Wapagazi chapeni kazi ,mishahara imepanda

Jun 20, 2023
55
52
Leo asubuhi wpagazi wanaofanyakazi ya kubeba mizigo ya wageni katika mlima Kilimanjaro maarufu kwa jina la 'wagumu'wamekutana mjini moshi na habari kubwa kwao ni kupanda kwa mishahara yao ambayo kwa miaka nenda rudi wamekuwa kwenye harakati za kupambania maslahi yao.

Mwaka 2008 yapata miaka 15,serikali kupitia Tangazo ya serikali(GN22)ilipandisha mishahara ya wagumu na kufikia dola kumi kwa siku lakini yapo baadhi ya makampuni ya wakala wa utalii yalikuwa yakiwalipa chini ya dola kumi kama ilivyopitishwa na Bunge.

Tangu wakati huo wagumu hawa wamepitia chnagamoto nyingi licha ya kufanyakazi ngumu ya kubeba mizigo yenye uzito wa kilo 20 kutoka lango la kupandia kadi juu haijarishi nyakati za masika ama nyakati za kiangazi .
Mawazi kadhaa wenye dhamana na utalii wamepita bila jambo la vijana hawa kupatiwa ufumbuzi na mwaka 2015 mapambano ya kudai nyongeza ya mshabara yalipamba moto kwa usaidizi wa Chama cha mawakala wa utalii Tanzania(TATO)idara ya kazi,mamlaka ya mapato Tanzania(TRA) na wizara ya maliasili na utalii.

Loishiye Lenoy Mollel kutoka Chama cha wapagazi Tanzania(TPO) ndiye aliyetoa tangazo la kupanda kwa mishahara hiyo kuanzia Januari mosi mwaka huu kwa mgumu kulipwa 25,000 kwa siku na malipo haya yatadumu kwa muda wa mwaka mmoja na kuanzia januari mosi 2025 mishara hiyo itapanda tena hadi kufikia sh,35,000 kwa siku .makubaliano yaliyofikiwa desemba 29 mwaka jana Mjini Arusha.

Hii ni habari njema kwa vijana hawa ambao hakika malipo yao hayaendani na kazi ngumu wanayoifanya ndani ya hifadhi ya Taifa ya mlima Kilimanjaro na huu ni mwanzo wa mabadiliko ya michakato mingine ikiwamo suala la mavazi ya kukabiliana na baridi kali ndani ya hifadhi.

Katika kuhakikisha malipo hayo yanafanyika bila longo longo,kila mgumu atalazimika kuwa na namba ya utambulisho wa mlipa kodi(TIN) itakayomwezesha kufungua akaunti benki na mishahara yao italipwa na wakala kupitia benki.

Ofisa mtendaji Mkuu wa TATO,Sirili Akko anasema ni jukumu la wagumu kulinda heshima yao kwa kutokukubali kulipwa ujira chini ya viwango vilivyoidhinishwa na kwa kufanya hivyo ni kuwahujumu wenzao pamoja na kuhujumu mapato ya serikali .

Akasisitiza pia suala la ulinzi na usalma kwa mali za watalii pamoja na kuendelea kuuweka katika hali ya usafi mlima Kilimanjaro ili kuendelea kuwavutia wageni .

Wapagazi kwa upande wao wakaiomba TATO kuwadhibiti mawakala utalii wanaoendesha kampuni zao mifukoni ambao wamekuwa chanzo cha kuwapa malipo duni huku baadhi yakidaiwa kununua vocha kwa mawakala wenye leseni ya mlimani (TALA).

"Tuna kesi nyingi sana Idara ya kazi zinazohusu malalamiko ya mawaka wanaowalaghai porters,hatuwezi kuboresha utalii kama tunawalaghai porters",amesema katibu wa KPA,salmin Mwita Kerangwe.
 
Sasawamepandishiwa malipo vipi wakati hio 25k ni chini ya $10 ya 15yrs ago? Wangejua hayo makampuni yana charge watalii kiasi kwa safari nadhani wangegoma jumla...
 
Sana,halafu nilijuaga hawajamaa wanavutaga mkwanja wa maana sana,kumbe kawaida tu.
Ugumu ni kazi ngumu kidogo.
Mshahara ni kidogo lakini kuna mboneka ambayo mara nyingi huwa ni around 70$ to 90$ per trip.

Anyway kazi ya ugumu ni ya kigumu
 
Back
Top Bottom