Kitaturu
===>Nashukuru kwa kunisaidia,Ndalichako ni mtu mdogo sana ambae hata kama angeondoka jana asingeweza kubadilisha matokeo ya watoto wetu,yapo matatizo ya msingi sana kwenye elimu yetu ambayo tunayachekea kwa sababu ya kuchonganishwa na haya mambo ya udini.
===>Mfumo wetu wa elimu umeyumba sana hapa nchini,nataka nimuulize Dada
FaizaFoxy kwa nini watoto wetu hawa wakiwa kwenye shule za msingi zile za academia wanasoma masomo yote kwa kiingereza isipokuwa somo la kiswahili lakini kwenye shule za maskini wanasoma kiswahili masomo yote isipokuwa kiingereza
===>Zamani kulikuwa kuna utaratibu wa kufunga na kufungua shule pamoja nchi nzima,hii ilikuwepo mpaka kwenye vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu,hii iliwezesha serikali kuweza kusimamia michezo kwenye ngazi shule ya msingi kwa maana ya (UMISHUMTA) na michezo ya shule za sekondari (UMISETA) ambayo kama sikosei ilikuwa ukifanyika katika kipindi cha mwezi waa sita ie wakati wa likizo maana shule zoote zilikuwa zimefunga kipindi hicho,sasa hivi hili haliwezekani,maana kuna shule za academia kipindi cha mwezi wa sita wao ndio wako darasani,wale kayumba ndio wamefunga,sintofahamu hii iko mpaka kwenye michezo ya michezo ya vyuo vikuu ambayo inaitwa SHIMIVUTA,mpaka muda huu UDSM wamefungua chuo sijajua taasisi nyingine,kichekesho kiko hapa wakati wao wako kwenye wiki za mitihani (test) ie labda wiki ya 8 na kuendelea,muda ambao watakuwa wamefunga ndio ilitakiwa waende kwenye michezo ya SHIMIVUTA,lakini haiwezekani maana vyuo vingine ndio navyo vinakuwa kwenye mitihani.
===>Kuna vijana katika nchi hii wamebadilishiwa mitaala ya Phsysic,Chemistry na Biology sijui waliita soma gani tu,hawa nao ni tatizo tayari,hembu fikiria watakapoomba kusoma kwenye vyuo vya nje ambavyo vianutambua mfumo wetu wa elimu unafikiri watatufikiriaje mara wanapoona vyeti vya hawa vijana?
Tusibishanie mambo ya ukristo na uislamu,ajenda ya udini inatufanya tusiwe na mshikamano wa kutatua matatizo yetu,tunagawanywa mpaka tunashindwa kumgundua mchawi wetu.