Kung'olewa kwa Mugabe.
Maana yake,sisi Watanzania siku zote tuna kubali wenyewe kwa moyo mmoja kutawaliwa na chama cha wezi CCM.
Iweje watu hawa walio chakazwa na kunyang'anywa matumaini yote na utawala wa Mugabe wanatushinda sisi Watanzania, tunaokula viporo vya Ugali wa muhogo na mchunga na kushiba, kukiondoa chama dharimu madarakani?
Siamini kwamba fedha za wizi za CCM ndiyo sababu pekee ya kuendelea kuwepo madarakani ulegevu wetu,utepetevu wetu na hamu yetu ya kujenga matumaini hewa vinachangia kwa sana.
Naamini sababu kubwa ni ulegevu wetu wananchi wenyewe, hasa pale tunadhanipo kwamba CCM ni wateule wa Mungu, na yote wayafanyayo ni bora kuliko utaratibu mwingine wowote duniani.
Hasa pale tunapoamini kwamba kwa sababu waasisis wa Uhuru wa nchi chama chao ni CCM basi chama hicho kina mamlaka ya kutenda udharimu wowote na sisi wananchi ni kundi la watazamaji tu.
CCM ni cham Kengeufu.
CCM ni chama kinacho kula matapishi yake chenyewe na matapishi ya Sir Richard Turnbull.
Kitendo cha watendaji wa CCM kukosa uzalendo na kuurudisha ukoloni Tanzania ni sawa na kula Matapishi yake.
CCM kiliweza kupigana vita ya Uhuru wa Bendera.
CCM kimeshindwa kupigana vita ya Uhuru wa Kiuchumi kwa hiyo si chama cha kukienzi tena.
CCM inabidi kikalishwa Benchi moja na KANU,ZANU na marehemu wengine wa kisiasa.
CCM wanatutia utumwani kama alivyofanya Karl Peters.
Kungekuwa na afadhari kidogo iwapo CCM wangetuibia BOT tu, kitendo chao cha kuingia mikataba ya kututia utumwani kwa mara ya pili ni kitendo ambacho sisi watanzania kamwe hatuwezi kubeba gharama yake.
Huu ni muda wetu watanzania wa kuwabebesha CCM gharama za maovu yao yatakayo walemea hadi kuzimu.
Kundi la watu ndani ya taifa lenye mawazo ya kutajirika kwa kuuza umiriki wa utajiri wa nchi kwa wageni, ni kundi la mahabithi, watumwa wa mawazo na watu wasio kuwa huru, ni kundi la watu wanao jali Uhuru wa Bendera tu.
Hatuwezi kuendelea kulikumbatia kundi la Maharamia wa CCM.
CCM ni kizuizi namba moja cha maendeleo ya Tanzania.
CCM ni lazima ing'olewe madarakani kwa gharama yeyote ile kwa Faida na maendeleo ya Tanzania na Watanzania wote.