Heshima, Thamani na namna unavyojiweka katika jamii

Jack Daniel

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2021
Posts
4,696
Reaction score
19,135
Habari JamiiForum.

Hope mko poa ladiz (ladies) & Gentlemen.

Waungwana ,

Kila mmoja wetu anahitaji kuheshimiwa na kuthaminiwa,iwe Kwa namna yeyote ile tajiri au masikini,mfupi Kwa mrefu,mweusi na mweupe n.k.

Kila mtu hujiona anapaswa kuheshimiwa,lakini je heshima na Thamani inakujaje?

Ni pale unapojitengenezea mazingira ya kuheshimiwa,yaani watu wakuheshimu automatically na siyo kulazimisha uheshimiwe.

Wapo watu ambao heshima kwao huja tu iwe isiwe,Matajiri,wenye vyeo vikubwa serikalini,wenye nyadhifa kadhaa zenye kueleweka,na baadhi ya viongozi wa dini na Elites wengine wengi.
Lakini heshima nyingine kubwa kuliko zote ambayo ni ya asili ni ile anayopewa mzazi e.g Baba na Mama, heshima nyingine kubwa ni ile anayopewa mgeni,yaani mtu fulani hujawahi kumuona sehemu ,so kwakuwa humjui unajikuta unampa heshima fulani Hadi pale atakapodhihirisha tabia zake.

Anyway heshima kwenye kizazi hiki ni kuwa na pesa😂 lakini hutapata heshima ya asili labda maigizo tu kutoka Kwa wanaonufaika na wewe.

Hebu tuone vitu kadhaa ambavyo vinakushushia heshima bila kujua.

1.Salimia kila mtu,ila kuwa na kiasi.

Waswahili wanasema salaam haigombi,hebu tengeneza utaratibu wa kusalimia ni nzuri hata kama upo kwenye usafiri wako ,wapigie watu honi wajue umewasalimu,wawashie taa wajue umewasalimu.
Inapendeza ,kiburi si uungwana.

2.Punguza kuongea sana kuwa na kiasi.

Stori za mpira upo, stori za siasa upo , geopolitics unazijua,stori za Persia na Israel unajua kama vile wewe ulishawahi ishi nchi hizo.
Punguza kuongea wape watu nafasi wachangie mjadala inanogesha na kuongeza ladha ya kijiwe.

3.Usiende kutafuta huduma mahali usipoheshimiwa.

Kwamfano,uko bar,club,vituo vya mafuta na maduka na super markets, hizi sehemu wahudumu au wafanyakazi wanaasili ya kujudge mtu Kwa muonekano wake,yaani upo bar unaweza usihudumiwe ,na akahudumiwa mtu aliyekukuta,pia kwenye maduka kuna kaubaguzi fulani Kwa kuangalia mtu mwenye pesa zaidi au mwenye ushawishi fulani.
Sasa ili kulinda heshima yako nenda sehemu za kawaida lakini zenye huduma nzuri, mbona zipo nyingi?

4.Punguza mashindano

Acha kuiga,Acha kaulimbukeni kutaka jamii au watu wakuone Una hela,hapa heshima si tu itashuka ila itaporomoka, yaani kununua kitu ambacho hutaweza kukimudu ili uonekane unazo, usishindane na watu.wapo wenye urithi mkubwa hawashuki Leo au Kesho,wapo wenye dili haramu,lakini wapo wanaoigiza maisha ,anaweza kutumia laki tano kumbe analala chini ,hana familia Hana nyumba ila anapendeza na kuspend pesa anazovuja jasho jingi hawa ni wengi mno.

5.Usilazimishe mapenzi.

Unalazimisha kupendwa?
Unataka mtu akupende Kwa lazima?
Serious?
Heshima yako itazidi kupungua huku jamii ikikuona mzembe na limbukeni fulani.

6.Tengeneza familia.

Oa au olewa,zaa watoto,
Hata kama Una pesa kiasi gani,kuna jamii zikijua huna uhusiano wa kueleweka na huna mtoto wanakushusha vyeo.
(NDOA SI LAZIMA LAKINI 😂)

7.Ipende familia yako.

Kuna mtu anafanya sifa na kufuru kwenye makongamano na sherehe,na anasifika Kwa kuwa mchangiaji mzuri,pesa kwake si Tatizo yote kuhakikisha shughuli haiharibiki. Lakini wazazi wake au mke na watoto wapo kwenye hali mbaya na yeye hajali,hii ni mbaya.

8.Acha kutoa lifti kwa watoto wadogo iwe wakiume au wakike.

Hata mkeau muse wa rafiki yako,kuna muda Bora umkwepe na ubadili uelekeo ,ukionekana mchoyo afadhali kuliko madhara utayopata.

9.Usimuombe mpenzi wako mapenzi kinyume na maumbile.

Acha mengine yakupite,usijishushie heshima,ujanja mwingine haufai.

10.Isikilize sauti yako ya ndani inasema nini ,Jack Daniel anaandika tu ila si sheria
 
Points za mwanzoni umezielezea vizuri kabisa tena kifalsafa ila za mwishoni umezimalizia kimahubiri, umekuwa mchungaji mchunga kondoo wa bwana.

Hapo ni kama umemtaja adriz de mbuzi maana hakuna kitu au mada yoyote ile asiyoijua na kuibishania
 
Mtu asipookota hata moja hapa basi hakuna sehemu atakayowezekanika tena!
 
Back
Top Bottom