Yathibitishwa, Dr Ndalichako aondoka NECTA

Yathibitishwa, Dr Ndalichako aondoka NECTA

Kwa hiyo kwa kuondolewa Ndalichako kitakuwa kitengo cha Bakwata au Answar Sunna? Sasa ni bora liende.

.............kile kigango kilikomaa mpaka kuwa parokia !.........Sasa kaanza Paroko kung'oka !:amen:
 
Tunataka hiyo nafasi aishike Muislaam haijawahi kushikwa na Muislaam toka ianzishwe ili kupunguza machungu na makali ya kuonewa na Ndalichako.

Hapo kwenye red ni nyie wangapi??
 
Pumba zote za nini hizo? soma hapa: Home

Duh FaizaFoxy!!...Mbona wewe unaaaonekana ni mama mmoja "mstaafu" mshari sana,usiyependa kujadiliana kwa hoja!!??...Hii taarifa imejibu hoja za huyo jamaa kweli? Mbona nao wanalalamika tu kuwa waislamu wanahujumiwa na kufelishwa pasipo kutuambia wanafelishwa/kuhujumiwa kivipi? Hivi inawezekana kweli kwamba Dr Ndalichako akaamuru mfumo mzima wa Baraza zima la Mitihani uwanyonge au uwafelishe au uwahujumu waislamu na uwabebe wa dini zingine na hasa wakristo? Kivipi na yeye ni nani hasa hata aweze afanye hivi? Hebu naomba nielimishwe namna hili linavyowezekana!!

Otherwise umeshindwa kujibu hoja za jamaa ambazo mimi pia nazikubali; kwamba mfumo wetu wa elimu kwa ujumla wake una matatizo lukuki nje ya baraza la mitihani na matatizo/mapungufu haya yanamuathiri kila mtoto/kijana na pia kila mmoja wetu bila kujali dini yake kwa maana ya mkristo au muislamu au hata wasio wa dini hizi!!..Tukidhani kuwa tatizo ni NECTA na Dr Ndalichako aisee tutakuwa tunapotea ile mbaya na jamaa kasema..... we will be fighting the wrong enemy and I think that is what some of you are doing!!..

Think about this
,tujadiliane na ombi langu kwako ni please tusitukanane!1
 
Tuache kuingiza udini katika mambo ya msingi jaman, Mwalimu nyerere alikemea udini, nyie mnaupandikiza!
Kama Ndalichako ameng'oka na atafutwe mtu mwingine mwenye uwezo wa kuchukua nafasi yake bila kujali dini wala kabila lake!
 
Tunataka hiyo nafasi aishike Muislaam haijawahi kushikwa na Muislaam toka ianzishwe ili kupunguza machungu na makali ya kuonewa na Ndalichako.

acha ujinga nchi inaongozwa na katiba na sheria kanuni hata akiwekwa nani lazima azingatie hayo! hatufanyi mambo kidini kesho mtataka mahakama, benki nk zifuate sharia hayo ni huko huko misikitini na wakristu na mambo yao huko huko makanisani!
 
images.jpeg

Uthibitisho huu umetoka kwa mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) Brof Rwekaza Mukandala kuwa Katibu Mtendaji wa NECTA Dr Joyce Ndalichako ameondoka NECTA na nafasi yake sasa inakaimiwa na Dr Charles Msonde aliyekuwa msaidizi wake.

Kwa mujibu wa Profesa Mukandala, ni kwamba Dr Ndalichako ameanza likizo ya utafiti (Sabbatical leave) ya mwaka mmoja kuanzia Oktoba mosi mwaka huu hadi Septemba 30 mwaka 2014 licha ya kuwepo kwa taarifa za kuwepo shinikizo la kisiasa lilikuwa likimzonga Dr Ndalichako kutakiwa kujiuzulu.

Nawasilisha
 
"Dr Ndalichako ameanza likizo ya
utafiti (Sabbatical leave) ya mwaka
mmoja kuanzia Oktoba mosi mwaka huu
hadi Septemba 30 mwaka 2014"
 
Duh FaizaFoxy!!...Mbona wewe unaaaonekana ni mama mmoja "mstaafu" mshari sana,usiyependa kujadiliana kwa hoja!!??...Hii taarifa imejibu hoja za huyo jamaa kweli? Mbona nao wanalalamika tu kuwa waislamu wanahujumiwa na kufelishwa pasipo kutuambia wanafelishwa/kuhujumiwa kivipi? Hivi inawezekana kweli kwamba Dr Ndalichako akaamuru mfumo mzima wa Baraza zima la Mitihani uwanyonge au uwafelishe au uwahujumu waislamu na uwabebe wa dini zingine na hasa wakristo? Kivipi na yeye ni nani hasa hata aweze afanye hivi? Hebu naomba nielimishwe namna hili linavyowezekana!!

Otherwise umeshindwa kujibu hoja za jamaa ambazo mimi pia nazikubali; kwamba mfumo wetu wa elimu kwa ujumla wake una matatizo lukuki nje ya baraza la mitihani na tukidhani kuwa tatizo ni NECTA na Dr Ndalichako we will be fighting the wrong enemy and I think that is what some of you are doing!!..

Think about this
,tujadiliane na ombi langu kwako ni please tusitukanane!1
Kitaturu
===>Nashukuru kwa kunisaidia,Ndalichako ni mtu mdogo sana ambae hata kama angeondoka jana asingeweza kubadilisha matokeo ya watoto wetu,yapo matatizo ya msingi sana kwenye elimu yetu ambayo tunayachekea kwa sababu ya kuchonganishwa na haya mambo ya udini.
===>Mfumo wetu wa elimu umeyumba sana hapa nchini,nataka nimuulize Dada FaizaFoxy kwa nini watoto wetu hawa wakiwa kwenye shule za msingi zile za academia wanasoma masomo yote kwa kiingereza isipokuwa somo la kiswahili lakini kwenye shule za maskini wanasoma kiswahili masomo yote isipokuwa kiingereza
===>Zamani kulikuwa kuna utaratibu wa kufunga na kufungua shule pamoja nchi nzima,hii ilikuwepo mpaka kwenye vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu,hii iliwezesha serikali kuweza kusimamia michezo kwenye ngazi shule ya msingi kwa maana ya (UMISHUMTA) na michezo ya shule za sekondari (UMISETA) ambayo kama sikosei ilikuwa ukifanyika katika kipindi cha mwezi waa sita ie wakati wa likizo maana shule zoote zilikuwa zimefunga kipindi hicho,sasa hivi hili haliwezekani,maana kuna shule za academia kipindi cha mwezi wa sita wao ndio wako darasani,wale kayumba ndio wamefunga,sintofahamu hii iko mpaka kwenye michezo ya michezo ya vyuo vikuu ambayo inaitwa SHIMIVUTA,mpaka muda huu UDSM wamefungua chuo sijajua taasisi nyingine,kichekesho kiko hapa wakati wao wako kwenye wiki za mitihani (test) ie labda wiki ya 8 na kuendelea,muda ambao watakuwa wamefunga ndio ilitakiwa waende kwenye michezo ya SHIMIVUTA,lakini haiwezekani maana vyuo vingine ndio navyo vinakuwa kwenye mitihani.
===>Kuna vijana katika nchi hii wamebadilishiwa mitaala ya Phsysic,Chemistry na Biology sijui waliita soma gani tu,hawa nao ni tatizo tayari,hembu fikiria watakapoomba kusoma kwenye vyuo vya nje ambavyo vianutambua mfumo wetu wa elimu unafikiri watatufikiriaje mara wanapoona vyeti vya hawa vijana?
Tusibishanie mambo ya ukristo na uislamu,ajenda ya udini inatufanya tusiwe na mshikamano wa kutatua matatizo yetu,tunagawanywa mpaka tunashindwa kumgundua mchawi wetu.
 
Nilikuwa nakuheshimu sana dada yangu lakini kwa mchango wako huu,

Umejipunguzia Heshima ya Utu wako na Umewapatia Heshima ya Mashaka

watu waliokuheshimu kwa muda mrefu pamoja na waislamu wenzako.

Nijambo la aibu ktk zama hizi kuingiza chembechembe za udini kwenye Professionalism
ktk utendaji. hupaswi kujutia kuwa muislamu, kinachotakiwa ni kusoma kwa juhudi
na mhimizane kubadilika. Nyinyi upande wa pili wa dini kuna mambo fulani mlishakosea
huko nyuma ndo kinachowatafuna hadi sasa na mnadhani adui yenu ni NECTA
chini ya NDALICHAKO, Real you are fighting the wrong enemy.

Hapa ndo mnaponikumbusha Luddism na chartism huko England.

I stand to be corrected.
ndugu unaweza ukadhani uko sahihi kumbe unakosea,waislam sio kwamba hawataki shule bali mfumo waliowekewa na watawala waliotangulia ndo umewafikisha hapo walipo, sioni tofauti waislam kumkataa ndalichako na wakristo kumsema vibaya dr dau wa nssf
 
acha ujinga nchi inaongozwa na katiba na sheria kanuni hata akiwekwa nani lazima azingatie hayo! hatufanyi mambo kidini kesho mtataka mahakama, benki nk zifuate sharia hayo ni huko huko misikitini na wakristu na mambo yao huko huko makanisani!
wewe wa wapi? mbona mabenki tayari wameshaanza kufuata sharia! nenda kcb, nbc amana pbz etc utaona.
 
peri
===>Kuondoka ataondoka maana hakuna mtu atakae kaa pale milele,lakini tuliangalie suala hili kwa jicho la tatu,
1---ubora wa elimu yetu na ufaulu wa watoto wetu utabadilishwa na kuondoka kwa ndalichako?
2---Maslahi ya walimu yanarekebishwa na kiongozi mpya wa NECTA atakae kuja?
3---Uhaba wa madawati,Maabara na nyumba za walimu zitaletwa na kiongozi mpya wa NECTA?
===>Twende mbali zaidi jamani,Ndalichako ni mpimaji tu wa hiyo elimu
sidhani kama upo sahihi kwa sana, kama hayo ndo yanasababisha kufeli iweje wafeli waislam tu?
 
Mwenye sifa......jk mwenyewe hana sifa..

Amma katika watu ambao hawana fikra kabisa mmoja ni wewe.

Nakuomba nioneshe moja jema aliloifanyia nchi hii Rais yeyote wa kabla ya Kikwete ambalo Kikwete hakulifanya mara tatu zaidi yake kwa uchache.

Jaribu bahati yako!
 
Back
Top Bottom