Zitto: Ndio ninautaka urais

Status
Not open for further replies.
Hapa kwenye RED umemlenga MM mwanakijiji!!?? kama kutumia jina lako ndio sio uwoga basi una tatizo la ufikiri. hivi unadhani watu wapo hapa kuuza sura!!??......
Kwanini awe mwoga while yupo ule upande wa "wenye nchi" na hata hoja zake ni za kujipendekeza? Watamfahamuje bila kuweka jina lake halisi!
 
Ben,

Huo mtandao wenu na akina Zitto utapeleka nchi pabaya.Nilishawahi kutaadharisha hapa kama mbowe atawania uenyekiti wa chama au urais atarajie kudhalilishwa na hawa vijana.

Hii makala nimeona mahali Zitto anasema atachukua maamuzi yatakayochukiwa na mabwana wakubwa wa magahribi. Ninachojiuliza hivi ben na akina Zitto mmeunganishwa kwa mrengo wenu wa kushoto au kumpinga na kumdhalilisha mbowe? Sijawahi kujua Zitto nae ni leftist basi naona huko mbele chadema ina kazi kuliko CCM. Zitto naona nae ameanza kuwa na chuki na wazungu kama ulivyo ila nilishamshauri Mbowe awe makini na hili kundi naona limebadili uelekeo na linavuta vijana wasomi kwa kasi.

Ben saanane na wenzako ni wasalaiti wa chadema, kisirani chenu na Mbowe kitawafanya mtoane roho sasa
Thibitisha maneno yako kwamba nina kisirani na mbowe.Wengine sitawasemea.Acha majungu kama huna hoja ya maana ni bora tu unyamaze.

Thibitisha ni wapi nilipokisaliti chama changu.Kwa hayo majungu yenu hamtaniweza hata kidogo na mnalielewa hilo ila ni kiwewe tu kinawasumbua.nikiwa nagombea uenyekiti BAVICHA mlileta majungu kwa njia zote hadi dakika za mwisho ikashindikana.Nakushangaa leo unaongelea kwamba nimesaliti chama changu bila kujua theme iliyotumika jana kwenye fundraising ya Arumeru Mashariki ya M4C ilikuwa signature yangu hapa JF wakati nagombea uenyekiti bavicha na kwenye vipeperushi vyangu 'Movement for Radical change" ambayo wewe na wenzako mliita ni ya kidikteta na kuleta upotoshaji.Wakati mwingine muwe mnakwepa fedheha kama inawezekana....

Yes,msimamo wangu dhidi ya uovu,ukandamizaji dhidi ya taifa langu na watu wangu siwezi kuuvumilia na siwezi kuogopa kupambana nao.

Kilichotuunganisha na Zitto ni msimamo dhidi ya uonevu,ukandamizaji,dhuluma bila kujali ni nani anayeonea au ninani anayedhulumiwa.Kilichotuunganisha ni msimamo juu ya utekelezaji wa demokrasia ya kweli na kutoa maono ya kule tunakotaka taifa letu lielekee.

Kuhusu kuwa chadema huko mbele itakuwa na kazi kuliko CCM ni matamanio yako tu.CHADEMA itaendelea kusimama na utaona tutakavyoingia uchaguzi mkuu tukiwa na nguvu mpya.

Kwa kuzingatia muafaka na mchakato ndani ya chama changu,kama Zitto ataamua kugombea nitamuunga mkono kwa kuwa nakubaliana na msimamo na dira yake kuhusu kule tunakotakiwa kwenda as a nation.

Kama tafsiri ya kupigania interest za Tanzania kwa kuchukua maamuzi magumu ni chuki kwa wazungu basi nakubali.But you obvisoulsy havent got your own mindset right thats why you are so quick to condemn a man who has refused to be bullied, intimidated and bamboozled by selfish racist imperialist powers.

kitakachokata mzizi wa fitina ni Zitto kuchapa kazi kwa bidii na wale wenye mtizamo unaofanana ijulikane kuwa there is no excuse zaidi ya kuchapa kazi kwa bidii,determination and objectivity.

Wengine jengeni majungu tu,this is what you are good at !Besides, please don't let your anger cloud this debate because I don't want this to disintegrate into meaninless tat for tat.


Ninyi ni waroho wa madaraka pamoja na uwezo wenu mkubwa wa kujenga hoja ila mnautumia kuwahadaa watanzania...wasaliti wakubwa.mmedhamiria kumdhalilisha mbowe na kumpindua.Uchaguzi wa BAVICHA uliopita uliona kundi lako lilivyodhibitiwa kwa mara ya tatu


Yap nimesoma[BOFYA -UDADISI].
Hakika CDM ndio kumekucha kama michezo yenyewe ndio hii,vijana wana miaka 35 wanawaza Urais hakika, tumepotea sana tena sana ukizingatia chama ambacho tuliamini kingepigania dhamila ya ukombozi wa Mtanzania,bali vijana wadogo baada ya kujituma kuprove wanaweza kumbe kwenye masaburi yao wanawaza kuwa Marais 2015.Mama Tanzania tusaidie wendawazimu huu wa mawazo mfu kwa sasa ufe hata kabla ya kuanza.

Nakumbuka kuna watu walionwa vijana ndani ya CCM,wakapewa kwa vigezo hivyo vya ujana lakini leo,imekuwa wazi kumbe kundi lile liloonekana ni vijana,walio kuwa na akili ni wachache waliosalia ni makapi tu, tena wamepewa wakiwa na umri wa miaka 55 sembuse miaka 35 upuuzi wa kuzungumzika tena aibu sana

Nilisha hisi [sense] ujio wa jambo ili,ila CDM ndio wakikosa umakini na kudela na watu ovyo wenye akili ovyo wasio fikilia kwa logic na kuamua kwa kutumia Analytical way basi wakiachiwa waendelee ndani ya CDM,hakika KIFO cha CUF kitakuwa na heshima maradufu zaidi ya CDM.

Nilimshauri zitto kwenye makara moja nikamwambia muda wa yeye kuwaza urais sasa ni aibu kwake aachane nao awaze kujenga na kusimama miaka ishirini ijayo kwa maana kwa sasa ndani ya miaka 35 + miaka ishirini [20] ijayo basi miaka 55 ni best Material President ever kwa kuwa ameiva kwa lolote lile.

Kama kuna watu wazima wanamwambia kuwa anaweza kuwa President na wanamwambia watampa support hakika kuna agneda ya siri,moja kuua upinzani Nchini yani kifo ambacho mwalimu alikihita Natural death, ama kuna watu wanatengeneza conflict of interest ili maeneo yao yawe laini kwa vitu vyao upande mwingine kupita huku CDM ikiwa kwenye kutoana meno,au kuna mtu anataka green pasture upande fulani hivyo anatafuta gear ya kuchomoka kwenda upande wa PIli kutimiza ndoto yake.

Nimetoka kusoma thread ya CDM wanamaongezi na EL,nimekutna na hii,nimeunga DOT,kama kweli CDM hakitaki natural dealth baada ya uchaguzi wa arumelu ni vyema wajipange kutoa jawabu la uozo huu wa kuondoa watu ambao spirtually awako pamoja na CDM kwa faida ya TAIFA.Waswahili tunasema ni heri ya nusu shali kuliko shali kamili,sio kuwa watanzania hawaoni na hawezi kuunganisha DOT.

Tatizo la wanasiasa wetu sometimes uwa wanafikilia kuwa wao ni Intelligent and smart kuliko raia huku mitaani kumbe wanasiasa wengine ni remote controlled na raia huku huku mitaani.Sikutegemea speech hiyo ya UDADISI kutoka kwa Zitto,kwa kuwa moja ya vitu ambavyo Zitto alipaswa kuwa navyo ni kuepuka mijadala au forum zozote zinazoonyesha kuchokonoa juu ya ufahamu wake kuhusiana na swala la urais akiwa kama Mwanasiasa kijana.

Tena ukitaka kujua Zitto ni mtoto hata blog iliyotoa taarifa yake iko accurate na dhamira ile ile ya watu intellictual kujua ana dhamira gani je,ni kijana anaefikilia kuhusu kufikilia au ndio wale wasio na chochote bali siasa za popularity.Pole Zitto kama kweli hiyo udadisi ni maneno yako UMEMALIZWA KIJANA, they used you pia watakudump.

