Pamoja na mambo mengine, sisi Watanzania tunataka kusikia ni kwa jinsi gani Ndg Tundu lisu atatutoa hapa tulipo kutupeleka mbele zaidi hasa kiuchumi.
Tunataka wagombea wetu waeleze kinaga ubaga ni kwa jinsi gani wataweza kuifikisha nchi yetu kwenye peek ya uchumi wa kati na jumuishi wa pato la kila mtanzania kufikia wastani wa dola 3000 hapo kufikia mwaka 2025,huku uchumi huo ukichagizwa na maendeleo ya viwanda.
Binafsi picha hizi hazisaidii, watu hawapigi kura kwa huruma bali kwa yule atakayewaletea maendeleo.