Zanzibar: Simai Mohamed Said, Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale ajiuzulu siku mbili baada ya kutangaza uhaba wa pombe kwenye hoteli na migahawa

FbUser

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
430
623
Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Simai Mohamed Said ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo leo usiku.

Mhe. Simai ambaye pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, ametangaza kujiuzulu akisema ni kutokana na kile alichokiita "MAmazingira yasiyo rafiki ya kazi."
---

Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Simai Mohamed Said amemuandikia Rais Dkt. Hussein Mwinyi barua ya kujiuzulu nafasi hiyo.

“Nimefikia uamuzi huu ambao hapa kwetu si rahisi katika utamaduni wetu. Kutokana na imani yangu kwamba jukumu namba moja la wasaidizi wa Mheshimiwa Rais wakiwemo Mawaziri ni kumsaidia kutekeleza Ilani ya chama, na inapotokea mazingira yasiyo rafiki katika kutekeleza jukumu hilo muhimu kwa ustawi wa wananchi, ni vyema kutafuta jawabu kwa haraka ili kazi ya kuwaletea wananchi maendeleo iweze kuendelea, na hata ikibidi kukaa pembeni.

Mimi nimefikia uamuzi huo mgumu wa kukaa pembeni.” - sehemu ya taarifa yake ya kujiuzulu

Siku mbili zilizopita, Januari 24 Waziri huyo mwenye dhamana ya Utalii alitangaza uhaba wa pombe katika hotel na migahawa

“masikitiko yamekuwa makubwa na imenibidi niitishe kikao kwa sababu nimeanza kunyooshewa mkono na Wadau, mimi kama Baba wa Mahoteli na Migahawa lazima nionane nao kwani Sekta ya utalii si vyema ikachezewachezewa”

“Tumeona maamuzi ya Bodi ya Vileo Zanzibar imewaondosha wale waliokua wanahusika kama ZMMI, Scoch na One Stop, nimeanza kuona athari hoteli nyingi wameanza kukosa huduma ya Vinywaji baada ya Bodi ya Vileo kufanya maamuzi hayo, niwaombe Wawekezaji waendelee kuwa Wavumilivu wakati huu ikitazamwa namna ya kutatua jambo hili”

Mwisho wa kunukuu.

Zaidi soma Waziri: Zanzibar inakabiliwa na upungufu wa Pombe kwenye Mahoteli
 
Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Simai Mohamed Said amemuandikia Rais Dkt. Hussein Mwinyi barua ya kujiuzulu nafasi hiyo.

“Nimefikia uamuzi huu ambao hapa kwetu si rahisi katika utamaduni wetu. Kutokana na imani yangu kwamba jukumu namba moja la wasaidizi wa Mheshimiwa Rais wakiwemo Mawaziri ni kumsaidia kutekeleza Ilani ya chama, na inapotokea mazingira yasiyo rafiki katika kutekeleza jukumu hilo muhimu kwa ustawi wa wananchi, ni vyema kutafuta jawabu kwa haraka ili kazi ya kuwaletea wananchi maendeleo iweze kuendelea, na hata ikibidi kukaa pembeni. Mimi nimefikia uamuzi huo mgumu wa kukaa pembeni.” - sehemu ya taarifa yake ya kujiuzulu
 
SOMO KWA MAWAZIRI WA SERIKALI YA CCM BARA, ZIARA ZA PAUL MAKONDA ZINAWAUMBUA, MJIUUZULU NAFASI ZENU
1706263537429.png

Picha: Katibu uenezi Paul Makonda ktk ziara yake ndefu aelezwa pia kukumbana na udhaifu wa viongozi ktk utekelezaji wa ilani ya CCM kuanzia wizara hadi ngazi ya kijiji

Mawaziri wa CCM Bara waige huu utamaduni wa wenzao visiwani, kuwajibika bila kungangania wakisubiri kutenguliwa au kubadilishwa wizara wakati dhahiri mambo hayaendi vizuri kuleta maendeleo endelevu tarajiwa. Uongozi uwe uwezo wa kuleta mabadiliko ukishindwa au ukiona unawekewa vikwazo jiuzulu kama huyu mheshimiwa sana waziri wa utalii na mambo ya kale alivyoamua .
mhe_simai_1.png

Mhe. Simai Mohammed Said
 
Hiyo ndio habari kuu usiku huu.

Waziri katika serikali inayoongozwa na Mh Dr. Hussein Mwinyi anayeshughulikia utalii na mambo ya kale ametangaza kujiuzulu mara moja

Hata hivyo hajaeleza sababu za kufikia uamuzi huo. Ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Rais na CCM.
 
Mwakilishi wa jimbo la Tunguu Mh. Simai Mohammed Simai
mhe_simai_1.png

Mhe. Simai Mohammed Said

Aina ya mwakilishi: kura
Jimbo : Tunguu
Chama cha siasa: CCM
Mwakilishi Tangu : 2016
Kipindi : Cha pili 2020

Naibu waziri 2019 2020

Memba Committee 2016 2020
Commonwealth Parliament
Association, Zanzibar Branch

Chairman 2016 2020
Stone Town Conservation and
Development Authority Board

Member 2014 2018
State University of Zanzibar (SUZA) Council

Member Constitution Review Commission Member 2012 2014

Busara Promotions Chairman, Board of Trustee 2003 To Date

Zanzibar Arts Council Board Member 2008 2010

Zanzibar Association of Tourism
Investors (ZATI) Chairman 2005 2010

Rotary Club of Zanzibar Charted Member,founder 2005 2006

Beckton Alpine Ski Centre, London Industrial Attachment 1997 1997

Spice Group Of Hotels, Zanzibar Front House Manager 1992 1995
 
MH SIMAI AJIUZULU UWAZIRI ZANZIBAR Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Simai Mohamed Said ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo leo usiku. Simai ambaye pia ni mwakilishi wa jimbo la Tunguu kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, ametangaza kujiuzulu akisema ni kutokana na kile alichokiita MAZINGIRA YASIYO RAFIKI YA KAZI.

images.jpeg
 
Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Simai Mohamed Said amemuandikia Rais Dkt. Hussein Mwinyi barua ya kujiuzulu nafasi hiyo.

“Nimefikia uamuzi huu ambao hapa kwetu si rahisi katika utamaduni wetu. Kutokana na imani yangu kwamba jukumu namba moja la wasaidizi wa Mheshimiwa Rais wakiwemo Mawaziri ni kumsaidia kutekeleza Ilani ya chama, na inapotokea mazingira yasiyo rafiki katika kutekeleza jukumu hilo muhimu kwa ustawi wa wananchi, ni vyema kutafuta jawabu kwa haraka ili kazi ya kuwaletea wananchi maendeleo iweze kuendelea, na hata ikibidi kukaa pembeni. Mimi nimefikia uamuzi huo mgumu wa kukaa pembeni.” - sehemu ya taarifa yake ya kujiuzulu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
WhatsApp Image 2024-01-26 at 08.59.46.jpeg

Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Simai Mohamed Said amemuandikia Rais Dkt. Hussein Mwinyi barua ya kujiuzulu nafasi hiyo.

“Nimefikia uamuzi huu ambao hapa kwetu si rahisi katika utamaduni wetu. Kutokana na imani yangu kwamba jukumu namba moja la wasaidizi wa Mheshimiwa Rais wakiwemo Mawaziri ni kumsaidia kutekeleza Ilani ya chama, na inapotokea mazingira yasiyo rafiki katika kutekeleza jukumu hilo muhimu kwa ustawi wa wananchi, ni vyema kutafuta jawabu kwa haraka ili kazi ya kuwaletea wananchi maendeleo iweze kuendelea, na hata ikibidi kukaa pembeni. Mimi nimefikia uamuzi huo mgumu wa kukaa pembeni.”

Mimi nadhani kama imani ya wazanzibar haiendani na TAMADUNI za watalii,hawataki pombe, hawataki watalii wafanye mapenzi, hawatakiw atalii wavae watakavyo basi wafunge kabisa utalii.
, NI BORA WAFUNGE KABISA SWALA LA UTALII KWA WASIO WA IMANI YAo,, waache unafki
 
Jengo juzi limeua watu ,sekta ya utalii mwaka jana ilipata kashfa ya kumleta yule jamaa ambaye ni shoga ili awatangaze🤣🤣
 
View attachment 2883087

Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Simai Mohamed Said amemuandikia Rais Dkt. Hussein Mwinyi barua ya kujiuzulu nafasi hiyo.

“Nimefikia uamuzi huu ambao hapa kwetu si rahisi katika utamaduni wetu. Kutokana na imani yangu kwamba jukumu namba moja la wasaidizi wa Mheshimiwa Rais wakiwemo Mawaziri ni kumsaidia kutekeleza Ilani ya chama, na inapotokea mazingira yasiyo rafiki katika kutekeleza jukumu hilo muhimu kwa ustawi wa wananchi, ni vyema kutafuta jawabu kwa haraka ili kazi ya kuwaletea wananchi maendeleo iweze kuendelea, na hata ikibidi kukaa pembeni. Mimi nimefikia uamuzi huo mgumu wa kukaa pembeni.”

Mimi nadhani kama imani ya wazanzibar haiendani na TAMADUNI za watalii,hawataki pombe, hawataki watalii wafanye mapenzi, hawatakiw atalii wavae watakavyo basi wafunge kabisa utalii.
, NI BORA WAFUNGE KABISA SWALA LA UTALII KWA WASIO WA IMANI YAo,, waache unafki
kazi imemshinda na asisingizie pombe
 
Back
Top Bottom