Gosbertgoodluck
Joined
Likes
32

Profile posts Latest activity Postings About

 • Mbaneingoma Zom
  Kaka umepatia hawa jama gahawa na wao, wao na gahawa mpaka inawafanya wasifikirie mambo kwa kina kabla ya kuyaongea. ENDELEA KUELIMISHA SISI WOTE NI NDUGU NI MITAZOMO TU NDO INATOFAUTIANA.
  Gosbertgoodluck
  Watanzania tuwe macho na magazeti na vyombo vingine vya habari. Kampeni ya kumpamba Kikwete tayari imeanza. Ujanja waliotumia kwenye uchaguzi ndiyo huohuo walioanza kuutumia hivi sasa. Bila shaka, sasa hivi watanzania tumefumbuliwa macho. Kimsingi, Kikwete nchi imemshinda. Anaendesha nchi kiusanii sanii tu na zaidi ya yote serikali yake imejaa wapiga domo tu. Hatuwezi kuendelea kuongozwa na mtu ambaye mpaka sasa hafahamu sababu za nchi yetu kuwa maskini. Shime watanzania, mwaka kesho lazima tumbwage chini arudi uraiani aendelee na maisha ya usanii na propaganda zake.
  Gosbertgoodluck
  CCM: GARI LISILOTENGENEZEKA

  Hivi sasa ni takriban miaka 40 imepita tangu nchi yetu ipate uhuru kutoka kwa Waingereza. Miaka 40 si michache kwa nchi yenye viongozi wenye upeo wa kuona mbali na kuwa na mikakati ya kuwakomboa wananchi wake kutoka kwenye lindi la umaskini. Hata hivyo, jambo la kusikitisha ni kuwa cha kinachojiita cha mapinduzi kimeshindwa kabisa kuwaongoza watanzania na kuwaletea maendeleo. Hili ni jambo la aibu sana. Awali, watu wengi walikuwa wanajiuliza inakuwaje nchi hii iwe kwenye orodha ya vinchi maskini Duniani wakati imejaliwa na Mwenyezi Mungu kila aina ya rasilimali kuanzia madini, wanyama na kubwa zaidi ardhi?!?!?!? Jambo la kutia moyo ni kwamba angalau sasa watanzania tumebaini kuwa kumbe mojawapo ya vikwazo vikubwa vya maendeleo ya nchi yetu ni UFISADI unaofanywa na viongozi waandamizi wa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi. Misingi mizuri ya kiuchumi kuanzia sekta ya kilimo hadi viwanda vidogovidogo na vikubwa imebomolewa na viongozi hao hao waandamizi wa Serikali. Kwa maneno mengine, pamoja na sababu mbalimbali zilizo nje ya uwezo wetu watanzania, kama nchi, umaskini wa Tanzania umechangiwa kwa kiasi kikubwa na Chama kinachojiita cha Mapinduzi. Kwa maoni yangu, watanzania kuzungumzia maendeleo chini ya CCM ni kuota ndoto za mchana.

  Hayati Mwl. Nyerere aliwahi kusema kwamba CCM anaipenda lakini si zaidi ya Tanzania. Maneno hayo aliyatamka wakati fulani akielezea uchafu uliokuwa ukifanywa na viongozi wa Serikali pasipo kukemewa na Chama. Mwalimu Nyerere alionesha masikitiko makubwa kwa jinsi chama kilivyokuwa kimepoteza mwelekeo na kuacha misingi yake muhimu. Leo hii chama cha CCM kipo kwenye hali mbaya zaidi ya wakati ule mwalimu alipokuwa akitoa maoni yake. Watanzania sasa Mungu amewafumbua macho na kubaini kuwa hiki si Chama Cha Mapinduzi bali ni Chama Cha Majambazi (Mafisadi) wanaodidimiza hali ya maisha yao kiuchumi na hata kisiasa na kijamii. Kila mwaka wa uchaguzi ukifika, watanzania tunadanganywa kwa kauli za kututia moyo; kauli za kutufanya tuvute subira. Lakini kikishinda uchaguzi basi hali inakuwa mbaya zaidi na zaidi. Fikiria, mbwembwe za Kikwete na mtandao wake. Eti sijui "maisha bora kwa kila mtanzania", mara ooohh, "tumaini lililorejea", n.k. Wote huu ni udanganyifu mkubwa na usanii wa kupindukia. Maisha ya watanzania yameendelea kudidimia siku hadi siku wakati wao wakiendelea "kutanua". Kila kukicha tunasikia Rais wetu yupo Marekani, Uingereza, Japan, n.k. Muda anaokaa Rais nchini mwake kushughulikia wapiga kura wake ni mfupi kuliko anaotembelea nchi za wenzie zenye "maziwa na asali". Yeye anadhani wenzie walijenga nchi zao kwa kutembeza bakuli kama anavyofanya yeye. Hayati Mwalimu Nyerere alisema na nanukuu "kazi ndiyo msingi wa maendeleo. Nchi maskini haiwezi kuendelea kwa msingi wa fedha. Nchi maskini haiwezi kujitawala kama inategemea misaada kutoka nchi za nje", mwisho wa kunukuu. Viongozi wetu wakiongozwa na Kikwete wanajidanganya na kupoteza muda mwingi “kutembeza bakuli” badala ya kutulia nchini mwao wakishirikiana na wananchi kufanya kazi kwa bidii na kujiletea maendeleo. Wanadhani maendeleo yataletwa na mabilioni ya akina MCC kumbe hata tukijaziwa fedha nyingi kiasi gani pasipo kufanya kazi kwa bidii na maarifa ni bure tu.

  Ndiyo maana nasema CCM imepoteza mwelekeo na hivyo haina jipya la kuwasaidia watanzania kuachana na umaskini. Chama kimekuwa kama gari kuukuu; lisilotengenezeka, ambalo kutolitumia ni faida zaidi kuliko kulitumia. Njia pekee ni kulitelekeza na kuangalia uwezekano wa kuwa na gari jingine imara linaloweza kutufikisha kwenye nchi ya “maziwa na asali”. Watanzania tusiogope kuleta mabadiliko ya kisiasa nchini. Tunaweza kuongozwa na chama chochote cha siasa. Wenzetu Wakenya, Wamalawi, Wazambia, Waghana, n.k., mbona wameonesha njia!!?? Kwa nini tusikiadabishe hiki Chama Cha Mafisadi.
 • Loading…
 • Loading…
 • Loading…