BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,376
- 8,120
ZANZIBAR: Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amekubali ombi la kujiuzulu kwa Simai Mohamed Said, aliyekuwa Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale.
Taarifa ya Serikali imesema Rais Mwinyi ameridhia ombi hilo kuanzia leo Januari 26, 2024 ikiwa ni muda mfupi tangu Simai atoe taarifa kuwa anaachia nafasi hiyo kutoka na mazingira ya utendaji kazi kutokuwa rafiki kwake.
Siku chache zilizopita, akiwa Waziri, Simai alinukuliwa akisema Hoteli za Zanzibar zinakabiliwa na upungufu wa Pombe.