Abiria wa Mwendokasi tuliotakiwa kutoka Kivukoni kwenda Kimara, Dereva katupeleka Morocco kisha akaturudisha Kivukoni

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
WhatsApp Image 2024-03-27 at 00.15.43_6c50a4e3.jpg
Jana Machi 26, 2024 nikiwa kwenye Kituo cha Mwendokasi cha Kivukoni, kulikuwa na nyomi la hatari mida ya jioni, mabasi mengi yalikuwa yamepaki pembeni na machache yaliyokuja hayakukidhi haja ya huduma iliyotakiwa kutolewa.

Watu walikuwa wengi na wengine wakionekana wanataka kuwahi kwenda kupata futari.

Tukiwa katika hali hiyo, Saa 1:00 Usiku likaja basi kushusha abiria Namba zake za usajili T 591 DWR, baada ya kumaliza kala halijaanza utaratibu wa kuja pale tulipokuwa tumepanga foleni ya kwenda Kimara, Dereva wa Basi hilo akaanza kupandisha Wafanyakazi wenzake na baadhi ya Walemavu.

Wakati akifanya hivyo idadi ya aliokuwa akiwapandisha ni kubwa, ikabidhi watu waanze kuvamia nao waingie bila kufuata utaratibu, nami nikachoma ndani.

Dereva akatutaka tushuke, watu tukakaza, kaona sasa atukomeshe, badala ya Kwenda Kimara akatupeleka Morocco, huko napo watu wakakaza kushuka, eti alitaka tushuke pale.

Baada ya ubishi wa muda mrefu akachoma mafuta akaturudisha Kivukoni, huko napo abiria wakakaza, akaja Msimamizi wake, naye badala atumie busara, akaanz kutuambia “Nyie si mnajifanya vichaa, sasa sisi vicha zaidi yenu, leo mtalala hapohapo.”

Kulikuwa na vijana na madogo kibao wanafunzi wakaanza kuimba nyimbo kama vile wanaandamana.

Ndipo kuna mtu mzima mmoja nikaona ameshika simu akampigia Waziri Mohammed Mchengerwa, akamweleza kinachoendelea, kwanza Waziri hakuamini, akamwambia apige picha au arekodi video amtumie, yule mdingi akafanya hivyo.

Ndipo baadaye nasikia huyu bosi mpya wa Mwendokasi naye akapiga simu na kusema anakuja eneo la tukio, kusikia hivyo yule supervisor na dereva wake wakasepa, wakaona msala huo.

Tukapata dereva mwingine safari ya kuondoka Kivukoni ikaanza Saa 3:25 Usiku, tukafika Kimara almost saa Nne usiku.

Imagine tumekata tiketi Saa 12 Jioni kisha tunafika Kimara Saa Usiku.

Hawa madereva wa Mwendokasi nadhani wanatakiwa kuangaliwa saikolojia ya akili yao, pia huduma kwa ujumla za Mwendokasi ni janga.

Serikali ina kazi kubwa ya kufanya katika huu mradi.

Majibu ya DART - DART kuchukua hatua dhidi ya Dereva na Wasimamizi wa Mwendokasi waliowapeleka Abiria Morocco badala ya Kimara

- DART yawasimamisha kazi Maafisa wa Mwendokasi walioshindwa kudhibiti vurugu zilizotokea Kituo cha Kivukoni
 
Itakuwa hawalipwi mishahara yao.

NDIO MAANA WANAWAKOMESHA ABIRIA MSIOKUWA NA HATIA NA MAGARI.

PambanaZaidi/CottonandMore
 
Jana Machi 26, 2024 nikiwa kwenye Kituo cha Mwendokasi cha Kivukoni, kulikuwa na nyomi la hatari mida ya jioni, mabasi mengi yalikuwa yamepaki pembeni na machache yaliyokuja hayakukidhi haja ya huduma iliyotakiwa kutolewa.

Watu walikuwa wengi na wengine wakionekana wanataka kuwahi kwenda kupata futari.

Tukiwa katika hali hiyo, Saa 1:00 Usiku likaja basi kushusha abiria Namba zake za usajili T 591 DWR, baada ya kumaliza kala halijaanza utaratibu wa kuja pale tulipokuwa tumepanga foleni ya kwenda Kimara, Dereva wa Basi hilo akaanza kupandisha Wafanyakazi wenzake na baadhi ya Walemavu.

Wakati akifanya hivyo idadi ya aliokuwa akiwapandisha ni kubwa, ikabidhi watu waanze kuvamia nao waingie bila kufuata utaratibu, nami nikachoma ndani.

Dereva akatutaka tushuke, watu tukakaza, kaona sasa atukomeshe, badala ya Kwenda Kimara akatupeleka Morocco, huko napo watu wakakaza kushuka, eti alitaka tushuke pale.

Baada ya ubishi wa muda mrefu akachoma mafuta akaturudisha Kivukoni, huko napo abiria wakakaza, akaja Msimamizi wake, naye badala atumie busara, akaanz kutuambia “Nyie si mnajifanya vichaa, sasa sisi vicha zaidi yenu, leo mtalala hapohapo.”

Kulikuwa na vijana na madogo kibao wanafunzi wakaanza kuimba nyimbo kama vile wanaandamana.

Ndipo kuna mtu mzima mmoja nikaona ameshika simu akampigia Waziri Mohammed Mchengerwa, akamweleza kinachoendelea, kwanza Waziri hakuamini, akamwambia apige picha au arekodi video amtumie, yule mdingi akafanya hivyo.

Ndipo baadaye nasikia huyu bosi mpya wa Mwendokasi naye akapiga simu na kusema anakuja eneo la tukio, kusikia hivyo yule supervisor na dereva wake wakasepa, wakaona msala huo.

Tukapata dereva mwingine sfari ya kuondoka Kivukoni ikaanza Saa 3:25 Usiku, tukafika Kimara almost saa Nne usiku.

Imagine tumekata tiketi Saa 12 Jioni kisha tunafika Kimara Saa Usiku.

Hawa madereva wa Mwendokasi nadhani wanatakiwa kuangaliwa saikolojia ya akili yao, pia huduma kwa ujumla za Mwendokasi ni janga.

Serikali ina kazi kubwa ya kufanya katika huu mradi.
Poleni watu wa MBezi na Kimara kilio chenu haukuna anaewasikia
 
Yaan umasikin unakusumbua...mi ningeshuka kuliko kupoteza masaa yote hayo...hivi ninyi muda kwenu huwa unasimama eeh....jaman hakuna serikali itayo hudumia familia yako...yaani mmekaa kama mazombi masaa zaid ya manne sa si bora hata mngeshusha kipondo kwa huyo dereva...unakuja lia lia jamii forum huku....mla kasa mkubwa wewe..
 
Sasa na nyie ndugu zangu watanzania ni wajinga kiasi fulani.
Mtu anapakia walemavu na staff wengine,nyie kiliwawasha nini kuvamia mkapande wakati hamuhusiki? Ingekua mwendokasi inaendeshwa na Jeshi ingetakiwa walau mkashushiwe lugalo walau na bakora mbili mbili za matako.
Jifunzeni ustaarabu
 
Mwendokasi ni usafiri special au
 
Back
Top Bottom