Zitto ahusishwa na Rostam Aziz - Mwana Halisi

Status
Not open for further replies.
Sio pumba hizi..kuna substance hapa...RA ni mtu wa kumwogopa kama ukoma...Ni maongezi gani marefu na frequent namna hiyo??..Network searching~~~~~~~!
Kuwa na urafiki wa pembeni na mtu mwenye rekodi mbaya mbele ya macho ya Watanzania wote ni namna ya usaliti...Urafiki gani huukati ya Simba na sungura...Urafiki gani huu kati ya mwanambuzi na Chui!..
Somewhere, sometime...........

Sawa kabisa PJ maana methali inasema ng'ombe mwizi akitembea na mwizi naye atakuwa mwizi. Chunga sana hiyo, mtoto akishilikiana na majambazi ukakaa kimya matokeo yake yatakuwa mabaya kwako pia.
 
Zitto naona ana genge lake naye. Kama ambavyo wanadai Mbowe ana genge lake.

Labda sasa ni wakati muafaka kwa Zitto na genge lake kuanzisha Chadema B.

Maana hata CCM wana CCM B yao.

Wasiwasi wangu ni kwamba Zito ni maarufu Kigoma tu.

Na umaarufu wa Chadema hautokani na uwepo wa Zito.

Kama mlizoea kuwa hizo siasa za majitaka huwa zinafanikiwa kuwafanya walioshindwa huo ujinga kuondoka hapa kwa Zitto mmenoa. Zitto alikuwa Chadema kabla hata ya hao wanaojifaragua kuwa ndio wenye Chama. Na atapambana huko huko hadi mwisho......Zitto ana ndoto ya aina ya Tanzania anayoamini tunapawa kujijenga na Chadema ni chagua lake katika kuhakikisha kuwa Tanzania makini inapatikana.....
 
sio wivu wewe.......!
weka hoja au logout.lazima tujiulize m'bunge wa kawaida unakuwa na magari SITA ya kifahari ya kutembelea.....HOW?

huo ni wivu na ndio kinacho watia upofu wa wasiko na akili.
 
Acha kupotosha, Mbowe hana jeuri ya kumuambia Lowassa hilo. Hivi unadhani Lowassa alipata wapi jeuri ya kumfuata Mbowe. Hivi unajua makubaliano ya Mbowe na hawa jamaa?

Zitto anawasiliana na kila mtu hata kama hakubaliani na mambo yao kwani in between analearn mengi zaidi kuliko hao wenzake ambao majukwaani wanawaita hao mafisadi jioni wanawatumia sms za kuomba wawachangie kampeni zao. Tena katika hilo wako hata wapambanaji vijana wenzetu ambao walifikia hata kuwa tayari kuhama Chadema ili wateuliwe ukuu wa wilaya na hawa viongozi wako wakaendorse....

Brother if what you are saying is correct then "Two Wrongs Dont Make it Right" Kwahiyo kama una evidence za hao wengine kukiuka maadili inabidi tuwajadili......... sio sababu wengine wanafanya na zitto afanye
 
hakuna lenye ukweli hapa.....!
ni USHABIKI na MAPENZI BINAFSI vimetawala.

utupe list ya watu waliomchangia zitto kwenye kampeni tuone
 
kumbuka kuwa zk na ra wote ni wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa tanzania.

Mbona mbowe kisha kwenda ikulu si mara moja tu, kama ni mawasiliano tu ya kawaida mbona la mbowe kwenda hadi ikulu haliulizwi?, mbowe hufata nini ikulu? Na pia tumeona mbowe katika picha na kikwete wakichangamkiana sana. Kina slaa na makinda mpka picha zao gazetin zimo.

Sasa hili la zitto na rostam na jack ndio iwe nongwa? Wote si system hao, au hamjuwi?

darisalama ikibindankoi,hata mbowe angekuwa amebadilika na kukiyumbisha chama tungemhoji.
Na kama hayo maongezi rostam ndiye angekuwa anaiyumbisha ccm tungejua wanaongelea maslahi ya cdm. Sasa hapo usichokielewa wewe kipofu bin akili fupi ni nini?
 
huo ni wivu na ndio kinacho watia upofu wa wasiko na akili.
hakuna wivu hapa.....

tunahoji tu.kuhoji MBUNGE wa miaka mitano bungeni anawezaje KUMILIKI hummer na magari matano zaidi ya kifahari ya kutembelea kuna ubaya gani?
 
Kwa kuzingatia msimamo (unpopular) aliouonesha Zitto kwenye suala la Dowans (tunayoaminishwa ni ya RA)...hivi hizi 'revelations' za kuwapo kwa uhusiano kati ya Zitto na RA inawezekana kwa namna yoyote kuwa na uhusiano wowote na Dowans?

Inaelekea mngependa sana kuona kuwa Tanzania inasheheni populist politicians mkiamini kuwa hao ndio watawakomboa katika majanga tuliyonayo? Hivi hata baadaya hasara ya mabilioni tunayolazimika kulipa kwa hao DOWANS, Kukosa mitambo na sasa miaka minnne ya kukosa umeme wa kutosha bado mnaamini kuwa msimamo ule wa Zitto hakukupaswa kuwepo kwa kuwa ulikuwa unpopular? Hivi hizo popular politics zenu kuhusu Richmond na Dowans zimemsadia vipi mtanzania hadi leo zaidi ya kuwezesha kuwafanya mahasimu wa siasa za makundi ndani ya CCM kumantain their position na huku watanzania wakiendela kusuffer...
 
All in all, Kuna mambo ZITTO ana mambo MAZITO! Huyu dogo amelaghaika na kudanganyika, hafai tena kuwa CDM-achilia mbali kushikilia cheo chochote katika chama. Naona watu na akili zao sasa wanamtetea huyu dogo.....! lazima tuangalie hawa watu anaoongea nao huyu dogo wana muelekeo gani....na yeye ana mwelekeo gani. Mwanakijiji ukimuona mwanao anajihusisha na kujenga urafiki na vijana wavuta bange usidanganywe ni urafiki tu-baadaye atafundishwa...JIULIZE, TAMBUA, CHUKUA HATUA.

HATA LEO ZITTO AKIULIZWA ANA MITKASI GANI NA RA ATAJIBU..."Sina cha kusema leo"
 
Kama mlizoea kuwa hizo siasa za majitaka huwa zinafanikiwa kuwafanya walioshindwa huo ujinga kuondoka hapa kwa Zitto mmenoa. Zitto alikuwa Chadema kabla hata ya hao wanaojifaragua kuwa ndio wenye Chama. Na atapambana huko huko hadi mwisho......Zitto ana ndoto ya aina ya Tanzania anayoamini tunapawa kujijenga na Chadema ni chagua lake katika kuhakikisha kuwa Tanzania makini inapatikana.....

kwa miendendo yake hii ya undulima kuwili, obviously atakuwa amenoa mwenyewe.
 
Brother if what you are saying is correct then "Two Wrongs Dont Make it Right" Kwahiyo kama una evidence za hao wengine kukiuka maadili inabidi tuwajadili......... sio sababu wengine wanafanya na zitto afanye

Hivi kiongozi kuzungumza na Rostam ama Afisa Usalama wa Taifa ni kukiuka maadili? Lakini pia ni lini uliwahi kukemea wanayofanya wengine dhidi ya Zitto zaidi ya kushabikia tu na kuhalalisha?
 
Hivi kiongozi kuzungumza na Rostam ama Afisa Usalama wa Taifa ni kukiuka maadili? Lakini pia ni lini uliwahi kukemea wanayofanya wengine dhidi ya Zitto zaidi ya kushabikia tu na kuhalalisha?
zitto kabwe wa 2005,
zitto kabwe aliyefukuzwa bungeni
zitto kabwe aliyekuwa na uchungu mkubwa na nchi hii kwenye dowans,richmond,epa etc

HAWEZI KUONGEA NA ROSTAM.....!WATAONGEA NIN?

halaf mifano tunayo.....mtikila ilikuwaje?
 
hakuna wivu hapa.....

tunahoji tu.kuhoji MBUNGE wa miaka mitano bungeni anawezaje KUMILIKI hummer na magari matano zaidi ya kifahari ya kutembelea kuna ubaya gani?

Mkuu, mienendo ya zitto hata mimi siiamini kabisa, lakn nadhani hakuanzia bungeni kutafuta pesa!
 
hakuna wivu hapa.....

tunahoji tu.kuhoji MBUNGE wa miaka mitano bungeni anawezaje KUMILIKI hummer na magari matano zaidi ya kifahari ya kutembelea kuna ubaya gani?

Wewe utasutwa. fuatilia mambo kwanza kabla ya kuropoka. Zitto hajwahi kumiliki Hammer. Hammer aliyokuwa nayo ilikuwa ni ya Kaka yake ambaye ni mfanyabiashara wa magari iliuzwa mika minne iliyopita. Gari pekee la gharama ambalo Zitto amewahi kununua halizidi shilingi milioni 30 na yote ni second hand tena second hand za hapa Tanzania. Zitto alipopewa fedha zake za ubunge mwanzoni aislimia kuwa alisurrender kwa Mbowe kama kumpunguzia mzigo wa michango yake katika kampeni kumbe fedha alizokuwa Mbowe anadai ni zake ni za kutoka kwa Rostam...zaidi ya milioni 100.

Lakini pia kumbuka Zitto sio mbunge wa vikao vya bunge tu. Anatumia sana eleimu yake kama consultant na hivyo kujipatia mapato zaidi ambayo yote huishia katika matumizi ya kibunge na chama. Zitto miaka yote hii amekuwa akijitolea kusaidia chama ama viongozi wenzake bila ya kuomba kulipwa kama wafanyavyo viongozi wenzake.

By the way acha ushamba, hivi unajua thamani ya used hammer? Its less than 25,000USD na kama Zitto angetaka kumiliki he could afford just kwa kutumia mkopo wa lazima wa magari wanaopewa wabunge....
 
Inaelekea mngependa sana kuona kuwa Tanzania inasheheni populist politicians mkiamini kuwa hao ndio watawakomboa katika majanga tuliyonayo? Hivi hata baadaya hasara ya mabilioni tunayolazimika kulipa kwa hao DOWANS, Kukosa mitambo na sasa miaka minnne ya kukosa umeme wa kutosha bado mnaamini kuwa msimamo ule wa Zitto hakukupaswa kuwepo kwa kuwa ulikuwa unpopular? Hivi hizo popular politics zenu kuhusu Richmond na Dowans zimemsadia vipi mtanzania hadi leo zaidi ya kuwezesha kuwafanya mahasimu wa siasa za makundi ndani ya CCM kumantain their position na huku watanzania wakiendela kusuffer...

Hapana, sio ishu ya popular politics. Ninachojaribu ku deduce ni kuwa...inawezakana msimamo wa Zitto kwenye suala la Dowans ulitokana na uhusiano/ukaribu wake na mmiliki wa Dowans? Au labda kuiweka hii kivingine: kama mawasiliano baina yake na RA yangelifichuliwa kipindi kile, hali ingekuwaje (assuming wameanza kuwasiliana muda mrefu...wote ni wabunge au sio?). Ni hayo tu.
 
Mkuu, mienendo ya zitto hata mimi siiamini kabisa, lakn nadhani hakuanzia bungeni kutafuta pesa!
sasa shida ndo ipo hapo......!
huiamini miendendo again unasema UNADHANI!

lakin mimi ninasimamia ninachokiamini kwamba SOMETHING IS NOT RIGHT SOMEWHERE!kumekuwa na mlolongo wa ''fanya fanya'' siku za usoni

tutajua tu....
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom