Zitto anataka kusaliti CHADEMA?

Zitto anataka kusaliti CHADEMA?

Status
Not open for further replies.
Siku zote nasema namkumbuka Zito toka Daruso, hajabadilika, sidhani kama atabadilika. Huyo ndio Zito.

Kama kura ilipigwa na wengi wakashinda, basi uamuzi huo unawabana wote, na ni lazima kila mmoja ashiriki! Hainiingii akilini kuwa uamuzi wa demokrasia unatekelezwa na baadhi na wengine kuacha. Collective responsibility bana! Zito sijui ni utoto au ni nini! Tena hakupaswa kwenda kwenye vyombo vya habari kueleza yaliyojiri na msimamo wake binafsi. Yeye ni Kaimu Katibu Mkuu, maamuzi ya chama ni ya wote, na hata hakubaliani nayo, ambalo ni jambo la kawaida, hana budi kuelezea msimamo wa wengi na kuacha haya ya ubinafsi.

Zito anafahamu yeye ni target number one, when it comes to partisan politics kati ya CCM na Chadema. He has to be careful in his statements as the CCM wata-manipulate hizo statements and in the end kufifisha nguvu za Chadema. Ni aibu huyu kijana hafikirii matokeo ya statements na vitendo vyake! Akumbuke ameshakua sasa, sio kila kitu anachokiona kinafanywa na Baba na Mama anakiweka hadharani!
 
Zitto Kabwe, ana misimamo yake na anajisimamia katika hayo. Hahitajii kumsikiliza mtu akishakuwa na jambo lake. Yaweza kuwa kweli amelewa sifa kama usemavyo lakini sidhani. Hebu nenda pale Mwanga Kigoma na uliza vijana Kabwe ni mtu aina gani toka utotoni utapata jibu. Sidhani kama Zitto aweza kuwa Amani Kaburu hawa watu wanatofautiana sana. Hebu pita pale Ujiji na uliza kuhusu Amani kwa watu wa makamo.

Hebu tumpe muda Zito Kabwe, kwani kuna mambo yamejificha huenda ndiyo yanayosababisha tushindwe kumjua Zitto. Kuna jambo kuu, kwa sasa hatulioni lakini punde litaonekana. Kwa mfano Zito anaonambali kuliko wengi wa Viongozi Chadema, ndio maana anafikia hatua ya kujitoa ili wengine wafaidike, lakini pia wakati mwingine analazimisha apate wengine wakose. Hahitajii kutufurahisha au kutuudhi.

Hakuwa Radhi kuona anatoka bungeni Mh. Rais akianza kuhutubia ili asije akashuhudia kiongozi wake nae anasusiwa kama kisasi na wabunge wa CCM :teeth:

Sioni wala sitoona ajabu (Kwa viongozi wengi walioko UPINZANI wakirudi CCM - MAJI HAYASAHAU BARIDI)😱
 
Zitto kachakachuliwa, anaogpa kutemwa kwenye kamati ya madini, hummer lake atalijazaje mafuta kupiga starta tu lita tano

ZITTO kabwe ni Naibu Kiongozi wa upinzani bungeni.......kama nimemuelewa alisema uamuzi wa kutoka waliupigia kura na uamuzi ulioshinda ndio msimamo wa chama .....sasa suala la kuingia ndani lilibaki uamuzi wa mmbunge...kwani kuna saababu nyingi za kutoingia ikiwamo dharura yeyote......
wanaopandikiza ugomvi CHADEMA hawataweza...kwani ingekuwa hawana msimamo baada ya kura wangeingia wote halafu wale ambao hawakupendelea kutoka ...wangebaki ndani pindi wenzao walipotoka.....mawazo huru ni msingi wa chama chochote cha kidemokrasia ....na kutambu msimamo wa kichama ni jambo linaloleta heshima kwenye chama...

CHADEMA shikamaneni wakati huu kuliko wakati wowote ule.....kulikoni RAis Alishajiapiza bungeni kuwa atatumia "gharama" yeoyote ile "kupambana" na wanaovunja "umoja".....wana JF wa ukweli huu sio wakati wa kumchimba mpambanaji yeyote ndani ya CHADEMA....kwani wao ni watu makini tofauti zikitokea watazimaliza kidemokrasia na si kwa kufukuzana.

Lingine nashauri kwenye baraza kivuli la upinzani ni vema milango ikaendelea kuwekwa wazi kwa vyama vidogo vya upinzani ie NCCR na TLP....na wabunge wa CUF hasa kutoka bara,,,,,..ni wazi kuwa its now official kuwa CUF zanzibar imejeuka ASP......ILIVYOUNGANA NA CCM MWAKA 1977..au ZPP ,UMMA na ZNP zilivyoungana na ASP ...ni historia tu itakuwa inajirudia ....na tusitegemeee wabunge kutoka ZANZIBAR kwa hali hii waje watetee wananchi wa Kigoma au BOMBA MBILI.....kwa kuwa CHADEMA wanao wabunge wa viti maalum toka zanzibar UMOJA wa kitaifa utakuwapo tu kwenye baraza kivuli!!
 
Mara nyingi sana watu kigoma huwa hawana msimamo na siyo watu wa kuwaamini sana, na pia wana tatizo la kujisahau, huyu MNAFIKI ZITO, hajui kuwa, akiwa nje ya CHADEMA yeye ni mtu wa kawida kabisa, na thamani yake ni neno CHADEMA, Uongozi itabidi wagundue huu unafiki wake mapema la sivyo utakuja kuwa cost
 
Lets wait and see!
Lakini waswahili wana Msemo kuwa dalili ya mvua ni mawingu.
Mhe. Zitto mara nyingi ameonyesha kuwa zaidi ya chama chake kwa mambo mengi,mimi naamini Chadema inautaratibu wa nani anatakiwa kusema nini,wapi ,kwanini na lini.
Namshauri Mhe.Zitto kupeleka Bungeni hoja au kumsapoti Mch.Mtikila kukata rufaa dhidi ya kesi ya Mgombea binafsi maana anachokionyesha ndicho kinacho mfaa.
Mifano ya hii ipo mingi ikiwa pamoja na hili la kutokuwepo Bungeni ili watoke wote wakati raisi wa NEC akianza kuhutubia.
 
zitto ameongea vizuri sana... tatizo humu jamvini tunataka mambo ya upinzani yaende kama mechi ya kinondoni muslim na tambaza

na hayo ya kupingana yangetokea ccm kesho ungesikia mtu katolewa chamani
si jamvini pekee ndugu. ni tatizo letu watanzania! TUNATAKA TUNACHOKITAKA NA HATUTAKI TUSICHOKITAKA, mara nyingi tunashindwa KUKUBALIANA KUTOKUBALIANA. Huku tukiimba kwamba tunajenga demokrasia. Sidhani kama tunaweza kujenga Demokrasi bila kukubali kupingana, bila kuwa wawazi, kwanini iwe siri? Iwe siri ili iweje? Zito Kabwe amefanya kitu sahihi kabisa na ninamuunga mkono kwa hilo. Alipata kujibu alipohojiwa "...Maslahi ya taifa kwanza!" Ndicho alichoangalia. Je kwanini ahukumiwe kwa hilo? Chadema si baba wala mama yake.
 
ZITTO KABWE ni mnafiki, na anaependa kuweka maslahi yake mbele wala sio ya chadema. yeye ndie aliihujumu CDM huko Kigoma mpaka ikakosa wabunge wengi. ni mtu anaependa sana kujitanua yeye kama yeye huku akijiona ni Mungu mtu pale chadema.

Anapenda sana makundi,fitna na chuki zisizo na msaada kwa CDM. ushauri wangu zitto hamia CCM ili ujiweke wazi usikae cdm huku unahujumu chama hiyo ni usaliti nao ni dhambi kubwa kwa mungu.
 
Zitto anahujumu CDM, wewe ndio Naibu katibu mkuu husimamii maamuzi ya chama je unafaa kweli? acha unafiki na kujiona wewe ni Mungu mtu.kama vipi timkia ccm ukawaulize akina Lamwai,Kabourou,Hiza.
 
Haya na huyu ni SHIBUDA!!!

Alisema kwa kutambua udhaifu huo, hata yeye hakuingia bungeni, lakini jioni alihudhuria hafla ya kupongeza wabunge wote iliyofanyika kwenye viwanja vya Bunge.

"Nilikwenda kwenye hafla hiyo kama mbunge wa Maswa Magharibi kwani kila mbunge alialikwa na nilishaamua kuhudhuria, kwa kuwa hakuna chama kilichobaguliwa kwenye mwaliko.

"Ikumbukwe mnapokutana katika hafla kama hizo hamwendi pale kusaka ulevi, bali kujadili masuala yanayohusu maslahi ya wananchi mkiwa mmetuliza fikra zenu na kubadilishana mawazo," alisema Shibuda ambaye kabla ya kuhamia Chadema, alikuwa CCM.

Alisema wakati anahama CCM hakukosana na mtu yeyote na pia chama hicho ni ndicho chenye uasilia wake kisiasa na kwamba kuhama Msikiti si kuacha Uislamu.

"Sijakosana na mwana CCM yeyote kwa jambo lolote, nami nilikwenda pale kuonana na Watanzania wenzangu, kama ambavyo Waislamu na Wakristo wanavyokaa pamoja bila matatizo," alibainisha Shibuda.

"CCM na Chadema tunahitajiana kwa ajili ya kujenga fikra endelevu kwa maslahi ya Watanzania," alisema Shibuda na kuongeza kuwa ni vizuri uamuzi wa jambo ukatumia zaidi busara badala ya harakati.

Source: HABARILEO
 
Zitto anahujumu CDM, wewe ndio Naibu katibu mkuu husimamii maamuzi ya chama je unafaa kweli? acha unafiki na kujiona wewe ni Mungu mtu.kama vipi timkia ccm ukawaulize akina Lamwai,Kabourou,Hiza.
:redfaces: na hao walikuwa CDM??? kuweni na uvumilivu wa kupingana.

Zito Kabwe yuko sawa kabisa, wala hajaihujumu CDM bali CHADEMA inajimaliza yenyewe :embarrassed:
 
- Mkuu kama ninakuelewa kura ilipigwa ndani ya Chadema kufuata Demokrasia, sasa ni Demokrasia gani hiyo inayomnyima Kiongozi msaidizi wa Upinzani bungeni kutoizungumzia hiyo Demokrasia to the public? Demokrasia haifanywi kwa siri mkuu wala kuzuiwa waliohusika kutosema to the public, rekebisha hilo mkuu!

- Kilichofanyika ilikuwa ni Demokrasia au siri? Chagua moja mkuu!

William.

kaka William naomba nikujibu kama hutojali.
Hapa hatuongelei issue hii kama ni mambo ya siri ya chama au demokrasia ya uwazi na kuongea na media, issue hapa ni kwanini Zitto ajipambanue kuwa yeye alipinga wazo hilo wakati yeye ni kiongozi wa chama ambaye anatakiwa asimamie maamuzi ya chama? Anataka kumfurahisha nani?
Kama alipinga kwa kuona hakubaliani na maamuzi ya wengi,ni bora angejiuzulu uongozi kuonesha dhamira yake.
 
Zito amekuwa ni mtu mwenye misimamo ya peke yake kwenye chama kwa mambo mengi mno.Hilo ni sawa ili mradi ana sababu.Lakini kwa nini amekuwa akiongelea masuala ya ndani ya chama kwenye vyombo vya habari?Zito anafikiri yeye ni muhimu kuliko chadema!Chama ni muunganiko wa watu wenye lengo moja.Hata kama kwenye mchakato wa kuwa na lengo moja kulikuwa na mawazo tofauti,yote hufa baada ya tamati kufika,na hakuna mwenye uwezo wa kuongelea hayo ila ni chama.Kama zito ameongea hivyo kwa niaba ya chama sina neno.Lakini kama ameongea kama zito basi kuna walakini!Watu wenye mapenzi mema na chadema mumtazame zito kwa jicho la3 na mtagundua kitu.Nakama kuna kipengele ndani ya chama amekiuka nashauri aonywe na apewe adhabu stahiki,asiachwe!Yeye sio mkubwa kuliko chadema.Bila chadema zito asingefika hapo alipo,na bila zito chadema ingefika hapo ilipo.
 
Ni vema sana kuipongeza CDM kwa uamuzi wa kutoka bungeni, uamuzi huo ndio uliotuwakilisha umma tuliowatuma bungeni. Mmekataa ushindi wa JK kwa uwizi wa kura. dunia nzima inajua hilo ndio maana EU wakataa kutoa ripoti mpaka baada ya miezi mitatu kuogopa kuchochea vurugu. Naamini pia ndio msimamo wa CDM.

Kuhusu haka kazito Chezo amesama vema kuwa "

I think Zitto has to go...amaekuwa ni virus ana ataharibu mikakati ya chama..Wamruhusu ajiunge CCM..I recall comments zake toka wakati Kafulila alipofukuzwa kazi CHADEMA,pili wakati wa uchaguzi wa mwenyekiti wa chama,thirdly ni jinsi anavojiona yuko above CHAMA..sasa he has to go...hatuwezi kuwa na team yenye beki anayekuwa hakabi mipira inapita tu
"

Zito ni hatari sana, mtu asiyefaa. Mimi nilikosa imani siku nyingi tena nawashangaa kumpa nafasi ya uongozi, wakati mnamwelewa fika!. Sasa uchaguzi umepita mtoseni kabisa. Huyu ni virus, kafisadi in making. Baada ya kulishwa kahawa ya akina Rostam alipokuwa anajificha kweneye yadi ya Habari cooperation alianza mambo ya ajabu ajabu kama kuitetea dowans, na kuwa mwiba kwa chama chenu. Tazama atawashawishi wajumbe wenu kama alivyosema kuwa yeye na wenzake hawakuhudhuria kikao cha bunge. Hii itwaletea sna matatizo.

Jipendeni wenyewe kwanza, vote this hypocrite out ajiunge na CCm ama sivyo msiba wakujitakia hauna kilio

You will loose nothing, just vote him out and you will enjoy
 
I dont see an issue (hapa tuna make a mountain out of a mole hill) kutokukubaliana ni kawaida kura zikapigwa wengi wakashinda thats normal lakini i think Zitto angekaa kimya tu there is no need awaambie vyombo vya habari what went behind the scenes

kazi kwelikweli wanazidi kuparaganyika huku wakiwapa ccm nguvu. tupo wengi tunaoweza kuimarisha chadema wala sio zitto tu, wakati mwingine ukiwa maarufu kwenyechama unaweza kutumia kama loop hole ya kupenyeza misimamo yako na sio ya chama,mbo ccm wakikaa hatu sikii wanayo yajadili,hata walipo mtoa sitta walifanya huko na hawakuwambia wa tz .sasa kujifanya kama yeye Zitto ni bora kulikowenzake haipunguzi lolote tz inawapenzi wengi sana wa chadema,na tuko tayari kufanya kazi na chadema asijifanye yeye ni bora sana hapo chadema.
 
Zitto anasema raisi ni alama ya bunge, sijamuelewa anamaana gani hapo? Kwani yeye zitto sio alama ya bunge? Mbona anataka kushusha mamlaka na uhuru wa bunge? Tunaambiwa mihimili 3 inayojitegemea ni bunge,mahakama na serikali, raisi ni mkuu wa serikali hana mamlaka ya kuingilia uhuru wa bunge, kama raisi anamamlaka juu ya bunge basi hakuna haja ya kuwa na bunge ni kupoteza ela bure. Nimepoteza imani kwa zitto kama anafaa kutetea hoja za maslahi ya taifa, nahisi anapenda kunyanyua juu umaarufu wake binafsi na maslahi yake,ni bora atangaze nia ya kwenda ccm tujue kimoja.
 
I dont see an issue (hapa tuna make a mountain out of a mole hill) kutokukubaliana ni kawaida kura zikapigwa wengi wakashinda thats normal lakini i think Zitto angekaa kimya tu there is no need awaambie vyombo vya habari what went behind the scenes

Kama hakuwaambia vyombo vya habari ata-score points vipi?
 
Zitto anasema raisi ni alama ya bunge, sijamuelewa anamaana gani hapo? Kwani yeye zitto sio alama ya bunge? Mbona anataka kushusha mamlaka na uhuru wa bunge? Tunaambiwa mihimili 3 inayojitegemea ni bunge,mahakama na serikali, raisi ni mkuu wa serikali hana mamlaka ya kuingilia uhuru wa bunge, kama raisi anamamlaka juu ya bunge basi hakuna haja ya kuwa na bunge ni kupoteza ela bure. Nimepoteza imani kwa zitto kama anafaa kutetea hoja za maslahi ya taifa, nahisi anapenda kunyanyua juu umaarufu wake binafsi na maslahi yake,ni bora atangaze nia ya kwenda ccm tujue kimoja.
 
Tatizo jamani sisi wana jf tuking'ang'ania jambo hatutaki kushindwa,zito ameweka wazi yaliyojili ktk mchakato mzima wa kupiga kura,ameonyesha kuwa kunakosa lilifanyika na wanasubili maamuzi ya chama dume
nampongeza zito,siasa ipo hivyo,ikiona umekosa unasema na ukiona huna kosa unasema
tuendelee kuwaunga mkono wapambanaji na ipo siku tutakuwa pale na sio hapa tulipo sasa
mapinduziiiiii daimaaaa
 
kwa wenye akili watakuwa wamemuelewa zitto,CHADEMA OYEEEEEEE,Msimamo mwanzo mwisho hatuwezi lala nje kulinda kura zisiibiwe na hawa wezi,2015 tunalinda hadi za Rais pumbavuuuuuuuuuuuu
 
Zito amekuwa ni mtu mwenye misimamo ya peke yake kwenye chama kwa mambo mengi mno.Hilo ni sawa ili mradi ana sababu.Lakini kwa nini amekuwa akiongelea masuala ya ndani ya chama kwenye vyombo vya habari?Zito anafikiri yeye ni muhimu kuliko chadema!Chama ni muunganiko wa watu wenye lengo moja.Hata kama kwenye mchakato wa kuwa na lengo moja kulikuwa na mawazo tofauti,yote hufa baada ya tamati kufika,na hakuna mwenye uwezo wa kuongelea hayo ila ni chama.Kama zito ameongea hivyo kwa niaba ya chama sina neno.Lakini kama ameongea kama zito basi kuna walakini!Watu wenye mapenzi mema na chadema mumtazame zito kwa jicho la3 na mtagundua kitu.Nakama kuna kipengele ndani ya chama amekiuka nashauri aonywe na apewe adhabu stahiki,asiachwe!Yeye sio mkubwa kuliko chadema.Bila chadema zito asingefika hapo alipo,na bila zito chadema ingefika hapo ilipo.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom