Maoni ya Wadau, Wasomi Kuhusu Hatua ya Rais Samia Kuagiza Kuanza Mchakato wa Katiba Mpya

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,035
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere, Dk. Philip Daninga, alisema Rais Dk. Samia, kuwa, anaishi anazidi kuonyesha misingi ya utawala bora na anatekeleza kwa vitendo yale anayoahidi.
Dk. Daninga alisema maelekezo ya Rais Dk. Samia kwa Jaji Mutungi inaonyesha yeye ni Rais anayekeleza mambo kwa vitendo ana dhamira ya kunakikisha suala la katiba mpya linatekelezeka.

Msajili wa vyama vya siasa, Jaji Francis Mutungi, akifafanua kuhusu maagizo aliyopewa na Rais Samia, Jaji Mutungi alisema watu watumie muda kuandaa hoja ambazo zitakidhi kiu ya katiba mpya.

"Kwa kweli itabidi tuandae mkutano mkubwa sana wa wadau, kwa sababu hili ni suala ambalo kila mtu analisubiri. Siwezi kuwaambia nimepata maagizo usiku kisha niwaambie mkutano huo tutaufanya kesho, itakuwa maandalizi hafifu, tunataka kufanya maandalizi haswa."

"Watu wakae wakijiandaa, watumie muda huu kujiandaa na hoja zao, tutafanya mkutano mkubwa sana utakaokidhi kiu ya wengi kuhusu hoja hiyo," alisema.

Mchambuzi wa masuala ya Siasa na Diplomasia Greyson Mgonja alisema hatua ya Rais Dkt Samia kutoa maelekezo kwa Jaji Mutungi inaleta tafsiri kuwa anaendeleza dhamira njema aliyonayo, katika kuendelea kujenga demokrasia, taifa moja na umoja.

Pia, Mgonja alisema kupitia mchakato wa katiba mpya, Rais Dk. Samia, ataweka historia nyingine kubwa duniani katika kusimamia misingi ya demokrasia huku akiwa anaonyesha mwendelezo wa kujenga taifa moja na wanasisa watakwenda kumwelewa zaidi.

"Kwa maelekezo ya Rais Dk. Samia kwa Jaji Mutungl, sasa mama (Rais Dk. Samia), anaonyesha mwendelezo wa kujenga taifa moja na umoja, anakwenda kujenga historia nyingine, kubwa Watanzania wengi hasa wanasiasa sasa watatamani aendelee kuwepo madarakani,"alisema.
Chama Cha ACT -Wazalendo, Chama Cha ACT-Wazalendo, kilisema kinaunga mkono maagizo ya Rais Dk. Samia ya kumwagiza Jaji Mutungi kuitisha kikao hicho na kwamba, kipo tayari kutoa ushirikiano. Pia, kimesema ni matumaini yao kwamba, kikao hicho kitapatiwa ratiba itakayohakikisha kuna sheria mpya ya uchaguzi na sheria mpya ya vyama vya siasa.

Taarifa iliyotolewa kwa umma jana na ACT- Wazalendo, ilisema nI mategemeo ya chama hicho kuwa, Baraza la Vyama vya Siasa, litakuwa n/ sehemu ya maandalizi ya mkutano wa kitaifa wa kujadili mambo mchakato kupata katiba mpya.

Unaweza kuongeza ya kwako uliyokutana nayo
 
Lissu: Umepita mwaka mmoja Hadi hivi sasa, Serikali haijajibu hata pendekezo moja kati ya mapendekezo lukuki yaliyoandikwa na CDM juu ya njia Bora za kupata KATIBA mpya na Tume huru ya Uchaguzi.

Dr SLAA: Serikali Haina Nia na maridhiano zaidi ya kubuy time ya Watanzania.

Nashauri CDM ijitoe katika maridhiano Ili wananchi wote tuidai KATIBA mpya barabarani.
 
Kwa uoga wa sisi watanzania nani anaweza kudiriki kuidai katiba barabarani.mh Rais tumpe muda wa kulitelekeza hilo kwani anaonesha kiu ya kutupatia katiba mpya kwani madhaifu ya katiba hii ameyashuhudia kwa macho yake mfano ndugu zake wanavyokula kichapo huko Zanzibar kipindi cha uchaguzi mkuu ambapo vyombo vya dola havijali hili wala lile
 
Ni hadaa inafanyika kumfanya atawale smooth.

Alichofanya ni kurudisha mpira Kwa Mtungi yule yule na kikosi KAZI.

Pesa za wananchi ziheshimiwe.

Wananchi Si wajinga, Tutaandamana kuidai mtaani Katiba mpya Nchi nzima.

Nchi hii ni yetu sote.

Ameeen
 
Msajili wa vyama vya siasa, Jaji Francis Mutungi, akifafanua kuhusu maagizo aliyopewa na Rais Samia, Jaji Mutungi alisema watu watumie muda kuandaa hoja ambazo zitakidhi kiu ya katiba mpya
Domo langu kaa kimya
 
Hongera mama kwa kuja na Stratejia mpya ya Kuunda katiba Mpya, Utawashangaza wengi , Lakini usije kuwashangaza watu kama alivyowashangaza Nyerer katika kuleta Muungano Butu ,ambao ulionekana Tunu kubwa kwa wakati ule.
Kosa la Nyerer na Karume ni kufanya Maamuzi yao WAWILI KUWA ndio Mkataba wa Muungano. Huku Bara Mwanasheria Mkuu akishiriki sawasawa , wakati kule Zanzibar Mwansheria mkuu hakushirikishwa, badala yake Mwalimu akamleta John Feefoot, Mshauri wake wa Sheria amuwakilishe Dorado wa Zanzibar na karume akalazimishwa Kumkubali.

Hatima Karume akaanza kuguna pindi nyaraka zilipoletwa mikononi mwake na kugoma kusaini hatimae kifo kikafuatia.
Mkataba ule haukuwa na Term of contracts, wala mashariti ya kubadilishana Uongozi, wala shariti la kuunganishwa taifa jingine ,wala kutatua mgogoro endapo kutatokea Mis understanding.

Hongera MAMA kwa kuwashirikisha watu wa Sheria na Mikakati, lakni tafadhali Pande za Muungano ziko 2
Usije ukasahau kuchukua wawakilishi pande zote.
 
Well
 
Back
Top Bottom