Yale yaliyotokea Kenya nadhani yanaweza kujirudia Zimbabwe lakini kwa style ya aina yake. Kuna baadhi ya tovuti zinadai kwamba Idara ya Usalama wa Mugabe (maana siyo usalama wa Taifa) wamezuia matokeo ya uchaguzi yasitangazwe, ni habari za ukweli kiasi gani, mimi sina uhakika. Hali hiyo inatokana na ushindi wa MDC kwenye huo uchaguzi.
Swali la kujiuliza: Je, Magereza, Polisi na Jeshi watayakubali hayo matokeo? Maana viongozi wao wa juu walitamka hadharani kwamba lazima Mugabe ashinde, akishanda mtu mwingine (kibaraka) hawatakubali kumtii. Je, ndiyo kusema watamuingiza Mugabe kwa nguvu hata kama kashindwa? Je, watafanya mapinduzi ya serikali ambayo haijasimikwa madarakani? Zimbabwe sasa inaelekea kubaya sana na SADC wanaweza kubeba mzigo wa lawama maana wamekuwa wakikaa kimya kila kasheshe ya Zimbabwe inapoibuka. Yangu macho ... ngoja tuone kitakachotokea!