Zitto anataka kusaliti CHADEMA?

Zitto anataka kusaliti CHADEMA?

Status
Not open for further replies.
Sina imani siku nyingi na huyu jamaa na naendelea kutokuwa na imani naye, hope soon his true colours will show, kwani hata rafiki wa kweli hujulikana wakati washida, sasa kama walipiga kura na wakakubaliana kuwa waingie na kutoka na ulikuwa ni uamuzi wachama, je ni kwanini yeye aligomea huamuzi wachama? Au ndio alitegemea kuwa chama kitamchukulia hatua na amejitamba kuwa yupo tayari kwahilo.
JE CHADEMA WANAWEZA KUMCHUKULIA HATUA? MANA AMIKIRI KUWA ANASTAHILI ADHABU NA ANASUBIRI UHAMUZI WA CHAMA NA YUPO TAYARI KWA HUAMUZI WOWOTE. JEURI HII ANATOA WAPI?
 
My advice to Zitto, what happens in Vegas stays in Vegas.
 
1. munapenda sana kuchukulia jambo moja kama ndio tathimini ya mambo yote ya chasema yanavyotakiwa yawe kwa vile kila mtu anaona yeye ndio mtathimini wa kila jambo chadema inafanya watu wanajia mbalimbali za kupeleka ujumbe au kupinga jambo kwenu nyie mungeona la maana kama 2. wangeitisha maandamano nvhi nzima munasemaje pale tume yenyewe inapokiri kutoa takwimu za kura zisizo sahihi watu waa ajabu sana nyakati za ndio mzee zilikwisha chadema wako sa hihi na njia muafaka kabisa wanastahili pongezi kwa ujasiri wao 3. hilo la zitto ni mambo yao ya ndani wewe na mimi hatuwezi kufikia hitimisho kwa hiyo 4. nakushauri usidhani wanatafuta cheap popularity kupishana mawazo hata mume na mke huwa wanapishana baba na mwana pia ndio dynamics za maisha


- Well sasa kwenye namba moja unataka kukimbia kivuli cha kawaida hapa JF, huwa linatokea tukio moja na tafsiri mbali mbali kwa vile leo tafsiri inagusa chama chako una tatizo na tafsiri nyingi za kitendo cha Mh. Zitto, kusema hadharani waliyoyafanya in the private kama chama! Vipi bro si ndio mwendo wa JF huu, kama vile kususa kwa wabunge zinazotolewa hapa si ndio tathmini zote au?

- Wangeitisha maandamano ya nchi nzima na wananchi wengi wakaitikia sasa hivi taifa zima tungekua tunaongelea kubadili katiba mkuu, sio tena kujadili kwa nini Mh. Zitto, hakubaliani na msiamo wa chama chake, chama chenye wabunge 46 tu sasa kama kati yao kuna wabunge wengi tu ambao hawakubakubaliani na msimamo wa chama na wanajisema wneyewe to the public, unataka JF tufanye nini tuogope kusema tunachokiona na tunachokiamini? Vipi mkuu mbona unataka sana kukimbia kivuli chenu mwenyewe Chadema?

- La Mh. Zitto lingekua ni la ndani ya chama basi asingelileta to the public, maana akishalileta huku ni haki yetu wananchi kulitathmini kama tunavyofanya hapa mkuu hatuvunji sheria hapa tunakata ishus tu kama zinavyokuja!

- Ya Cheap popularity umeyaleta wewe mkuu ni wapi imesemwa ya Cheap popularity, unasema enzi za ndio mzee zimeisha na wewe unajaribu kulazimisha hiyo hiyo kutoka kwetu yaani ndio mzee, vipi mkuu unakataa unachokifanya? toa tathmini ya ishu mkuu kama huna si unaona wapo wengi wenye nazo, tubishane kwa hoja sio kutishana!, taifa ni letu wote mkuu!



William.
 
Wandugu,

Suala lililo kubwa la kulijadili ni impact ya Chadema walkout!..........CCM wapende wasipende hili suala limewaathiri.............i.e. limeamsha taswira mpya kabisa kw abaadhi yao (CCM) kuhusu siasa za Tanzania mbeleni................Majambazi CCM ni wajanja wanatumia maoni ya Zitto kuzima HOJA KUBWA ya kasoro za Uchaguzi..................sasa naona watu hapa JF are taken away na rhetoric za CCM kuhusu demokrasia iliyoko Chadema.........which has nothing to do with them Majambazi.........

Please people........tusidanganyike na majambazi CCM..................hakuna cha ajabu kutofautiana kimtizamo.........Ndani ya CCM hakuna demokrasia ya KWELI...............kumbuka wale viongozi waliokuw ana mitazamo tofauti.........wako wapi leo hii......sitaki kuwataja majina.......

Notwithstanding the above.............Zitto ni kiongozi mzuri........ni aina kiongozi "vuvuzela type"......atasema kile kinachomsibu.......kuna wakati binafsi nakubaliana naye e.g mosi ni suala la Kafulila na pili ni suala lake la kugombea uenyekiti wa Chadema...............kwenye hayo mambo ndio Chadema walitakiwa waonyeshe Demokrasia imekomaa ndani ya chama chao..........having said that STILL Zitto anahitaji mtu makini wa kumshauri kabla hajaongea hadharani......ili kuona effect kwa chama chake kwakile atakachoongea.............

Kuna wakati sikubaliani naye....e.g suala la manunuzi ya mitambo ya Dowans....siwezi kumsahau kwa hili.....na mpaka kesho nitaendelea kumshangaa..........aina ya compromise anayoweza fika .........which in bigger terms ni RISK kubwa sana kw aTaifa kwa kiongozi kuwa na compromise za aina ile.............na ndio maana nasisitiza anahitaji kuwa guided.........ni wakakti umefika kwa viongozi wetu kuwa na washauri katika nyanja mbali mbali...........

Sikukubaliana naye (Zitto) pia kwenye suala la Uongozi wa Tanesco i.e. eti Dr. Idriss kama vile ndiye "Muarobaini" wa TANESCO...........another compromise kutoka kwake...........imagine kuona mtu kama Dr. Idriss anafaa....mtu anayehusishwa na tuhuma za RADAR.....damn! no wonder......... hata sasa ana-compromise na results za NEC!!!!!!!!!........results "mguu wangu" .......

Narudia.......wana JF mustakabali wa Taifa ni jambo MUHIMU zaidi kuliko compromises za Zitto............hivyo tuendelee kupambana na hoja za ku-challenge mapungufu ya katiba yetu na Majambazi yaliyopora madaraka...............
 
jk kasema baraza lake la mawaziri litaangalia uadilifu zaidi bila kujali chama wala dini, itakuaje mkisikia zito kapewa wizara na JK???? nadhani mjadala huu utakuwa umeisha.
 
Zitto wewe ni kiongozi wa chama na kama mlipiga kura na maamuzi yakafikiwa kwa mujibu wa kura hizo, hustahili kutuambia hayo unayotuambia leo bali kusimamia maamuzi ya kikao hicho na kuelezea msimamo wa walioshinda.

Hata kama ni demokrasia, kama kiongozi unapaswa kusimamia maamuzi ya chama.

Mnaoshabikia upuuzi huu wa Zitto kwa kisingizio cha demokrasia ndani ya CHADEMA hamjui maana ya uongozi.
Naanza kujiuliza vizuri ni kwanini john mnyika bado anakaimu madaraka ya Zitto ilhali yeye zito yupo.
 
Hivi CHADEMA haina msemaji? Manake hizi kauli za mtu mmoja mmoja ndizo zinazoleta mgawanyiko. Pamoja na kwamba CHADEMA walipiga kura, suala hilo ni suala la ndani ya chama ambalo halikupaswa kuzungumzwa na mtu mmoja mmoja bali na msemaji wa chama tena kwa protokali...! Haikupaswa Zitto kuja na kusimama kwenye TV na kuanza kujielezea yale ambayo walishaamua kwa pamoja, na haswa kwa nia ya kujisafisha au kufanya wengine waonekane walikosea...!

With this background, bado nahoji sana credibility ya Zitto na aina ya Siasa anazofanya...! Amekua anajisahau sana na kuleta siasa za ki-ulaya kwa kufikiri kujitangaza ovyo ovyo misimamo yake (kwenye facebook, twitter etc) itamfanya aonekane ni bora zaidi.

Kauli kama hizi ambazo zinaonyesha wazi wazi mgawanyiko wa CHADEMA (kwa nia ya kujitangaza ili aonekane yeye alikua na msimabo bora zaidi ya wengine) zinapunguza credibility badala ya kuongeza credibility ya CHADEMA...! Hapo tu ndio Zitto pamoja na umahiri wake anapojisahau...! It will cost him in a long run...!
 
zito wewe ni kiongozi wa chama na kama mlipiga kura na maamuzi yakafikiwa kwa mujibu wa kura hizo, hustahili kutuambia hayo unayotuambia leo bali kusimamia maamuzi ya kikao hicho na kuelezea msimamo wa walioshinda.
Hata kama ni democrasia,kama kiongozi unapaswa kusimamia maamuzi ya chama.
Mnao shabikia upuuzi huu wa zito kwa kisingizio cha demokrasia ndani ya chadema hamjui maana ya uongozi.
Naanza kujiuliza vizuri ni kwanini john mnyika bado anakaimu madaraka ya zito ilhali yeye zito yupo.
Hili nalo neno
 
Hivi CHADEMA haina msemaji? Manake hizi kauli za mtu mmoja mmoja ndizo zinazoleta mgawanyiko. Pamoja na kwamba CHADEMA walipiga kura, suala hilo ni suala la ndani ya chama ambalo halikupaswa kuzungumzwa na mtu mmoja mmoja bali na msemaji wa chama tena kwa protokali...! Haikupaswa Zitto kuja na kusimama kwenye TV na kuanza kujielezea yale ambayo walishaamua kwa pamoja, na haswa kwa nia ya kujisafisha au kufanya wengine waonekane walikosea...!

With this background, bado nahoji sana credibility ya Zitto na aina ya Siasa anazofanya...! Amekua anajisahau sana na kuleta siasa za ki-ulaya kwa kufikiri kujitangaza ovyo ovyo misimamo yake (kwenye facebook, twitter etc) itamfanya aonekane ni bora zaidi.

Kauli kama hizi ambazo zinaonyesha wazi wazi mgawanyiko wa CHADEMA (kwa nia ya kujitangaza ili aonekane yeye alikua na msimabo bora zaidi ya wengine) zinapunguza credibility badala ya kuongeza credibility ya CHADEMA...! Hapo tu ndio Zitto pamoja na umahiri wake anapojisahau...! It will cost him in a long run...!
I still believe Zitto was sending a message. To whom I do not know. Kwamba yeye hakuunga mkono hoja ya kususia hotuba ya Kikwete.
 
kuna mtu mmoja katuhabarisha kuwa TBC1 wamemnukuu ]Zitto Kabwe akieleza yaliyojiri kwenye kikao cha ndani cha chadema kilichokubaliana kwa wingi wa kura kuwa watoke nje ya bunge wakati rais alikihutubia............... na mhabarishaji ameendelea kuwa naibu katibu mkuu huyo wa chama alienda mbali kiasi cha kusema wazi kuwa yeye alikuwa miongomwa waliopinga ndio maana hakuhudhuria kikao kile.............

mi naona kuwa .............. pengine wakati mwingine ukongwe wa ccm utaonekana una maana yake na chadema wasiogope kunakili kutoka huko ili kuimarisha chama hasa nidhamu ndani ya chama....................... japo inasemekana kuna nidhamu ya woga ndani ya ccm lakini inasaidia kwamba mwenyekiti akishasema neno wanachama wengine wote wanasiamam nyuma yake japo wengine hawakukubaliana na msimamo ule.......... na hii ni itifaki rahisi kabisa kwama huwezi kutofautiana na kiongozi wako mbele ya kandamnasi............... tena kwa yale ambayo ulishapewa fursa ya kuyaongea ndani ya vikao halali vya chama..................

huyu zito ni moja ya matatizo makubwa ya chadena............. sasa gaya mambo gani ya kuzungumza na media ?........................... badala ya kutumia fursa ile kufafanua nia na madai ya chama chake yeye anafafanua 'ufa" wa chama chake!!!!!!!!!!! tena huyu ni naibu katibu mkuu wa chama chake............... huyu mtu ana grade ya kushika madaraka hata ya huo ubunge????..........sasa hapo kuna uongozi wa pamoja kweli???......... time will tell.................
 
nadhani chadema wanapaswa kupongezwa kwamba uamuzi wa kutoka nje haukuwa wa mtu mmoja bali ilitumika njia ya kidemokrasia ya kupiga kura, na sio shinikizo la m/kiti au mgombea uraisi, na maamuzi ya wengi yanakuwa ndio maamuzi ya wote, tunapaswa kuwapongeza kwa kufata njia za kidemocrasia ktk kufikia maamuzi ya chama. watanzania wanataka katiba mpya, binafsi ninawaunga mkono, harakati hizi za kudai mabadiliko sote tumeshuhudia ni wakina nani wameziasisi, ccm wanadai watawafukuza bungenpi (maele
 
harakati hizi za kudai mabadiliko tumeshuhudia ni wakina nani wameziasisi, ccm wanadai watawafukuza bungeni (maelezo ya chiligati) lakini naomba watz tuendelee kuwaunga mkono siku si nyingi watageuka (ccm) na kujifanya wao ndio walioiasisi hoja ya katiba mpya, si mnakumbuka hoja ya epa? walisema wangemfikisha mahakamani slaa, lkn walipoona watz wameielewa nao wakairukia na kujifanya ndio wameianzisha eti ni yao na wapinzani wameirukia, tusubiri tutaona.
 
Mheshimiwa William
Heshima sana Mkuu!
Mara nyingi nimeona unatumia NENO WABUNGE 46 TU. UNAMAANISHA NINI???
 
Me nadhani katika hili Zitto anakosea wajibu wake wa kuwa naibu Msemaji mkuu wa Kambi ya Upinzani. Ni bora saa zingine akawa anapima maamuzi anayoyachukua. Huwezi kuelezea umma unakutegemea eti ni maamuzi yako wakati wenzako wanafanya analysis ya impact ya wanachokifanya. Huu si mda wa kuirudisha nyuma Tz kwa madai kuwa ni maamuzi ya kukubaliana kutokubaliana.

Tufanye utafiti na si kukwepa lawama. Kama upo ndani ya chama by the way, unakubaliana na misingi ya chama sasa huu kutoka nje ya chama na kukimbilia kwenye vyombo vya habari kunatoka wapi. Kwanza, is Zitto Msemaji wa chama? nadhani huyu Mh anapaswa kuangalia vizuri namna ya kuhandle media. Media people brought Lowasa and Kikwete into power and they are now almost killing them except those owned by Rostam
 
Mjumbe anapokuwa kwenye kikao ni ruhusa kabisa kupinga jambo wakati wa majadiliano lakini jambo hilo likihitimishwa kwa kura na ikionekana wengi ndiyo wanaounga mkono basi huo ndiyo unakuwa msimamo wa chama na kila mwanachama anapaswa kuutetea. Sasa kama Mhe. Zitto bado anaendelea kuupinga nje ya kikao, basi huo utakuwa ni utovu wa nidhamu na lazima akemewe na chama kupitia vikao vyake halali. Alichopaswa kueleza Zitto (kama ilikuwa ni lazima aeleze) ni kusema kwamba wakati wa kikao alikuwa na msimamo tofauti lakini uamuzi wa kikao ndiyo anaouheshimu na kuutetea. Hiyo ndiyo GHARAMA ya demokrasia.
 
Chadema kisogope kupoteza jimbo kwa ajili ya wanachama wasiokuwa na msimamo na kuvuruga chama.

Kumbumbuka mficha maradhi kifo kitamuumbua
.
 
Mjumbe anapokuwa kwenye kikao ni ruhusa kabisa kupinga jambo wakati wa majadiliano lakini jambo hilo likihitimishwa kwa kura na ikionekana wengi ndiyo wanaounga mkono basi huo ndiyo unakuwa msimamo wa chama na kila mwanachama anapaswa kuutetea. Sasa kama Mhe. Zitto bado anaendelea kuupinga nje ya kikao, basi huo utakuwa ni utovu wa nidhamu na lazima akemewe na chama kupitia vikao vyake halali. Alichopaswa kueleza Zitto (kama ilikuwa ni lazima aeleze) ni kusema kwamba wakati wa kikao alikuwa na msimamo tofauti lakini uamuzi wa kikao ndiyo anaouheshimu na kuutetea. Hiyo ndiyo GHARAMA ya demokrasia.

Mkuu umeongea vizuri sana, Chadema hawakuona umuhimu wa kukurupuka kwa hili jambo, ilibidi watumie demokrasia ya kupiga kura na maana ya kupiga kura ni kuwa kulikuwa na misimamao tofauti, kwa waliokubali na wasiokubali hiyo move ilikuwa ni haki yao kidemokrasia, na tukumbuke kuwa hilo zoezi lilikuwa ni la siri, lilikuwa ni la wabunge tu labda na viongozi wengine wa juu
Swali la kujiuliza ilikuwaje Zitto aende kwenye vyombo vya habari kuliongelea hilo suala ambalo ahlikuwa la Public, hapa Zitto anatuonyesha yafuatayo:

1) Zitto anataka kuonyesha kwa baadhi ya "watu wake (Rafiki zake)" kuwa yeye hakuhusika, lakini swali linakuja watajuaje kuwa yeye hakuusika na zoezi lilikuwa ni la siri? jibu ni lazima aende kwenye vyombo vya habari

2) Zitto anajionyesha kuwa yeye yupo juu ya kila mtu kwenye Chama, kama chama kina viongozi wa juu kuliko yeye na labda ndio wangepaswa kulizungumzia hilo swala kwa nini yeye ndio alichukua uamuzi wa kuelezea kilichotokea? je aliutaarifu uongozi kuwa anaenda press kuongelea hilo swala?

3) Zitto anazidi kujitoa uaminifu wake na imani yake katika Chama, inatia hofu sana, kama siri za Chama zinafikia point ya kuwa published, watu watamwamini vipi Zitto?, je kweli anaweza kutunza siri za chama za ndani zaidi?
 
- Mkuu kweli ninakusoma sawa sawa, eti kuwafukuza walio na mawazo tofauti na yako si ndio yamelifikisha hili taifa lilipo sasa, au?


William.

Great Thinker William;
Zitto kutofautiana na wenzie sio tatizo, na Chadema walijua wanatofautiana kwa hilo na ndio kisa wakaamua Demokrasia ichukue mkondo wake kwa kupiga kura
watu wanachomlaumu Zitto ni kwenda public na kuongea issue za siri za kichama, na kama Chadema walitaka kuliongea hilo kuna Viongozi wakuu kuliko Zitto

Please elewa hapo, hata kama ni wewe kiongozi ungemfanya nini mtu anayeku-bypass
 
zitto ameongea vizuri sana... tatizo humu jamvini tunataka mambo ya upinzani yaende kama mechi ya kinondoni muslim na tambaza

na hayo ya kupingana yangetokea ccm kesho ungesikia mtu katolewa chamani

Acid,
Hoja la wale wanaompinga Zitto katika thread hii, na mimi nikiwepo sio maneno ya Zitto,la hasha! Tatizo ni kwa nini Zitto akaamua kwenda kuyasema hayo ya ndani kwenye media??

kwasababu walipiga kura na wengi wakashinda basi Zitto kama kiongozi wa chama alipaswa kubeba hoja ya wengi, na hakukuwa na haja ya kueleza kuwa yeye ni mmoja kati ya waliopinga. Hii kwangu mimi naona itamfanya Zitto apate credit kwa baadhi ya wananchi hasa kwa walioko nje ya chama ila kwa walioko ndani ya chama Zitto ataonekana kama ni msaliti kwa kutoheshimu maamuzi ya chama(Uamuzi wa wengi kwa kura)
 
Me nadhani katika hili Zitto anakosea wajibu wake wa kuwa naibu Msemaji mkuu wa Kambi ya Upinzani. Ni bora saa zingine akawa anapima maamuzi anayoyachukua. Huwezi kuelezea umma unakutegemea eti ni maamuzi yako wakati wenzako wanafanya analysis ya impact ya wanachokifanya. Huu si mda wa kuirudisha nyuma Tz kwa madai kuwa ni maamuzi ya kukubaliana kutokubaliana
Tufanye utafiti na si kukwepa lawama. Kama upo ndani ya chama by the way, unakubaliana na misingi ya chama sasa huu kutoka nje ya chama na kukimbilia kwenye vyombo vya habari kunatoka wapi. Kwanza, is Zitto Msemaji wa chama? nadhani huyu Mh anapaswa kuangalia vizuri namna ya kuhandle media. Media people brought Lowasa and Kikwete into power and they are now almost killing them except those owned by Rostam

I think Zitto has to go...amaekuwa ni virus ana ataharibu mikakati ya chama..Wamruhusu ajiunge CCM..I recall comments zake toka wakati Kafulila alipofukuzwa kazi CHADEMA,pili wakati wa uchaguzi wa mwenyekiti wa chama,thirdly ni jinsi anavojiona yuko above CHAMA..sasa he has to go...hatuwezi kuwa na team yenye beki anayekuwa hakabi mipira inapita tu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom