kuna Kaushauri labda naweza kukutupilia kidogo..
kwanza ujue mimi nafurahi na kuunga mkono matamshi, michango na vuguvugu la wabunge wetu hasa Vijana wa vyama vyote vinavyoliunda Bunge, Kumbuka Mhe Sita aliwahi kusema vijana wabunge hukesha kwenye maktaba za Bunge wakikokotoa taarifa na kujenga semi zenye hoja na mashiko wanapowakilisha maada au wanapouliza maswali.. na Hutoa Changamoto chanya kwa serikali. Na Kumbuka Mhe Zitto ulijichotea umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi yako. kuna kitu kina nituma niwaze kwamba kipindi kile ulikuwa wewe kama wewe Zito ukitegemea hazina ya mawazo na utashi wako. Lakini Zito wa Leo umebadilika sana, sizuiliki kuwaza pia kwamba umezungukwa na mamluki wapambe ambao inawezekana kula yao inategemea na uhai wako, na wapambe hao mara zote ni ndio mzee, na ushauri wao daima umekuwa ukikuzuzua, ukikulimbuka. sidhani kama una muda wa kusoma na kuelewa utitiri wa vyombo vya habari ambavyo kila kukicha kwa namna moja au nyingine wamekuwa wakikuandika, kwa maana hiyo mara zote lazima utegemee taarifa za marafiki na "feedback" zako. Nadhani hupewi taarifa sahihi kutoka kwa wapambe hawa. mara baada ya uchaguzi ulikumbwa na wingu baya la kuchukiwa sana na wale waliokupenda, na unakumbuka mama mmoja alipiga magoti ndani ya Ndege alipowaona mabosi wa chama chako akiwalilia wakung'oe kwenye chama haraka ila nadhani mabosi wale walimjibu vizuri kwa hakma ingawa hawakutarajiwa kupatwa na ugeni ule ndani ya chombo cha usafiri.
Najua wewe ni mwoga sana inapotokea kitu physical atack, ndio maana mara zote kwenye mikiki ya chama hutokei anyway hakuna mwenye nafasi ya kukuhukumu kwa hilo kwa sababu sisi binaadam wote tuna degree tofauti za woga. lakini una uwezo wa kushawishi ambao ni kitu kizuri kwenye medani ya siasa. SASA niseme kwa uwazi tu kwamba UMEKOSA WASHAURI WAZURI. na ukiendelea na tabia hii utajikuta unatokomea gizani kwenye pori la wasiojulikana tena kwa aibu.
Hoja yako uliyolimwa na mwana zuoni ambaye unajua ni si wa chama chako, unatutumuka this way kumjibu sidhani kam ni dhana yenye mantiki.. mwanasiasa gani aliyekomaa yuko hivi. ina maana kila post ikiandikwa kuhusu wewe lazima uijibu?, zito kanya karimjee..."utajibu", zito kaiba kuku .. "Utajibu" zito kampiga flan.. ujibu, utajibu mangapi.. si kujibu kunako leta maana but why now, why soon.. Yaani huna moyo wa kusikiliza neno na kulihifadhi.. Unashindwa hata na Lowassa, kasemwa mangapi na hawa "mboga za CHAMA" .. mwaka mzima ila jamaa yuko kimya na ilipotengwa CC ya chama chake akajimimina vilivyo, sasa wewe hata hujui wapi useme nini kiongozi gani Jukwaa hili na majukwa mengine yote ya mitandaoni ni majukwaaa huria. Yanatiwa mikono na raia wa aina mbalimbali, watoto kwa wakubwa.. seuze ni mwanafunzi tu wa chekechea aliyeleta hoja ile umejitutumua this way kumnanga kwa majibu. Wewe kiongozi wa wapi usiyejua kwamba kuna vikao halali ndani ya Chama ambavyo unaweza kuweka vuguvugu lako. Upwayukaji wa namna hii mapema kiasi hiki unanipa shaka sana. Si bure unaweza kuwa na kasoro. Wagonjwa wengi walioathirika na propaganda za kisiasa si rahisi wakakiri kwamba hapo kuna tatizo. Usikariri siaza za kizayuni na za nje wala historia. Jamii ya Tanzania ni tofauti sana na jamii za Nchi nyingine Duniani. Nakushauri Pata washauri makini, linda sana Kinywa chaweza ponza kichwa. .. Kama una maarifa utaelewa usipoelewa hayanihusu.. if you lost who cares.. na akina muddy mdogo (mtoi) watalost vilevile..