Wizi Mtupu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wizi Mtupu!

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by klorokwini, Aug 17, 2011.

 1. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #1
  Aug 17, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  Eti wanasema "Heshima ni kitu cha bure", mbona sisi walalahoi hatuitwi "waheshimiwa"? au hatustahili "heshima" au "kuheshimiwa" ?


  Wanasiasa bana!

  Nilikuwepo!
  wasalimieni JF Chit Chat
   
 2. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #2
  Aug 17, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,261
  Trophy Points: 280
  kuitwa 'mheshimiwa' haimaanishi kuwa na 'heshima' ama kuheshimiwa! wanasiasa sio wote wenye kuheshimika/heshimiwa.
  japokuwa siamini kama heshima ni kitu cha bure. wazungu wanasema 'respect is earned'. kitu ambacho nadhani wanasiasa wetu wanasahau, kuwa kwa kuitwa mh na kugawia watoto pipi huwezi kupata heshima. there is no free lunch, heshima inclusive!
   
 3. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #3
  Aug 17, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  Nimekupata king'asti, lakini suala la kizushi! hivi mwenye cheo espesheli serikalini au kwenye chama cha siasa kama hana heshima au haheshimiki tunapomuita muheshimiwa Je muktadha huu unakubaliana na Lugha ya kiswahili? na iwapi thamani ya neno "heshima"

  offu topik: nilitaka kulog out lakini Gun lako limeniturn on ghafla
   
 4. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #4
  Aug 17, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,261
  Trophy Points: 280
  muktadha huu haukubaliani na kiswahili. ingebidi iwe voluntary kuita mtu mheshimiwa. aisee, kuna mtu unamuita mheshimiwa wakati moyoni mwako unamdharau (despise inakolea zaidi,samahani ukoloni umeniweka ukungu akilini,kha!). ila ndo wanaoita hivyo kula yao iko hapo. haina tofauti na jamaa wa ngwasuma na papaa msoffe, wasipompamba hawaendi nanilii
  offutopiki: this gun was meant to turn u off, not on! hujanitendea haki wallah!
   
 5. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #5
  Aug 17, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,130
  Likes Received: 6,615
  Trophy Points: 280
  nimepotea njia.
   
 6. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #6
  Aug 17, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,062
  Likes Received: 24,061
  Trophy Points: 280
  Hata mimi nachoka sana fellow tablet.......hebu angalia
  Mheshimiwa Anna Makinda
  Mheshimiwa mstaafu Lawrence Masha
  Mheshimiwa Januari Makamba
  Mheshimiwa mstaafu Rostam Aziz
  Mheshimiwa Edward Lowasa

  Afu cheki hii

  Askofu Mokiwa........si Mheshimiwa
  Sheikh Yahya Hussein (RIP)...Si Mheshimiwa
  Mchungaji Mama Rwakatare si mheshimiwa kanisani mpaka atinge bungeni
  Padre Karugendo.........Si mheshimiwa
  Profesa Seng'ondo Mvungi, si mheshimiwa, mpaka atinge bungeni
  Mkuu Invisible......si mheshimiwa
  Mkuu Klorokwini........hategemewi kuwa mheshimiwa labda aondoke jukwaa la MMU na Chit Chat
  Babu Asprin...........Mheshimiwa kwa mkewe tu......... watoto wanamwita baba, wajukuu wananmwita babu

  Wanasiasa bana. Mia.Mia.Mia
   
 7. First Born

  First Born JF-Expert Member

  #7
  Aug 17, 2011
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 5,315
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  klorokwin, my head is aching.
   
 8. daughter

  daughter JF-Expert Member

  #8
  Aug 17, 2011
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 1,275
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Nyie matablet mmenitengenezea asubuhi yangu
   
 9. Lily Flower

  Lily Flower JF-Expert Member

  #9
  Aug 17, 2011
  Joined: Oct 16, 2009
  Messages: 2,555
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Babu on the move, habari yako binafsi babu.
   
 10. Lily Flower

  Lily Flower JF-Expert Member

  #10
  Aug 17, 2011
  Joined: Oct 16, 2009
  Messages: 2,555
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Nauliza tu hivi kuna kosa usipotanguliza hilo neno muheshimiwa????
   
 11. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #11
  Aug 17, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  utamwita muheshimiwa kama anakupa ugali
  mf waziri kwa rais
  lakini kwetu sisi wajasiria mali huo unafiki hatuna.
   
 12. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #12
  Aug 17, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135

  Fellow tablet unajua inauma sanaaa aisee! samtaimu mtu unapitisha jihada zako zote , unaazima suti na mokasi rangi ya udongo, halaf unajifanya kuamkia shkamoo kila unaemkuta ili uitwe muheshimiwa lakini hauitwi. Kuna njemba inaiba kura, inaiba hela za mikataba, haifungi ramazani, haitoi sadaka kanisani na unaiskia inaitwa "mheshimiwa", nazani tuanzishe petition ya kuliomba razi dikshineri la kiswahili, tumelikosea heshima sana.

  Leo niko serious kweli! baada ya hii sredi kukamilika lazma mtaskia mawaziri kadhaa wamejiuzulu. stay tuned! fellow tablet
   
 13. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #13
  Aug 17, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  Dah! tangu ujiunge JKT umekuwa na mapwenti kuliko shwaznega! nimekupata vizuri sana kwakweli
   
 14. bht

  bht JF-Expert Member

  #14
  Aug 17, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  wewe ulieksipaya kitambo....
   
 15. vivian

  vivian JF-Expert Member

  #15
  Aug 17, 2011
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,704
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135

  Unashtakiwa kwa kosa la kumvunja m2 mbavu. unakiri shtaka?
   
 16. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #16
  Aug 17, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  Suali langu kwanini waitwe waheshimiwa? sio lazima umuite wewe! unajua mtu akiwa una uhakika anakuibia halafu kwenye media anamsikia anakuwa adressed kama mheshimiwa inauma aisee! halaf inachafua jina la JF.
   
 17. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #17
  Aug 17, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  hata kama hakuna kosa! kwanini mwizi ikubalike kuitwa mheshimiwa?. halaf kuna wengine wanaitwa waheshimiwa hata kukoga hawakogi! Heshima iko wapi? leo nina hasira kweli hata waifu kakimbia home.
   
 18. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #18
  Aug 17, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,062
  Likes Received: 24,061
  Trophy Points: 280
  Sipendi kucheza na wewe una mikono michafu.........
   
 19. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #19
  Aug 17, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  Hehehheh mheshimiwa Bht bana!
   
 20. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #20
  Aug 17, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,062
  Likes Received: 24,061
  Trophy Points: 280
  Hahahaha...... Hiyo mambo ya kuiba kura peleka kule jukwaa la mastress wakaidiskasi kwa mapovu........ Hapa tujadili hiyo mokasini, ukitaka uitwe mheshimiwa labda ukaazime ya Mbu. Hivi siku hizi yuko wapi huyu mtu?.........BTW ile tabia yako ya kukaribisha wanachama wapywa wa JF wenye ID ya kike umeshaacha? Kabla bado nakushauri uwakaribishe kwa mkwala kuwa wewe ni MOD na wasipokuita Mheshimiwa utawahamishia fesibuku au Michuzi blogu wakauze sura..........

  Hivi hapa tupo jukwaa gani vile?

  Nitendee heshima kwa kuniita mheshimiwa. Na hiyo kesi si itasikilizwa na mheshimiwa hakimu?.....Hivi Nyerere alikuwa mheshimiwa au Ndugu?
   
Loading...