Chimbuko la taifa la Israel, chanzo cha utumwa wake na chanzo cha uhasama kati yake na Palestina

mchawi wa kusini

JF-Expert Member
Apr 18, 2018
805
807
Habara wana JF, naamini mmetuliza akili Kwa kusoma uzi mrefu sina muda wa kupoteza hadi sasa naomba mniazime dakika 3 za kusoma uzi huu

Kabla sijaelezea kuhusu mwanzo wa taifa la Israel pamoja na mwanzo wa utumwa wa Waisraeli, huu ni unabii uliotolewa na Nabii Amosi kuhusu wayahudi na nchi yao ya Israel, pamoja na sharti waliopewa na Mungu:

Amosi 1:6-7, "Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya Gaza, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu waliichukua katika hali ya kufungwa kabila nzima, wawatie katika mikono ya Edomu; lakini nitapeleka moto juu ya ukuta wa Gaza, nao utayateketeza majumba yake."

Tunaona hapa kwamba Mungu alisema kabisa kutatokea moto (vita vikali) eneo la Gaza.

Mambo ya Walawi 24:23, “Nayo nchi haitauzwa kabisa kabisa; kwani nchi ni yangu mimi; maana ninyi ni wageni na wapangaji wangu.”

Tunaona tena hapa kwamba Waisrael waliambiwa hakuna kuuza ardhi huko Kaanani, kwa sababu nchi hiyo ni ya Mungu.

Sasa ingawa nitazungumzia Esau na Yakobo baadaye, lakini ni muhimu kujua ukweli kwamba Edomu (yaani "nyekundu” kwa lugha ya Kiebrania) walikuwa taifa la Kisemiti lililoshi kusini kwa Bahari ya Chimdi katika eneo ambao leo limegawanyika kati ya Israeli na Yordan. Hawa ni uzao wa Esao, mjukuu wa Ibrahimu!

Biblia inawataja mara nyingi kama washindani wa taifa la Waisraeliambao walikuwa na undugu kutokana na mababu zao kuwa watoto mapacha wa Isaka, mwana wa Abrahamu.

Mataifa hayo mawili yaliendelea kushindana mpaka Edomu ilipomezwa na Israeli wakati wa Wamakabayo (karne ya 2 KK).

Baada ya hapo, Mwedomu Herode Mkuu alipata kuwa mfalme wa Israeli (37 KK - 4 KK) na kuacha ukoo ulioendelea kutawala chini ya himaya ya Dola la Roma kwa miaka 100 hivi.

Haya sasa!

Baba yetu wa Imani Ibrahimu alizaliwa katika nchi ya URU wa WAKALDAYO (Wakaldayo ni wenyeji wakongwe wa mji wa Babeli, mji wa Babeli ulikuwepo maeneo ya nchi ya Iraq wa sasa) baba yake aliitwa TERA (mwana wa NAHORI). Ibrahimu alitokea katika uzao wa SHEMU, mtoto wa pili wa NUHU.

Tera alikuwa na watoto watatu wa kiume ambao ni Abramu a.k.a IBRAHIMU, Nahori(huyu alimpa jina la baba yake) na Harani. Baadaye TERA aliondoka na mwanawe Ibrahimu, mke wa Ibrahimu(SARAI) pamoja na LUTU ambaye ni mtoto wa nduguye, wakaenda mpaka Harani wakakaa huko. Harani hii ni mji na ni tofauti na jina la mtu (Harani) ambaye ni mtoto wa Tera. Harani ni eneo la kiakiolojia lililo kusini-mashariki mwa Uturuki ya leo. Tera alifia huko akiwa na miaka 205!

Hapa ndipo safari ya Ibrahimu ilianzia. Mungu alimuamuru na kusema “TOKA KATIKA NCHI YAKO, NA JAMAA ZAKO, NA NYUMBA YA BABA YAKO, UENDE MPAKA NCHI NITAKAYOKUONYESHA, NAMI NITAKUFANYA WEWE KUWA TAIFA KUBWA, NA KUKUBARIKI, NA KULIKUZA JINA LAKO, NAWE UWE BARAKA, NAMI NITAWABARIKI WAKUBARIKIYO, NAYE AKULAANIYE NITAMLAANI.”

Na baadae Mungu akamtokea na kufanya agano naye katika kitabu cha Kutoka 17:4 na kusema, “ MIMI AGANO LANGU NIMEFANYA NAWE, NAWE UTAKUWA BABA WA MATAIFA MENGI….” Alafu Kutoka 17:6, “NITAKUFANYA UWE NA UZAO MWINGI SANA, NAMI NITAKUFANYA KUWA MATAIFA, NA WAFALME WATATOKA KWAKO.” 17:8, “NAMI NITAKUPA WEWE NA UZAO WAKO BAADA YAKO NCHI HII UNAYOIKAA UGENI,NCHI YOTE YA KANANI, KUWA MILKI YA MILELE, NAMI NITAKUWA MUNGU WAO.”

Baadaye utaona kwamba agano hili Mungu alilirudia kwa mtoto wa Ibrahim, na hata kwa mjukuu wake pia.

Ibrahimu aliondoka akaenda kama alivyoamuriwa, LUTU akaenda pamoja naye. Ibrahimu alikuwa na miaka 75 alipotoka Harani. Walikwenda mpaka nchi ya Kanani. Ibrahimu alipita katikati mwa Kanani mpaka mahali patakatifu pa SHEKEMU.

Baada ya mihangaiko sana, ndipo Mungu akamtokea Ibrahimu huko Gerari (sehem iliyopo pwani mwa Mediterania, kusini mwa Gaza, bondeni ambamo kulikuwa na njia inayotokea Palestina hadi Misri) na kumuahidi mtoto, ni baada ya Ibrahim kumlalamikia Mungu kuwa hana mrithi.

Ni wakati huo pia ambapo Mungu alimwambia Ibrahimu kuwa uzao wake utaishi ugenini katika nchi isiyo yao, watawatumikia watu hao, na watateswa kwa muda wa miaka mia nne. Pia alimuahidi kuwa atawaokoa kutoka katika nchi hiyo!Mungu alimwambia tena, kwama amewapa uzao wa Ibrahimu nchi hiyo ya Kanani, kwanzia mto wa Misri mpaka mto mkubwa wa Frati na enelo lote la Kanani (Euphrates)-Soma Mwanzo 15:18-21.

Ni hukuhuku Gerari ambapo mfalme Abimeleki alitamani mke wa Ibrahimu na kumchukua, lakini hakumfanya kitu, baada ya kuota ndoto ya kutisha kutoka kwa Mungu. Ni baada ya hayo ndo Ibrahimu alipewa eneo la kuishi, na utajiri, pamoja na mjakazi Hajiri ili kumtumikia. Ni huku Gerari ambako Ibrahimu aliondoka na mali nyingi kupita kiasi. Gerari ilikuwa chini ya utawala wa Misri kipindi hicho.

Hata hivyo, baadaye Hajiri alimzalia Ibrahimu mtoto aliyeitwa ISHMAELI, ni baada ya Sara kutoweza kuzaa na kuamua kumpa Ibrahimu mjakazi wake ili amzalie mtoto. Huyu naye alibarikiwa na Mungu,alikaa katika jangwa na akawa mpiga upinde(Mwanzo 21:20).

Isaka alizaliwa na Sara baadaye, naye akafanya agano na Mungu ambapo Mungu alimzuia kwenda Misri, akamuamrisha kukaa Kanani, nchi ya ugenini, Mungu akamuahidi kumpa hiyo nchi na uzao wake, kwa kurudia ahadi zilezile alizompa Ibrahimu(Kutoka 26:3-5). Sara alifariki akiwa na miaka 127, akazikwa katika pango ya shamba aliyonunua Ibrahimu huko Makpela, kuelekea Mamre, ambayo ni Hebroni(Kanaani).

Hilo shamba alipewa Ibrahimu baada ya kuinunua kwa gharama ya shekel za fedha 400. Baadaye Ibrahimu alimuoa mwanamke mwingine wa tatu(KETURA),aliyezaa watoto sita (Zimrani, Yokshani, Medani, Midiani, Ishbaki, na Sua(Mwanzo 25:1-4). Ibrahimu alifariki akiwa na miaka 175, akazikwa na wanae Isak ana Ishmaeli katika shamba la Makpela, hukohuko alikozikwa Sara.

Baadaye Isaka alimuoa Rebeka, binti wa Bethweli, huyu Bethwel ni mtoto wa Milka. Na huyu Milka ndo alikuwa mke wa Nahori (ndugu yake Ibrahimu na mtoto wa Tera aliyepewa jina la babake Tera). Isaka alifariki na akazikwa na wanae wawili (Esau na Yakobo) katika pango la Makhpela,karibu na mji wa Hebron.

Esau alioa wake wawili Yudithi na Basemathi (wote wahiti), na baadaye akaongezea wa tatu ambaye alikuwa binti ya Ishmael (Mahalathi). Yaani Esau alimuoa mtoto wa Ishmael ambaye alikuwa ni ndugu yake(wa baba mmoja) Isaka. Baadaye Yakobo alitorokea Beersheba (ni sehemu ya jangwa katika eneo la kusini mwa Kaanani) kutokana na gadhabu na hasira za Esau.

Beersheba ndiko ambako Ibrahimu alipigana vita na kisha kufanya agano na mfalme Abimeleki. Yakobo alitembea na kufikia ‘nchi ya watu wa mashariki’ ambako aliingia kwa mjomba wake anayeitwa Labani,mtoto wa Nahori (ukumbuke Nahori ni ndugu yake Ibrahimu).

Labani alikuwa kaka yake Rebeka (Mwanzo 24:29). Ni huko ambako alikutana na Raheli kwenye kisima. Ni kwa Labani ambapo aliapa kumuoa Raheli lakini Labani akafanya njama akamuozesha binti yake wa kwanza aliyeitwa Lea. Yakobo alitumikia miaka kumi nan ne kuwapata mabinti wawili wa Laban, kwanza Lea na kisha Raheli. Ni huko ambako mjomba wake alimpa wajakazi wawili, Zilpa kwajili ya kumtumikia Lea, na Bilha kumtumikia Raheli.

Ni hawa wanawake wanne waliwazaa watoto wa kiume 12 aambao ndiyo makabila 12 za nchi ya Yakobo au ukipenda, nchi ya Israel. Yakobo alikaa kwa mjomba wake kwa miaka 20, kisha aliondoka na kurudi kwa watu wake. Alimbebea kaka yake Esau zawadi kibao na kumuomba msamaha, na alisamehewa na Esau.

Alipokuwa Betheli (hapo awali iliitwa Luzi katika Biblia) iko katika eneo lenye milima la Samaria karibu kilometa 17 kaskazini mwa Yerusalemu), Mungu akafanya naye agano lilelile alilofanya na Ibrahimu na Isaka, akamuahidi nchi ya Kanani na baraka kwa uzao wake, ni huko ndiko Mungu alimpa jina la Israeli (Mwanzo 35:9-12).

Ni huku ambako mwana wa Yakobo anayeitwa Yusufu aliuzwa na ndugu zake kama mtumwa kwa Waishmaeli wakiwa malishoni sehem inayoitwa Dothani. Waishamaeli hao walifika naye nchini Misri ambako aliuzwa kwa Potifa, akida wa Farao, mkuu wa askari wa Misri. Aliuzwa kama mtumwa na huu ukawa ndo mwanzo wa utumwa wa wana wa Israeli nchini Misri.

Ni huko ndiko ambako Potifa alimwajiri akampenda na kumpa nafasi ya kusimamia shughuli zote za nyumbani na wafanyakazi wote wa Potifa. Kwa kuwa alikuwa mwaume mzuri, mke wa Potifa akamtamani akataka kufanya naye uzinzi ambapo Yusufu alikataa katakata. Hii hali ilizidi ambapo akiwa kwenye kazi zake ndani ya nyumba ya Potifa, mke wake Potifa alimshika kwa nguvu, lakini Yusufu akatoroka na kwa bahati mbaya shati likabakia kwenye mikono ya huyu mke wa Potifa. Mwanamke akaamua kwenda na nguo za Yusufu chumbani kwake ili kumsubiria mumewe aje ili 'amchome' Yusuf.

Mwanamke huyo akamshtaki Yusufu kwa mumewe, kwamba alitaka kumbaka, na kwa hasira Potifa akamtia Yusuf gerezani, lakini hata huko Yusufu akawa maarufu, akapendwa sana na mkuu wa magereza, akamfanya msimamizi wa wafungwa wote humo gerezani. Ni huko ambako Yusufu alitia fora kwa kutafasiri ndoto mbalimbali za wafungwa. Ni kipawa hicho ndicho kilichomuokoa kutoka gerezani baada ya mfalme Farao kuota ndota ambayo walishindwa watu wote kutafasiri, lakini Yusufu akaweza kuitafasiri na hivyo kumfurahisha mfalme.

Yusufu aliletwa kwenye nyumba ya Farao kwa amri zake,akafanywa kuwa mkuu wa nchi na sheria zote za Misri, na kwa neno lake Yusufu watu wa Misri walitawaliwa. Yusufu akawa kama Waziri mkuu wa nchi ya Misri. Yusufu alioa huko Misri, alimuoa binti ya Potifera (kuhani wa Oni) aliyeitwa Asenathi, na kupata watoto wawili (Manase na Efraimu), Baadaye ukame na njaa ilitoke katika nchi ya Kanani, lakini kwa hekima za Yusufu, wamisri waliifadhi nafaka na chakula cha kila aina.

Ikabidi watu kutoka nchi na maeneo mbalimbali watembelee Misri kununua chakula. Baadhi ya watu waliokuja kununua chakula walikuwepo ndugu zake Yusuf wa damu, ndugu wa baba moja (Yakobo au Israel) kutoka Kaanani. Wakati Yusufu alipofunua utambulisho wake wa kweli kwa kaka zake, aliwashukuru badala ya kuwashutumu kwa jinsi walivyomtendea yeye.

Aliamini matendo yao yamesaidia kutimiza mapenzi matakatifu ya Mungu, hata ingawa ndugu zake waliomuuza wakiwa wamejaa wivu na chuki. (Mwanzo 45:4-15). Aliwakaribisha huko Misri, akawaombea kibali cha kuishi Misri kutoka kwa Mfalme Farao, wakapewa siyo kibali tu cha kuishi lakini pia eneo la ardhi huko katika nchi ya wenyewe, ambako walihamia pamoja na mifugo yako yote.

Kwa ushauri wa Yusufu, iliwabidi wamwambia Farao wao ni wafugaji na watumwa tu. Wafuga mifugo walikuwa ni chukizo kwa Wamisri na kwa hivyo waliwaona Waisraeli kama watu wa hali ya chini sana. Waisraeli wakapewa eneo la Gosheni, katika nchi ya Misri(Mwanzo 46:31-34). Waliishi vizuri, walilima na kufuga bila shida katika eneo hilo la Gosheni.

Baada ya muda njaa ilikumba nchi ya Misri, pamoja na Kaanani kutokana na ukame mbaya. Watu kutoka Kaanani na Misri walinunua nafaka naye Yusufu aliamrisha pesa zikisanywe kote. Fedha nyingi zililetwa nyumbani mwa Farao, walitumia fedha mpaka zikaisha na watu wakamwendea Yusufu kumuomba chakula ambacho hawakuwa tena fedha za kulipa. Yusufu akafanya mbinu ya kukusanya mifugo na wanyama wengine kutoka kwa Wamisri na Wamisri ili kuwapa chakula badala ya mifugo yao.

Yusufu alikusanya farasi, kondoo, ng’ombe, punda na wanyama wengine wote. Baada ya miaka, mifugo yote walipelekwa kwa Farao, Yusufu akaanza kununua na ardhi ya Wamisri, kila kitu kikawa chini ya mfalme.

Polepole watu wote wakawa watunwa wa Farao, wakawa wanamtumikia ili waweze kula na kuishi! Aliwakusanya watu wote katika miji mbalimbali, yaani alifanya mfumo kama wa kisosiolisti au ujamaa! Yusufu akawatangazia watu wote, kwamba wamenunuliwa na Farao, pamoja na mali zao zote, watu wakakubali kuwa watumwa wa Farao.

Yakobo aliishi katika nchi ya Misri kwa miaka 17, aliishi jumla ya miaka 147 akawabariki wanae na wajukuu zake(Mwanzo 49), akafia huko Misri. Yakobo alipakwa dawa na waganga wa Yusufu asioze, akapakwa dawa na kuhifadhiwa kwa siku 40 huko Misri, na Wamisri wakaomboleza kwa siku 70. Kutokana na ombi lake wakamsafirisha hadi Kaanani kumzika huko kwenye makaburi ya mababu zake,huko ambako alinunua Ibrahimu, ambako alizikwa Sara, Ibrahimu, Isaka, Rebeka na hata Lea.

Yusufu alikufa huko Misri akiwa na umri wa miaka 110, naye akapelekwa kuzikwa hukohuko kwa mababu zake, nchini Kaanani. Lakini baada ya muda akaibuka mfalme mwingine kutawala Misri.

Yeye alikuwa na wivu kwa Wakaanani, Wamisri wakaanza kuwabagua na kuwatesa Wakaanani. Pia aliamuru watoto wakiume wote wa Wayahudi wasiruhusiwe kuishi, wauawe wote wanapozaliwa. Lakini badaye alizaliwa Musa ambaye alifichwa hadi alipokuwa na umri wa miezi mitatu akatupwa kando ya mto, karibia na kwa mfalme.

Huyu Musa aliokotwa na binti ya mfalme, akalelewa kwenye nyumba ya mfalme. Baada ya kukua akaona Mwebrania akipigwa na Mmisri, kitu alichoshindwa kuvumilia, akaenda akampiga Mmisri hadi kufa, akaficha mwili wake. Kesho yake alipohisi amejulikana ilibidi akimbilie Midiani (karibu na Saudi Arabia wa sasa) ambako alipata ajira ya kuchunga mifugo kwa Kuhani wa Midiani (Yethro). Ni huko ambako aliitwa na Mungu kwenda kuwaokoa wana wa Israel/Yakobo. Ieleweke kuwa Midiani alikuwa ni moja wapo ya watoto wa Ketura.

CHANZO CHA UHASAMA KATI YA ISRAEL NA PALESTINA:
Hivi ni vita kati ya uzao wa watoto wawili wa Rebeka na Isaka, wajukuu wa Ibrahimu,yaani kati ya uzao wa ESAU na uzao wa YAKOBO (ISRAEL).

Mapacha hawa waliofarakana tangia wakiwa tumboni mwa mama yao.Esau alizaliwa kwanza lakini Yakobo alizaliwa akiwa ameshikilia kisigino cha Esau! Mungu alinena na mama yao Rebeka na kumwambia kuwa mataifa mawili yapo tumboni mwake. Pia alimwambia kabisa kwamba hao watafarakana na kwamba mkubwa (ESAU) atamtumikia mdogo (YAKOBO). Na pia tunaona huyo mtoto wa kwanza alikuwa mwekundu kabisa mwili wote (ESAU),tofauti na mdogo wake. Ebu soma Mwanzo 25:25.

Hawa wawili baadaye walitengana baada ya Yakobo kumsaliti Esau na kuchukua urithi kwa baba yake kwa msaada wa mama yake aliyempenda kuliko Yakobo (Unaweza kusoma stori yote kwenye kitabu cha Mwanzo 27. Esau kwa upande wake alioa wake wawili Yudithi na Basemathi (wote wahiti), lakini baadaye akaongezea wa tatu ambaye alikuwa binti ya Ishmael (Mahalathi).

Huu siyo mzozo mpya, ni mzozo uliokuwepo kwa kabla na baada ya miaka 100 sasa. Ingawa kwa sasa tunaweza tu kukumbuka mzozo wa kwanzia ndani ya miaka 100 hivi.

Uingereza ilichukua na kudhibiti eneo linalojulikana kama Palestine baada ya mtawala wa eneo hilo la mashariki ya kati mfalme wa Ottoman kushindwa katika vita vya duniani vya kwanza(1911-1918).

Ardhi hiyo ilikuwa ikimilikiwa na Wayahudi walio wachache na Waarabu walio wengi.

Uhasama baina ya makundi hayo mawili ulianza wakati jamii ya kimataifa ilipoipatia Uingereza jukumu la kuwapatia makaazi Wayahudi katika eneo la Wapalestina.

Kwa upande wa Wayahudi eneo hilo lilikuwa la mababu zao, lakini Waarabu Wapalestina pia nao walidai kumiliki ardhi hiyo na hivyobasi wakapinga mpango huo.

Kati ya mwaka 1920 na kwenye miaka ya 40, idadi ya Wayahudi iliowasili katika eneo hilo iliongezeka, huku wengi wakitoroka kuuawa barani Ulaya na kutafuta eneo la kuishi baada ya mauaji ya Holocaust ya vita vya pili vya dunia(1939-1945).

Ghasia kati ya Wayahudi na waarabu na dhidi ya utawala wa Uingereza ziliongezeka, na hatimaye mwaka 1947, Umoja wa Mataifa ulipiga kura kwa Palestina kugawanywa kati ya mataifa ya Wayahudi na Wapalestina huku mji wa Jerusalem ukiwa mji wa kimataifa. Mpango huo ulikubaliwa na Wayahudi lakini ukakataliwa kabisa na Waarabu na haukutekelezwa.

Mwaka 1948, baada ya kishindwa kutatua mzozo huo, watawala wa Uingereza waliondoka na viongozi wa Kiyahudi wakatangaza uanzishwaji wa taifa la Israel. Wapalestina wengi walipinga na vitaa vikaanza.

Israel likinyakua asilimia 78 la ardhi ya Wapalestina, huku maeneo yaliosalia ya West Bank, Jerusalem mashariki na ukanda wa Gaza yakidhibitiwa na Misri na Jordan.

Unyakuzi wa Israel katika ardhi ya Wapelestina uliendelea 1967, baada ya vita vya pili vya Arab-Israel ambavyo vilisababisha Israel kukalia eneo la mashriki mwa Jerusalem, kabla ya kuunyakua mji wa Jerusalem, ikiwemo ule wa zamani na al-Aqsa.

Mwaka 1980, Israel ilipitisha sheria ikitangaza kuuteka mji wa Jerusalem kinyume na sheria ya kimataifa.

UMUHIMU WA MJI WA YERUSALEM KIIMANI

KANISA LA MT SEPULCHER
Ndani ya mji huo wa zamani kuna kanisa la mtakatifu Sepulcher, mojawapo ya maeneo takatifu ya Wakristo duniani. Lipo katika eneo ambalo historia yake inamuhusisha Yesu Krsito, kifo chake, kusulubiwa kwake na kufufuka kwake.

Kulingana na tamaduni za Wakristo, Yesu alisulubiwa hapo katika eneo la Golgotha ama Mlima Kalvari, na kaburi lake lipo hapo na ndipo eneo alilofufuka.

Kanisa hilo linasimamiwa na wawakilishi wa makanisa tofauti ya Kikristo, hususan Kanisa la Orthodox la Ugiriki, kanisa la Katholiki la Franciscan Friars na kanisa la Armenia Patriarch. Lakini kanisa la Ethiopia la Coptic na kanisa la Syria pia yanahusishwa. Ni eneo moja linalotembelewa sana na mamilioni ya mahujaji Wakristo kote duniani ambao hutembelea kaburi ya Yesu na kuomba katika eneo hilo.

MSIKITI WA AL AQSA
Msikiti wa Al Aqsa ndio mkubwa kati ya maeneo matakatifu yaliopo katika mji huo katika eneo linalojulikana kama Haram al Sharif.

Msikiti huo ndio eneo la tatu takatifu kwa ukubwa na husimamiwa na ufadjhili wa fedha unaojulikana kama Wakfu.

Waislamu wanaamini kwamba mtume Muhammad alisafiri kuelekea eneo hilo kutoka Mecca wakati wa safari ya usiku na kuombea roho za mitume yote.

Hatua chache kidogo, The Dome of The Rock linamiliki jiwe ambalo linaaminika mtume Muhammad aliipanda wakati anapaa kwenda kwenye mbingu la saba.

Waislamu hutembelea eneo hilo takatifu kila mwaka, lakini kila Ijumaa wakati wa mwezi mtukufu wa Ramdhan, mamia ya maelfu ya Waislamu huenda katika eneo hilo kufanya ibada.

Israel imeweka vikwazo kadhaa karibu la lango la msikiti wa al-Aqsa , ikiwemo ukuta uliowekwa mwaka 2000, unaowazuia Wapalestina kutoka West bank kuingia.

Kati ya Wapalestina milioni 3 katika eneo la West Bank ni wale walio zaidi ya umri wa miaka 40 wanaoruhusiwa kuingia Jerusalem siku ya Ijumaa huku wengine wakipatiwa sharti la kuwasilisha ombi la kibali kutoka kwa mamlaka ya Israel.

Wasio Waislamu huruhusiwa kutembelea eneo hilo kwa saa kadhaa lakini hawaruhusiwi kufanya ibada ndani yake.

UKUTA UNAOLIA
Eneo linalojulikana kama “ukuta unaolia”, mojawapo ya sehem ya milima iliosalia ya mlima Moria.

Wayahudi wanaamini kwamba eneo hilo ndio eneo la jiwe la msingi ambapo dunia iliundwa.

Wanaamini ni eneo ambalo mtume Ibrahim alitaka kumchinja mwanawe Isaac.

Wayahudi wengi wanaamini kwamba The Dome of The Rock ndio eneo la maeneo yote matakatifu.

Hata Wakristo wanaamini Daudi alichagua Mlima Moria, au Mlima wa Hekalu, ambapo iliaminika kuwa Ibrahimu alikuwa amejenga madhabahu ya kumtolea mwanawe Isaka dhabihu.

Inaaminika Hekalu la Kwanza lilijengwa katika eneo hilo wakati wa utawala wa mwana wa Daudi, Sulemani, na kukamilika mwaka 957 KK. Mnamo mwaka wa 70 BK, Warumi waliharibu hekalu la Yerusalemu na kupora vitu vitakatifu vilivyokuwa ndani yake. Wanaamini ni baada ya Wayahudi kutoweka ndipo Waislam walijenga “the dome of the rock” katika eneo hilohilo.

Hivyo ukuta huo unaolia ndio ulio karibu zaidi kwa Wayahudi kufanya ibada unaongozwa na Rabbi na mamilioni ya wageni hutembelea eneo hilo kila mwaka.

Sasa endapo baado huamini kuwa Yerusalem, mji mkuu unaogombaniwa kati ya Wapalestina (Waislam) na Israel (Wayahudi) ni mji takatifu, na endapo unajiuliza kwanini Marekani ni rafiki namba moja wa Israel, na kwa nini watu wa dini karibia zote wanaamini eneo hili ni maalum, huu hapa ni uthibitisho na sababu za kutosha kutoka kwenye Biblia kabisa, soma nawewe uone, na ufanye uhakiki:

Za 122:1 Isa 49:10; Yere 31:6; Zek 8:21-Nilishangilia pamoja na wale walioniambia, “Twende nyumbani ya Bwana.” Ee Yerusalemu, miguu yetu imesimama malangoni mwako.

Za 122:3 2, Sam 5:9; Efe 2:21-Yerusalemu imejengwa vyema kama mji ambao umeshikamanishwa pamoja.

Za 122:4; Kum 16:16; Kut 16:34-Huko ndiko makabila hukwea, makabila ya Bwana, kulisifu jina la Bwana kulingana na maagizo waliopewa Israeli. Huko viti vya enzi vya hukumu hukaa, viti vya enzi vya nyumba ya Daudi.

Za 122:6; Za 26:8; Isa 62:6; Yer 51:50-Omba kwa ajili ya amani ya Yerusalemu: “Wote wakupendao na wawe salama.

Za 122:7; 1Sam 25:6; Za 48:3-Amani na iwepo ndani ya kuta zako na usalama ndani ya ngome zako.” Kwa ajili ya ndugu zangu na marafiki, nitasema, “Amani iwe ndani yako.
 
Ugomvi wa israel na palestina hauhusian na dini ...icho ni kichaka tu

Kwani ugomvi umeanza after 1948 huko nyuma walikuwa hawasali?
 
Back
Top Bottom