Mimi naamini kila mtu anao uhuru wa kusema anautaka uraisi, hii ndio freedom yenyewe. Lakini timing ya kauli kama hizi ndio inayoleta maswali ya kujiuliza pengine wengi wetu tunaishia kukosa majibu. Hiki kijitabia cha mtu kuona watu wanamuandika andika kwenye magazeti kila siku akafikiri kila kitu anaweza ni hatari sana. Mh. Zito anakurupuka mambo mengi sana, siasa makini haziendi namna hiyo, mtu anajengwa kwenye chama na kuna wakati unafika unakuwa automatic choice, sio lazima ujitangaze bila taratibu.
Wakati ule anataka kugombea uenyekiti, ijapokuwa ni haki lakini mtu unajiuliza hivi kweli kwa umri wake wakati ule tuseme 33 hata ukiupata huo uenyekiti je unaweza kuvutia watu wa rika zote kujiunga na chama? je umekomaa kiasi cha kutosha kuweza kuhimili hiyo nafasi? Hekima nyingine jamani zinakuja na umri, kwa nchi zetu za kiafrika na tamaduni zake Mh Zito bado hawezi kukabidhiwa chama akiongoze, ni mtu anayetakiwa kulelewa na kukuzwa na chama kwa ajili ya miaka ijayo.
Hata nafasi anayosema anaitaka ya uraisi bado mda wake, he is not matured enough. Amelewa sifa na anatumiwa vibaya. Chadema lazima msimame makini na mtu wa namna hii, akileta za kuletwa mnafanya maamuzi magumu maana he always create unnecesary distractions. Chama ni taasisi lazima kiheshimiwe kama taasisi, chama kinapogeuka kuwa ni majina ya watu huwa hakina muda kinakufa. Kunao watu wengi tu, wazuri wenye mvuto mkubwa wa kiuongozi ijapokuwa huwezi kuwasikia kwenye magazeti kila kukicha, wapewe nafasi.
Chaguzi ndani ya vyama ziwe mahali ambapo talents zinavumbuliwa, mtu anasikilizwa hoja zake,vision zake na strategies zake na kama ziko convincing mtu apate nafasi, sio hii tabia ya kushabikia majina yasiyo na chochote ndani yake. Ndio maana vyama vya siasa huwa vinakufa maana vimejengwa juu ya majina ya watu. Ati watu wanakuwa na makundi, upuuzi mkubwa kabisa huu badala ya kuangalia ni nani anatoa sera za maana yunashadadia majina, mara Zitto, mara Slaa mara Mbowe n.k Haiwezekani mtu ambaye ni mwanachama wa kawaida tu wala hana kashfa wala nini akapewa nafasi mbele ya kamati akajieleza akapita kwa ubora wa hoja zake! lini tutafika hapo?