Yathibitishwa, Dr Ndalichako aondoka NECTA

Yathibitishwa, Dr Ndalichako aondoka NECTA

Tunataka hiyo nafasi aishike Muislaam haijawahi kushikwa na Muislaam toka ianzishwe ili kupunguza machungu na makali ya kuonewa na Ndalichako.
Kumbe Ndalichako ndo alikuwa anawafanyia mitihani na kusahihisha mwenyewe!!!!! Ooh
 
Huyu Dau alikataliwa kwa udini au ni kushindwa ku-perform? Je, NSSF ni kigango cha parokia ipi? Jamani, watu acheni kuonesha ujinga wenu kwenye kadamnasi. Kwani hilo ni shirika la dini? Kweli mwasisi wa udini nchi hii alifanya jambo baya mno.

Hawa viumbe wanaopenda kubebwa bila wao wenyewe kujibidiisha wamekuwa sababu ya majanga kila kona ya Nchi hii,Mwangalie Dau anavyoiharibu NSSF bora JK amalize muhula wake tu tupate Rais mwenye akili timamu...I am sick of him!He is the reason why this Country is going down the toilet!!!
 
Faizafoxy;
Muislam ni nani na mkristo ni nani? Kwa tafsiri ya mkristo mimi kama mkristo; NI MTU ANAYEISHI KATIKA MISINGI YA KIKRISTO,MWENYE TABIA KAMA KRISTO.Hivyo mlevi,muongo,mwizi,mzinzi nk kwa tafsiri ya ukristo si mkristo ni mtu mwenye jina la kikristo kama wewe ulivyo na jina lako.Majina yasikuzuzue tu!

Katika siku ambazo nimeukubali mchango wako ni leo.
Kwa upande wngu nilikuwa sijua kuwa hata ninyi mnaweza kuwatofautisha kwa njia hii.Ina maana mlevi na mzinifu sio mkiristo mbona wengi hawalijui hilo!
 
Au dada umezungumza hivi ulikuwa kwenye heat??????? Maana ya kuwa kwenye heat mfano ng'ombe jike akiwa kwenye heat ni vurugu kali za kutafuta madume yampande sasa dada yangu kwa statement yako madume yamekupanda fuatilia comments walizotoa dhidi ya statement yako

Wewe ungekuwepo duniani bila mama'ko kuwa kwenye heat? wala hilo usilionee ajabu ni nature.

Madume ulitaka wakupande wewe? unanchekesha!
 
Hivi ww darasa la ngapi? Kati ya waziri na ndalichako nani mwenye nguvu? Hata baraza liwe la waislam wote bado si solution. Je hii itasaidia huhamasisha waislam kusoma kwa juhudi? Si pingi ulichosema lkn kwa maoni yangu hii itakuwa hatari km performance ya wanafunzi wa kiislam itaendelea kuwa mbaya zaidi ina maana ukweli utajulikana

Wewe panda ushuke, darasa langu hulipati hilo amini nakueleza.

Wewe unafikiri Waziri ndio anafanya kazi ya kusahihisha mitihani au hiyo ni kazi ya Ndalichako? Soma ujuwe unachokiandika.
 
Ponera
1---Hakuna asiejua chanzo cha mgogoro wa kufeli kwa vijana wetu kwenye somo la Islamic Knowledge,na ufafanuzi ulishatolewa na kwangu mimi ufanunuzi uliotolewa una mashiko kwa sababu tatizo la kimfumo lililosababisha tukio lile liletolewa ufanunuzi na iliundwa kamati ya viongozi wa kiislamu kwenda kuangalia uhalisia wa mambo ulivyokuwa na naamini wao waliridhika ma majibu yaliyopatikana au yaliyotolewa.
2---Katika mchango wa awali nimemuomba FaizaFoxy na hata Ritz na pia nakuomba na wewe Ponera ujitahidi kufanya uchunguzi wako kwa kuwauliza walimu ambao wanakwenda kusahihisha mitihani wakueleze utaratibu wa usahihishaji uko vipi ili mjue kwamba ni vigumu sana kumhujumu mwanafunzi mmoja mmoja au wengi kwa kutumia kipengele cha shule anayotoka au jina lake,hii itawasidia kupata ukweli ili kupunguza hizi chuki baina yetu sisi wananchi
3---Katika michango yangu iliyopita nimejaribu kuongea kufeli kwa wanafunzi kwa ujumla bila kujali dini ya mtu au wewe Ponera unaridhika na matokeo ya vijana wetu?unafurahia vijana wetu kupewa madaraja ya ufaulu ambayo hawakustahili?unajenga taifa gani?makosa yaliyofanyika miaka iliyopita ndio yameleta madaktari wanaopasua kichwa badala ya mguu,mafisadi tulionao sasa hivi,wanasheria wasiojua kulinda maslahi yetu kwenye mikataba mablimbali nk
4---Sina uhakika hawa wasomi waliopewa madaraja wasiostahili watakuja kufanya nini au madhara watakayoleta wakati ujao siyajui,tuombe mungu atupe uhai.
Umeandika vizuri,tatizo hufahamu kitu kimoja uchakachuaji haufanywi wakati wa usahihishaji, uchakachuaji hufanywa wakati wa kuingiza data kwenye computer kwa ajili ya kutoa matokeo,Ndio maana waislamu wengi wasiolizika na matokeo na wanapoenda kudai matokeo watazane scripts zao wanakuja kugundua kuwa wamefaulu kwa daraja la juu sana,watu mkuu hawakurupuki. Hilo ndalichako analijua.
 
Dr Joyce Ndalichako>Charles Msonde

Hapa wahuni akina Mohamed Said na Ponda Issa wameula wachuya,

Walidhani atashika Imamu nafasi hiyo.
 
Hawa viumbe wanaopenda kubebwa bila wao wenyewe kujibidiisha wamekuwa sababu ya majanga kila kona ya Nchi hii,Mwangalie Dau anavyoiharibu NSSF bora JK amalize muhula wake tu tupate Rais mwenye akili timamu...I am sick of him!He is the reason why this Country is going down the toilet!!!
Tatizo lako unaongea ukiwa na chuki za kidini zimekukaa kichwani kwako. Fanya utafiti,usiongee kwa kukurupuka, hivi unafikiri katika mifoko yote jamii ni upi unaofanya vizuri kama siyo NSSF. Kaa ufikiri Dr Dau ni level nyingine ile.Kwa taarifa yako Dr Dau hakuteuliwa na Kikwete,muulize mpaka vigezo gani alivitumia kumteua, alimwona kuwa yeye ni machine.
 
mkuu bandiko lako nimelipenda hata mimi naungana nawe 100% sio rahisi kumhujum mwanafunzi kwa kigezo cha dini"

Ndugu yangu Cheche Mtungi

Mimi by professional ni mwalimu na nafundisha katika moja ya hizihizi shule za Sekondari za kata ktk moja ya wilaya na mkoa kanda ya ziwa.Nina miaka kumi na tano sasa (nimeanza kazi mwaka 1998). Hivyo mm niko field na ninaelewa na nakuelewa sana kwa kila unachoandika na wengine wanajaribu tu kuingiza siasa ktk hii kitu ELIMU. Ndugu yangu tunapambana na mataizo mengi sana ktk kazi yetu hii na hasa ktk awamu hii ya JK!!..

Pamoja na matatizo mengi ya msingi uliyaeleza yanayousonga mfumo wetu wa elimu, mimi pia naona kuna matatizo mengine mawili ya msingi ambayo yamekuja na kubadili kabisa mwelekeo wa elimu yetu;
  1. Kuifanya elimu isimamiwe na zaidi ya wizara mbili kwangu mimi kama mwalimu hili ni tatizo la msingi limetuletea matatizo zadi kuliko ufumbuzi wa yale yaliyokuwapo
  2. Sisi walimu tunadharauliwa sana na serikali hii na wakati huohuo tunabebeshwa lawama zote kila kunapotokea kufanya vibaya kwa wanafunzi tunaofundisha,mfano ni mtihani wa kdt cha 4 mwaka 2012 sehemu kubwa ya lawama zilitupwa kwetu kwa sbabu ndiyo sehemu ya wanasiasa kuficha udhaifu wao. Hili sisi walimu kudharauliwa limeshusha sana morali ya kazi ya walimu. Mfano ni walimu kuendelea kudai madeni yao miaka na miaka,madeni yasiyoisha ya malimbikizo ya mishahara,likizo,uhamisho nk. Na hakika mimi nilishashindwa kuelewa ni mfumo wa namna gani unaotumika kuendesha mambo ktk serikali hii. Mfano hai kabisa ni mimi mwenyewe nadai malimbikizo ya mshahara wangu ya tangu mwaka 2008. Nimeandika barua na barua, nilishafika mpaka wizara ya elimu lakini wapi bwana, nilishakata tamaa na nimeamua labda mpaka watakapokuja jisikia watanilipa. Huyu ni mimi, sasa jiulize ni walimu wangapi wako ktk hali hii? Watakuwa na moyo wa kufanya kazi? Halafu,nikuchekeshe kitu? Siku hizi hata ukiandika barua ya jambo lolote iwe unadai au kuomba kitu chochote ni nadra sana kujibiwa!!.....Ukitaka majibu basi wewe mwenyewe ufuatilie kwenye hizo ofisi na utapambana na urasimu balaa wenye kila harufu ya rushwa!

Kwa hiyo ndugu hawa ndo sisi walimu!
BEDO NYALUTOGO na Kitaturu
1---Ni vizuri tukajadili mambo kwa hoja ambazo zinaweza kuijenga nchi yetu,ndio maana inabidi tuelimishane kidogo matatizo yetu makubwa yaliyosababisha mpaka tukafikia hapa, haya maneno ya Ponera na Dada FaizaFoxy hayajengi zaidi ya kubomoa,hakuna mtanzania hasa hasa huku bara ambae hana ndugu mkristo au muislamu,sasa kama tunaacha kujadili mambo muhimu humu na kuanza kuhubiri udini hautufikishi popote kila mtu afikirie tatizo la elimu kwa jicho la tatu,tuchunge sana midomo yetu na tuache ubinafsi,tuweke misingi ya upendo ili watoto wetu wakute kuna kitu tulifanya sisi kama wazazi wao.
2---Tuyajadili matatizo yetu kwa njia ambayo inatoa majibu ya matatizo yetu,sio kulalamika,tuwaeleze wanaotuongoza wapi wamekosea bila kuoneana haya,na wanaokosea wawajibike,mimi sikatai mama Ndalichako kuondoka pale maana hawezi kukaa pale maisha,kama urais unabadilishwa kwanini Ukatibu Mtendaji usibadilishwe?lakini hatupaswi kuweka viongozi wetu kwa misingi ya UDINI,hili ni kosa na kila mtanzania alikemee kwa nguvu zote,tuweke watu ambao wataweza kusimamia taratibu zilizowekwa,siasa ziondoke kwenye mambo nyeti hasa elimu,haiingii akilini mwanafunzi ameanza darasa la kwanza mpaka la saba hajui kusoma na kuandika halafu tunacheka,mwanafunzi anaanza kidato cha kwanza mpaka cha nne hajui kuandika halafu tunacheka,kibaya zaidi tunataka aongezewe daraja ili aende kidato cha nne au chuo cha ufundi,atatusaidia vipi mwanafunzi huyu?
3---Tuwaambie hawa viongozi wetu kwamba turudishe zile kali mbiu za zamani za PANDA MTI KATA MTI,na miti tunyoikata tutengeneze madawati ya watoto wetu,sio kusafirsha magogo ulaya na china,tuwaambie na tukatae haya wanayoyafanya,nchi inakuwa jangwa,mvua hazinyeshi,miti inakatwa kila siku,watoto wetu hawana madawati hivi hamuoni kuwa haya ni matatizo ya msingi ya kuwaambia hawa watawala wetu?
4---Walimu wetu hawana maisha mazuri,mazingira ya ufundishaji mabovu,hawana nyumba za kuishi,wao wameuzia nyumba zoote za serikali nchi nzima,wanakaa maeneo mazuri na watoto wao,wanakula vizuri na watoto wao wanasoma shule za bei mbaya,sisi tumekaa kimya tu,na inawezekana wanaua elimu yetu na ya watoto wetu maskini ili wawe wajinga wa kufikiri ili waendelee kutawala,kwa elimu hii ya shule za kata,interview ya kiingereza,kujuana kama kawaida,ushindani wa ajira unaanzia kwenye matokeo ya kidato cha nne mpaka chuo kikuuu,unafikiri mtoto wangu anaesoma shule ya kata atapata kazi BOT au TRA?,ataisia kufanya kazi kwenye makaampuni ya ulinzi basi.
5---Wana JF tuwe na hoja na tuache udini,nchi hii ni yetu sote.
 
Last edited by a moderator:
Dr Joyce Ndalichako>Charles Msonde

Hapa wahuni akina Mohamed Said na Ponda Issa wameula wachuya,

Walidhani atashika Imamu nafasi hiyo.

Hatutaki ashike Imamu au askofu,tunataka nafasi ishikwe na mtanzania yeyote mzalendo na mwadilifu kwa nchi na watanzania wanzake. Dr ndalichako mwenyewe kajinyang'anya tonge mdomoni kwa kuendekeza udini wake,tena bora ameondoka mwenyewe kabla ya maandano ya kumshinikiza atoke. Alikuwa analihujumu taifa,waliomtuma wako kimya sasa.Huyo ndiyo sababu ya Tanzania kuwa masikini,wenye uwezo wanafelishwa,vilaza ndiyo wanaopitishwa.Haishangazi kuona mang'orofa yakidondoka ni wasomi wa mama ndalichako wanaopewa maksi zisizo zakwao tukikutananao advance wanachemka.
 
Hapo hajawahi kushika Muislaam toka paanzishwe. Ikiwezekana kila nafasi kama usemavyo, itakuwa ni vizuri sana kwani wenzetu hamfundishwi kuongoza mnafundishwa kuongozwa (kondoo) tu.

Polycarp Pengo akiingia Uislaam kama wanavyoingia wachungaji wenzake kwa makundi itakuwa ni vyema sana, atakuwa kajijuwa kuwa alipotea na kupoteza wenzake. Hana msamaha ila akiingia kwenye Uislaam tu.
ndgu yang big up sana kwa michango mizuri sana japokuwa inawauma sana! Allah akuzidishie.
 
Hatutaki ashike Imamu au askofu,tunataka nafasi ishikwe na mtanzania yeyote mzalendo na mwadilifu kwa nchi na watanzania wanzake. Dr ndalichako mwenyewe kajinyang'anya tonge mdomoni kwa kuendekeza udini wake,tena bora ameondoka mwenyewe kabla ya maandano ya kumshinika atoke.
hivi mkuu unaweza kunipa ushahidi wa udini wa Dr Ndalichako??
 
Back
Top Bottom