Zitto: Ndio ninautaka urais

Zitto: Ndio ninautaka urais

Status
Not open for further replies.
Kuna watu wengine bana yaani wao wanata muda wote tuwe tunajadili uchaguzi wa Arumeru mashariki tu na Ubaya wa CCM........... HAIWEZEKANI.

Maisha mengine lazima yaendelee jamani, hizi habari za kusema ukileta hoja nyingine zaidi ya uchaguzi wa Arumeru mashariki eti ni kudivert attension za watu mimi naona ni yakipuuzi sana.

Nahakika wapiga kura asilimia 99.9 ya wakazi wa Arumeru hajui kitu chochote kinachoendele humu JF zaidi yetu sisi wa Kutoka nje ya Arumeru na wanaokaa nje ya nchi huko
Sasa hii dhana ya kudevert inakuja vipi hapa? hivi tunadhani tukidivert ndio labda itaisaidia CDM au CCM kushinda?

Acheni watu wajadili mambo yanayojiri bana, hauwezi kusimamisha mijadala ya matukio yanayojiri au kugundulika sasa eti kwasababu kuna uchaguzi Arumeru

VINGINEVYO ITAKUWA NI KAMA TUNAPASISHA KUWA HILI NI JUKWAA LA CDM TU KUPIGIA KAMPENI CHAMA CHAO.........maana zimeanzishwa Sredi nyingi tu sana humu kuhusu CCM na watu wanafunguka kweli kweli lakini huwezi sikia eti una divert attension

hivi kwa ufahamu wako uchaguzi wa urais ni lini? Elewa, waoga hukimbia wasipokimbizwa na walevi huongea wasivyovijua kutokana na nguvu ya kilevi ndani yao.
 
Mkuu nadhani Zitto amekumbushia tu. Nakumba 2010 wakati anaomba kura kule MWandiga aliwaambia wazi wazi wapiga kura wake kwamba hiyo ni mara ya mwisho anaenda pale kuwaomba kura za ubunge, akirudi atakuwa akiwaomba kura za Urais. Pia mkuu uchaguzi wa Arumeru unasimamisha mambo yooote hapa nchini? Yaani watu wanatakiwa wakiamka ni Arumeru wakila ni Arumeru? Twende navyo kwa pamoja Arumeru na mambo mengine pia.


Kiongozi, tatizo hapa sio kukumbushana. Zitto sio mwanachama wa kawaida CHADEMA. Huyu ni naibu katibu mkuu wa CHADEMA na naibu kiongozi wa upinzani bungeni. Akiwa kama kiongozi kwa priority yake kwa week hii ya mwisho ya uchanguzi Arumeru ni nini? Angepata hasara gani kama angeleta huu mjadala mara baada ya Arumeru.

Kwa bahati nzuri siku hizi wananchi tunapata taarifa zaidi kuliko huko zamani. Habari za huyu bwana mdogo zitawa-dissapoint wengi, tumalize kwanza uchaguzi. Ukiona mtu anakimbilia Ikulu kwa nguvu kubwa ni lazima uulize ni kwa nini? Hii Haraka ya Zitto inatokana na nini?
 
zitto-kabwe-top-safi.jpg


NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), Zitto Kabwe ameibuka na kusema kuwa anataka kuwa rais wa Tanzania mwaka 2015.Wakati Zitto akitoa kauli hiyo nzito, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta naye amesema anashangazwa na watu wanaoweweseka wanaposikia kuwa mwanasiasa huyo anayeongoza vita dhidi ya ufisadi ambaye pia ni Mbunge wa Urambo Mashariki, anataka kuwania urais.

Kauli hiyo ya Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini na Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni huenda ikaibua mjadala mzito ndani ya chama chake, ukiacha zile mbio za vigogo wa CCM wanaotajwa kuutaka urais 2015.

Katika taarifa yake aliyoituma jana kwa gazeti la Mwananchi Jumapili, Zitto alisema; " Kwanza niseme wazi kabisa kuwa Urais ninautaka, nchi inahitaji kiongozi wa juu atakayekabili changamoto hizi. Ninaamini ninaweza kuwaongoza Watanzania wenzangu kukabili changamoto hizi." Alitamba anao uwezo kwa kuwa ni mzalendo, mwenye utashi wa kuleta mabadiliko stahiki kulingana na nchi inavyoongozwa. Katika taarifa hiyo ameeleza kuwa kwa sasa nchi imesahau maendeleo ya watu badala yake imejikita katika maendeleo ya vitu.

"Ninajua kuwa hivi sasa viongozi wetu wengi wanaangalia zaidi mitindo badala ya mambo ya msingi," Zitto amesema taarifa na kuongeza: "Ninajua kuwa maendeleo vijijini yamesahaulika, ninajua nchi yetu inahitaji uongozi wa kufanya mabadiliko makubwa badala ya mabadiliko ya juujuu."

Alieleza kuwa mabadiliko makubwa yanahitaji maamuzi magumu yatakayoudhi wengi hasa vigogo wa nchi za Magharibi huku akitoa mfano kuwa ni pamoja na kuzuia nchi kuuza malighafi pekee. Alisisitiza kuwa rushwa, ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma ndio kikwazo kikubwa cha maendeleo ya nchi na kwamba lazima hatua madhubuti zichukuliwe kuzuia na kutokomeza ufisadi.

"Rasilimali kama madini, mafuta, gesi asilia, ardhi na nyinginezo ni lazima zifaidishe wananchi wa nchi yetu," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo. Sababu za kutaka Urais Katika taarifa hiyo Zitto alieleza kuwa kwa sasa nchi inahitaji kiongozi wa juu atakayekabili changamoto muhimu na kwamba yeye anaweza kuwaongoza Watanzania kukabiliana na changamoto hizo. "Sio kazi rahisi, lakini ni kazi ambayo lazima Mtanzania mmoja aifanye, mimi nataka kuifanya, nina uwezo wa kuifanya," alitamba katika taarifa hiyo.

Alieleza kuwa hata kama anaitaka kazi hiyo, ni lazima Watanzania walio wengi waamue, pia ni lazima Chadema kiseme wazi kuwa yeye ndio anastahili kuifanya kazi hiyo na kwamba kuitaka tu nafasi hiyo hakutoshi bila ridhaa hizo. "Kama wananchi watasema huyu Zitto anapaswa kubeba jukumu hili mwaka 2015 tuache iwe. Kama watasema hapana wewe bado mpaka mwaka 2020 au 2025 tuache iwe hivyo. Pia Kama hawataki kabisa tuache iwe hivyo," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Umri wa kugombea urais Katika taarifa hiyo, Zitto alieleza kuwa mjadala wa umri wa kugombea urais umekuwa mkali na kwamba baadhi ya watu kwa sababu zao binafsi, wameamua kuuita ni mjadala wake na Mbunge wa Bumbuli January Makamba ambao unaowabagua wazee.

Alisema kuwa mjadala huo aliouita wa ‘kupandikiza chuki na sumu za kibaguzi' ni wa kitabaka, unaonyesha kuwa Zitto na January sio tabaka stahili la vijana walio wengi. Huku akionyesha kujibu makala katika moja ya magazeti(sio ya Mwananchi Communications Limited) ambayo haikupinga umri bali hoja ya wanaoujadili urais na vyama wanavyotoka kutowapika vilivyo vijana kuwa viongozi, Zitto alieleza kuwa hali hiyo inaonyesha ubaguzi wa wazi.

"Ingawa sisi sio waanzilishi wa hoja hii lakini ni hoja ya kibaguzi. Nawashangaa wasomi wa siku hizi kwa kujadili watu badala ya hoja," ilieleza taarifa hiyo. Chadema kukuza vijana Alieleza kuwa Chadema kinalea na kukuza vijana kuwa viongozi na kwamba yeye alijiunga na chama hicho akiwa na umri wa miaka 16 huku akipewa majukumu mbalimbali.

Alisema kuwa wakati akisoma Chuo Kikuu Dar es Salaam(UDSM), Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe wakati huo akiwa Mbunge wa Jimbo la Hai, alimuomba kushiriki kikamilifu kukijenga chama hicho kutokana na kukimbiwa na wanachama isipokuwa wale waliokuwa wakitokea Kigoma, Kilimanjaro, Shinyanga, Karatu na Ukerewe.

"Mwaka 2001 muongo mmoja uliopita ni mimi na Mbowe ndio tuliofanya mabadiliko yote yanayoonekana Chadema. Tumeingiza watu wapya na tumeandika Katiba upya, tulichambua mambo mengi na Mbowe kuijenga Chadema," alieleza katika taarifa hiyo.

Alieleza kuwa mwaka 2005 Mbowe aligombea urais na kwamba walijua kuwa watashindwa ila walitaka kukijenga chama hicho na walipata wabunge na kuongeza kuwa mwaka 2010, Chadema kilishiriki uchaguzi mkuu kama chama imara kinachokwenda kuchukua dola. Huo ndio ukawa mwanzo wa kuibuka kwa wabunge John Mnyika (Ubungo), Halima Mdee (Kawe), wabunge ambao alieleza kuwa awali walionyesha wasiwasi mkubwa kujiingiza katika siasa.

"Baadhi ya watu wazima waliingia Chadema kwa sababu ya vijana, nani anasema hatulei vijana kuwa viongozi wazuri, nani haoni hazina ya viongozi vijana hivi sasa ndani ya Bunge kutoka vyama vyote. Kuna namna bora ya kulea viongozi zaidi ya kuwapa majukumu?" Alihoji katika taarifa hiyo.

Hoja ijadiliwe Katika taarifa hiyo Zitto alifafanua kuwa hoja ya umri wa kugombea urais iwe na mahali pakuanzia na inapaswa kujadiliwa bila kuangalia majina ya wanaotetea hoja hiyo. Suala hilo lijadiliwe kwa faida na hasara zake na kufafanua kuwa hakuna anayejua kuwa yeye atakuwa hai mwaka 2015 na kwamba isiandikwe katiba yenye kupanua wigo wa kutoa haki ya kugombea urais kwa sababu yake.
Samuel Sitta

Akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali katika Tamasha Vyombo vya Habari lililofanyika jana kwenye Ukumbi Msasanki Beach, Dar es Salaam, Sitta alieleza kuwa anashangazwa na watu wanaoweweseka wakisikia anataka kuwania urais mwaka 2015.

"Nashangaa watu wanapata kiwewe kusikia nataka kuwania urais, kuwania urais ni haki ya kila Mtanzania na Watanzania ndiyo watakaoamua nani ni mzuri na atawafaa," alisema Sitta na kushangiliwa na waliohudhuria tamasha hilo.

"2015 tunataka kuwa na mwelekeo mzuri, nikiwa na maana mambo ya hongo, ubadhirifu hatutaki yawe na nafasi, alisema Sitta na kuongeza:

"Kuna hadithi moja, siku moja trafiki mmoja alikamata gari pale Mwenge (Dar es Salaam) akaomba, leseni, akaangalia kadi ya gari sasa yule mama alikuwa na mtoto wake ana miaka kama minane, akamwambia mama yake, mpe kitu kidogo...hivi imefikia hatua hata mtoto wa miaka minane anajua rushwa."

Alisema rushwa imesababisha nchi kuingia mikataba ya uongo, kuna mikataba mingi ya uongo na ndio maana leo hii nchi imefika hapa ilipo.

"Hii imesababisha matatizo hadi ya umeme, tungeweza kuuza umeme wetu nje, lakini leo haiwezekani, nasema haya kama mzee wenu na kiongozi wenu.

"Sasa, nawaasa waandishi, msikubali kuwa mawakala wa viongozi waongo, msikubali uongo na kama tungeendelea kule uongo, nchi ingeharibika...hatuwezi kusonga mbele kwa uongo na vyombo vyenu visitumike kusambaza mambo ya uongo," Sitta alishauri.

Alisema watu wanatumia fedha nyingi kusaka urais na hata wengine kutumia ndumba kwa kwenda Mlingotini, Bagamoyo, kwa nia ya kutaka uongozi na matokeo yake kama watu hao watashinda lengo la kwanza linakuwa kurudisha fedha walizotumia.

Alivipongeza vyombo vya habari kwa kazi nzuri ya kufichua maovu ndani ya jamii na kuwataka viongozi wawe wastahimilivu wanapoandikwa maovu yao.Aliwaasa viongozi wenzake kutanguliza uzalendo kwa nchi na kuwataka wachape kazi kwa maslahi ya taifa vinginevyo watarudisha nyuma maendeleo ya nchi.

Source: Mwananchi
 
kusema tu Nautaka Urais ni Kigezo tosha cha Kutokomaa kisiasa, ni UTOTO unaosumbua maana tabia ya mtoto mara zote "nataka pipi", "nataka mdori nataka".."nataka.. nautaka." mie simo niko ki-arumeru zaidi kwa sasa.
 
Hata mimi nautaka urais.........

Ila nitaanzia na ule wa TFF
 
kwa katiba la tz la kuwa rais on 10 years bases.. Mtu mwenye miaka 35 akiukwaa urais given kwenye 45 atalazimika kuwekwa kando kama sio 40. Na kwa umri huu ndio wa ujana lakini unapachikwa jina la mstaafu.

Ni wazi sehemu ya maisha yako itakuwa kula kulala. Mara nyingi kwenye nchi ambazo hawana democracy hata mtoto anaweza kuwa mtawala but he/she will be there hadi anazeeka.. Na ikitokea nchi ya kidokrasia yenye mafungu ya kuongaza kwa miaka kadhaa na ikatokea kiongozi kijana.. Lazima atafanya jitihada za kuchakachua katiba ili ajinemeshee miaka zaidi.

Vijana wengi wa kwetu ni wakirupukaji, wabi nafsi na wasaliti. Hang'ang'ania vyeo na nafasi za juu sana za uongozi bila kufikiria after uongozi kuisha itakuwaje.. Mtu hata familia hana, hajajua house management and children care ikovipi leo anag'ang'ana kuwa rais. Ni kukurupuka sana.

Sisemi rais lazima awe ameoa ila kwa utanzania wetu na maisha haya, familia ni uongozi kamili na ukishindwa kimanage fimilia sahau kiwamanage wananchi.. Kama huamini njoo huku ccm, angalia kati ya wabunge wote, nani mwenye historia nzuri ya ndoa yake.. Hamna, naskia alikuwa warioba tu, njoo kwa wabunge wanawake, orodhesha wenye ndoa... Kapa.. Kama ipo ya kuunga sana kwa vijiti. Sasa kama viongozi hawa weledi tu wa family care ulishawashinda saa ngapi wataweza kuliongoza taifa.
ww unachuki na zitto, zito ana mke na kama unataka kumjuwa nenda kwake tabata, mbona slaa hajaoa, ameiba mke wa mtu husemi? Hv itakuwaje mtu mwenye zaidi ya miaka 65 aendelee kuishia maisha ya uchumba?
 
hakuna atakayemzuia kama ana ubavu wa kupenya kwenye mchakato wa chama.
 
Hakuna tatizo kusema ninautaka urais hizo ni ndoto zake ambazo anazipigania, kila mtu na ndoto zake na matamanio yake.
 
huu woga kuhusu zitto unatoka wapi.?nimemini chadema wanajua nguvu ya zito ndio maana wanagongana vichwa pale anapotoa kauli.!!
 
Zitto mwache Dr. Slaa afungue kwa kushika madaraka ya nchi hii kwa wapinzani.
Naapa ukigombea wewe watu wengi hawatavutika na CHADEMA hata mie ntawapigia hao ninaowachukia CCM.
Zitto unafaa kuwa mtendaji such as Prime minister au minister wa fedha n.k

plz nakuomba na naahidi ntaku PM kwa kirefu.

Believe me or not, Dr. SLAA ana ushawishi sana second to Hayati Baba wa Taifa (shame on Ben)

najickia uchungu wa ndani sana km Dr. Slaa hatapitishwa tena kwani tofauti na Slaa 2015 ni kuwasindikiza CCM.

Na hii dhambi Zitto itakuandama nafsini mwako na watanzania wote wapenda mageuzi watasononeka kwa ajili yako na nyota yako itafifia 80%.
Tulia bro tafuta hekima tunakuheshimu sana.
 
US election 2012: How to run for president

Election Day comes after as much as two years of campaigning
Continue reading the main story
US Presidential Election 2012
As it happened: Super Tuesday
Delegate counter
Where do they stand?
Who's backing whom?
The US presidency is described as the world's hardest job and the election campaign is said to be its toughest job interview. How do you run for president? BBC News explains the process.

The early stages

A politician with presidential ambition usually forms an exploratory committee to test the waters and raise money. This can begin up to two years before the election.

The US constitution requires only that a person be a "natural born citizen" of the US, at least 35 years old, and a resident of the US for 14 years.

But not just anyone can credibly stand for election: In the last 70 years, every non-incumbent major party presidential nominee has been either a sitting or former US senator, governor, vice-president or five-star general.

If the candidate attracts significant favourable notice from the news media, party officials, prospective campaign strategists, and donors, he or she formally declares his or her candidacy and launches campaigns in key early states.

Barack Obama's campaign began to coalesce in late 2006 and he formally declared he was running in February 2007.

Mitt Romney, meanwhile, has essentially been running for president for nearly five years.

Having failed to capture the Republican nomination in 2008, Mr Romney quietly maintained a behind-the-scenes campaign through the first two years of Mr Obama's term in the White House and formally declared his candidacy for the 2012 nomination in June 2011.

The nomination fight


Then-Senator Obama declared his candidacy for president in February 2007 in Illinois
After declaring, the candidates begin vying for their party's nomination for the presidency.

Typically - but not always - they spend the next several months campaigning heavily in the early
 
Namuona mheshimiwa yumo ndani ya nyumba

1.eti mhe yasemwayo yana ukweli?
2.je ni kweli kwenye chama hakuna mtu mwingine ila slaa peke yake?
3.je Dr akisema hagombei hamtaweka mgombea urais 2015? kumbuka kila kitu kinawezekana as we are human beings and not machines/angels.

WAKUU.
tusipotoshane hapa.
slaa sio mgombea urais wa chadema 2015 isipokuwa alikuwa mgombea 2010. yeye mwenyewe alitamka hadharani kuwa alikuwa hautaki urais lakini alilazimishwa. sasa kama kuna mtu amejitokeza kuutaka urais mimi nadhani anapaswa kuungwa mkono sana mana huwezi ivaa nguo nusiyoipenda ukaenda nayo safari. slaa alifanywa chambo na mbowe na sasa mnataka kumlazimisha kuwa yeye ndiye mgombea urais wa chadema.
shame on you.
 
Zitto, mimi huko pia Urais nautaka na kama ni UWEZO TUNAO haya twende basi tukaupate huo urais ukiwa wa moto moto bada.

Pengine Urais wa Tanzania upo on Sale lakini wengine hamna taarifa. Mzee Mtikila kwani wewe urais hautaki, je mzee mapesa, na wewe hapoPasco vipi twendeni tukajipakulia urais wa JMT.

Masou wa Kipanya, urais ndio huu hapa twenzetuni basi maadam kuna vijisenti mfukoni mengi MAFISADI watatuongezea huko mbele ya safari ili tukawalinde kwa kusema mwacheni akina Ndugu X na Y wakapumzike basi kwisha mchezo.

Hakika,waovu wanatafuta ngao ya ushindi,wanatafuta ngao ya kujikingia,katika hili m.kwere nampongeza kwani amethubutu kuwaza sana akaona karata zote hazichangiki ila hii itampa ngao,watu tunaletewa hoja ya tukio nasi tushanshangilia,kwa ufupi hii ni next series toka pale magogoni ikiwa na waandishi wa script wachafu na wanamweka stering wao sokoni sasa na kwenye location!!! So sad mazafanta!!
 
Zitto
Tunanjaa, tunaumwa, hapa dawa Hakuna, Maji tabia, mavazi yametatuka tatuka, jua kali, kiduka cha jiran hapa mchele2300, hili la urais twaona Kama umevimbewa, sasa unabeua na kutoa mashuzi, jamani mmeomba ubunge, tumewapa, mkainua vidole hewan tukawakubalia, mkaita pipos tukaitika pawa, bado hamuwezi tusaidia, tukiwapa urais c mtatutia vidole machoni
 
Nionavyo mimi hata kama nia hiyo anayo, kuna haja gani ya kuitangaza leo! Maana yake anataka wanachama wagawanyike makundi, kuanzia sasa, wanaomuunga mkono, na wale ambao wanaona Dk Slaa aliwakilisha vyema na hivyo anastahili kuendelea kushika bendera ya chama, labda "mungu akiamua vinginevyo"
Nionavyo mimi, kama kauli hii ya Zitto ilikuwa na dhamiri ya kukigawa chama, basi atakuwa amekosea mikakati kwani angetoa kauli hiyo mwanzoni au katikati ya 2015, hapo kweli ndio angekigawa chama na mpasuko wake ungekuwa haugangiki kirahisi. Lakini kwa kuwa ameitoa sasa na kama chama kitameguka kwa sababu hiyo, basi chama kina muda mrefu wa kuponya makovu hayo hadi kufikia 2015. Lakini zaidi, mtu akisoma maneno haya ya Zitto: "Hata hivyo kazi hii hata kama naitaka ni lazima wenye nchi waamue kunipa kazi hii. Ni lazima kwanza Chama changu kiseme wewe ndio mwanachama unaestahili kuifanya kazi hii..... Kuitaka tu haitoshi". (Msisitizo kwenye nyekundu).

[/QUOTE] kuporomoka kwa umaarufu aliokuwanao Zitto hapo awali kabla ya kuanza kujiingiza katika matukio yaliyotishia kuvuruga chama, kama lile la kugombea uenyekiti na mara nyingi kuwa na msimamo tofauti na chama tena adharani, mfano kuhsiana na mapendekezo ya kuuzwa kwa mitambo ya Dowans, na ukaribu wake na Makamba jr ambaye kwa bahati mbaya, intelligency (kama wanavyomsifia) haiwezi kunifanya nimwamini, na kwa bahati mbaya sitamwamini hata rafiki yake[/QUOTE].

Hapa kuna masuala mawili: 1. Kwa maelezo yako na pengine ndivyo ilivyo, "ubunifu" wa Zitto unamharibia mwenyewe zaidi kwa "kuporomoka umaarufu" na wala sio kukiporomosha chama, kwani kama alivyosema mmoja hapa, CDM itasonga mbele hata bila ya Zitto, Slaa wala Mbowe kwani CDM ni chama cha watu na sio chama mtu. 2. Bado inaonesha Watanzania tumeganda katika mawazo kuwa "mpinzani wako ni adui wako", kwa maana yeyote aliye upande wa pili wa itikadi yao (wengine huingiza hata ukabila na dini), hupaswi kuwa rafiki yako. Zitto kama kijana wa umri wa Manyika, Mdee, Jr. Makamba, Nape, Ridhwan na wengine wengi, hawapaswi kuchukiana kama watu bali kushindana kwa sera, wanaweza kuwa marafiki na bado wakawa wapinzani. Kwa nini hatuchukui mfano wa wachezaji wa mpira? Nadharia yangu, "ukitaka kumjua na kumshinda mpinzania wako kuwa karibu yake, umjuwe ili iwe rahisi kupambana naye."
 
Kiongozi, tatizo hapa sio kukumbushana. Zitto sio mwanachama wa kawaida CHADEMA. Huyu ni naibu katibu mkuu wa CHADEMA na naibu kiongozi wa upinzani bungeni. Akiwa kama kiongozi kwa priority yake kwa week hii ya mwisho ya uchanguzi Arumeru ni nini? Angepata hasara gani kama angeleta huu mjadala mara baada ya Arumeru.

Kwa bahati nzuri siku hizi wananchi tunapata taarifa zaidi kuliko huko zamani. Habari za huyu bwana mdogo zitawa-dissapoint wengi, tumalize kwanza uchaguzi. Ukiona mtu anakimbilia Ikulu kwa nguvu kubwa ni lazima uulize ni kwa nini? Hii Haraka ya Zitto inatokana na nini?

Mkuu mambo ya Arumeru yanaendelea, Udiwani Kirumba unaendelea, kule kigamboni mambo yanaendelea, uchangia wa CDM unaendelea na mambo ya siasa zingine yanaendelea. Hivi wana Arumeru wakisikia kuwa Zitto ana nia ya kugombea Urais 2015 hatawampigia kura Nassary? Kama hawatampigia kura ni kwa nini? Mimi naamini haya mambo yanaweza kuendelea bila kuathiri kura za Nassary Arumeru, vinginevyo useme kuna issue nyingine.
 
Kwani kuna ubaya kwa Zitto kugombea urais? ni haki yake kikatiba, na chadema ni chama cha kidemocrasia ilani ya chama chetu haimzuii Zitto kufanya hivyo.

Ilani ya chama chenu 'CCM' inafanyaje kazi Chadema wakati wewe Magamba.
 
Hii ngoma imekuwa ndefu sana nipeni fursa kuweka SUMMARY,

  • Wenye busara wamemshauri Zitto pamoja na nia yake nzuri ya kutaka kuwa rais aendelee kusoma alama za nyakati ili wakati ukifika aingie ulingoni akiwa na nafasi nzuri kushinda/ kuchaguliwa na chama chake
  • Pro CCM members wamefurahia sana uamuzi huu wa Zitto, hii imewapa mashaka makubwa sana Pro CDM members kwamba kwa nini akina Ritz, Topical, Geniusbrain nk wamfurahie Zitto katika nia yake ya kugombea against chama chao? Kuna ujumbe mzito sana behind this scene...
  • Wengine wameegemea kwenye age ain't nothing but a number kwamba ujana au uzee sio ishu sana kwani kuna vijana tumewaona ni wahuni kama Adam Malima na pia kuna wazee wengine hawana busara kama Wassira. Cha muhimu ni kuwa na sifa na uwezo wa kukabiliana na matatizo yaliyopo hapa nchini na sio changamoto kwa kuwa changamoto hata zisipotatuliwa hakuna wa kulaumiwa but matatizo kama ajira kwa vijana na umaskini lazima yamalizwe na rais ajaye, Na Zitto amesema anayajua vizuri sana
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom