CCM yakana kumhoji Simai

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,816
4,566
Chama cha Mapinduzi CCM Jimbo la Tunguu kimekanusha taarifa zilizoenea kwenye mitandao ya kumwita Mwaakilishi wa Jimbo hilo kwaajili ya kumhoji kwenye kamati ya maadili

Akizungumza na wasafi media Mwenyekiti wa CCM Jimbo la Tunguu Mtumwa Ali Mgeni amesema kuwa kikao kilichofanyika leo ni kikao cha kawaida cha kamati ya siasa na sio kikao cha maadili hivyo amewataka wananchi kutoeleza taarifa ambazo hawana uhakika nazo

Aidha ameongezea kuwa kikao hicho kililenga kujadili hali ya siasa ndani ya Jimbo pamoja na tathmini ya maendeleo Jimboni humo

Alipohojiwa Simai alisema yeye hana mamlaka ya kueleza kilichofanyika kwenye kikao lakini alisema kilikua ni kikao cha kawaida

Taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ambazo zimekanushwa na Mwenyekiti huyo zilieza kuwa Simai ameitwa kuhojiwa kutokana na uamuzi wake wa kujiuzulu uwaziri na kile kilichoelewa kumjibu Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali.

Pia soma:
- Zanzibar: Simai Mohamed Said, Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale ajiuzulu siku mbili baada ya kutangaza uhaba wa pombe kwenye hoteli na migahawa
 
Laiti nchini kwetu Tanzania kungekuwa na Utawala wa haki na sheria basi tungekuwa na viongozi wengi sana imara walio na uchungu wa kuipambania nchi yao.
 
Back
Top Bottom