Zitto anataka kusaliti CHADEMA?

Zitto anataka kusaliti CHADEMA?

Status
Not open for further replies.
Huyu jamaa ingawa ni kiongozi wetu lakini akiamua kutoka leo nitafurahi sana, ninachoomba Chadema iende naye taratibu wasimpe cheo kikubwa wala wasimfukuze ajiondoe mwenyewe, walikuwapo kina Kabouru enzi chama hakina mvuto atakuwa Zitto wakati chama kina vichwa vya uhakika, kwa busara za uongozi huwezi mlinganisha Zitto na Lissu.

Ye mwenyewe anahitaji kutumia busara na hekima sana na nadhani akigeuka nyuma atajifunza kwamba wananchi wanawaamini wao na hawataki kusikia hadithi hadithi wanataka kuona baada la hili la juzi nini kinafuata hizi hadithi hadithi wakati wake sio huu
 
Kikwete sasa hata akistaafu asahau UN au AU mission za kusuruhisha migogoro itokanayo na uchaguzi. Hawezi kusema lolote kwani ataulizwa mbona wewe ulichakachua hadi wabunge wako wakatoka nje?
 
Kwa hiyo ungependelea na sisi Tanzania tuwe na utawala wa mtu mmoja dikteta kama Rwanda au? Katiba itasaidia kutuondolea watawala wabovu kama hawa tulio nao sasa hivi ndani ya CCM. Hii ni hatua ya kwanza kuleta maendeleo endelevu. Sasa hivi CCM wanasema (Makamba) kwamba lazima wao washibe kwanza ndio waanze kufikiria matatizo ya wananchi. Tanzania hatuna Kagame, katiba itatusaidia kuweka mfumo wa kuwapata watawala bora na kuwaondoa mamlakani wanapoboronga. Bila hiyo tutaendelea kusikiliza ngonjera tu za akina Makamba.

Najua unajua hapo juu umeandika shudu,, Ni lini Makamba aliwahi kusema hivyo?? Acheni uchochezi, ongeleeni maswala na sio watu kila saa. Acheni ukabila,
 
Nashukur kwamba umeprove huna uwezo wa kunihakikishia ni kwa nini Katiba ndio iwe national Priority yetu badala ya maendeleo? Na umeshindwa kunihakikishia ni jinsi gani katiba yetu inachangia kua nyuma kimaendeleo?? Umenidhihirishia ninaongea na mtu mwenye vidato vingapi. Ni wakati wa kuacha kuota, ni wakati wa kudiscuss vitu in reality. Si TZ tu, Africa kwa ujumla. Katiba ya tanzania haipo Msumbiji, Malawi, Zambia, Namibia, Congo, n.k. Nchi zote hizo ni maskini, unataka kuniambia ni Africa nzima ni masikini kwa sababu ya CCM na katiba ya Tanzania?? Think further my friend.

Lazima tubadilike, badala ya kua tunadiscuss ndoto, tudiscuss vitu vya kutuondoa kwenye umaskini. Tushikamane kwa pamoja kwa ajili ya kizazi kijacho. Nikuhakikishie kwamba mie sina tatizo la uelewa hata kidogo, ndio maana nimekataa kunyweshwa sumu na waroho wa madaraka na wafanya biashara ya Ruzuku. Hiyo analysis yako ndio hiyo hiyo nimekua nikiiona kwenye gazeti la tanzania daima. Think more than that, Katiba, katiba, utafikiri hiyo ndio inasimamia kilimo, viwanda, na uzalishaji kwa ujumla. Katika ni guide tu, kinachotakiwa ni strategies na mapendekezo mazuri ya kujenga. Sio kugoma kama watoto
Usijaribu kuidhinisha umaskini wa Tanzania wa
kujitakia ukasema eti ndio sayansi unayoijua wewe.Tanzania ambayo haijawahi kuwa kwenye vita imetawaliwa na madiikteta wa kati CCm watu wa pole na kila kitu kilichoko chini ya mbigu chenye kuleta tija kwa maisha ya mtanzania na bado tukawa zero kwa miaka yote hii halafu wewe ukataka ulinganishe na kongo wako vitani miaka zaidi ya 15 Ruanda wamechinjana juzijuzi hapa Malawa Kamuzi aliwakaba koo na bado wako zaidi yetu wee vipi Tanzania Daima ni gazeti lililosajiliwa na hata sina shida ya kulisoma kama msaafu na wala sio mhariri ukweli ni kuwa mawazo yako mgando ya kulinganisha mbofu kwa mbofu ndio yanayonifanya niamini kuwa sayansi ina formular ulizozitunga mwenyewe kwa kuishi kwenye ndoto ya uzumbukuku kwa kukumbatia ujinga wa kutrudisha nyuma kifikra
 
nadhani ni sehemu ya kujifunza siasa za demokrasia na nafasi ya upinzani. Tusiwe wakali sana.
 
Hiyo ndiyo sera ya Chadema?

Hon Zito ameng'amua kuwa uongozi wa Chadema umewehuka na mafanikio waliyoyapata, sasa ni kukurupuka kwa kwenda mbele.

Hon, If I may give an advice;
....achana na wasanii wa kisiasa. Mungu amekujalia talanta ya uongozi na tunakujua kuwa una uchungu wa dhati kwa nchi yako. You are our potential next president.

So go for real serious politics!

CCM is one of the living examples in that domain.
Usimpoteze mwenzako Zitto hawezi kumaliza hata mwezi mmoja CCM atafukuzwa, huko akiwa anaropoka ropoka hawamcheleweshi labda awe bubu kama kina Lwamwai kitu ambacho Zitto hakiwezi.
 
Usijaribu kuidhinisha umaskini wa Tanzania wa
kujitakia ukasema eti ndio sayansi unayoijua wewe.Tanzania ambayo haijawahi kuwa kwenye vita imetawaliwa na madiikteta wa kati CCm watu wa pole na kila kitu kilichoko chini ya mbigu chenye kuleta tija kwa maisha ya mtanzania na bado tukawa zero kwa miaka yote hii halafu wewe ukataka ulinganishe na kongo wako vitani miaka zaidi ya 15 Ruanda wamechinjana juzijuzi hapa Malawa Kamuzi aliwakaba koo na bado wako zaidi yetu wee vipi Tanzania Daima ni gazeti lililosajiliwa na hata sina shida ya kulisoma kama msaafu na wala sio mhariri ukweli ni kuwa mawazo yako mgando ya kulinganisha mbofu kwa mbofu ndio yanayonifanya niamini kuwa sayansi ina formular ulizozitunga mwenyewe kwa kuishi kwenye ndoto ya uzumbukuku kwa kukumbatia ujinga wa kutrudisha nyuma kifikra

Ipo siku utakuja kusoma maelezo yako na utajiona ulikua bado Bikra kifikra. Sitakubaliana na mtu yeyote anayedai kwamba Tanzania itapiga hatua zaidi ya hapo ilipo endapo CHADEMA wataingia madarakani. Nitakubaliana na mtu yeyote atakayesema Tanzania itasogea endapo tutafata strategy 1,2,3.. Hayo mawazo yako ya ki-uruho wa madaraka siwezi kuyashiba hata siku moja. Wewe mwenyewe ni shabiki wa CHADEMA lakini nina uhakika hujui chama chako kinaamini katika dini gani (Capitalism, socialim or Cetralists)? maana mnyika ni kiongozi wa muda sasa ndani ya chadema lakini hajui strategies za chama zake zina base wapi. Na ndio maana nakuahakikishia vyama vya CUF, CHADEMA, TLP, NCCR ni biashara za wachache wanaoishi kwa ruzuku. Lazima tuanzie squre one kwamba tatizo la kwa nini tuko maskini linatokana na mfumo wa soko la dunia. Na kama sisi tutaendelea kurumbania katiba badala ya kuface the reality, basi kazi ipo. Na inasikitisha kuona mtizamo wa vijana kama wewe uko hivyo.

Narudia tena, umeshindwa kuprove ni jinsi gani Katiba inatusababishia matatizo ki-uchumi, badala yake na wewe unaongea maneno ya porojo yaliyompa Dr Slaa kura kadhaa
 
Chadema ni chama makini sana chini ya viongozi makini sana hasa katibu wake mkuu na mwenyekiti. Viongozi hawa wamemlea huyo mtoto wao zitto na amefika hapo alipo. Wanachama wa chadema tunaamini watamchukulia zitto kwa upole japo mara kadhaa ameonyesha udhaifu wa ukomavu kisiasa na utovu wa nidhamu. Zitto uelewe sisi hatuna tatizo na msimamo wako katika kura yako ya kutokutaka kutoka nje ya bunge wakati wa hotuba ya rais. Sisi wasi wasi wetu kwako ni kule kutokuheshimu maamuzi ya walio wengi ndani ya kikao chenu cha siri. Maana kama ungeyaheshimu basi ungeliyachukulia kama ni maamuzi ya chama na kisha kufunga mdomo wako wakati demokrasia uliyoishiriki mwenewe ikitekeleza uamuzi wa wengi wape. Zitto nilikuamini sana huko nyuma lakini kwa hili la kuenda kwenye vyombo vya habari kwa nia ya kuthoofisha harakati zinazohitaji kuungwa mkono na kila mwenye kupenda katiba mpya na nec huru Tanzania nimefadhaishwa sana juu yako. Nisikufiche baada ya kuona wewe sasa ndio umekuwa lulu ya wana ccm na faraja ya kibano walichokuwa wamekipata baada ya wabunge wa chadema kutoka nje, nimekuchukia gafla. Sikuwahi kufikiri kafikia hali kama hii ila naomba Mungu anisaidie hasira hii nilioipata juu yako iondoke. Sina uhakika kama zitto umeishaoa ila kama bado nakushauri muda muafaka ndio huu wa wewe kupata msaidizi wa kukusaidia. Be blessed Zubeiry.
.
 
Wewe wala usijaribu kudandia treni kwa mbele,, Kasoro kasoro, nataka unitajia priority zetu 20 kwa sasa hapa nyumbani, ukianza na Afya, Elimu, barabara, maji, n.k ukishaorodheshwa vyote, naomba uniambie Katiba umeiweka namba ngapi. Thats my point, katiba ni maelekezo tu yaliyo kwenye vitabu, katiba haiendi viwandani au kwenye mashamba kuongeza kilimo. Fikiria zaidi ya hapo mdogo wangu
Wewe ni hopeless fulani unasema katiba ni karatasi tu haisaidii kweli wewe zimo? kwanza kachunguze expiry date ya akili zako naiona imeshapita, unailinganisha katiba na miradi ya barabara hujui hiyo miradi haiendi bila katiba rudi shuleni.
 
Waza maendeleo na toa strategy za kweli zinazoweza kutuondoa kwenye umaskini, acha kushabikia mchezaji wakati mpira wenyewe unasikilizia radio mbao (Lunyamila na mpiraaaaa gooooooooool, laaaaa). Pili, nashukuru kwa kunitukana ila sasa naomba ujibu swali langu kwa kutoa hoja kwamba ni kivipi Katiba inatusababishia uchumi duni?? Usitoe porojo maana huelewi hata ndani ya katiba kuna nini??
 
kuna jambo moja nimenotice miongoni mwa wachangiaji wa thread hii ni kuwa wengi wa members waliojiunga na JF baina ya august-november wamekuwa na maneno makali na lugha ya kejeli dhidi ya zitto, ilhali wengi wa waliojiunga zamani wamekuwa na mixed feelings ila lugha ni ya kistaarabu. sasa sijui hawa wanabodi wenzetu wageni wana nini vichwani mwao???

tukija kwenye mada, MIMI NINGEPENDA kumuunga mkono mheshimiwa zitto kabwe,kwani hata iweje JK ni rais wa tanzania, tutapiga kelele tutalia na tutaomboleza but nothing will change, ni sahihi tufanye mabadiliko ya katiba ,tuweke tume huru ya uchaguzi na mengineyo lakini bado rais wetu ni kikwete tu.
jamani sote tunakumbuka uchaguzi wa mwaka 2000 marekani, jimbo la florida lililoamua rais wa marekani, al gore na bush walivutana kwelikweli lakini bush alipotangazwa mshindi al gore alimpigia simu bush akampa hongera na nchi ikaendelea mbele, the democrats wala hawakususia chochote iwe bunge, sherehe wala baraza gani sijui ijapokuwa ilijiulikana bush aliingia madarakani kwa hila.

kwa hiyo mimi binafsi, sioni mantiki ya kususa, wakati mbunge huyohuyo ameapa kuitetea na kuilinda katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania, na ni katiba hiyohiyo iliyomuingiza kikwete madarakani!!!! huu ni wakati wa kujenga nchi.

vilevile zitto mimi naamini mara zote anazodaiwa kuwa analeta vurugu ni kuwa anajitahidi kutumia haki zake za kidemokrasiaaidha kugombea uongozi au kutoa mawazo yake na si kuwa mnafiki kama viongozi wengine au viongozi wa CCM ambao wanaweza kuwa wanapiga kelele lakini wanapopigwa mkwara basi wao huifyata mikia yao
 
Zitto Kabwe ameeleza kuwa ni kweli walipiga kura na kukubaliana watoke wakati Rais akizungumza, lakini wao walipinga na ndiyo maana aliamua bora asiingie ndani ya Bunge, amesema kuwa yeye kama Zitto na wenzake aliona ni bora kutoingia kuliko kuingia na kutoka wakati Rais ambaye ndiye alama ya Bunge na Amiri jeshi mkuu akiongeaa.

Kwa vile kutoka ulikuwa msimamo wa chama, basi yeye na wenzake wamekosea na hilo ni swala la Chama kwani wanaweza kuadhibiwa na chama kwa vile kura za kukubaliana kutoka ilishinda.

Zitto alisema kuwa wanasubiria hatma yake katika chama na kusema kuwa hiyo ndiyo gharama ya Demokrasia. Ila amekanusha kuwa jambo hilo lisifikiliwe ni mgawanyiko bali mtazamo tofauti wa mawazo.

Source: TBC 1 News Bulletin

Safi!! na hii ndo tunaita demokrasia makini, kwamba hata ndani ya chama mnaweza kutofautiana katika mitazamo
 
Waza maendeleo na toa strategy za kweli zinazoweza kutuondoa kwenye umaskini, acha kushabikia mchezaji wakati mpira wenyewe unasikilizia radio mbao (Lunyamila na mpiraaaaa gooooooooool, laaaaa). Pili, nashukuru kwa kunitukana ila sasa naomba ujibu swali langu kwa kutoa hoja kwamba ni kivipi Katiba inatusababishia uchumi duni?? Usitoe porojo maana huelewi hata ndani ya katiba kuna nini??
Wewe unayesema katiba ni karatasi haitusaidii hata nikikuelimisha ni kazi bure endelea na ujuha wako.
 
Zitto kachakachuliwa, anaogpa kutemwa kwenye kamati ya madini, hummer lake atalijazaje mafuta kupiga starta tu lita tano
 
Ipo siku utakuja kusoma maelezo yako na utajiona ulikua bado Bikra kifikra. Sitakubaliana na mtu yeyote anayedai kwamba Tanzania itapiga hatua zaidi ya hapo ilipo endapo CHADEMA wataingia madarakani. Nitakubaliana na mtu yeyote atakayesema Tanzania itasogea endapo tutafata strategy 1,2,3.. Hayo mawazo yako ya ki-uruho wa madaraka siwezi kuyashiba hata siku moja. Wewe mwenyewe ni shabiki wa CHADEMA lakini nina uhakika hujui chama chako kinaamini katika dini gani (Capitalism, socialim or Cetralists)? maana mnyika ni kiongozi wa muda sasa ndani ya chadema lakini hajui strategies za chama zake zina base wapi. Na ndio maana nakuahakikishia vyama vya CUF, CHADEMA, TLP, NCCR ni biashara za wachache wanaoishi kwa ruzuku. Lazima tuanzie squre one kwamba tatizo la kwa nini tuko maskini linatokana na mfumo wa soko la dunia. Na kama sisi tutaendelea kurumbania katiba badala ya kuface the reality, basi kazi ipo. Na inasikitisha kuona mtizamo wa vijana kama wewe uko hivyo.

Narudia tena, umeshindwa kuprove ni jinsi gani Katiba inatusababishia matatizo ki-uchumi, badala yake na wewe unaongea maneno ya porojo yaliyompa Dr Slaa kura kadhaa

Kama mimi ni muumini wa chadema manake nitakuwa nimeamua kutokana nakujua kwamba chadema inasimamia nini sitaingia chadema kama msukule
kama umekuja jamvini mimi nikutafsirie katiba maana yake nini basi hapo napenda nikwambie akili yako uchwara inakusumbua kwa sababu hujengi hoja ndio nyie ukiambiwa huu ni mkono wa kulia utaita kushoto kwa sababu ya mazoweq mulio lELEWA VIBAYA KWAMBA JAMII YA KITANZANIA INAYOKUWA NA MAONO NA IMANI TOFAUTI NA KWAKO HAWAFAI UMEPOTOKA SANA NADHANI DHANA YAKO NI YA KUJIKINGA ZAIDI ZAIDI YA KUKABILI HOJA NAKUMBUKA NIKIWA CHEKECHEA KULIKUWA NA WATOTO WALIKUWA NA TABIA KAMA YAKO
 
Najua unajua hapo juu umeandika shudu,, Ni lini Makamba aliwahi kusema hivyo?? Acheni uchochezi, ongeleeni maswala na sio watu kila saa. Acheni ukabila,
Makamba aliyasema hayo Tarime wakati ule wa uchaguzi mdogo. Kuna video yake vile vile unaweza kuiangalia nadhani phillipmogendi.blogspot.com. Siandiki shudu mimi. Lini kuwasema viongozi wa CCM umekuwa ukabila?
 
Nashukur kwamba umeprove huna uwezo wa kunihakikishia ni kwa nini Katiba ndio iwe national Priority yetu badala ya maendeleo? Na umeshindwa kunihakikishia ni jinsi gani katiba yetu inachangia kua nyuma kimaendeleo?? Umenidhihirishia ninaongea na mtu mwenye vidato vingapi. Ni wakati wa kuacha kuota, ni wakati wa kudiscuss vitu in reality. Si TZ tu, Africa kwa ujumla. Katiba ya tanzania haipo Msumbiji, Malawi, Zambia, Namibia, Congo, n.k. Nchi zote hizo ni maskini, unataka kuniambia na Africa nzima ni masikini kwa sababu ya CCM na katiba ya Tanzania?? Think further my friend.

Lazima tubadilike, badala ya kua tunadiscuss ndoto, tudiscuss vitu vya kutuondoa kwenye umaskini. Tushikamane kwa pamoja kwa ajili ya kizazi kijacho. Nikuhakikishie kwamba mie sina tatizo la uelewa hata kidogo, ndio maana nimekataa kunyweshwa sumu na waroho wa madaraka na wafanya biashara ya Ruzuku. Hiyo analysis yako ndio hiyo hiyo nimekua nikiiona kwenye gazeti la tanzania daima. Think more than that, Katiba, katiba, utafikiri hiyo ndio inasimamia kilimo, viwanda, na uzalishaji kwa ujumla. Katiba ni guide tu, kinachotakiwa ni strategies na mapendekezo mazuri ya kujenga. Sio kugoma kama watoto

Huyu Nyerereist amekuwaje akawa JF senior Expert member na utumbo huu? how? inakuwaje awe amepost posts 420 lakini amekuwa thanked mara moja tu? nadhani huyu ni junior member tu kama siye au ni mropokaji tu!
 
Jamani hili ni moja tu mnashtuka saa hizi, ZITTO NI KIBARAKA WA CCM. Mwenye masikio na asikie. Ni mtu hatari sana kwa CHADEMA.

nahisi kaahidiwa wizara ya nishati na madini na rafiki yake JK ili aivuruge chadema
 
Wengi wa members wapya wa JF walijiunga wakati wa uchaguzi ni UWT na Zitto ni point yao kwa kutaka kuisambaratisha CHADEMA! Wanachokonoa Chadema. Ni lazima wajue Chadema ina toa nafasi ya kutofatiana... si kama CCM kikipitiswa na Mwenyekiti na Mafisadi ni kama msaafu vile! Tumeona walivyomtosa Sitta! Chadema tusikubali kuwa na msimamo na mawazo ya ki-CCM kwamba kutofautiana ni uaini na uhalifu, si kweli! Tusikubali kuchongaanishwa na baadhi ya UWT ambao wametumwa na siasa za maji taka za CCM!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom