Viongozi wa Muungano igeni Utaratibu mzuri wa Kujiuzulu kama Zanzibar

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
15,126
22,626
Salaam, Shalom!

Ziku chache zilizopita, palitokea taarifa njema za uwajibikaji Kwa waziri wa Serikali ya MAPINDUZI Zanzibar Kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kuadimika Kwa Pombe visiwani humo akituhumu kubadilishwa waagizaji. Waziri aliyejiuzulu ni Waziri wa Utalii na mambo ya kale ndugu Siami.

Kinachoshangaza zaidi ni kiongozi wa CCM aliyechukua hatua hiyo ya kuwajibika tofauti na Mategemeo ya wengi kuwa CCM ni wagumu kijiuzulu kukwepa uwajibikaji.

Ninachojiuliza kuwa, ikiwa uwajibikaji Kwa hatua ya kujiuzulu ni Kwa viongozi Kutoka Zanzibar, mbona Hali hiyo haitokei Kwa viongozi wenye asili ya Zanzibar wawapo huku bara kwenye Muungano? Mfano mzuri ni Waziri wa uchukuzi Makame Mbarawa.

Ndugu Makame Mbarawa amepitia tuhuma za wazi kama ununuzi wa Vichwa vya treni chakavu nk nk lakini mbona hawajibiki Kwa nafasi yake?

Tuliambiwa SGR itaanza mwezi January 2024, lakini Leo ni February 2024, halijaanza route lakini waziri Mbarawa hachukui uwajibikaji kama wenzie Zanzibar wafanyavyo.

1. Pesa za kigeni Hadi sasa zimeadimika, waziri husika mbona hawajibiki Kwa nafasi yake?

2. Umeme ni kizumgumkuti, mbona waziri wa nishati hawajibiki Kwa nafasi yake?

3. Ujenzi holela wa vituo vya mafuta katika makazi ya raia umeendelea kushamiri, na Waziri husika aliapa kulikomesha, sasa ameshindwa kuchukua hatua na hawajibiki Kwa nafasi yake, kwanini?

4. Sukari haipatikani, na Bei ziko juu Hadi 5000 Kwa kilo, lakini waziri husika mbona hawajibiki Kwa nafasi yake?

Mawaziri na viongozi wengine wa kisiasa na watumishi wa Umma, tafadhari igeni ukomavu aliouonyesha Ndugu Simai, aliyekuwa waziri wa Utalii na mambo ya kale, Kutoka Zanzibar, jambo hili ni zuri kuhakikisha wananchi wanatumikiwa Kwa HAKI na uharaka.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿.

Karibuni🙏
 
Hongera ndugu Simai Kwa hatua nzuri ya kuonyesha uwajibikaji.
 
Tuliambiwa mgao wa umeme mwisho January 2024.

Nani awajibike?
 
Onaongelea hawa akina Madelu wanaokesha kwa Wachawi na Waganga ili wasifukuzwe halafu unasema Kujiuzulu?🤣
 
Onaongelea hawa Madelu wanaokesha kwa Wachawi na Waganga ili wasifukuzwe halafu unasema Kujiuzulu?🤣
Mbona Zanzibar ni CCM vile vile na amejiuzulu?

Huku tatizo nini?

Makame Mbarawa ni mwislamu, na mzanzibari vile vile,

Mbona hajiuzulu kama Siame?
 
Salaam, Shalom!

Ziku chache zilizopita, palitokea taarifa njema za uwajibikaji Kwa waziri wa Serikali ya MAPINDUZI Zanzibar Kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kuadimika Kwa Pombe visiwani humo akituhumu kubadilishwa waagizaji. Waziri aliyejiuzulu ni Waziri wa Utalii na mambo ya kale ndugu Siami.

Kinachoshangaza zaidi ni kiongozi wa CCM aliyechukua hatua hiyo ya kuwajibika tofauti na Mategemeo ya wengi kuwa CCM ni wagumu kijiuzulu kukwepa uwajibikaji.

Ninachojiuliza kuwa, ikiwa uwajibikaji Kwa hatua ya kujiuzulu ni Kwa viongozi Kutoka Zanzibar, mbona Hali hiyo haitokei Kwa viongozi wenye asili ya Zanzibar wawapo huku bara kwenye Muungano? Mfano mzuri ni Waziri wa uchukuzi Makame Mbarawa.

Ndugu Makame Mbarawa amepitia tuhuma za wazi kama ununuzi wa Vichwa vya treni chakavu nk nk lakini mbona hawajibiki Kwa nafasi yake?

Tuliambiwa SGR itaanza mwezi January 2024, lakini Leo ni February 2024, halijaanza route lakini waziri Mbarawa hachukui uwajibikaji kama wenzie Zanzibar wafanyavyo.

1. Pesa za kigeni Hadi sasa zimeadimika, waziri husika mbona hawajibiki Kwa nafasi yake?

2. Umeme ni kizumgumkuti, mbona waziri wa nishati hawajibiki Kwa nafasi yake?

3. Ujenzi holela wa vituo vya mafuta katika makazi ya raia umeendelea kushamiri, na Waziri husika aliapa kulikomesha, sasa ameshindwa kuchukua hatua na hawajibiki Kwa nafasi yake, kwanini?

4. Sukari haipatikani, na Bei ziko juu Hadi 5000 Kwa kilo, lakini waziri husika mbona hawajibiki Kwa nafasi yake?

Mawaziri na viongozi wengine wa kisiasa na watumishi wa Umma, tafadhari igeni ukomavu aliouonyesha Ndugu Simai, aliyekuwa waziri wa Utalii na mambo ya kale, Kutoka Zanzibar, jambo hili ni zuri kuhakikisha wananchi wanatumikiwa Kwa HAKI na uharaka.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿.

Karibuni🙏
Kamba zetu za kula tumuachie bani🤔
 
Back
Top Bottom