KAMA KWELI NIMANENO YAKO ULIKUWA KIJANA SANA KUSHNDWA SIASA ZA TANZANIA KATIKA UMRI MCHANGA WA CHINI YA MIAKA 35.

I doubt kama umesoma makala husika kwa umakini .Sijui umefikiaje hitimisho hili.Tujenge hoja tuache kujadili kitu kwa kuzunguka mantiki au nje ya mantiki(logic)

Baba mchungaji Mzito nakubaliana na wewe kabisa kuwa Zitto amekuwa affected na 'mahaba' ya urafiki sio na JK bali hata na vigogo wengine wa ccm. Na hili limefanya watu waanze kuhoji dhamira na hata loyalty yake iko upande gani.

Zitto nakuona uko online, kwa moyo safi kabisa na kwa nia njema nataka nikuleze kuwa you are young fine politician with great potential lakini unatakiwa sasa uamue na kila mtanzania including wana-CHADEMA wenzake wasihoji dhamira yako. Kwenye vita kila askari ananatakiwa aamue you are either with your fellow comrades or against them, lakini huwezi kuwa 'indifferent' - huwezi kuwa hapo katikati. Huwezi kuwa vuguvugu. Nitaeleza:

1. Wakati rais Kikwete anahutubia bunge kwa mara ya kwanza baada ya uchaguzi wa 2010, wabunge wa CHADEMA walitoka nje kwa kile walichodai kuwa hawakukubaliana na 'mchakato' uliotumika kumpata rais. Wewe Zitto sio tu hukuingia bungeni siku hiyo bali ulikimbilia kwenye vyombo vya habari na kutoa kauli za (a)kupingana na hatua ya wenzako na (b) kueleza umma mambo yaliyozungumzwa ndani ya kika cha CHADEMA - hiki kilikuwa ni kikao cha ndani.

Wako wabunge wengine wa CHADEMA ambao hawakuafikia hatua ya kutoka nje na kura ilipigwa ili kupata a way forward lakini wewe ulienda zaidi kwa kuonesha utoafauti wako mbele ya vyombo vya habari. Hapa uko na comrades wenzako au uko against them?

2. Siasa za vyama vingi sio uadui. Sasa nilitaka tu kuhoji inakuwaje unaonekana kuwa karibu ki-mkakati na wanasiasa wa chama unachopingana nacho CCM kuliko CHADEMA? Huu ukaribu wako na January Makamba ni kwa sababu wabunge wote wa CHADEMA ni wazee? au hawaelewi kitu? Au you just dont like them? Kauli kwamba unafanya jambo fulani 'bila kujali itikadi za vyama' does not holder water. You are either with your fellow comrades or against them. Hata kama wewe unadhani una uelewa mkubwa kuliko watu fulani fulani ndani ya chama chako unalo jukumu la kuwasaidia ili wafike mahala unapoamini ni pa zuri. Wewe ulianza kidogo kidogo na sasa umepiga hatua nzuri. Uko CHADEMA, do your things with your fellow CHADEMAs. Hawa wengine mnaweza kukutana Rose Garden or elsewhere.

Kwa kifupi niseme unaonekana kujitenga sana na wenzako na ndio maana mara nyingi nimekuwa nasema nampenda zaidi Zitto wa 2007 kuliko huyu wa sasa. Umejiweka kwenye mazingira ambayo unapogombea nafasi ya juu kwenye chama chako watu wanauliza nia na dhamira yako. Hili sio jambo jema kisiasa.

Nadhani aliyetuingiza mkenge kwa demokrasia ya magharibi alituweza.Hebu tutende haki,hivi ni zitto tu ndani ya chadema aliye karibu na watu wa CCM?Hata Mwalimu J.K Nyerere alikaa mezani na waingereza.Unaweza kuwa rafiki wa mtu bila kuathiri principle zake na taasisi yake

Isipokuwa katika harakati kwa wanamapinduzi wote,kila sekunde ni ya tahadhari.Tusije tukajikuta tu tunafanya maamuzi ambayo hayaleti reform ya kweli.Wengine tunahoji sasa ni kwa nini Mwl. Nyerere alikwepa Africanisation baada ya uhuru badala yake Akina Oscar kambona ndiyo wakalisimamia.tunahoji kuhusu mkataba wa kuipatia Tanganyika kama walivyofanya mataifa mengine ya Africa kule Lancaster house
 
Ndio tatizo lenu watu wa kaskazini mnalazimisha Slaa 2015 agombee urais ili hali atakuwa mzee na hatufai tena. Na isitoshe mzee hana jipya kwa sasa, awaachie vijana wakina Zitto. Kuhusu umri katiba ijayo tunalirekebisha hilo na Zitto ambae ni chaguo la CDM wengi ata qualify.

Umefanya utafiti ukapata jibu kuwa zitto ni chaguo la CHADEMA WOTE nyie ndo mtamwalibia zitto
 
nimesoma makala vizuri, kuna mengi mheshimiwa ameyaandika, hili la kuzungumza jinzi akina J J Mnyika na Mdee kwenye chadema, ina lengo la kuwajenga ? au ndio kuwabomoa. watu waone kuwa kumbe ni watu walioingia chadema kwa kusit sita, kwa hio ni maopportunist. mheshimiwa sidhani kama ni sawa kuandika kila kitu kama ulivyofanya, kufanya hivi ni kuwapa nafasi maadui zenu kukumalizeni. pili punguza sana kujisifu, fanya kazi na umma utaaamua wakati ukifika nnakushauri kama mmoja alivyokushauri hii mada achana nayo. fanya kazi ukileta mchezo itakugharibia na kukutengenezea maadui wengi zaidi
Zitto ni kigeugeu, anapenda kuponda wenzie, na anauwezo wa kusaliti wowote ule
 
Kwanini awe mwoga while yupo ule upande wa "wenye nchi" na hata hoja zake ni za kujipendekeza? Watamfahamuje bila kuweka jina lake halisi!
Nimekuelewa vyema mkuu, hii fomular inaitwa jipendekeze ili upendekezwe, ndio maana sikushangaa Richard Kasesera kusikia ameteuliwa kwenye ulaji wa bodi ya madini.
 
Ndugu zangu. Naomba msome makala nzima kabla ya kuchangia. Msichangie kwa kusoma kichwa cha habari tu. Hii ni makala nimeandika kama majibu kwa makala ya mwanazuoni mmoja kuhusu umri wa Urais.

Nimesema wazi, kuutaka Urais na kuupata ni mambo mawili tofauti. Kwanza lazima chama changu kiniteue. Kama chama kikiona bado lazima nikubaliane na chama. Kama chama kikiona kuna mwanachama mwingine ana uwezo zaidi yangu lazima nimwunge mkono huyo. Hata kama chama kikiniteua lakini wananchi lazima wakubali. Kwa hiyo unaweza kuutaka Urais lakini usiupate!

Pili nimejibu hoja za ubaguzi, hatari na matabaka za mwanazuoni huyo. Ni vizuri MoD akachukua makala hiyo na kuiweka juu kabisa ili watu wachangie jambo walilolisoma.

Miye nitaweka makala hiyo kwenye blog yangu zittokabwe.com
Hello Zitto,

Mimi nimesoma yote ...umeandika vyema sana kuhusiana na umri na urais.

Mimi nadhani watu wengi waliokuwa wakikuamini hasa wanaopata updates za whats going on wamepunguza imani na ww that is an issue na wala sio agenda zima ya umri.Imani kushuka juu yako inaonekana kusababishwa na mambo kadha wa kadha ,,,mengi yamesha zungumziwa humu is up to you to come clean kwa kuyatolea maelezo.Hapo ambao bado wana imani na wewe nadhani wengi ni waleambao propaganda hivi tulizopata mwanya sisi wengine kuzisikia na kuzifanyia kazi wao hawanazo...wana jua Zitto yule yule wa jana na leo .Kuna sehemu niliandika matatizo ya vijana wetu tunaojua kwenye siasa wewe kwako nili point out kuwa you are not Royal to your part ...misiguano ipo ila haitakiwi kuonyesha wazi wazi na na katika kujadiliana lazima mpinga ila mwishoni resolution ndio inayobebwa na chama na kila member.

Zito wengi tunataka mabadiliko ,na mimi no matter yanatoka wapi kwa wazee,vijana ,CDM ,CCM ...Kwangu mimi sijali ..najali uadilifu wa mtu maana hata CCM kilichokosekana ni uadilifu ..ambao unatoa imani.So jenga imani kwa wapiga kura wako pamojana wana chama wa CDM watakao kupitisha kama ulivyosema na kulitambua...

Katika point zako nzuri ulizo weka napenda kuwaambia kuwa angenda ya umri ni ngumu kutenganishwa na maslahi ya kijana mlioko kwenye siasa kwa sasa na hasa nyie mliyo iamsha sasa, kwa maana kama itapitishwa vijana mtakao nufaika nayo ni nyie .Kama Mtei aliyosema you can't select someone from nowhere to lead …lazima wale mnao wajua na mna good track record zao.

Kama utapita kwenye chujio la CDM more likely utaukwa urais be royal to party brother jenga imani kwa sisi wenye shaka nawe ,every vote count.

NB
Sehemu ambayo naweza kusema ungeangalia siku nyingine wakati wa kuandia ni pale ulipo andika kuhusu Kwa mfuga mbwa,Tabata na Masaki watu wa kwa mfuga mbwa wanaweza kuwa offended you may be right but not political correctiveness. Hakuna tatizo ku portray Masaki kama sehemu ya high class, Tabata kama sehemu ya middle class but Kwa mfuga mbwa kukuita lower class na haukai huko ni tatizo sawa sawa mzungu amwite black Niga ila black kwa black kuitana niga haina noma (Part haihusiani na suala la umri Vs. urais so maelezo yako kuhusu umri nayapa A+)
 
Thibitisha maneno yako kwamba nina kisirani na mbowe.Wengine sitawasemea.Acha majungu kama huna hoja ya maana ni bora tu unyamaze.

Thibitisha ni wapi nilipokisaliti chama changu.Kwa hayo majungu yenu hamtaniweza hata kidogo na mnalielewa hilo ila ni kiwewe tu kinawasumbua

Ndiyo msimamo wangu dhidi ya uovu,ukandamizaji dhidi ya taifa langu na watu wangu siwezi kuuvumilia na siwezi kuogopa kupambana nao.

Kilichotuunganisha na Zitto ni msimamo dhidi ya uonevu,ukandamizaji,dhuluma bila kujali ni nani anayeonea au ninani anayedhulumiwa.Kilichotuunganisha ni msimamo juu ya utekelezaji wa demokrasia ya kweli na kutoa maono ya kule tunakotaka taifa letu lielekee.

Kuhusu kuwa chadema huko mbele itakuwa na kazi kuliko CCM ni matamanio yako tu.CHADEMA itaendelea kusimama na utaona tutakavyoingia uchaguzi mkuu tukiwa na nguvu mpya.

Kwa kuzingatia muafaka na mchakato ndani ya chama changu,kama Zitto ataamua kugombea nitamuunga mkono kwa kuwa nakubaliana na msimamo na dira yake kuhusu kule tunakotakiwa kwenda as a nation.

Kama tafsiri ya kupigania interest za Tanzania kwa kuchukua maamuzi magumu ni chuki kwa wazungu basi nakubali.But you obvisoulsy havent got your own mindset right thats why you are so quick to condemn a man who has refused to be bullied, intimidated and bamboozled by selfish racist imperialist powers.

kitakachokata mzizi wa fitina ni Zitto kuchapa kazi kwa bidii na wale wenye mtizamo unaofanana ijulikane kuwa there is no excuse zaidi ya kuchapa kazi kwa bidii,determination and objectivity.

Wengine jengeni majungu tu,this is what you are good at !Besides, please don't let your anger cloud this debate because I don't want this to disintegrate into meaninless tat for tat.

Hizi Alliance/ coliation zitakupeleka pabaya sana Young Man........kama unataka kujifunza siasa na ufike mbali fuata nyayo za John Mnyika hizi akili za kushikiwa na mtu hazitokusaidia.
Wamekuja akina Mr 2 Sugu wamechukuwa kadi mwezi mmoja baada ya miezi mitatu wamekuwa Wabunge na wewe kama unajiamini ni mwanasiasa wa kweli nenda kajijenge kwenu na usimame kwa miguu yako miwili na ushinde ubunge. kama wewe ni Mwanasiasa mzuri unaweza kunieleza sababu za kisayansi ni kwa nini kura za ushindi wa Zitto Kabwe mwaka 2010 zilipunguwa jimboni kwake?
 
Suala hapa siyo Zitto,suala la kujadili ni umri wa kugombea urais.Mnajadili mtu badala ya hoja!
 
Baba mchungaji Mzito nakubaliana na wewe kabisa kuwa Zitto amekuwa affected na 'mahaba' ya urafiki sio na JK bali hata na vigogo wengine wa ccm. Na hili limefanya watu waanze kuhoji dhamira na hata loyalty yake iko upande gani.



2. Siasa za vyama vingi sio uadui. Sasa nilitaka tu kuhoji inakuwaje unaonekana kuwa karibu ki-mkakati na wanasiasa wa chama unachopingana nacho CCM kuliko CHADEMA? Huu ukaribu wako na January Makamba ni kwa sababu wabunge wote wa CHADEMA ni wazee? au hawaelewi kitu? Au you just dont like them? Kauli kwamba unafanya jambo fulani 'bila kujali itikadi za vyama' does not holder water. You are either with your fellow comrades or against them. Hata kama wewe unadhani una uelewa mkubwa kuliko watu fulani fulani ndani ya chama chako unalo jukumu la kuwasaidia ili wafike mahala unapoamini ni pa zuri. Wewe ulianza kidogo kidogo na sasa umepiga hatua nzuri. Uko CHADEMA, do your things with your fellow CHADEMAs. Hawa wengine mnaweza kukutana Rose Garden or elsewhere.

Kwa kifupi niseme unaonekana kujitenga sana na wenzako na ndio maana mara nyingi nimekuwa nasema nampenda zaidi Zitto wa 2007 kuliko huyu wa sasa. Umejiweka kwenye mazingira ambayo unapogombea nafasi ya juu kwenye chama chako watu wanauliza nia na dhamira yako. Hili sio jambo jema kisiasa.

Itakuwa jambo la busara sana mumchagulie Zitto marafiki na wengine mumuambie sio asiwakaribie tu bali awanunie hata wakikutana kwenye korido za pale mjengoni. January ni kijana mwenye vision na mwenye uelewa mkubwa sana. Binafsi namkubali sana January kwani kauli zake na matendo yake yanajipambanua na wazee waliopo ndani ya ccm. Haitakuwa jambo la busara kuanza kuchokonoana nani rafiki wa nani kwani kwenye siasa kuna zaidi ya mambo ya majukwaani kwani nani hakustaajabu Rev Mtikila kupewa mil 3 na Rostam? unadhani kila jambo likiwekwa hadharani na uswahiba wanasiasa na nyie mnavyochukulia uadui mtabaki chamani?

Tujaribu kuwa wastaarabu kuwa na uswahiba na mtu mnaetoka itikadi au dini tofauti sio tatizo! angalieni hilo kwa jicho la tatu tukianza hivyo tutaanza kukatazana tusiwe na marafiki na zile sehemu ambazo cdm haina wawakilishi itafika mwisho kwa wale wa dini au dhehebu fulani maana hawakutupa kura! Siasa sio ugomvi wote wana leo la kutuongoza iwe slaa au zitto sioni tatizo ila nyie mashabiki ndio wenye matatizo jaribuni kupunguza umbumbumbu wa siasa.
 
Nashukuru mkuu Ben kwa kutuwekea hii makala hapa. Labda tujikumbushe ule usemi wa 'walk the talk and not talk the talk.

Niliposoma hii artickle nimemkumbuka Barack Obama. Huyu rais ni mzuri mno wa kuongea, anajenga hoja zenye mashiko na ukisikiliza hotuba zake unaweza hata kumkabidhi fungo za gari maana ni rahisi sana kuamini mwisho wa mikosi umewadia, kumbe wapi. Obama sio kama ni sifuri kwenye utendaji lakini he is just as weak as the man standing next to him.

Zitto ni mzuri sana wa kujenga hoja, hilo halina ubishi, je, yukoje kwenye utekelezaji? Wakati wa Speaker Sitta, Zitto alipigania (kwa nguzu zake zote na kwa gharama kubwa) utata wa Barrick/Buzwagi. Fast foward, Barrick hao hao wanampa mabati Zitto kwa ajili ya huko jimboni kwake - ceteris paribus!

Lugha/nguvu aliyokuwa anatumia bungeni kipindi hicho wakati anajadili Buzwagi/Barrick ni tofouti kabisa na sasa. Kuna thread moja inaongelea hii issue ya mabati ya Barrick hapa jf, na Zitto alijaribu sana kutoa maelezo na hata kusema kuwa (tafsiri yangu) amekuwa, uelewa wake umekuwa mpana.

Katika hali ya kawaida, ni vigumu kumsimamia vema mtu wakati huo huo unamtegemea akupe push (hata kama ni push ndogo kama ya mabati). Kisiasa unakuwa umesha-compromise your position.

Labda nikumbushe, mwaka jana waziri mkuu Pinda alisoma majina ya makampuni 15 yanayoongoza kwa kulipa kodi kwa miaka 5 iliyopita. Barrick hapo! Hili lilikuwa bunge la bajeti 2011/12. Mchango wa Zitto kwenye hicho kikao ni pamoja kuweka utaratibu wa 'windfall tax' ili bei ya dhahabu inapoongezeka kwenye soko la dunia basi ongezeko hilo liwe reflected kwenye kodi wanayolipa. Lakini sijamsikia Zitto akiongelea kwa kina kuhusu Barrick na kodi kwa ujumla hasa ukizingatia kuwa hawapo kwenye top 15. Sasa leo anataka watanzania waamini kuwa akiwa kwenye top position atasimamia vizuri madini na gas? Hapa ndio Zitto anatakiwa ku- walk the talk and talk the talk.

Sisemi haya kwa kumvunja moyo, hata kidogo. Nataka Zitto ajue exactly ni mambo gani anatakiwa aangalie, na vipi anaweza kujijengea imani mbele ya watanzania - wapiga kura. Mabati yanaweza kuwa ni kitu kidogo sana lakini yanatoa taswira kwamba huyu ni mwanasiasa wa aina ipi?. Huwezi kuniambia kwamba shughuli za mtu huyu zina walakini wakati huo huo unapeleka bakuli kwa hiyo mtu akusadia kutokana na mapato ya shughuli zile zile zenye walakini!. Utanicha na maswali.

Ushauri wangu Zitto, be yourself, rudi kwenye principles zako za zamani. Hauna sababu ya kuzibalisha. Achana na mashorabo wa mjini. Hawaaminiki.
 
Zitto kasema anautaka urais, lakini kuupata urais ni mchakato unaoanzia katika chama, cdm wana taratibu muafaka na bora kabisa katika kusimamia chaguzi zao, yeyote anayeutaka urais aseme tu, hilo si tatizo kabisa, taratibu zitafuatwa
 
kwanza nataka ku-declare interest yangu kwenye mjadala huu.....umri wangu hauangukii kwenye kundi la ujana.

zitto & co wanapo-champion vijana kukamata uraisi ninawaunga mkono kwa 110%.
kwani umri ni nini? si ni namba tu? kinachotakiwa kuzingatiwa ni maturity, and zitto is more than mature already.

i think wa-TZ wengi bado "tuna-suffer" from modesty ya mwalimu nyerere (ambayo kusema za ukweli lilikuwa ni jambo nzuri).
as far as mwalimu was concerned, dhamana ya utumishi kwa umma ni kitu ambacho mtu alitakiwa kwanza asiwe anakitafuta yeye binafsi kwa bidii sana na pili hata pale atakapokuwa ameombwa alitarajiwa kujitathimini sana mwenyewe (in fact he/she should be seen doing it) kabla ya kuikubali.

"syndrome" hii ndiyo inayomfanya zitto aonekane kama vile ni mtu asiyefaa, mwenye tamaa ya madaraka, nk.
ushauri wangu kwa zitto na wenziwe ni kuwa katika desire yao ya ku-aspire for that highest post, their approach should take into consideration this "nyerere factor", probably not in content, but at least in context.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom