Zitto: Ndio ninautaka urais

Zitto: Ndio ninautaka urais

Status
Not open for further replies.
Binafsi huyu jamaa simwamini kabisa awakilishe chama, CDM inaweza kwenda kuwa CCM-D
 
Huyu kaka anamapungufu. Nasikia eti hajaoa!!!!. Hii post ni ya wababa, kijana kama huyu hajatulia, wachumba watamsumbua, Ikulu itajaa vichupi so badala ya ku deal na issue atadeal na vichupi

Mkuu Nyange, Rais Khama wa Botswana hajaoa lakini anachapa kazi vizuri sana. Kwangu mimi cha muhimu ni kumpata mtu anayeelewa matatizo ya nchii na aoneshe nia, dhamira na uthubutu wa kuyatatua. And if takes mpenda vichupi to fix this country mimi binafsi sioni shida. Kwani vichupi wamelazimishwa? Si unaona hawa wenye ndoa lakini?
 
Na wewe tangu lini ukawa mshauri wa Chadema?

Pamoja na kwamba chama kina utaratibu wake wa kumpata mgombea, na mwanachama yeyote anaweza kuteuliwa kupeperusha bendera ya chama katika uchaguzi mkuu ujao pamoja na chaguzi nyengine zitakazofuatia, ni jambo la kushangaza kuona kwamba mashabiki na wanachama wa ccm na cuf walioko hapa JF na ambao wamejipambanua hivyo, kwamba ndio wanaonekana "kushikia bango" hoja ya Zitto kugombea uraisi, kwamba ndiye pekee anayefaa kuliko wanachama wengine.

Pamoja na kwamba Zitto amejieleza kwa ufasaha sana ni kwanini anakusudia kuwania uraisi wa nchi hii, kitu ambacho ni haki yake, na kwa kijana kama yeye mwenye ushawishi mkubwa miongoni mwa wanachama wa chadema pamoja na watanzania kwa ujumla amefanya jambo la maana sana kuweka nia hiyo ili wakati utakapofika wananchi watakuwa wamesha mchambua vizuri na kujiridhisha kwamba anafaa kukabidhiwa majukumu ya kuiongoza nchi hii.

Sasa swali langu kubwa hapa ni kwa namna hawa mashabiki na wanachama wa ccm na cuf walivyojitokeza kwa nguvu kumpigia debe naibu katibu mkuu wangu kwamba ndiye pekee anayefaa kupeperusha bendera ya chadema. Hii inanifanya nimuulize naibu katibu mkuu wangu Zitto maswali machache;

1.Mh. Zitto unadhani ni kwanini hawa wapinzani wetu wanashabikia sana wewe kugombea uraisi 2015?
2.Mh. Zitto unadhani kwanini hawa wapinzani wetu wanaonekana kuwa na imani zaidi na wewe kuliko mwanachadema mwengine yeyote?
3.Mh. Zitto unadhani wanafahamu udhaifu wako hivyo wanaamini kwamba itakuwa ni kazi rahisi kwao kukushinda?
4.Mh. Zitto unadhani hawa wapinzani wetu wamewachoka ama hawana imani na wagombea wa vyama vyao na kwahiyo wanaamini kwamba unaweza kufanya mambo makubwa yenye manufaa kwa taifa hili hadi wanaamua kukupigia debe bila kujali kwamba uko chama tofauti na wao?
5.Mh. Zitto kwakuwa hakuna chama kinachopenda kushindwa uchaguzi na kwahiyo hakuna chama chochote makini kinaweza kukishauri chama pinzani chake kisimamishe mgombea ambaye ni tishio kwake, unadhani ni kwanini unapata uungwaji mkono mkubwa sana toka kwa wapinzani wetu?

Mh. naibu katibu mkuu wangu naomba unitoe wasiwasi huo, kwani pamoja na imani kubwa niliyonayo dhidi yako lakini naona ni muhimu ukasafisha huu ukungu ninaoanza kuuona hapa. Natanguliza shukrani kamanda.
 
Huyu kaka anamapungufu. Nasikia eti hajaoa!!!!. Hii post ni ya wababa, kijana kama huyu hajatulia, wachumba watamsumbua, Ikulu itajaa vichupi so badala ya ku deal na issue atadeal na vichupi

ndiyo maana wanapigiana upatu na Ben saanane.mzee wa totoz inafikia hatua akiwa karibu na mtu au ndugu yako unaanza kutoa tahadhari kwa machapisho.mtu aliona ugumu kuwa na demu wa kudumu akawa anamega mademu za watu.tabia hii imejaa sana huko chadema na itafikia siku badala ya kugombania hoja mnagombania wanawake wenye makalio makubwa.hawaaminiki wanapenda totoz.hao ni akina jacob zuma na akina jk in the making.nilisikitika sana kusikia pia akina mnyika wamo kwenye post ya tuntemeke.kumbe hizi sura laini ni mapango.watu waoe wadhibitiwe na wake zao kimaadili hapo sisi tunaweza kuwaamini kwenye ofisi za umma.

jamaa anaona njia ya kuvuruga uongozi wa akina heche ni kumuingia kimahaba makamu mwenyekiti juliat shonza.namuonea huruma huyo dada kwa kuwa jamaa akishapata anachotaka atasepa tu.chadema inaishia kuwa chama cha wahanga wa mahaba na wajane wasio na ndoa
 
Basi akagombee chama kingine lakini sio chadema. Lazima chama kiwe na malengo. dr.Slaa alishapiga jaramba 2010 kilichobaki ni kuingia uwanjani(ikulu). Zitto bado anao mda wa kujipanga na umri unaruhusu. hatutaki kupoteza nguvu kazi kama Slaa ipotee hivihivi. Inabidi dr.Slaa atoe mchango wake kwa taifa lake nasi tumfaidi.

Mtu akipenda chake bana...Hivi ninyi sio ndio mmekuwa mkipiga kelele kuwa CUF inakosea kwa kuwasimamisha Maalim Seif na Prof Lipumba kila mara?. Hivi mmesahau ule mtazamo kuwa siri kubwa ya kukua kwa CHADEMA ukiondoa ile ya kuchokwa kwa mauzauza ya CCM ni huu utaratibu wa kubadilisha vinara (visura) wa chama katika ngazi za Ugombea Urais na Uenyekiti? Ama kuna mengine yanayofunda mioyo yenu mnaficha kuyasema???
 
Mkuu Nyange, Rais Khama wa Botswana hajaoa lakini anachapa kazi vizuri sana. Kwangu mimi cha muhimu ni kumpata mtu anayeelewa matatizo ya nchii na aoneshe nia, dhamira na uthubutu wa kuyatatua. And if takes mpenda vichupi to fix this country mimi binafsi sioni shida. Kwani vichupi wamelazimishwa? Si unaona hawa wenye ndoa lakini?

wazinzi huku jf mko wengi.nahisi umekuwa too sensitive kwa hili kwa kuwa una maslahi nayo au ni tabia yako.sio utmie kigezo cha walioshindwa katika ndoa zao kuhalalisha ubazazi na uzinzi wenu.hatutaki kodi zetu zitumike kulipia mahawara.kuna wengine wanastahili kugombea u-big brother kwa kuwa hata kampeni zao kihistora tangu chuo ziliteka wanawake zaidi na kwa jinsi alivyo sidhani kama dada na wake zetu watasalimika.kuna watu wakishinda urais nchi hii tutahamisha wake na mabinti zetu
 
Hoja ni lazima imwangalie pia mtoa hoja. Hili ni jambo la lazima katika uandishi wowote ule ndiyo maana ''about the author''. Hoja inaangaliwa kwa ujumla wake pamoja na mtoa hoja. Tatizo ni pale unapomjadili mtu huku ukiacha kando hoja.

Hoja inapotolewa maswali yafuatayo yanaweza kuulizwa:
  • Nani katoa hoja?
  • Wakati gani?
  • Mazingira aliyotolea hoja
  • Hoja inmnufaishaje mtoa hoja
  • Je, kuna makundi mengine yatakayonufaika?

Ukijadili hoja huku ukimfumbia macho mtoa hoja utakuwa na mapungufu katika nyanja za wasomi hali kadhalika ukimjadili mtoa hoja na kuacha mantiki ya hoja utakuwa pia hujakamilisha uchambuzi wako. Utamu na ukamilifu wa uchambuzi ni kuangalia jambo kwa pandenne za dunia 4 angle perspective
 
Na kwa cdm huyu ndio mtu anae faa kuwa Rais. Wengine wote wakina M & S Company wana tamaa tu za madaraka. Nawaomba wana cdm muungeni mkono zitto na apitishwe na chama

Zito bado sana ktk suala zima la kuweza kuongoza nchi
 
Matola,

1.Ati Alliance na coalition zitanipeleka pabaya?pabaya ni imagination tu,ni wapi huko? Acha kunitisha,sitishiki!

2.Kama nataka kujifunza siasa ili nifike mbali?Mbali ni wapi mkuu? Naona huu ni mwendelezo wa siasa za ubinaqfsi/unafiki.Unamanisha nijikite kwenye siasa za kujineemesha?huku ndiko unakopaita mbali? Sihitaji kujifunza siasa ya aina hii.

Kuhusu kufuata nyayo za mtu,mimi siyo aina hiyo ya copy and paste.siasa za copy and paste ndizo zilizotufikisha hapa.nina misiammo yangu na nina principles zinazoniongoza kwenye siasa na uongozi hata kama ni nje ya siasa.

Kuhusu kufuata Nyayo za Mnyika nimeshakujibu hapo juu,huyu ni kiongozi wangu ni rafiki na huwa tunashauriana mambo mengi na tunaheshimiana ila usinichagulie kitu cha kufanya/kufuata

3.kuhusu akina sugu sijui wamefanyaje,hayo ni yao.Kila mtu ana historia yake.Kuhusu kugombea ubunge Mungu akipenda nikifika salama 2015 nitagombea hilo halina mjadala.Hata 2010 ilikuwa nigombee lakini nilikuwa nje nikimalizia mitihani yangu ya Masters.Nilipokuja mchakato ulikuwa umefika mbali,hivyo niliamua kutogombea na nikaelekeza nguvu kukisaidia chama changu hasa Rafiki yangu John mnyika,Halima mdee,Regia Mtema (R.I.P) na majimbo ya Moshi mjini na jimbo la Rombo ambako waliamini kwamba mramba hawezi kushindwa uchaguzi.

Ati kama najiamini?Ndiyo ninajiamini sana.....!

4.Kuhusu kusimama kwa miguu yangu miwili: Hata sasa nasimama kwa miguu yangu miwili,nina kazi na ninafanya kazi kwa bidii.

Kwenye siasa sitegemei kubebwa,siamini katika siasa za kubebabana labda tubebane katika msimamo na vision basi.Naamini katika principles.Niligombea uchaguzi wa BAVICHA sikubebwa zaidi ya kutarajia kubebwa na wapiaga kura ambao wangekubaliana na kile nilichokuwa ninaamini.Ninaamini katika maamuzi ya ballot box,siamini katika remote control.

Watu wa kubebwa wanajulikana,cowards wasiojiamini na kusiamamia wanachoamini wanajulikana.Mkuu hapa utanitaka radhi

Chadema msipomdhibiti huyu mtatuandalia bomu.

Huu ushirika wako Ben saanane na akina Zitto huko mbele utazaa uasi wa kutisha siyo ndani ya chama tu hata usalama wa nchi. Naona kila dalili za uasi wa vijana dhidi ya wazee.

Usalama wa taifa sasa inabidi ufanye kazi kushughulikia hizi mbegu mapema. Kwa bahati mbaya huyu ni mtu wa visasi na hata sasa nilishaongelea kuhusu chuki yake dhidi ya wazungu na wakenya, tunaandaa akina Julius Malema au akina Adolf Hitler bila kujijua.

Kujiamini najua unajiamini sana sijui ni kitu gani kinakupa jeuri kiasi hicho; hata balozi Eva Nzavo kipindi kile baada ya kikao cha jumuiya ya watanzania alichomshutumu balozi kwamba anagawa watanzania kwa misingi ya chama balozi alisikitika sana na kuuliza huyu mwenzenu jeuri hii anaitoa wapi hasa. Kama hapendezwi na mimi balozi kufungua matawi ya CCM huku ughaibuni ni kwa nini na yeye asifungue ya chadema?
 
Zitto bana? acha hizo mkuu huwezi kuwa rais JMT kupitia CDM..NEVER!

Rais kupitia cdm ni Mbowe au Slaa au Mnyika etc..

Wewe endelea kubeba mabegi ya wakubwa wako..

Oh boy keep on crying..watakutumia kama toilet paper..soon wakikupatia watakutupa nje ya ulingo kwa hoja maalum..(siri yao)..

Acha hizo dream, msaidie Slaa na Mbowe period that is maximum we can offer kwenye chama chetu has kwa watu kama nyie..(kazi yenu ni kawawa type ok!)
 
Uzi huu unaangaliwa sana na wagombea watarajiwa wa ubunge, nimemuona mrithi wa Lusinde anachungulia
 
Ndio tatizo lenu watu wa kaskazini mnalazimisha Slaa 2015 agombee urais ili hali atakuwa mzee na hatufai tena. Na isitoshe mzee hana jipya kwa sasa, awaachie vijana wakina Zitto. Kuhusu umri katiba ijayo tunalirekebisha hilo na Zitto ambae ni chaguo la CDM wengi ata qualify.

Anafaa kuwa rais wa nini? Maana Tz tuna maraisi kibao mfano rais wa TFF rais wa nchi nk ila kama rais wa tff anaweza akatufaa ila wa nchi bado sana kwani hata katiba haimruhusu na hajakomaa kisiasa na mbaya zaidi bei yake anajulikana
 
Chadema msipomdhibiti huyu mtatuandalia bomu.

Huu ushirika wako Ben saanane na akina Zitto huko mbele utazaa uasi wa kutisha siyo ndani ya chama tu hata usalama wa nchi. Naona kila dalili za uasi wa vijana dhidi ya wazee.

Usalama wa taifa sasa inabidi ufanye kazi kushughulikia hizi mbegu mapema. Kwa bahati mbaya huyu ni mtu wa visasi na hata sasa nilishaongelea kuhusu chuki yake dhidi ya wazungu na wakenya, tunaandaa akina Julius Malema au akina Adolf Hitler bila kujijua.

Kujiamini najua unajiamini sana sijui ni kitu gani kinakupa jeuri kiasi hicho; hata balozi Eva Nzavo kipindi kile baada ya kikao cha jumuiya ya watanzania alichomshutumu balozi kwamba anagawa watanzania kwa misingi ya chama balozi alisikitika sana na kuuliza huyu mwenzenu jeuri hii anaitoa wapi hasa. Kama hapendezwi na mimi balozi kufungua matawi ya CCM huku ughaibuni ni kwa nini na yeye asifungue ya chadema?
Na wewe bana..acha uoga wa kijinga na kutishwa na so called usalama..wazungu wanakupenda wewe? mbona hujiulizi hilo swali kabla ya kumtwisha Ben mzigo huo?
 
Kweli itakuwa ccm ndo waanzilishi wa hii chokochoko ya hii thread
 
Kama mtanzania mwenye sifa, ana haki ya kutangaza nia yake.
Siyo dhambi Zitto kusema anataka urais
Tatizo wagonjwa ndo wanautamani urais, matokea wakiupata wanapoteza muda mwingi kujitibu badala ya kufanya yale waliyoyahidi e.g Mkwe.re
 
Nimepitia hii mada ya Zitto na hakika inahitaji mjadala mpana sana.

Binafsi sidhani kama kuna haja yoyote kwa sasa kufanya wagombea urais kuanzia miaka 35. Hii ni hoja changa sana tena ya kitoto. Ni hoja iliyopikwa kwa sababu maalum na kwa malengo maalum. Tunajua mwasisi wa hoja hii ni Rais Kikwete pale alipowaeleza siri hiyo kina Zitto na Kafulila kule Kigoma. Na baada ya pale ndipo Zitto akalibebea bango.

Niwe mkweli kwamba CDM wafanye kazi ya kuimarisha chama chao waachane na porojo za urais. Ni upuuzi badala ya kuimarisha chama watu wanaanza kujipigia kampeni za kugombea urais. CDM nadhani wana mgombea bora kabisa wa Urais ambaye bado ni kipenzi cha watu Dr Slaa. CDM wanapaswa kumsaidia Dr Slaa ili aje awe Rais bora.

Kinachomnyima Zitto credit kugombea kupitia CDM ni sababu moja tu kwamba anapigiwa debe la nguvu na wale maadui wote wa CDM. Wajanja wanajiuliza Kulikoni? Adui yako akikusifia ujue there is something wrong!
 
Chadema msipomdhibiti huyu mtatuandalia bomu.

Huu ushirika wako Ben saanane na akina Zitto huko mbele utazaa uasi wa kutisha siyo ndani ya chama tu hata usalama wa nchi. Naona kila dalili za uasi wa vijana dhidi ya wazee.

Usalama wa taifa sasa inabidi ufanye kazi kushughulikia hizi mbegu mapema. Kwa bahati mbaya huyu ni mtu wa visasi na hata sasa nilishaongelea kuhusu chuki yake dhidi ya wazungu na wakenya, tunaandaa akina Julius Malema au akina Adolf Hitler bila kujijua.

Kujiamini najua unajiamini sana sijui ni kitu gani kinakupa jeuri kiasi hicho; hata balozi Eva Nzavo kipindi kile baada ya kikao cha jumuiya ya watanzania alichomshutumu balozi kwamba anagawa watanzania kwa misingi ya chama balozi alisikitika sana na kuuliza huyu mwenzenu jeuri hii anaitoa wapi hasa. Kama hapendezwi na mimi balozi kufungua matawi ya CCM huku ughaibuni ni kwa nini na yeye asifungue ya chadema?
Mkuu,

Umeamua kuingia kwenye personal vendatta baada ya kubanwa kwenye hoja.Ndiyo sikatai kwamba kufungua matawi ya vyama vya siasa nje ya nchi niligomea na nililisema wazi mbele ya Balozi.tukiwa nje ya Tanzania sisi huwa tunajulikana kama watanzania na si wanachadema wala wana-CCM.Tunatakiwa tuungane tuwe kitu kimoja kwani tulikuwa wachache.Wenzetu wanigeria walikuwa wengi na hawakuwahi kufanya jambo la kijinga kama lile.

Balozi mzima aliyosomea protocal anasimamia zoezi la kuwagawa watanzania?ulitaka nimchekee?

Tangu lini hapa Tanzania tukaona wamarekani wamenzisha matawi ya Republican na democrats hapa Tanzania kwa kuzingatia utashi wa vyama vyao?huku si ndiko tulikoiga demokrasia ya mfumo wa vyama vingi?ni kwa nini sasa tuingie kwenye siasa kizuzu hadi tutie fedheha ugenini? Kwangu mimi ni Tanzania kwanza mengine baadae na siwezi kumuogopa Balozi,waziri au mwanasiasa yoyote

Nadhani hizi nguvu tunazotumia tuelekeze kujadili maudhui ya katiba mpya,tuweke foramal debate kuhusiana na mambo ambayo ni nguzo kuu ya huko tutakako.

Tupiganie tume huru ya uchaguzi n.k kwa maana hata tukipata rais mzuri kiasi gani kwa mazingira yalivyo bado itakuwa tatizo na linazidi kukua kwa kasi

Vijana wote wenye uwezo usiotiliwa shaka msiogope kujitokeza kuwania nafasi za uongozi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom