Kada aliyefukuzwa kwa kutomheshimu Rais Mwinyi adai kuna jambo linafichwa kujiuzulu kwa Waziri Simai

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120

ZANZIBAR: Mwanachama zamani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mohamed Shamte amedai kuwa suala la kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, Simai Mohamed Said lina kitu ambacho hakiwekwi wazi juu ya uamuzi huo.

Shamte ambaye alifukuzwa uanachama wa CCM mwaka 2022 kwa kilichoelezwa kuwa ni kutomheshimu Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi, amesema kama kitu hicho kitaendelea kufichwa, kuna Mawaziri wengine watajiuzulu.

Mwanasiasa huyo ambaye amekuwa akitajwa kuwa na misimamo inayopingana waziwazi na kilichokuwa chama chake (CCM) ameongeza kuwa kujiuzulu kwa Simai ni sehemu ya Demokrasia ya Vyama vingi.

Ikumbukwe, Januari 24, 2024 Simai aliilalamikia Bodi ya Vileo kubadilisha Mawakala wa kuingiza Vinywaji Zanzibar. Januari 26, 2024, Simai aliamua kuachia nafasi yake katika Serikali ya Zanzibar akidai mazingira yake ya kikazi si rafki kwake.
 
View attachment 2884263

CCM ni mivurugano kote kwa dada na kaka na hiyo mikorogano si kwa maslahi ya mataifa haya mawili bali ni makundi kuelekea 2025, maslahi binafsi na maokoto

Sent using Jamii Forums mobile app
 
fine,
and that is your opinion
BREAKING: Chanzo chetu cha uhakika kinatutaarifu kwamba, Mh. Simai amejiuzulu kutokana na swala la ufutwaji wa leseni za kampuni 3 za vileo. Huu ni uamuzi ambao umefanywa na Rais Hussen Mwinyi ili makampuni yake yachukue hizo nafasi. Tuna taarifiwa kuwa Mwinyi ana ikamua Zanzibar
20240127_102607.jpg
20240127_102603.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siasa Siasani, Fitna, Chuki, Husda, Roho Mbaya, Umimi, Undugunization
CCM Jamani Imetushinda Tabia Imeoza Sana
 
Back
Top Bottom