaa kiasi cha kutosha kuweza kuhimili hiyo nafasi? Hekima nyingine jamani zinakuja na umri, kwa nchi zetu za kiafrika na tamaduni zake Mh Zito bado hawezi kukabidhiwa chama akiongoze, ni mtu anayetakiwa kulelewa na kukuzwa na chama kwa ajili ya miaka ijayo.

Hata nafasi anayosema anaitaka ya uraisi bado mda wake, he is not matured enough. Amelewa sifa na anatumiwa vibaya. Chadema lazima msimame makini na mtu wa namna hii, akileta za kuletwa mnafanya maamuzi magumu maana he always create unnecesary distractions. Chama ni taasisi lazima kiheshimiwe kama taasisi, chama kinapogeuka kuwa ni majina ya watu huwa hakina muda kinakufa. Kunao watu wengi tu, wazuri wenye mvuto mkubwa wa kiuongozi ijapokuwa huwezi kuwasikia kwenye magazeti kila kukicha, wapewe nafasi.

Chaguzi ndani ya vyama ziwe mahali ambapo talents zinavumbuliwa, mtu anasikilizwa hoja zake,vision zake na strategies zake na kama ziko convincing mtu apate nafasi, sio hii tabia ya kushabikia majina yasiyo na chochote ndani yake. Ndio maana vyama vya siasa huwa vinakufa maana vimejengwa juu ya majina ya watu. Ati watu wanakuwa na makundi, upuuzi mkubwa kabisa huu badala ya kuangalia ni nani anatoa sera za maana yunashadadia majina, mara Zitto, mara Slaa mara Mbowe n.k Haiwezekani mtu ambaye ni mwanachama wa kawaida tu wala hana kashfa wala nini akapewa nafasi mbele ya kamati akajieleza akapita kwa ubora wa hoja zake! lini tutafika hapo?

Much respect mkuu, michango kama hii ndio tunayoitarajia toka kwa great thinkers.
 
Leo founder wa chama amekuwa pandikizi la CCM? Pandikizi wa ccm ni slaa anayekipeleka chama kuwa cha kimaeneo na watu wa mrengo fulani.ZItto,Mbowe hawa wapo neutral na wanaweza kupeperusha bendera ya CDM sio SLAa mropokaji. Ikulu inahitaji mtualiye balanced

Mkuu hembu fafanua-aliyebalanced kivipi?? Maana umeandika maneno tu yasiyo na mashiko halafu unamkandia mtu,unapomuita mtu ***** basi taja na kitendo cha ubwege wake,unapomuita mtu mteja basi taja na uteja wake,mathalani uteja wa simba na yanga au uteja wa madawa ya kulevya,na hata pia mteja wa bidhaa za dukani. Hoja zenu za nusu matusi kwa mnaowapinga ndio hupelekea na wengine kujibu kwa povu kama sio na matusi juu,tuwe kama kweli ma-great thinker na sikama ma-great stinker (wa kinywa)!!
 
Nimekuwa nafuatilia mjadala wa Zitto upande mwingine alipokuwa akisoma bandiko la mwandishi kutwa nzima ya jana. Kumbe huku JF mambo ndio yameiva. Zitto, Zitto Zitto mkuu wangu bado una safari ndefu sana ya kujifunza siasa...

Pamoja na kwamba Zitto hakusema lolote baya tena nilitegemea sana vijana wengi wangemkubali kutokana na dhana aloiweka kupambana na utawala huu wa kifisadi ambao unaongozwa na sura zile zile, viongozi wale wale (wazee) kuudanganya Umma wakitumia jina la chama CCM kwamba wao ndio wenye mamlaka ya kuitawala nchi yetu..

Nilitegemea vijana wangevuka kingo na viunzi vya kichwa cha habari na kumshangilia kijana mwenzao anayetaka kugombea Urais ili kuwakilisha harakati na mtazamo wao dhidi ya viongozi wakongwe waliotufikisha hapa tulipo, kumbe ndani ya vijana wenyewe wanatofautiana sana kimawazo na inaonyesha hawapendi nguvu kubwa ilosisitizwa maana nimesoma kusara nyingi za huu mjadala karibu zote zinapingana na mawazo ya Zitto. Na hawa wote ni vijana wale wale wanaopiga vuvuzela hapa JF kupinga mwelekeo wa Tiafa letu.

Hivi tukitaka kutazama ukweli, ikiwa vijana kweli wanataka kuchukua jukumu la kufanya mageuzi nchini ni nani kwa mtazamo wao anafaa kugombea Urais?. Vijana twmbieni hizi mbio zenu za mageuzi mnataka nani asimame Urais!..Mimi nilidhani Zitto katanguliza mbele nia na dhamira yake kwa kuwawakilisha vijana kumbe hata vijana wenyewe hawamkubali, sasa kijana gani anakubalika? hizi harakati za mageuzi ikiwa hamna mtu ama kiongozi mnayefikiria anaweza kusimama ktk uchaguzi wa mwaka 2015 kuwakilisha harakati zenu, Je ni lini mtaziweka ktk vitendo maana mmwaka huu vijana mmesema sana kuhusu mageuzi..

Vijana, ndio maana nilisema UMRI una matter hata kama hamkubali mantiki ya maneno haya..Kwetu sisi watu wazima (sii wazee) tunaelewa wazi kwamba kijana hawezi kudai elimu ya chuo kikuu akiwa na Umri wa miaka 15, umri una matter kutokana na hatua za makuzi ya mwili, bongo na kuchukua elimu ktk kuelimika na hata kama mtu huyo yupo basi ni exceptional case, vile vile mtoto kuanza darasa la kwanza umri pia una matter. Umri pia ni kikwazo kwa vijana wenye umri wa miaka 10 hadi 17 wana kuwa protected na sheria ya kutoolewa ilihali ndoa ni mapenzi ya mtu. Kijana anaweza kujiona tayari kufunga ndoa akiwa na miaka 14 baada ya barehe lokini haina maana kuwepo kwa sheria ya kupinga ndoa hiyo ni kumyima haki kijana huyo bali kumlinda..Na hakika ukiweza kumhoji kijana kama huyu utamwona akikurupuka na maneno ya kusadikika..simply because he has never been there before!.

Bandiko la Zitto linabeba uzito mkubwa sana na kielelezo kikubwa cha UMRI...Haikuwa Hekima kwa Zitto kujibizana na mwandishi wa makala ile. Haikuwa busara kwa Zitto kuandika NAUTAKA URAIS japokuwa anayo kila haki ya kusema hivyo maana ndio ukweli lakini kisiasa maneno kama hayo yanakula kwako. Haikuwa hekima wala busara kwa Zitto kukubali picha ilochorwa kutafsiri mahusiano yake yeye (CDM) na Makamba (CCM) ktk utetezi wa vijana ambao hakuwa na ridhaa yao kama mwakilishi bali ni mtazamo wake...Hivyo ni Ujana wa Zitto umedhihirisha mapungufu haya na mjadala upo wazi.

Mkuu wangu Zitto, I have said many times wewe sii mwanasiasa na nimekuomba mara kibao ujifunze SIASA.. Mara nyingi sana inashindwa kutambua ni wakati gani mwanasiasa anakuwa independent na wakati gani hatakiwi kuwa independent.. Mara nyingi sana umefanya mambo kinyume japokuwa una nia nzuri na hii imetokana na elimu ama kutumia Logic. Siasa hazitaki LOGIC bali IMANI kwanza ndio hujenga logic.

Maelezo uloandika yalibeba uzito mkubwa sana kiasi kwamba ilitakiwa kuwa umepikwa ukaandaliwa na sasa ulikuwa tayari kugombea, hili sio swala la jinsi unavyofikiria wewe bali urais ni sawa na kichwa cha treni na kazi yake ni kuvuta mabehewa nyuma, ni lazima ufikirie uzito wa kazi hiyo na sii safari yako wewe binafsi..Nakuomba sana tazama sinema ya Good Deeds watazame ndugu wawili walivyokuwa wakilumbana kwa jambo dogo sana na hakika mkuu wangu utaweza kujisoma vizuri japokuwa inawezekana wewe ndiye mwenye mawazo mbadala...

Mwisho vijana wetu mkitaka kugombea Urais basi tangulizeni hata kuonyesha Vision yenu andikeni hata kitabu tuwasome tujue tofauti zenu kimawazo na kimsimamo maana hii kupiga vita Ufisadi bila kutuonyesha zana ama silaha mlizo nazo ni hadithi za kufikirika. Mtu hujawahi kuongoza hata ofisi ya kazi au kuonyesha chochote basi ukubaliwe tu kugombea urais kwa sababu ya umri wakati hatujaona uwezo wanu?.. Hata mashindano ya world cup walishusha umri baada ya vijana kuonyesha uwezo wao wakiwa na umri mdogo lakini sii washushe tu kwa sababu vijana wanataka kuingia world cup ya wakubwa..Show us you can..bila shaka utachaguliwa ama tutashusha umri - Hizi nyingine ni wishful thinking ambazo haziwezi kuhalalisha madai yenu japokuwa kweli tunawategemea sana vijaa ktk mageuzi na sio kuendeleza yale yale yaliyotufikisha hapa tulipo kupitia sanduku la kura.
 
USHAURI WA BURE KWA BWANA ZITTO

Kwa sasa itakuwa ni mapema mno bwana Zitto kugombea uraisi. Kitu nilichokifurahia kwako ni kwamba you are thinking on bigger things. Nina uhakika kama utaendelea hivi na ukavumilia kidogo, utaongoza nchi hii tena kwa ridhaa ya wananchi walio wengi na si kama kwa viongozi wetu wa sasa.

Mbona watu mnasahau kuwa Mwl Nyerere alianza kuongoza nchi hii akiwa na umri wa miaka 39 na kulikuwa wazee wengi tu.....

Mbona watu mnasahau kuwa Mwl Nyerere alianza kuongoza nchi hii akiwa na umri wa miaka 39 na kulikuwa wazee wengi tu.....

Kwa sababu waliotuletea Uhuru wetu karibu wote walikuwa Vijana, vijana waliotoka vitani Burma na kuja na wazo la kuikomboa nchi yetu hivyo Nyerere alichaguliwa na vijana wenzake kuongoza mageuzi na wala umri haukuwa kigezo kabisa. Nyie vijana hamna hata lengo moja, hamna ushirika, hamna vision wala silaha tosha ya kupambana na uongozi wazee ambao mnawatumikia..Mtaweza vipi kutafuta uongozi ktk mageuzi kupitia Umri ktk sanduku lile lile la wazee hii inaonekana ni kutekeleza ambition zaidi ya changes..

Zitto hajakosea kabisa isipokuwa pale tu msomaji anapomsoma kwamba hawakilishi mawazo wala mtazamo wa kundi la vijana. Ndio maana anajikuta katengwa lakini kama mngemwandaa na kufikia maamuzi ya kumsimamisha 2015, makala kama hii ingewashutua wengi sana na hakika mageuzi yangeanza kupamba moto!..
 
Thibitisha ni wapi nilipokisaliti chama changu.Kwa hayo majungu yenu hamtaniweza hata kidogo na mnalielewa hilo ila ni kiwewe tu kinawasumbua.nikiwa nagombea uenyekiti BAVICHA mlileta majungu kwa njia zote hadi dakika za mwisho ikashindikana.
You must come clean usaliti mnaoufanya hautawaacha mmesimama
Walioenguliwa katika uchaguzi huo ni Greyson Nyakarungu, Mwampamba na Bernard Saanane

"Ndugu yangu napenda kusema kuwa chama hiki sasa kinaenda pabaya walitafuta kila njia ya kuwamaliza vijana na njia waliyoipata ni kuwatutafutia tuhuma zitakazowafanya waondoke katika kuwania nafasi hiyo...lakini tulipigana na ikashindikana," alisema mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo.(???????) who is this?????

"Tuhuma nyingine iliyoelezwa ni wagombea hao kutaka kupindua chama hicho kwa kuhamisha agenda za chama hicho na wengine walihofiwa kuwa ni usalama wa taifa," kilisema chanzo chetu.

Akizungumza na majira jana akiwa katika uchovu, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Wilbroad Slaa, pamoja na kutotaka kuzungumzia tuhuma hizo za rushwa kwa undani akisema "mengine yanahitaji maamuzi ya juu", alisema kuwa wagombea hao watatu walioenguliwa baada ya kuthibitisha kuwa wamekwenda kinyume na katiba na kanuni za chama, kifungu cha 10, wamekiri pia kuwa wao walijihusisha kutengeneza agenda ya BAVICHA.

"Sasa hilo ni suala kubwa agenda ya BAVICHA ni suala la mkutano na haliwezi kuwa la wao watatu lakini walibainika kujihusisha na kundi la Bw. Habib Machange ambapo ilibidi chama kiingie gharama ikiwemo wajumbe wa kamati hizo kufanya kazi tangu saa saba usiku wa juzi mpaka asubuhi jana na baadhi ya wajumbe walishindwa kurejea kwao," alisema Dkt. Slaa.
 
Mwanzoni nilifikiri Zitto alikuwa ameandikia article kwa unknown news media. Lakini gazeti la Mwananchi Jumapili limeandika hii habari kwa kina na according to this paper ni kwamba Zitto alifanya nao mahojiano! Infact kule Mwananchi Sunday Zitto more explicity kuwa 2015 anautaka urais!

Shida niliyonayo hapa ni timinig. Kwanini Zitto ameamua kuwa kwa sasa mjadala unaofaa ni kuhusu mikakati yake ya kupata urais wakati anajua kuna uchaguzi huko Arumeru? Amebadilisha public dabate kabisa kwanini?

FJM,
Naona mnapotosha maana ya "Zitto kuutaka urais" kwa kujua au kwa kutojua. Zitto mwenyewe kaweka wazi kuwa maelezo yake yalilenga kumjibu mwandishi aliyeandika makala ya kupotosha dhidi yake. Na kwa mtu mweledi na makini kama Zitto asingeweza kukaa kimya bila kuweka kumbukumbu sawa juu ya jambo ambalo linapotoshwa kwa makusudi. Unadhani angefanya hivyo? Kamwe Zitto sio mtu wa hivyo! Na hakuna mwenye haki ya kumchagulia juu ya mambo ya kujibu au kutojibu.! Wanaoona kuwa hakutakiwa kuijibu ni wale wenye uoga,ambao wanaona kutangaza nia mapema watakuwa "screened" na umma na maovu yao kujulikana. Zitto anajiamini na ndio maana amelitolea ufafanuzi hili!

Timing:Mnaposema timing mnamaanisha nini, kuwa ili aupate urais ilibidi apige kampeni za chinichini ndani na nje ya chama? Halafu baadae aje kujitokeza ghafla kuwa sasa nautaka urais,ili iweje? Unajua athari za kumtangaza mgombea wa nafasi kubwa kama ya urais mbele ya watu kwa kushtukiza,na malengo yake huwa ni nini? Tena wanasiasa wa namna hii ni wanafiki wakubwa na huwa hawana lolote zidi ya ulafi tu wa madaraka. Leo Zitto kajitokeza kusema hili wazi,watu watasema negatives about Zitto,na pengine mambo ambayo watu walikuwa hawayajui kuhusu Zitto tutayajua,good or bad! Laiti angekuwa anaogopa kuwa "screened" kwa wananchi na makundi yote ya jamii,do you think Zitto angethubutu kutangaza hivi? Au Zitto halijui hilo? I am sure anajua!
Kama kundi fulani limejipambanua kuwa wanamabadiliko,iweje tena watu haohao wanakuwa waoga wa mabadiliko? Kwa nini mnataka masikio yetu yasisikie wimbo tofauti na Slaa! Au mnataka kuturudisha miaka 50 nyuma za zidumu fikra za Mwenyekiti!! Kwa mtanzania anayetaka mabadiliko ya kweli na yenye tija,hawezi kukubali hilo. Hebu tuwekeeni nyimbo zote tusikilize..
Halafu kuna kitu kimoja kinanipa taabu,mtu anaposema kuwa "tulimlazimisha,au tulimuomba" kugombea nafasi fulani,unadhani huyo ni kiongozi anayetufaa.? Kwa nini yeye mwenyewe asiwe na msukumo na utashi wa kugombea badala ya kulazimishwa? Na hili jambo lipo Tanzania tu,labda na baadhi ya nchi za kiafrika,nchi zilizoendelea hakuna hata kidogo.. Sasa hivi Marekani wagombea urais wako bussy utadhani uchaguzi ni mwezi ujao,na kila mwenye azma ya kugombea kwa chama chochote anajulikana! Wake up Tanzanians!
Arumeru: Binafsi sioni sababu ya kutaka watu zaidi ya milion 40 ku-pay attention kwenye uchaguzi wa jimbo 1 kati ya majimbo zaidi ya 300,unless watanzania wana matatizo ya kiakili. Mnataka issues zote na challenge zinazotukabili ziwekwe pending kwa sababu kuna uchaguzi wa ubunge Arumeru? Hivi tutaamka lini? Uchaguzi mdogo wa ubunge Arumeru sio public debate,sio hata kidogo!
 
.......mmmh, sina hakika kama zitto yule aliyeombwa kukijenga chama enzi zile, ndio huyu tuliyenaye sasa, huyu ni wa kichina china! (mtazamo wangu)
Mbali na ishu (utata) wa timing ya tamko lake, lakini katika nyingi ya hizo sababu Zitto alizotoa kuwa ndio msingi wa hoja yake ya kutaka urais yapo mapungufu makubwa sana, ambayo kwa urahisi tu yanaonesha huyu jamaa ni mbinafsi, mdanganyika, hatari na hajakomaa kisiasa wachilia mbali kufikiria taasisi nyeti kama urais.Au ndio level tulofikia WaTz kwa vile Kikwete kaidhalilisha taasisi hiyo basi kila mtu anaona anaweza kuwa rais?Zitto is selfish, divisive, hypocrite and elusive in all matters he's propagate to stand for. Unfit for any good cause...me think.
 
Leo founder wa chama amekuwa pandikizi la CCM? Pandikizi wa ccm ni slaa anayekipeleka chama kuwa cha kimaeneo na watu wa mrengo fulani.ZItto,Mbowe hawa wapo neutral na wanaweza kupeperusha bendera ya CDM sio SLAa mropokaji. Ikulu inahitaji mtualiye balanced
Wewe si mwana ccm/magamba?
 
FJM,
Naona mnapotosha maana ya "Zitto kuutaka urais" kwa kujua au kwa kutojua. Zitto mwenyewe kaweka wazi kuwa maelezo yake yalilenga kumjibu mwandishi aliyeandika makala ya kupotosha dhidi yake. Na kwa mtu mweledi na makini kama Zitto asingeweza kukaa kimya bila kuweka kumbukumbu sawa juu ya jambo ambalo linapotoshwa kwa makusudi. Unadhani angefanya hivyo? Kamwe Zitto sio mtu wa hivyo! Na hakuna mwenye haki ya kumchagulia juu ya mambo ya kujibu au kutojibu.! Wanaoona kuwa hakutakiwa kuijibu ni wale wenye uoga,ambao wanaona kutangaza nia mapema watakuwa "screened" na umma na maovu yao kujulikana. Zitto anajiamini na ndio maana amelitolea ufafanuzi hili!

Timing:Mnaposema timing mnamaanisha nini, kuwa ili aupate urais ilibidi apige kampeni za chinichini ndani na nje ya chama? Halafu baadae aje kujitokeza ghafla kuwa sasa nautaka urais,ili iweje? Unajua athari za kumtangaza mgombea wa nafasi kubwa kama ya urais mbele ya watu kwa kushtukiza,na malengo yake huwa ni nini? Tena wanasiasa wa namna hii ni wanafiki wakubwa na huwa hawana lolote zidi ya ulafi tu wa madaraka. Leo Zitto kajitokeza kusema hili wazi,watu watasema negatives about Zitto,na pengine mambo ambayo watu walikuwa hawayajui kuhusu Zitto tutayajua,good or bad! Laiti angekuwa anaogopa kuwa "screened" kwa wananchi na makundi yote ya jamii,do you think Zitto angethubutu kutangaza hivi? Au Zitto halijui hilo? I am sure anajua!
Kama kundi fulani limejipambanua kuwa wanamabadiliko,iweje tena watu haohao wanakuwa waoga wa mabadiliko? Kwa nini mnataka masikio yetu yasisikie wimbo tofauti na Slaa! Au mnataka kuturudisha miaka 50 nyuma za zidumu fikra za Mwenyekiti!! Kwa mtanzania anayetaka mabadiliko ya kweli na yenye tija,hawezi kukubali hilo. Hebu tuwekeeni nyimbo zote tusikilize..
Halafu kuna kitu kimoja kinanipa taabu,mtu anaposema kuwa "tulimlazimisha,au tulimuomba" kugombea nafasi fulani,unadhani huyo ni kiongozi anayetufaa.? Kwa nini yeye mwenyewe asiwe na msukumo na utashi wa kugombea badala ya kulazimishwa? Na hili jambo lipo Tanzania tu,labda na baadhi ya nchi za kiafrika,nchi zilizoendelea hakuna hata kidogo.. Sasa hivi Marekani wagombea urais wako bussy utadhani uchaguzi ni mwezi ujao,na kila mwenye azma ya kugombea kwa chama chochote anajulikana! Wake up Tanzanians!
Arumeru: Binafsi sioni sababu ya kutaka watu zaidi ya milion 40 ku-pay attention kwenye uchaguzi wa jimbo 1 kati ya majimbo zaidi ya 300,unless watanzania wana matatizo ya kiakili. Mnataka issues zote na challenge zinazotukabili ziwekwe pending kwa sababu kuna uchaguzi wa ubunge Arumeru? Hivi tutaamka lini? Uchaguzi mdogo wa ubunge Arumeru sio public debate,sio hata kidogo!
Hapo kwenye "timing", ina maana anataka urais wa Arumeru?
 
Mbali na ishu (utata) wa timing ya tamko lake, lakini katika nyingi ya hizo sababu Zitto alizotoa kuwa ndio msingi wa hoja yake ya kutaka urais yapo mapungufu makubwa sana, ambayo kwa urahisi tu yanaonesha huyu jamaa ni mbinafsi, mdanganyika, hatari na hajakomaa kisiasa wachilia mbali kufikiria taasisi nyeti kama urais.Au ndio level tulofikia WaTz kwa vile Kikwete kaidhalilisha taasisi hiyo basi kila mtu anaona anaweza kuwa rais?Zitto is selfish, divisive, hypocrite and elusive in all matters he's propagate to stand for. Unfit for any good cause...me think.
 
FJM,
Naona mnapotosha maana ya "Zitto kuutaka urais" kwa kujua au kwa kutojua. Zitto mwenyewe kaweka wazi kuwa maelezo yake yalilenga kumjibu mwandishi aliyeandika makala ya kupotosha dhidi yake. Na kwa mtu mweledi na makini kama Zitto asingeweza kukaa kimya bila kuweka kumbukumbu sawa juu ya jambo ambalo linapotoshwa kwa makusudi. Unadhani angefanya hivyo? Kamwe Zitto sio mtu wa hivyo! Na hakuna mwenye haki ya kumchagulia juu ya mambo ya kujibu au kutojibu.! Wanaoona kuwa hakutakiwa kuijibu ni wale wenye uoga,ambao wanaona kutangaza nia mapema watakuwa "screened" na umma na maovu yao kujulikana. Zitto anajiamini na ndio maana amelitolea ufafanuzi hili!

Timing:Mnaposema timing mnamaanisha nini, kuwa ili aupate urais ilibidi apige kampeni za chinichini ndani na nje ya chama? Halafu baadae aje kujitokeza ghafla kuwa sasa nautaka urais,ili iweje? Unajua athari za kumtangaza mgombea wa nafasi kubwa kama ya urais mbele ya watu kwa kushtukiza,na malengo yake huwa ni nini? Tena wanasiasa wa namna hii ni wanafiki wakubwa na huwa hawana lolote zidi ya ulafi tu wa madaraka. Leo Zitto kajitokeza kusema hili wazi,watu watasema negatives about Zitto,na pengine mambo ambayo watu walikuwa hawayajui kuhusu Zitto tutayajua,good or bad! Laiti angekuwa anaogopa kuwa "screened" kwa wananchi na makundi yote ya jamii,do you think Zitto angethubutu kutangaza hivi? Au Zitto halijui hilo? I am sure anajua!
Kama kundi fulani limejipambanua kuwa wanamabadiliko,iweje tena watu haohao wanakuwa waoga wa mabadiliko? Kwa nini mnataka masikio yetu yasisikie wimbo tofauti na Slaa! Au mnataka kuturudisha miaka 50 nyuma za zidumu fikra za Mwenyekiti!! Kwa mtanzania anayetaka mabadiliko ya kweli na yenye tija,hawezi kukubali hilo. Hebu tuwekeeni nyimbo zote tusikilize..
Halafu kuna kitu kimoja kinanipa taabu,mtu anaposema kuwa "tulimlazimisha,au tulimuomba" kugombea nafasi fulani,unadhani huyo ni kiongozi anayetufaa.? Kwa nini yeye mwenyewe asiwe na msukumo na utashi wa kugombea badala ya kulazimishwa? Na hili jambo lipo Tanzania tu,labda na baadhi ya nchi za kiafrika,nchi zilizoendelea hakuna hata kidogo.. Sasa hivi Marekani wagombea urais wako bussy utadhani uchaguzi ni mwezi ujao,na kila mwenye azma ya kugombea kwa chama chochote anajulikana! Wake up Tanzanians!
Arumeru: Binafsi sioni sababu ya kutaka watu zaidi ya milion 40 ku-pay attention kwenye uchaguzi wa jimbo 1 kati ya majimbo zaidi ya 300,unless watanzania wana matatizo ya kiakili. Mnataka issues zote na challenge zinazotukabili ziwekwe pending kwa sababu kuna uchaguzi wa ubunge Arumeru? Hivi tutaamka lini? Uchaguzi mdogo wa ubunge Arumeru sio public debate,sio hata kidogo!

Nimekupuuza pale uliposema uchaguzi wa Arumeru si kitu cha maana kwa CDM bali la maana ni kupigana vikumbo kugombea urais 2015.CDM is not cheap like this!
 
Nimeshindwa kuelewa inakuwaje baadhi ya watu wanashindwa kusoma makala na kisha ndiyo wachangie?Inakuwaje waje wengine waibuke na kutaka au kuonyesha dalili za kuzima mjadala kwa visingizio kibao kuhusu chaguzi ndogo zinazoendelea? binafsi mimi nina-discourage majungu na fitina katika kipindi hiki cha chaguzi ndogo ila nashindwa kuelewa tumefikiaje hatua ya kumzuia mtu asiweke sawa upotoshaji uliofanywa na mtu kwenye makala.

Kama Zitto angekaa kimya na mjadala ukaendelea kwa jinsi ambavyo watu walikuwa wameanza kuupotosha kwa vyovyote vile ungekuwa na madhara.Watu wangesubiri hadi tarehe 2 Aprili huku wengine wakiendelea kuamini ndivyo sivyo.je ndiyo tulikuwa tunataka iwe hivyo?kwa maslahi ya nani?Halafu sijui tunapata wapi moral authority ya kuchagulia watu kitu cha kusema?Wengine wamedhani linalojadiliwa ni umri tu wa Urais,makala iliyoandikwa iko wazi.

Kuna Mwingine ameibuka na kuanza kushambulia kuhusu siasa za Alliance.Mwingine alitunga jina "BENZITTO" alliance kwa sababu anazozijua yeye mwenyewe.Labda pengine kwa kuonyesha msimamo wangu,kama Zitto atagombea nafasi hiyo ndani ya chama na chama kikamteu kwa kuzingatia muafaka ndani ya chama NITAMUUNGA MKONO.Hata makala hii NIMEIUNGA MKONO.Tatizo tumezoea kuwa na wanasiasa wanafiki na wanaofanya hila kwenye siasa.sijui ni nani alisema kuweka msiamo wako wazi ili watu wakujue na wakupime bila kuathiri utangamano ndani ya chama ni tatizo?

Nina uhakika makala hii iliyoandikwa na Zitto,kwenye jina lake angekuwa ameandikwa mwingine mjadala ungekuwa tofauti.pia niweke wazi sina Alliance yoyote ndani ya chama,na hata hivyo ninashangaa sana watu wanaoharamisha siasa za Alliance.Tangu lini siasa za Alliance zikawa haramu?Nilishawahi kusema tena,siasa za alliance haziepukiki.

Hata chama changu kilifanya alliance na NCCR-Mageuzi mwaka 1995.Mwaka 2000 Chadema hakikusimamisha mgombea urais kwa kuwa kilifanya alliance na CUF na mwaka 2005 chama kilisimamisha mgombea urais halikadhalika mwaka 2010.Kama kijana ninayeelewa vyema nadharia za siasa na kwa vitendo napata shida kuona baadhi ya watu wenye akili timamu wanataka kuharamisha siasa za Alliance.

Kenya mwaka 2002,siasa za Alliance ndizo zilizoiondoa brutal party (KANU) madarakani. Raila Amolo Odinga alimuunga mkono Mwai Emilio Kibaki wa chama cha DP.Pale Uhuru Park Raila alimu-endorse Kibaki kwa kusimamia "Kibaki Tosha".Muungano wa NAARC ulifanikiwa kukipoteza chama tawala cha KANU katika ramani ya siasa za Kenya.
Uchaguzi wa juzi hapo Congo DRC,Mgombea wa Upinzani nusura amuangushe the Incumbent Joseph Kabila baada ya kufanya alliance na wagombea wengine.Tshisekedi aliiungwa mkono hadi naJean pierre Bemba akiwa The Hague

Tusiharamishe vitu bila kufuat principle za siasa kwa kusukumwa na utashi binafsi na matamanio ya upotoshaji tu.Sasa wanaosema kuhusu kuunga mkono hoja ya kutanua wigo wa ugombea urais,wanaopinga hawaji na logic yoyote kisiasa,kisheria wala kiuchumi.Mwandishi na mwanafalsafa Nguli Jenerali Ulimwengu aliandika kuhusu hili kwenye makala yake nadhani ni the East African Standard wiki 2 zilizopita.Nilifurahi jinsi alivyojadili hili ndani ya mantiki na kujenga hoja nzito ya kiunafalsafa.Hakuna mtu aliyemuhusisha na alliance,pia mwandishi mahiri na msomi aliyebobea Comrade Ayoub Rioba ameandika makala kuhusu hili na akaitendea haki taaluma yake na kufafanua kwa weledi kuhusu hili jambo.Hakuna aliyemuhusisha na Alliance.Ninachoona hapa ni hofu zaidi kuliko logic.

Jamii forums(Where we dare to talk openly) ni jukwaa la hoja ndani ya mantiki na inajulikana hivyo.Pia,tusikubali kuyumbishwa na upotoshaji wa watu wachache kwa maslahi yao tu.

Vijana msikubali/tusikubali kutumika kama daraja kwa baadhi ya wanasiasa.kuna baadhi ya wanasiasa wana-take advantage ya matatizo ya vijana hasa ajira n.k. mmewasikia CCM wakigombea hoja ya ukosefu wa ajira upande mmoja ukitoa takwimu na upande mwingine ukitoa tuhuma.Aliyeituhumu serikali alikuwa waziri mkuu na alikuwa na uwezo wa kulisiammia hilo angalao angetoa data kwamba alilisimamia hapa hadi pale serikali ikashindwa.kumbe mwenzetu tunaweza kumhoji ilikuwaje akasimamia mradi wa shule za kati huku akijua sera hiyo inakuja kutuzalishia failures ambao leo hii ndiyo wako mtaaani na kulifikisha taifa katika alarming stage.(bomu linalokaribia kulipuka)Upande mwingine wa CCM hawakuonyesha jitihada zozote zaidi ya kutoa takwimu na kumshambulia kada wao aliyejiuzulu uwaziri mkuu bila kutoa suluhisho au kuainisha mkakati madhubuti wa kupamabana na tataizo hilo. Hii inaonyesha ni jinsi gani wanasiasa hawa walivyozoea kutumia mataizo ya vijana kujipatia political mileage

Tusikubali kucheka na wale waliochangia taifa hili kufikia hapa,tufanye kazi na tuungane na wale wanaotekeleza kwa vittendo yale wanayosema.Vijana tusikubali sasa kuamuliwa hatima yetu kwa kigezo tu cha umri ati mtu akishafikisha umri wa miaka 40 tayari ana hekima na busara.Katika mikataba yote ya ufisadi hakuna katibu mkuu yoyote wa wizara ambaye alikuwa below 40,wote walikuwa juu ya miaka 40. Hizi ndizo buasara tunazosimamia?

Zitto kuweka hadaharani msimamo wake hakuna tatizo lolote.Mbona wenzetu huko magharibi tunakoiga demokrasia wanaweka misimamo yao mapema?Seneta Barack Obama aliweka nia yake hadharani mwaka 2004,ndiyo 4 years before General Election.Iweje leo hili suala liwe tatizo?au huwa tunaangalia majina ya watu?hebu tujenge hoja ndani ya mantikiVijana tusikubali kuwa daraja,tusikubali kufanywa door mart.

Tatizo kubwa ninaloliona hapa ni kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi bila kuaandaa watu kifikra.Lazima tuapambane na hii status quo haramu.Vijana tujisimamie,tujenge taifa lenye kuzingatia merits na siyo hisani.Tusitumie kigezo cha dini,kabila wala rangi na tusitumie kigezo cha umri bali tuzingatie uwezo wa kufikia kule kwenye change,not only change but Radical change/reforms.

Sasa hili ndilo lengo la Youths patriotic movement(YPM) iliyozuiwa katika usajili kwa ghiliba za wanasiasa wachache wenye hofu na matamanio mfu tu.We are an assemblage of young Tanzanins whose primary aim is to change the course of governance, not from the sidelines this time, but from inside the system. We plan to build a membership of, at least, 20 million people -from every tribe and religion - who will participate in educating Tanzanins about the need to destroy the existing order that is fast running our country out of existence and instituting a new order that will birth equity, fairness, justice and development for all. We will be partisan becausepolitics is too serious a business to leave for the politicians alone.

We will participate fully in the politics of this country. Our army of 20 million people will organize themselves, pick intelligent, courageous, transparent and detribalized candidates for all positions in the 2015 elections and run their campaigns from ground up. There is no age limit, but leadership of the movement will be restricted to young people alone.We are tired of just becoming critics. Aluta Continua isn’t one of our favorite quotes. We won’t continue with the struggle. WE SIMPLY WILL END THE STRUGGLE by ending the grip of the corrupt in our polity. We owe our generation the duty of saving this country, building it to become a force to be respected in the world, and passing down to our children a nation they can be proud of.

Alliance ndani ya the same part, same slogan,the same vision, the same mwenyekiti,why all that for?Sijapata kusikia Alliance ndani ya chama kimoja,nimeshuhudia alliance kiaina ndani ya CCM ikabatizwa jina MTANDAO [NETWORK] madhara yake tiba yake mpaka leo ndio ugonjwa unaotka kuitia CCM matatizoni.
 
kiukweli 2015 akibadilishwa mgombea wa u raisi kwa tiket ya chama..ile kasi ya chama itapungua na kitaonekana kina watu wenye tamaa ya madaraka..zitto anatumiwa kukiua chama chetu..
 
Hata kama Zitto Kabwe anataka u-Rais na ni candidate mzuri,sasa ni mapema mno kwa CHADEMA kuamua. Mwaka 2015 ni mbali.

Vijana na watu wazima pamoja na wazee wapo, na wanaweza kuingia wanachama wapya. Hata wengine wako nje ya nchi wanaostahili kufikiriwa na chama makini kama Chadema.
 
1.Mh. Zitto unadhani ni kwanini hawa wapinzani wetu wanashabikia sana wewe kugombea uraisi 2015?
2.Mh. Zitto unadhani kwanini hawa wapinzani wetu wanaonekana kuwa na imani zaidi na wewe kuliko mwanachadema mwengine yeyote?
3.Mh. Zitto unadhani wanafahamu udhaifu wako hivyo wanaamini kwamba itakuwa ni kazi rahisi kwao kukushinda?
4.Mh. Zitto unadhani hawa wapinzani wetu wamewachoka ama hawana imani na wagombea wa vyama vyao na kwahiyo wanaamini kwamba unaweza kufanya mambo makubwa yenye manufaa kwa taifa hili hadi wanaamua kukupigia debe bila kujali kwamba uko chama tofauti na wao?
5.Mh. Zitto kwakuwa hakuna chama kinachopenda kushindwa uchaguzi na kwahiyo hakuna chama chochote makini kinaweza kukishauri chama pinzani chake kisimamishe mgombea ambaye ni tishio kwake, unadhani ni kwanini unapata uungwaji mkono mkubwa sana toka kwa wapinzani wetu?

Mh. naibu katibu mkuu wangu naomba unitoe wasiwasi huo, kwani pamoja na imani kubwa niliyonayo dhidi yako lakini naona ni muhimu ukasafisha huu ukungu ninaoanza kuuona hapa. Natanguliza shukrani kamanda.
Mwita Maranya umeuliza maswali ya msingi kabisa sijui kama Mh. Zitto ameshayajibu hasa kwenye red.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom