Yanayofanyika viwandani Tanzania ni utumwa. Kazi ngumu, maslahi duni. Serikali haina mpango na wananchi wake, inachoangalia ni kodi tu

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,705
36,154
Kuna kiwanda kiko Pale Keko karibu na ukumbi wa DDC nadhani ni cha cello. Malipo kwa siku ni sh. 3500 kwa siku ilikuwa kwa muda mrefu. Sasa ni sh. 4000, kazi masaa 12 yaani lisaa limoja sh. Mia tatu na centi.

Viwanda vingi malipo ni sh. Elfu 5000 kwa siku, hii maana yake lisaa limoja la kazi ni sh. 400. Viwanda vyenye majina makubwa malipo kwa siku ni sh. 7000 hii maana yake lisaa limoja sh mia 6.

Hata kama ni non skilled labor ni haki Mtanzania alipwe sh. Mia 4 kwa lisaa limoja? Ni utumwa wa wazi uliopata baraka za serikali.

Hawa mabilionea wetu akina Bakhressa na Mo huwabebesha Watanzania viroba vya unga wa ngano kwa sh. 50 au pungufu kwa kiroba kimoja. Ni utumwa.

Nimewahi kufanya kazi siku moja tu kwa wahindi Kariakoo ni zaidi ya utumwa , kula juu yangu, nauli juu yangu malipo 7500 kwa siku na kazi very risk. Kazi ya kupeleka mizigo ghorofa ya 12 kutoka chini. Sikurudi tena.
 
dunia haina huruma. unalipwa kwa jinsi unavyojipa thamani.

kwa sasa Tanzania hela ipo kwenye content creation ukiweza kujitoa akili, kina mwijaku wanajenga maghorofa, makonda wa ma bus Tilisho huko wananunua vi IST sababu ya content zinazoleta hela za matangazo. jitoe akili pata ma followers hela itakuja yenyewe
 
Mkuu hio upo dunia nzima, unaposikia Wazungu wanakimbilia china kwa ajiili ya cheap labor ndio kama hao, saizi wanatoka china wanaenda India kwa ajiili ya watu kana hao,
Unskilled labor dunia nzima mishahara yao ni mbuzi tu, mana wanakuwa hawana mikataba, day worker tu,

Kwa kusema hivyo tuhimizane ndugu zangu kusoma sanaa
 
Kuna kiwanda kiko Pale Keko karibu na ukumbi wa DDC nadhani ni cha cello. Malipo kwa siku ni sh. 3500 kwa siku ilikuwa kwa muda mrefu. Sasa ni sh. 4000 . Kazi masaa 12. Yaani lisaa limoja sh. Mia tatu na centi.

Viwanda vingi malipo ni sh. Elfu 5000 kwa siku , hii maana yake lisaa limoja la kazi ni sh. 400. Viwanda vyenye majina makubwa malipo kwa siku ni sh. 7000 hii maana yake lisaa limoja sh mia 6.

Hata kama ni non skilled labor ni haki Mtanzania alipwe sh. Mia 4 kwa lisaa limoja? Ni utumwa wa wazi uliopata baraka za serikali.

Hawa mabilionea wetu akina Bakhressa na Mo huwabebesha Watanzania viroba vya unga wa ngano kwa sh. 50 au pungufu kwa kiroba kimoja. Ni utumwa.

Nimewahi kufanya kazi siku moja tu kwa wahindi Kariakoo ni zaidi ya utumwa , kula juu yangu, nauli juu yangu malipo 7500 kwa siku na kazi very risk. Kazi ya kupeleka mizigo ghorofa ya 12 kutoka chini. Sikurudi tena .
Kazi kisheria ina mkataba between muajiri na muajiriwa. Wewe unacholalamikia ni kibarua, vibarua viko regulated na sheria gani?
 
Back
Top Bottom