Yuko wapi yule dereva "Giriki" wa basi la Tawaqal?

Mkuu huyu Giriki simjui ila wanaomjua mambo zake wapo humu wanathibitisha makorokocho yake ya udereva.
Giriki ni kweli alikua anakimbiza sana bus na sifa yake kuu hajawahi pata ajali alikua makini mno mimi nimepanda bus zote alizoendesha maana kila mwenye bus mpya anapanda dau ili kutengeneza soko ila zingine ni chai tuu sio katili wala hana roho mbaya ya kuwasababishia watu ajali na alikua na roho ngumu mno kwa kutowaogopa trafiki na polisi yeye dakika chache kupelekwa central bus na abiria ilikua kitu cha kawaida ilifikia mpaka RTO wa Iringa akatoa angalizo kwake akipita na bus yeyote akiiendesha ataenda jela ikabidi abadili njia ya Mwanza aliipoona wanamfatilia akaingia kwenye maroli ya songea yanayobeba makaa ya mawe sasa hivi alikua kwenye roli za Tanzania zinazopeleka mizigo DRC mimi mwenyewe alikua rafiki wa ndugu yangu ila nikiona dereva ni yeye hilo bus narudisha tiketi nisharudisha mara mbili ukikata unaambiwa dereva sio giriki baadae ukimuona unaleta uzushi na tiketi wanarudisha fedha kwa sababu ishu ikiwa mbaya wanajua jamaa ana misala vituo vyote vya barabarani bora mmalizane mnazi mmoja hapo...
 
mtemiwaWandamba! Hawijeee!!! Hawijeee!! Kaimuka Bamboo!! Ha ha ha! Long time kitambo!

Nimeishi kwa miaka mingi sana huko Kilombero miaka ile ya 90's mpaka mwanzoni mwa 2000!! Nimeishi Nyandeo, Mang'ula, Ifakara, Mahenge, Namwawala, Chita,nk.
DAh! Kwa hiyo Tate umepanda zile Bus za Charongite, Bangaseka na Said Abeid toka Ifakara to Namwawala!
 
Daaah. Na sisi wa enzi za Kiswele na Comfort tujikumbushege basi
Kuna siku nikiwa mtoto nilikabidhiwa kwenye kiswele Dar-songea ..kufika tanangozi gari ikashika Moto bahati nzuri abiria wote tulipona lkn mizigo iliungua..nilikuwa mdogo hata sijui nilitokaje kwenye Basi mule....konda kajisahau anakumbuka kwamba alikabidhiwa mtoto gari limeshateketea..ananitafuta kumbe mie nilijiokoa kitambo
 
Back
Top Bottom