Dereva wa basi namba T331 BMM achunguzwe haraka kabla hajaua watu!

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
36,082
40,734
Dereva wa basi hili namba T331 BMM jana tarehe 04/08/2023 wakati tunaelekea Dodoma alinifanyia overtaking mbaya sana na kidogo anisababishie ajali.

Kani-overtake bila tahadhari ya kutosha ambapo kulikuwa na Semi-trailer inakuja kwa kasi kwenye njia yake ya kurudi Dar, hamadi Uso kwa Uso anakuta na nalo mita chache tu mbele yangu.

Isingekuwa huruma kubwa , na ujasiri wa kutisha wa yule mwenye semi, kwa kweli angelisaga lile basi pale pale na abiria wote. Dereva wa Semi aliamua kujitoa mhanga kwa kulitupa semi lake kwenye korongo, basi na basi ndio likapata upenyo wa kutoba maana alikuwa anatuovertake wawili kwa mpigo, na lililokuwa mbele yangu lilikuwa lorry kubwa pia, na halikumpa upenyo hata kidogo.

Lile semi lilipoingia korongoni likadunda kama kitenesi na kurudi kwenye lami katika angle iliyokuwa ikinielekea mimi, hamadi na mimi naangaliana nalo uso kwa uso, nikifikira nina watoto nimepakia nyuma, moyo ulisimama ghafla!!

Basi kwa huruma kuu, na ujasi wa ajabu sana, akalirudisha kwa kasi kunikwepa na kuliingiza tena korongoni, bila kujali kwamba angeweza kufa yeye, na sisi ndio tukapona hapo. Kuangalia kwenye side mirror nikaona limedunda tena na kurudi barabarani, akalistabilize na kuendelea na safari. Nilishukuru sana Mungu.

Ila kama kawaida, mimi jambo halipiti hivi hivi, nilimfukuzia hadi nikampata walau nipate namba za gari, maana hata abiria anaondesha kila siku wapo hatarini, na picha hiyo hapo chini.

5782E0DE-0678-4DC3-BEFB-80BF5D737561.jpeg


Nilikamripoti kwa moja wa wana usalama barabarani, na wakafanya mawasialiano na watu wa mbele walau apigwe faini, nadhani walimpiga faini pale pale, ila naona haitoshi!
 
Shida ndiyo hiyo, maana hata hiyo faini angeweza kuikana, ndio maana sijasema akamatwe wala kufutiwa leseni, bali achunguzwe...!
Tena anaikana mbele ya abiria ambao nusura awaue na wanakaa kimya. Hivi sisi ni ujamaa wa nyerere ndo umetufanya hv au ni nini? Hatuwezi kuwajibishana kabisa.
 
kuna haja sasa, dunia ya kidigitali barabara kufungwa Camera.
Hapo ndipo nchi hii inafeli,yaani watawala wameshajua upumbavu wa watanzania ndio mtaji wao, wenzetu sasa wanaanza kutumia demerits systems, yaani kila mwaka dereva anapewa 12pts, za kutumia mwaka mzima, zikiisha kabla driving license yake automatically inajifunga,kwa kosa hapo juu, huyu dereva wa bus la abiria angepoteza pts zote, na mwisho madereva hawa wa public transport ni lazima pia wawe na PDP ili waendeshe magari haya
 
Sheria butu+ barabara finyu na mbovu+ madereva wapumbavu+ matrafic wala rushwa

Hii nchi imeoza
Vunja jeshi la police, wote above 40yrs wastaaafishwe kwa manufaa ya umma, Botswana 🇧🇼 traffic officer's wamethibitisha kuwa zero corruption kwenye barabara inawezekana, Zambia 🇿🇲 they doing well na sasa hakuna check points from Lusaka hadi livingstone (more than 500km),Dar hadi Moro (200km)kuna check points zaidi ya 20!!
 
Back
Top Bottom