Zitto anataka kusaliti CHADEMA?

Status
Not open for further replies.

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
111,728
2,000
Zitto: Kuna njama

na Mwandishi Wetu
Tanzania daima


Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Kabwe, amesema chama hicho kimegundua kuwapo kwa njama mahususi zinazoendeshwa na baadhi ya watu wenye lengo mahususi la kuwasambaratisha.

Akizungumza katika mahojiano na gazeti hili jana, Zitto alisema njama hizo zinafanywa na watu hao ambao hakuwa tayari kuwataja ambao wamekuwa wakitumia baadhi ya vyombo vya habari.

"Tumegundua kuwapo kwa juhudi za makusudi za kutaka kutugombanisha CHADEMA. Hiki ni chama makini, kimezibaini njama hizo na kwa hakika hakiwezi kusambaratishwa na njama hizo," alisema Zitto.

Akifafanua, Zitto, ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, alisema kuwa wapo wanaotumia jina lake, wakilihusisha na matukio fulani, kwa lengo la kutaka kuonyesha kuwa yeye ni maarufu zaidi, au muhimu zaidi kuliko chama hicho.

"CHADEMA ndiyo imenipa umaarufu mimi… mimi si maarufu kuliko chama. CHADEMA ni taasisi, ni chama ambacho kina misingi ya uanzishwaji wake," alisema Zitto.

Akitoa mfano katika hili, alisema wakati alipoamua kugombea ubunge alikuwa ndiyo kwanza amemaliza masomo yake ya chuo kikuu na kimsingi kulikuwa hakuna watu waliokuwa wakimfahamu.

"…eti nilishinda kwa umaarufu wangu binafsi, si kweli. Niligombea ubunge nikitokea shule, sikuwa najulikana. Nilikuta grassroots network ya chama, hakikujengwa na mimi.

"CHADEMA ilijengwa na uongozi uliokuwepo, nilikuta uongozi intact (imara). Katika kila kijiji kulikuwa na uongozi na hata katika vitongoji vyote. Wakati naingia kugombea ubunge kulikuwa na wanachama wa CHADEMA wenye kadi wanaofikia 10,800 katika jimbo zima. Hawa sikuwatafuta mimi, niliwakuta na ndio waliofanikisha ushindi wangu.

"Katika mazingira kama haya utasemaje kuwa mimi ni maarufu kuliko chama wakati chama ndicho kimenipa umaarufu?" alibainisha Zitto akinukuu habari na taarifa za vyombo kadhaa vya habari.

Katika kile kinachoweza kuelezwa kuwa ni kuwakatisha tamaa watu aliosema wana nia mbaya na chama hicho, Zitto alisema kuwa ni vigumu kuisambaratisha CHADEMA kwa propaganda kama hizo kwani tayari imeshajijenga katika misingi ya kitaasisi.

Alisema kuwa CHADEMA ni moja kati ya vyama vichache vya upinzaani nchini ambavyo kimeendelea kuwa na viongozi wastaafu ambao wanaenziwa ndani ya chama.

"CHADEMA ni chama ambacho wenyeviti wake wastaafu wanaendelea kuenziwa na kuhudhuria vikao vyote vya chama… institutional memory ipo kuliko katika vyama vingine vya upinzani," alisisitiza akiwazungumzia Edwin Mtei na Bob Makani.

Alisema kuwa wanaodhani kuwa watu binafsi ndio wanaoipa CHADEMA umaarufu wanakosea, kwa sababu wapo watu wengi maarufu ambao awali ilikuwa ikiaminika kuwa wakihama katika chama hicho kitasambaratika, lakini hilo halijatokea.

"Alipohama (Dk. Aman Walid) Kabourou wengi walidhani ndio mwisho wa CHADEMA Kigoma, lakini leo hii CHADEMA ni moto Kigoma kuliko ilivyokuwa awali," alisema Zitto.

Zitto alikuwa akijibu hoja zinazolenga kuonyesha kuwa kuna uwezekano mkubwa wa CHADEMA kusambaratika iwapo yeye ataondoka kwenye chama hicho.

Hoja hizo zinajengwa katika misingi kuwa Zitto ni mtu ambaye anakijengea umaarufu chama hicho, kwa hiyo kumfanya yeye kuwa msingi wa uhai wa CHADEMA.

Kikubwa kinachotajwa sasa katika vyombo mbalimbali vya habari hivi sasa ni uamuzi wa Rais Jakaya Kikwete kumteua kuwa mjumbe katika kamati ya kuchunguza mikataba ya madini, hatua ambayo iliibua msigano wa maoni ndani ya chama hicho cha upinzani.
 

Susuviri

JF-Expert Member
Oct 6, 2007
3,713
2,000
Naona kijana Zitto yuko makini! Hata hivyo sisiem waache kutumia njama za kitoto, enzi za kutoa misleading information na propaganda zimepitwa na wakati. Mijitu mizima inazunguka kusambaza umbea tu kwenye vyombo vya habari!
Kama RA na co. wanadhani that they are spin masters wajue kwamba ndio kwaaaaaanza wameanza na ni better to look for Spinmaster DIY book in order to even enter the beginner's level!
 

Kitila Mkumbo

Verified Member
Feb 25, 2006
3,350
2,000
Hapa amewavua nguo na kuwatupa kwenye dimbwi sijui watatokaje tena huko, ngoja tusubiri.

BTW: Naona siku hizi Jangala mdogo Makamba kimya, sijui baada ya Dodoma aliambiwaje. Wana kazi sana maana kumziba mdomo mtu kama Makamba si kazi ndogo!
 

reandle

JF-Expert Member
May 6, 2009
11,207
2,000
SITANII, nimeota nikimlilia Zitto Kabwe! Zitto Kabwe ana kiburi cha kufahamika (kukubalika?)! Ni kiburi hicho hicho wakati fulani kikataka kumfanya alitose jimbo lake lililomtoa kisiasa na kutaka klugombea Kinondoni! Na wakati fulani akanukuliwa kwamba ameombwa akagombee Kahama na Geita! Katika akili ya Zitto Kabwe, popote atakaposimama yeye ni mshindi! Inawezekana yupo sahihi, lakini SIASA ni SIHASA!

INGAWAJE ilikuwa ni ndoto, lakini hivi sasa najihisi kujiandaa kumlilia rasmi Zitto Kabwe! Hisia zangu hizi ningependelea ziwe tahadhali kwa Mheshimiwa Zitto Kabwe badala ya kuona ni porojo! Jeuri, ama kiburi cha kukubalika kwa Zitto Kabwe nahisi zimeshamjengea dhana kwamba tayari yeye ameshapita ubunge na kazi iliyokuwepo mbele yake ni kuongeza nguvu zaidi kumnadi Mheshimiwa Slaa ili CHADEMA ikamate iingie Ikulu!

Popote ulipo, Mheshimiwa Zitto lazima ukumbuke kwamba CCM popote ndani ya nchi hii (may be with exception of PEMBA) ni DUBU lenye roho saba lisilokufa kirahisi! CCM ndani ya nchi hii ni dubu ambalo hata ulisurubu vipi, litaishia kuzimia tu na ukijisahau kwamba limeshakufa utashitukia limezinduka na kukutia mabao wewe mwenyewe na kukugaragaza!

Mheshimiwa Zitto Kabwe, nakutahadhalisha kwamba ukijiona tayari umeshalihodhi Jimbo la Kigoma then am sure utawasababishia BP na Kiharusi (Stroke) wapenzi wako ambao labda bado hawajajiandaa kukulia kama ilivyo kwangu mimi!

MHESHIMIWA Zitto, ukijisahau na kuona PRIORITY ilyopo kwenu hivi sasa ni Urais, then am afraid hautarudi Mjengoni kwa kura za wananchi, labda kwa kuteuliwa! Naamini wakati wewe ukiamini Kigoma ni yako, hivi sasa DUBU lisilokufa kirahisi lipo ndani ya mikakati mizito ya kulitwaa jimbo la Kigoma Kaskazini. Wala sitashangaa kuona kwamba one of their strategic areas kwa CCM kwenye uchaguzi huu ni Kigoma! Lazima Kigoma liwe eneo lao la kimkakati ili kulirudisha Jimbo lako mikononi mwao na kuhakikisha kwamba wanapunguza kura za wananchi kwenda kwa Dr. Slaa!

MWENYE AKILI, AHAMBIWI AJUMLISHE MOJA NA MOJA!
 

Mkulima mimi

JF-Expert Member
Dec 12, 2009
233
225
Labda kweli lakini mh. Zitto niliye mfahamu kabla nahisi ni tofauti sana na huyu! Nikimuangalia naona kama msimamo wake namuona kama waziri kwenye serikali ya kikwete na maanisha mtetezi wala sio mkosoaji ukianzia kwenye utetezi wa ununuzi mitambo ya dowans mpaka juzi alipotetea ujenzi wa nyumba ya gavana wa BOT.

Naona tayari mpiganaji amevuka mstari au kwa kujisahau ama kwa kukubali kuwa wazee wa ccm kuwa washauri wake zitto amekubali kuwa na msimamo wa wastani. Hata akikosa kwenda bungeni wala sitasikitika saaana! Nitasikitika tu sababu viti vya upinzani vimepungua lakini vinginevyo kila kitu kipo sahihi.
Ni mtizamo tu sio lazima ukubaliane nao!
 

Zogwale

JF-Expert Member
Jul 10, 2008
14,226
2,000
Kwani mnategemea Zito Kabwe arudi tena mjengoni? Ni ndoto za Abunuasi. Tena niwaambie Chadema kuwa huu kijana anajiandaa kuliuza jimbo kwa ccm. Ni mamluki wenu huyo. Wekeni tarehe ya leo kumbu kumbu na baada ya uchaguzi mtakubaliana na mimi.
 

Gagnija

JF-Expert Member
Apr 28, 2006
8,849
2,000
NasDAz na wenye hofu kama wewe,
CCM sasa hivi hawana cha strategic area tena baada ya kukamatwa na Dr Slaa. Trust me, kuna majimbo ambayo hata kabla ya uchaguzi tayari tunayahesabu kuwa ya CHADEMA, na kwa Zitto ni moja ya majimbo hayo.
Waliposikia kuwa Dr amebeba makombora 20 hawana amani tena kwani hawajui ni makombora ya masafa gani.
Kwa mazoea, wengi hawaamini kinachokuja baada ya Oktoba 31 lakini nakuhakikishia kuwa itakuwa Tanzania tofauti kabisa na hii ya leo na hiyo ndiyo inayomsukuma Msekwa kutafuta kuokolewa na Lewis Makame.
 

reandle

JF-Expert Member
May 6, 2009
11,207
2,000
NasDAz na wenye hofu kama wewe,
CCM sasa hivi hawana cha strategic area tena baada ya kukamatwa na Dr Slaa. Trust me, kuna majimbo ambayo hata kabla ya uchaguzi tayari tunayahesabu kuwa ya CHADEMA, na kwa Zitto ni moja ya majimbo hayo.
Waliposikia kuwa Dr amebeba makombora 20 hawana amani tena kwani hawajui ni makombora ya masafa gani.
Kwa mazoea, wengi hawaamini kinachokuja baada ya Oktoba 31 lakini nakuhakikishia kuwa itakuwa Tanzania tofauti kabisa na hii ya leo na hiyo ndiyo inayomsukuma Msekwa kutafuta kuokolewa na Lewis Makame.

NI HIZO CONFIDENCE NDIZO ZINANIOGOPESHA MKUU! AM AFRAID KWAMBA WANA JF BADO KABISA HAWAWAFAHAMU WATANZANIA WALIO WENGI!!! CHONDE CHONDE, YAKUMBUKENI YA BWANA CHAKUFWA SIYANA(am not sure kama nimepatia hilo jina) ambae alikuwa presidential candidate nchini malawi miaka kadhaa iliyopita! Jamaa alishaingia Ikulu kabla ya uchaguzi lakini uchaguzi ukaamua Muluzi(if am not mistaken) ndiyo anayestahili!
 

Andrew Nyerere

Verified Member
Nov 10, 2008
3,010
2,000
Mimi binafsi napinga Zitto Kabwe kwamba atagombea Kinondoni kushindana na yule Zungu,kwa sababu yule Zungu alikuwa anasoma Tambaza,na mimi nilikuwa nasoma Tambaza.
 

Mutu

JF-Expert Member
Mar 30, 2008
1,330
0
Mimi binafsi napinga Zitto Kabwe kwamba atagombea Kinondoni kushindana na yule Zungu,kwa sababu yule Zungu alikuwa anasoma Tambaza,na mimi nilikuwa nasoma Tambaza.

Kwa nini tusihoji kwa nini yeye anataka kugombea kinondoni? Then tukapima hoja yake .

Kwa sababu ya Zungu kusoma Tambaza ndio kushinda sielewi ,yaani mtoto wa hapa hapa si ndio?Ila popularity ina change with time sijuhi wapiga kura wangapi wanajali hilo kwa mji unaokuwa na wageni kama kinondoni.
 

reandle

JF-Expert Member
May 6, 2009
11,207
2,000
Mimi binafsi napinga Zitto Kabwe kwamba atagombea Kinondoni kushindana na yule Zungu,kwa sababu yule Zungu alikuwa anasoma Tambaza,na mimi nilikuwa nasoma Tambaza.

KUSOMA au kutosoma Tambaza sio issue kv wapiga kura wa Kinondoni si kwamba wote wamesoma au wana-entertain waliosoma Tambaza! Jambo la msingi ni endapo anaamini kwamba anakubalika kuliko anavyokubalika Zungu!
 

Bourgeoisie

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
656
250
Nikimlinganisha Zitto wa 2005 na wa sasa kisiasa naona ni watu wawili tofauti. Kadiri siku zinavyokwenda naona machachari ya Zitto yanamezwa na CCM. Wala sitashangaa kuona kaliuza jimbo.
 

kinya

JF-Expert Member
Feb 20, 2009
495
225
wakuu hii ni changamoto nzuri kwa mh. zitto chonde usidharau lisemwalo kwani mdharau mwiba..!Pia lisemwalo lipo kaka zitto si wenye uchungu na nchi hii twakuomba ujifanyie self evaluation then ujipange kuchukua jimbo lako la kg kask.KILA HERI MH.
 

kanda2

JF-Expert Member
Apr 22, 2007
1,318
1,225
Mimi binafsi napinga Zitto Kabwe kwamba atagombea Kinondoni kushindana na yule Zungu,kwa sababu yule Zungu alikuwa anasoma Tambaza,na mimi nilikuwa nasoma Tambaza.

Mbunge wa Kinondoni sio Mh Zungu bali ni Idd Azza. Kama ni kweli nyote mmesoma Tambaza then sidhani ungeweza ku state the obvious mistake!
 

mpangwa1

JF-Expert Member
Jul 19, 2009
279
0
Kweli mheshimiwa kisha lewa sifa na kusahau kazi ya mbuge ni kutetea watu wake sielewi nini kimemfanya angombe kinondoni kuliko kigoma kwenye matatizo na yanahitaji watu kama yeye, wacha afanyemakosa. majuto ni mjukuu
 

Kachanchabuseta

JF-Expert Member
Mar 8, 2010
7,274
1,195
23 September 2010
Na waandishi wetu


kabwee_fr.jpg


WAKATI kampeni zikipamba moto, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe, amekiri serikali ya CCM imejenga uchumi imara. Amepongeza utendaji kazi wa serikali za CCM na mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa Ilani yake ya uchaguzi.

Zitto anayewania ubunge Kigoma Kaskazini, alisema hayo juzi jioni katika Uwanja wa Mashujaa, alipomnadi mgombea ubunge wa Mtwara Mjini, kwa tiketi ya chama hicho, Jetha Othuman. Akizungumzia mafanikio ya serikali ya CCM, Zitto alimmwagia sifa Rais mstaafu Benjamin Mkapa, akisema amefanya mambo makubwa katika uongozi wake na kama kuna makosa ni ya kibinadamu.

"Hakuna anayeweza kila kitu kama yapo yaliyomshinda huo ni ubinadamu," alisema Zitto na kuongeza kuwa, uchumi imara uliwezesha kushuka kwa mfumko wa bei. Aliwaponda watu wanadai serikali ya CCM inabagua wapinzani, akisema imekuwa ikitekeleza Ilani kwa kufikisha maendeleo hata kwenye maeneo yanayoshikiliwa na wapinzani.

"Wanaosema serikali ya CCM inabagua katika kugawana keki ya taifa hao ni waongo, imefikisha maendeleo hata kwa wapinzani," alisema huku akitoa mfano wa maendeleo yaliyofanyika katika majimbo ya Karatu, Kigoma na Sumbawanga. Alisema Kigoma ni ngome ya upinzani, lakini imepiga hatua kubwa katika maendeleo, akitaja miradi mikubwa iliyotekelezwa ya barabara, maji na umeme.


Source: UHURU
 

Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
14,545
2,000
Heshima kwako Jeykeywaukweli,

Hapana hayo maneno hakutamka Zitto sipati picha kwenye kampeni naibu katibu mkuu wa chama cha upinzani anasifu serekali iliyoko madarakani ?.Ingekuwa Mzee wa Kiraracha kasema nakwambia mitusi ingemiminika kama maji ya mto Ruvu.

Nasubiri michango ya wanajamvi wengine mimi nimeishiwa nguvu.
 

Albedo

JF-Expert Member
Feb 24, 2008
5,560
1,195
Zitto: CCM imejenga uchumi imara nchini


alisema Zitto na kuongeza kuwa, uchumi imara uliwezesha kushuka kwa mfumko wa bei.

From 600TShs of 1 Kg Sugar to 2000Tshs?

Haya maneno hayajatoka kwenye Kinywa cha Zitto! Naona Uhuru wamemlisha maneno Zitto
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom