Zitto: Ndio ninautaka urais

Zitto: Ndio ninautaka urais

Status
Not open for further replies.
Zitto na kuunga mkono naamini dhamira yako ni sahihi
Kama umri ni tija tungetegemea maajabu na si vituko kama tunavyoshuhudia kwa mkapa na m.kwere wake
 
Watanzania basi angalau tuwe tunafanya kazi za kutupa kapiriensi katika mambo ya utendaji. Unamaliza shule. Unaingia kwenye siasa na unataka urais. Lini tunapata rais aliye na uzoefu wa viwanda, biashara au uchumi?
 
Tuna tatizo la kufagilia watu kishamba ndio maana watu uhishia kujiona special, Zitto asimami wala si hata nusu ya mchambuzi kisiasa tazama walipo kwenye ufahamu wakijamii kuhusu hawa wanasiasa wawili. Ndio Khali.
 
Na kwa cdm huyu ndio mtu anae faa kuwa Rais. Wengine wote wakina M & S Company wana tamaa tu za madaraka. Nawaomba wana cdm muungeni mkono Zitto na apitishwe na chama

Mimi namkubali Zito kuwa kiongozi mwenye umakini wa hali ya juu, lakini dhana inayojengeka hivi sasa ya kudhani kila kiongozi mzuri ni lazima awe katika ngazi ya urais siiungi mkono! Mtazamo wangu kiongozi mwenye kuleta mabadiriko anatakiwa kutoka katika chama chenye dhamira ya kufanya mabadiriko, ambamo wabunge wake, madiwani, pamoja na wafuasi wake wote wataamua kuyaendea mabadiriko. Na wala si msimamo wa mtu mmoja. Tunayashuhudia yanayotosha kuwa mafundisho. Kiongozi anakuwa na dhamira ya kufanikisha jambo lakini anakosa uungwaji mkono wa kutosha kutoka kwa wahafidhina wa kwenye chama chake au jamii. Katika mazingira kama hayo ni rahisi sana Rais kugeuka DIKITETA. Ninaipenda mno kazi anayoifanya Zito hivi sasa ya kuipa challenge Serikali kwa kuukosoa utendaji usiofaa wa Serikali na kutoa shule pana kwa uma kuujua udhaifu wa serikali kwa upana wake katika sekta mbalimbali.

Hilo ndilo linalomjengea Heshima hivi sasa na kumpa umaarufu. Sitashangaa umaarufu huo ukipungua sana baada ya kuupata urais. Umaarufu aliokuwa nao JK kabla ya urais si huu alionao leo!
 
Napenda kijana awe Rais, lakini kama katiba itabadilishwa ili kijana awe madarakani (Rais), itashindikana nini kuibadili ili 'kijana huyuhuyu (au wenzake)' akiwa 'mzee' aendelee kuwa Rais....???hapa lazima kuthink 'BIG'!
 
ZITTO KABWE ANAFAA KUWA RAIS. Kijana ana Vision ya kuleta mabadiliko!
 
Zitto ni kiongozi mzuri anafaa. Lakini mbona anapokuja na hoja kama hizi huzipitishia mbali ambako magwiji wa uchambuzi hawafiki? Kwa nini huwa hadondoki na thread moja kwa moja hapa JF watu tukamiminika nayo kuliko kuletewa kutoka wapi sijui huko wakati naye anapatikana hapa hapa. Au anawagwaya wakuu wake kwa kuwa nao wamo humu?
 
Zitto anafaa walau kuanzia 2025 atakuwa amepikwa na kukomaa vizuri.Kwa hivi sasa ni nafasi ya Dr Slaa.Dr Slaa kwa sasa hana mbadala ndani ya CDM.Ni kujilisha upepo kudhani kuna mtu mwingine atapitishwa kugombea Urais zaidi ya Dr wa ukweli walau kwa sasa.CDM ina vijana wengi na hakika huko Mbeleni kina Zitto na Mnyika na wengine ni hazina kubwa ya chama

This is true.
 
Kamwe Slaa hawezi kuwa rais wa nchi hii amin usiamini. Vile vile Slaa hana muda mrefu wa umaarufu baada ya Uchaguzi mkuu wa Chadema mwakani. Kuna wapya wanaenda kuibuka usiowatarajia. Zitto ni pandikizi la CCM lakini hata Slaa vile vile ameanza kuonesha udhaifu wa kuingia ubia na Kikwete. Awali alipinga kuwa hamtambui Kikwete kama rais halafu leo anajipeleka Ikulu kwa huyo aliyemkataa mwanzoni, huu ni unafiki mkubwa. Bora Mbowe au Tundu Lissu mana Slaa amepanga Ukatibu mkuu urithiwe na Lissu wakati muda huo Zitto naye anauhitaji.
 
Duh maneno mazito sana haya toka kwa Zitto. Hapa ndipo ninapomkubali Zitto kwa kujenga hoja. Anasema kama Chama chake na watu watakubali iwe hivyo na iwe na kama hawatakubali na isiwe. Haya ni maneno yanayoashiria demokrasia na wala si yale maneno ya kwameba hii ni zamu ya fulani na fulani kwa sasa hana nafasi! Pia ni vyema mtu kujitokeza hadharani na kusema nautaka uongozi ili apimwe mapema na siyo kuutaka huku ukijijengea mitandao ya siri ndani ya chama. Kama wengine ndani ya chama nao wajitokeze hadharani kama Zitto ili watanzania kwa ujumla wao wawapime. Kama CDM itachukua dola basi rais wake atakuwa Rais wa watanzania wote hivyo ni haki y watanzania wote kuwajadili. Hivyo hivyo hata hao wa CCM wanaoutaka urais wajitokeze hadharani tuwajue. hakuna dhambi kujitokeza.
Suala la umri pia nadhani liko sawa; miaka 40 ni sahihi kabisa kwa mtu kuiongoza nchi huku akiwa na akili changamfu na uwezo wa kupambana na changamoto zinzoikabili nchi. Kwani kijana akiwa rais atawauwa wazee, wazee si watakuwepo na watakuwa wakitoa ushauri? Kuna ubaya gani? Mbona JKN alianz kutuongoza akiwa na umri chini ya miaka 40. Zitto jipambanue na endeleza nia yako ya kuomba ridhaa ndani ya chama na kwa watanzania. Na hata kama January naye anataka ajitokeze. Kila la kheri.
 
Mimi namkubali Zito kuwa kiongozi mwenye umakini wa hali ya juu, lakini dhana inayojengeka hivi sasa ya kudhani kila kiongozi mzuri ni lazima awe katika ngazi ya urais siiungi mkono! Mtazamo wangu kiongozi mwenye kuleta mabadiriko anatakiwa kutoka katika chama chenye dhamira ya kufanya mabadiriko, ambamo wabunge wake, madiwani, pamoja na wafuasi wake wote wataamua kuyaendea mabadiriko. Na wala si msimamo wa mtu mmoja. Tunayashuhudia yanayotosha kuwa mafundisho. Kiongozi anakuwa na dhamira ya kufanikisha jambo lakini anakosa uungwaji mkono wa kutosha kutoka kwa wahafidhina wa kwenye chama chake au jamii. Katika mazingira kama hayo ni rahisi sana Rais kugeuka DIKITETA. Ninaipenda mno kazi anayoifanya Zito hivi sasa ya kuipa challenge Serikali kwa kuukosoa utendaji usiofaa wa Serikali na kutoa shule pana kwa uma kuujua udhaifu wa serikali kwa upana wake katika sekta mbalimbali.

Hilo ndilo linalomjengea Heshima hivi sasa na kumpa umaarufu. Sitashangaa umaarufu huo ukipungua sana baada ya kuupata urais. Umaarufu aliokuwa nao JK kabla ya urais si huu alionao leo!
Mkuu kuna tofauti kubwa kati ya umaarufu wa Zitto na JK. Zitto ameonyesha kuokosoa serikali na kujenga hoja zinazokubalika, sijui JK alijenga hoja gani zilizompatia umaarufu ukilinganisha na Zitto.
 
Ndugu zangu. Naomba msome makala nzima kabla ya kuchangia. Msichangie kwa kusoma kichwa cha habari tu. Hii ni makala nimeandika kama majibu kwa makala ya mwanazuoni mmoja kuhusu umri wa Urais.

Nimesema wazi, kuutaka Urais na kuupata ni mambo mawili tofauti. Kwanza lazima chama changu kiniteue. Kama chama kikiona bado lazima nikubaliane na chama. Kama chama kikiona kuna mwanachama mwingine ana uwezo zaidi yangu lazima nimwunge mkono huyo. Hata kama chama kikiniteua lakini wananchi lazima wakubali. Kwa hiyo unaweza kuutaka Urais lakini usiupate!

Pili nimejibu hoja za ubaguzi, hatari na matabaka za mwanazuoni huyo. Ni vizuri MoD akachukua makala hiyo na kuiweka juu kabisa ili watu wachangie jambo walilolisoma.

Miye nitaweka makala hiyo kwenye blog yangu zittokabwe.com

Swali kwa zito & pro Zito plus mamluki wa ccm- je kwa sasa ina maana haujaona mgombea yoyote anayefaa zaidi yako??? Umekuwa ni mshabiki mkubwa sana wa panafricanisim kama Mwalm /yerer na umekuwa una kili Nyerere ni role model kwako-e unasemaje kuhusu onyo la mwalm Nyerere kuwa tuwaogope watu wanaokimbilia ikulu?? Kwa sasa naomba niishie hapo tu ndugu japo nina mengi!!
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Mwanzoni nilifikiri Zitto alikuwa ameandikia article kwa unknown news media. Lakini gazeti la Mwananchi Jumapili limeandika hii habari kwa kina na according to this paper ni kwamba Zitto alifanya nao mahojiano! Infact kule Mwananchi Sunday Zitto more explicity kuwa 2015 anautaka urais!

Shida niliyonayo hapa ni timinig. Kwanini Zitto ameamua kuwa kwa sasa mjadala unaofaa ni kuhusu mikakati yake ya kupata urais wakati anajua kuna uchaguzi huko Arumeru? Amebadilisha public dabate kabisa kwanini?
 
Mkuu Nyerere alipohutubia pale Kilimanjaro hotel alisema watu wanaoutaka urais wajitokeze mapema ili watanzania wawapime. Pia alikosoa mfumo wa CCM wa kukaa kwenye halmashauri kuu na kutoa majina matatu na siku hiyo hiyo yanapigiwa kura na wajumbe wa mkutano mkuu bila hata kuwapa wajimbe hao fursa ya kuwapima. Nyerere hakukataza watu kujitokeza ila iliwaonya wale wanaojitokeza kwa hila na hasa wakiwa wanatumia pesa.
 
Kuna watu wengine bana yaani wao wanata muda wote tuwe tunajadili uchaguzi wa Arumeru mashariki tu na Ubaya wa CCM........... HAIWEZEKANI.

Maisha mengine lazima yaendelee jamani, hizi habari za kusema ukileta hoja nyingine zaidi ya uchaguzi wa Arumeru mashariki eti ni kudivert attension za watu mimi naona ni yakipuuzi sana.

Nahakika wapiga kura asilimia 99.9 ya wakazi wa Arumeru hajui kitu chochote kinachoendele humu JF zaidi yetu sisi wa Kutoka nje ya Arumeru na wanaokaa nje ya nchi huko
Sasa hii dhana ya kudevert inakuja vipi hapa? hivi tunadhani tukidivert ndio labda itaisaidia CDM au CCM kushinda?

Acheni watu wajadili mambo yanayojiri bana, hauwezi kusimamisha mijadala ya matukio yanayojiri au kugundulika sasa eti kwasababu kuna uchaguzi Arumeru

VINGINEVYO ITAKUWA NI KAMA TUNAPASISHA KUWA HILI NI JUKWAA LA CDM TU KUPIGIA KAMPENI CHAMA CHAO.........maana zimeanzishwa Sredi nyingi tu sana humu kuhusu CCM na watu wanafunguka kweli kweli lakini huwezi sikia eti una divert attension
 
Mwanzoni nilifikiri Zitto alikuwa ameandikia article kwa unknown news media. Lakini gazeti la Mwananchi Jumapili limeandika hii habari kwa kina na according to this paper ni kwamba Zitto alifanya nao mahojiano! Infact kule Mwananchi Sunday Zitto more explicity kuwa 2015 anautaka urais!

Shida niliyonayo hapa ni timinig. Kwanini Zitto ameamua kuwa kwa sasa mjadala unaofaa ni kuhusu mikakati yake ya kupata urais wakati anajua kuna uchaguzi huko Arumeru? Amebadilisha public dabate kabisa kwanini?
Mkuu nadhani Zitto amekumbushia tu. Nakumba 2010 wakati anaomba kura kule MWandiga aliwaambia wazi wazi wapiga kura wake kwamba hiyo ni mara ya mwisho anaenda pale kuwaomba kura za ubunge, akirudi atakuwa akiwaomba kura za Urais. Pia mkuu uchaguzi wa Arumeru unasimamisha mambo yooote hapa nchini? Yaani watu wanatakiwa wakiamka ni Arumeru wakila ni Arumeru? Twende navyo kwa pamoja Arumeru na mambo mengine pia.
 
mi sio mwana CMD ila zitto akigombea hakyamama nampa kura yangu . hii itaondoa manee kuwa CMD ni chama cha wachaga na wakristo.
 
Mimi namkubali Zito kuwa kiongozi mwenye umakini wa hali ya juu, lakini dhana inayojengeka hivi sasa ya kudhani kila kiongozi mzuri ni lazima awe katika ngazi ya urais siiungi mkono! Mtazamo wangu kiongozi mwenye kuleta mabadiriko anatakiwa kutoka katika chama chenye dhamira ya kufanya mabadiriko, ambamo wabunge wake, madiwani, pamoja na wafuasi wake wote wataamua kuyaendea mabadiriko. Na wala si msimamo wa mtu mmoja. Tunayashuhudia yanayotosha kuwa mafundisho. Kiongozi anakuwa na dhamira ya kufanikisha jambo lakini anakosa uungwaji mkono wa kutosha kutoka kwa wahafidhina wa kwenye chama chake au jamii. Katika mazingira kama hayo ni rahisi sana Rais kugeuka DIKITETA. Ninaipenda mno kazi anayoifanya Zito hivi sasa ya kuipa challenge Serikali kwa kuukosoa utendaji usiofaa wa Serikali na kutoa shule pana kwa uma kuujua udhaifu wa serikali kwa upana wake katika sekta mbalimbali.

Hilo ndilo linalomjengea Heshima hivi sasa na kumpa umaarufu. Sitashangaa umaarufu huo ukipungua sana baada ya kuupata urais. Umaarufu aliokuwa nao JK kabla ya urais si huu alionao leo!

Kwa mimi ninayeufahamu utendaji mbovu wa serikali, kulielezea hilo kwangu hakunishawishi nimu envy zitto, labda nimwambie, wakikusanyika wanaojidhani ni wajanja, piga uwa garagaza atakuwepo mjinga wa wajanja hao, isije ikawa yeye ndiye!!!!!!
 
Swali kwa zito & pro Zito plus mamluki wa ccm- je kwa sasa ina maana haujaona mgombea yoyote anayefaa zaidi yako??? Umekuwa ni mshabiki mkubwa sana wa panafricanisim kama Mwalm /yerer na umekuwa una kili Nyerere ni role model kwako-e unasemaje kuhusu onyo la mwalm Nyerere kuwa tuwaogope watu wanaokimbilia ikulu?? Kwa sasa naomba niishie hapo tu ndugu japo nina mengi!!

Zitto si mwana panafrikanist, ni oppotunist, kwa jk niliwaambieni mkaziba masikio, narudia kuwaambia, mara hii ni zitto.
 
mi sio mwana CMD ila zitto akigombea hakyamama nampa kura yangu . hii itaondoa manee kuwa CMD ni chama cha wachaga na wakristo.

Lengo lenu linafahamika!!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom