Why TTCL is not the leading Cellular and internet Operator?

Labda sikusoma vizuri title ya thread!

Anyway, TTCL ina watu,culture na structure ambayo inatokea kwenye monopoly (or let's call it a dominant position in the market)...hivyo hawawezi hawawezi ushindana katika soko la simu lilivyo sasa(hata kama kusingekuwa na 'mkono wa mtu' kama baadhi ya watu wanavyotaka tuamini)! Ni lazima kufanyike revolution. Ni kama leo hii ukitokea ushindani kwenye nishati ya umeme, kwa watu,culture na structure ya Tanesco hawataweza kushindana.
Umesema hukusoma vizuri content ya hoja iliyoletwa mezani na funny enough umerudi na jibu hilo hilo! unachekesha kweli!
 
Mimi kitu ambacho huwa kinaniuma sana kuhusu baadhi ya Watanzania wenzetu ni hili la kukosa uzalendo; si hilo tu vile vile tuna tabia nyingine ya kufanya mbinu za kuwakwamisha wataalamu wa kutoka nje wanapokuja kujaribu kuweka mambo sawa kwenye mashirika yetu ya umma ambayo tumeyafirisi sisi wenyewe.

Chukulia hili shirika la TTCL ambalo lilikuwa na miundo mbinu hiliyo jengwa siku nyingi Tanzania nzima and beyond na lingeweza kabisa kuwapiku cellular operators wote, lakini kwa kukosa uzalendo wakashirikiana na Wachina wajanja kuingiza mfumo wa CDMA ambao walijuwa fika kwamba ni nchi chache duniani zinazo tumia mfumo regardless ya uzuri wake kiusamabazaji mawimbi.

Viongozi walio husika na scam hii hawakuwa na muda hata wa kutumia akili kidogo kwa kujiuliza hivi ni kwa nini CELTEL/ZAIN, VODACOM, TIGO/MOBITEL na Ulaya nzima inatumia GSM na siyo CDMA, kwani wanataka kusema kampuni zote hizo ni wajinga hawajuhi cost benefit za CDMA? Hivi leo hii wanaweza kueleza ni wateja wangapi wanatumia simu zao za mikononi ni mteja gani atakubali kutumia simu ambayo inamfunga kwenye kampuni moja tu. \

Mimi nilitegemea Serikali yetu tukufu ingewachukulia hatua kali watu walio tia Taifa hasara ya kijinga kwa ukosefu wao kuwa Wazalendo wakati walisomeshwa na Taifa hili bure lakini wala hawajali hasara waliyo litumbukiza Taifa hili kimaksudi. Mimi nimesoma hoja zote zilizo andikwa humu kuhusu matatizo ya TTCL, lakini jamani tuwe wakweli tuache kulaumu Serikali; wenye matatizo ni Wakuu wa Mashirika kukosa ubunifu na uzalendo, mimi siamini kwamba wakuu wa mashirika wakienda na maoni mazuri tu ya kuendeleza mashirika yao bila ya kuweka mbele masirahi yao Serikali inaweza kuwakatalia - hiyo si kweli.

Kuna wakati fulani TTCL ilikuwa na wahandisi mahili kuhusu mawasiliano, hawa wangeweza kabisa kununua transmitters/repeaters/antennas, SERVERS na software zake kwa ajili ya kuongozea mfumo mzima wa GSM Network nchi nzima. Shirika lenyewe lilikuwa na minara ya microwave nchi nzima walicho kuwa wanatakiwa ni kuongezea urefu wa minara yao inapobidi ni hiyo ingekuwa ni gharama ndogo tu.

Samahani nita andika maoni marefu kidogo, hii nafanya kwa nia nzuri tu baada ya kuchoshwa na visingizio ambavyo havitajenga nchi hii hata kidogo tunapashwa kubadirika, sina shaka watu watauliza hivi kweli ingewezekana TCCL kununua hivyo vifaa wakavifunga wakawa na network ya GSM? Jibu ni kwamba wangeweza kabisa na wataalamu wa mawasiliano sina shaka wapo wakufanya kazi hiyo. Kumbuka si VODACOM, TIGO, AIRTEL wala ZANTEL wanaunda vifaa hivyo vya RADIO wote wananunua kutoka makampuni ya Motorola, Siemens, Erricsson, Phillips na kampuni za Kichina Huewei na ZTE cha muhimu hapa ni kujuwa utataka mfumo gani wa mawasiliano ya simu na data: CDMA au GSM basi.

Vifaa hivyo vya mawasiliano vinapatikana kirahisi tu na Watanzania wenye huwezo kufanya kazi hii wapo lakini kasumba ya baadhi ya viongozi wa mashirika hawapendi kabisa kuwatumia. Wanao nisikitisha ni wafanyakazi wa kawaida wa TTCL, mimi natoa rahi kwa viongozo wa Shirika hili wawe wabunifu na kuwa na bussiness acumen wahachane na mambo ya kulalamika tu, kama hamko tayari kubadilika sioni mantiki ya kuomba sijuhi mabillioni mangapi kutoka Serikalini eti kufufua Shirika.

Humu nimeandika kwa lugha ya kawaida tu not in technical jargon hili watu wa kawaida tu waelewe ninacho zungumza na kiswahili changu siyo kizuri sana, lakini nafikiri ujumbe umefika, mwisho nisije kueleweka kwamba labda namshambulia mtu binafsi, hapana mimi ninacho fanya hapo ni kusema ukweli kwa ajili ya ustawi wa nchi hii.
Ninamiliki mitandao ifuatayo 0713,0767,0786,0776, na 0732.
Kwa uzoefu nilionao leo ni 0732 tu inayofanya kazi kwa usikivu uliotulia kuliko mitandao taka taka mingine yote. Na ni mtandao wa ttcl mobile. Anayebisha afanye majaribio na ndipo aanze kulaumu CDMA. Watu wengine wepesi kuandika andika bila utafiti.
 
Mkuu afadhali nimepata mtu mwenye inside information.., kulingana na aliyosema Shingo hapo juu, wewe unadhani ni hatua gani ingebidi ichukuliwe ili kunusuru hili janga? au inatakiwa wafanye nini sasa ili watoke kwenye hili janga?
Nina mashaka kama utajibiwa swali lako hili. Huyu katoka kambi ile ile unayoijua.
 
Biashara ya mobile services ni matangazo, ubunifu wa kutoa product mpya kila mara pamoja na kumsikiliza mteja - vyote hivi havipatikani TTCL. Hivi karibuni Kampuni ninayofanyia kazi ilipatwa na matatizo ya FIBRE kati ya point A na B ambayo imekodi TTCL. Tuliripoti tatizo TTCL usiku huohuo na kufuatilia kila baada ya nusu saa lakini ilibidi tutume gari asubuhi yake ili waje kumaliza tatizo, hii haikubaliki na hivi sasa tumeshaanza kujenga fibre network yetu wenyewe to get rid of TTCL poor service.

Unaweza ukatembea DSM mzima si ajabu usilione hata bango moja la matangazo la TTCL.

Nadhani shirika lingepewa viongozi wenye VISION na wanaojali maslahi ya taifa kama Mzee Ole Kambainei lingepaa.
Nakubaliana na wewe kwamba ni kweli mmetuuzia matangazo kweli kweli lakini service ya mitandao yenu mingi ni za chini sana. Mtu hasikii anayezungumza naye, mitadao ni kula pesa zetu tu. Kwa hilo umesema ukweli.
 
Nani hakusikia hivi karibuni ttcl wakilalamikia serikali kuwa haijawalipa sh. bilioni 9 za huduma kwao?
 
Mr. KAA LA MOTO


Nakushauri huwe unakuwa makini kusoma maoni ya watu, jazba zako na kudhalau binadamu wenzako
haiwezi kuleta tija yoyote katika nchi hii. Nakuomba usome paragraph ya pili ambayo nakili kwamba CDMA ina superior voice Quality kuliko GSM, lakini nimesema katika ufanyaji biashara ma-investors wana angalia ni mfumo gani ambao huko popular na wide spread basi na wenyewe wanafuata mkumbo, ndiyo maana VODACOM,TIGO,AIRTEL etc wamefuhata mkumbo huo huo, kwani unafikili walikuwa hawajuhi kuhusu CDMA na uzuri wake.

We unasema eti GSM ni crap CDMA ya TTCL balabala, je unaweza kuwaeleza Watanzania TTCL na TAIFA limefaidika nini kibiashara kwa mfumo wa CDMA?

Ndugu mimi sijakurupuka kuandika maoni yangu bila ya kuwa na weledi kwa ninayo zungumzia, huwezi kuwa una dismiss maoni ya wenzako off hand just like that, hapa tunazungumzia mambo ya kujenga siyo kubomoa; mimi nilifikili labda kuwepo kwako Bristol kama ni kweli kungeweza kukuelimisha jinsi wenzetu wanavyo heshimiana kwa kutoa constructive critism bila dhalau ambazo hazijengi.

Mwisho naona unalalamika sijuhi simu namba:0713,0767,0786,0776 ni vigumu kupatikana, hivi wewe katika mawazo yako unafikili tatizo ni nini? Sababu kubwa ni traffic kuwa kubwa kumbuka mitandao hiyo ina wateja wengi sana, sasa unawezaje kulinganisha traffic ya TTCL ya voice ambayo sijuhi hata kama wateja wake wanazidi laki moja ni hii ya wenzetu ya mamilllioni! Sina huakika kama kuna kitu umejifanza.
 
Mr. KAA LA MOTO


Nakushauri huwe unakuwa makini kusoma maoni ya watu, jazba zako na kudhalau binadamu wenzako
haiwezi kuleta tija yoyote katika nchi hii. Nakuomba usome paragraph ya pili ambayo nakili kwamba CDMA ina superior voice Quality kuliko GSM, lakini nimesema katika ufanyaji biashara ma-investors wana angalia ni mfumo gani ambao huko popular na wide spread basi na wenyewe wanafuata mkumbo, ndiyo maana VODACOM,TIGO,AIRTEL etc wamefuhata mkumbo huo huo, kwani unafikili walikuwa hawajuhi kuhusu CDMA na uzuri wake.

We unasema eti GSM ni crap CDMA ya TTCL balabala, je unaweza kuwaeleza Watanzania TTCL na TAIFA limefaidika nini kibiashara kwa mfumo wa CDMA?

Ndugu mimi sijakurupuka kuandika maoni yangu bila ya kuwa na weledi kwa ninayo zungumzia, huwezi kuwa una dismiss maoni ya wenzako off hand just like that, hapa tunazungumzia mambo ya kujenga siyo kubomoa; mimi nilifikili labda kuwepo kwako Bristol kama ni kweli kungeweza kukuelimisha jinsi wenzetu wanavyo heshimiana kwa kutoa constructive critism bila dhalau ambazo hazijengi.

Mwisho naona unalalamika sijuhi simu namba:0713,0767,0786,0776 ni vigumu kupatikana, hivi wewe katika mawazo yako unafikili tatizo ni nini? Sababu kubwa ni traffic kuwa kubwa kumbuka mitandao hiyo ina wateja wengi sana, sasa unawezaje kulinganisha traffic ya TTCL ya voice ambayo sijuhi hata kama wateja wake wanazidi laki moja ni hii ya wenzetu ya mamilllioni! Sina huakika kama kuna kitu umejifanza.
Bwakeile na gandi,
Heshima yako mkubwa. Kwanza samahani naomba usiniite Mr mimi ni miss:laugh:
Sawa bana kwa mchango wako. Na wewe umechangia kama nilivyochangia, sawa. Umekwazika? Pole na samahani! Nilikuwa natumia haki yangu sikujua kuwa itakuumiza kiasi hicho. teh teh teh teh ndio jf bana.
Bado unanirudisha kwenye argument ya inefficiency ya mitandao niliyoita ovyo kwa sababu tu ya wingi wa wateja? unataka niamini hivyo? Nakuhakikishia kama si kuhujumiwa ttcl kama wangekuwa na wateja wengi kama walionao wengine wangeweza kufanya vizuri. Na ndio sababu hawajajaza wateja wengi sana ili tu kuongeza idadi ya wateja na kuwa na huduma duni.
Nakwambia hawa unaodhani wazuri ni wezi tu. Naweka pesa napiga simu simsikii kabisa mtu aliye on the other side na pesa yangu imeliwa. Naambiwa naweza kupewa credit ya 500 au 200 ambayo nailipia faida ya sh.50 nakubali napiga simu nyingine nasikia simu imepokelewa na simsikii kabisa wa upande wa pili pamoja na kumuita haloooooo halooooooooooo kwa muda nagundua hata salio walilonikopesha limeliwa. Hawa ndio unawapa credit kisa eti wana wateja wengi! Hiyo kweli inaweza kuwa sababu ya kuniridhisha mie mteja niliepoteza vipesa vyangu?
Sina ugomvi na mitandao hiyo niliyokwambia kwa sababu ninamiliki kila mtandao nilioutaja na zote ziko hewani sasa hivi ninavyoshughulika na keyboard yangu, lakini hadi sasa ni ttcl mobile tu ndio ninayoitumia kwa raha na wala sipati shida. Kwa hapo mie sijali ina wateja wachache au la lakini nadhani technology wanayotumia ni ya kisasa sana na kwa sababu hiyo ina performance nzuri pia. Bahati mbaya kwa sababu mie hutumia simu zangu kupiga kila mtandao kwa simu yake ili kukwepa gharama, ni mara chache sana naitumia hiyo namba kwa watu wengine maana haimilikiwi na wengi. Sana sana naitumia nyumbani kupiga kwenye landline, na wanangu na mme wangu wanatumia hiyo hiyo na hivyo naitumia kuwapigia na nasema bado nafurahia usikivu na upatikanaji wake. Bei ya ttcl kwenda ttcl na kwenda international ni nzuri kuliko mtandao mwingine.
Shida waliyonayo ttcl ni kutojitangaza kama wafanyavyo wengine lakini shida ni ukata utokanao na liquidity ndogo katika biashara yao. Nakumbuka waliomba kukopeshwa na serikali ikakataa kuwadhami kwa kuwa Celtel wakati ule iliiwekea ngumu serikali kutokubali kuidhamini kampuni hii kupewa mkopo na serikali ikakubali. teh teh teh teh teh na hapo ukisikia hujuma ya serikali yetu dhidi ya mali za wananchi ndio hii! na nadhani unaweza kuelewa mkuu wangu. Kuna watu wengi hapa wameeleza ukweli mwingi kuhusu shida wanayokutana nayo ttcl na hata wewe ungekuwa meneja bora duniani lakini kama directors wako wa bodi kama wana muelekeo tofauti na wewe utakwama tu. Na hayo ndio wanayokutana nayo ttcl.
Samahani kama ulikwazika!
 
Bwakeile na gandi,
Heshima yako mkubwa. Kwanza samahani naomba usiniite Mr mimi ni miss:laugh:

Hata mimi nilizani wewe ni Mr. good to know..., kweli JF hatujuani vizuri..., Ingawa Mkuu hapo juu amesema una Jazba mimi naona hizo ni passion tu na uchungu na nchi yetu, heri wengi wetu tungekuwa na huo uchungu..., Naona Uzalendo wako Mzalendo mwenzangu... :)
 
Nakubaliana na wewe kwamba ni kweli mmetuuzia matangazo kweli kweli lakini service ya mitandao yenu mingi ni za chini sana. Mtu hasikii anayezungumza naye, mitadao ni kula pesa zetu tu. Kwa hilo umesema ukweli.

Miss, kwanini pamoja na service ya TTCL kuwa nzuri kuliko mitandao mingine lakini mbona bado TTCL ipo nyuma??
 
Hata mimi nilizani wewe ni Mr. good to know..., kweli JF hatujuani vizuri..., Ingawa Mkuu hapo juu amesema una Jazba mimi naona hizo ni passion tu na uchungu na nchi yetu, heri wengi wetu tungekuwa na huo uchungu..., Naona Uzalendo wako Mzalendo mwenzangu... :)
Teh teh teh teh siku tukikutana wana jf itakuwa kichekesho kabisa maana utashangaa kuniona mimi ni kibibi fulani kimejaa mimvi kichwani na mme wangu ni kijana mbichi. teh teh teh teh teh teh.
Ni kweli nauchungu sana na wana na wana wa wana wangu kukuta nchi iliyochakachuliwa na ikiwa fukara kwa ufukara wa kujitakia. Linaloniumiza zaidi ni kuona tunaendelea kuwa na taifa la wajinga na si wajinga wa kujitakia bali wa kutengenezwa ili waendelee kuwa wajinga na waendelee kutawaliwa.
 
kuwa na taifa la wajinga na si wajinga wa kujitakia bali wa kutengenezwa ili waendelee kuwa wajinga na waendelee kutawaliwa.

Hapo kwenye ujinga nimegundua kwamba siku zinavyokwenda mbele wakati wenzetu wanaendelea kuwa werevu sisi ndio tunazidi kuwa wajinga.., yaani babu zetu walikuwa na akili kushinda baba zetu ambao wana akili kuliko sisi..., sijui hao watoto wetu watakuwaje. Yaani kama ni gari sisi tupo kwenye reverse gear
 
Blue Balaa, Point of correction,it's NOT TCCL it IS TTCL=Tanzania Telecommunications Company Limited-TTCL

Thanx for this vital thread to be discussed by Great Thinkers. First of all I do not concur with your comments here!
Let me say this concerning TTCL,The Tanzania Telecommunications Co. Limited being one of the giant Telecommunication companies in Tanzania despite being disregarded by the Government.
What is happening in TTCL now has no difference to what is happening in other Parastatol Organizations in Tanzania. Look at TANESCO, look at ATCL, look at TRL, look at NIC, etc etc. There is no difference at all. Every Organization is in a very bad shape financially, economically and operationally. But who is behind all theme mess up in our Organizations? It is the GOVERNMENT; I am saying this with big letters to insist my point.FOREIGNERS coming in the name of INVESTORS in collaboration with Greedy and Corrupt government officials are KILLING OUR ORGANISATIONS,TTCL included.
We can remember very well back in year 1995 when the Government under CCM introduced the so famous Policy of PRIVATISATION in Tanzania. The policy was implemented with a supersonic speed whereby all Parastatols were privatized to FOREIGNERS like nobody’s business. Initially the Policy stated that only those LOSS making Organizations were to go private.
Besides the gear was changed or engaged to another direction. The Policy was directed to PROFIT making corporations like NBC Bank separated to NMB/NBC, TTCL,TBL, CEMENT Factories like Tanga Cement,Twiga Cement etc,etc.
Now,back to TTCL. It was in 2001 when the so called STRATEGIC INVESTORS going by the name M/S MSI/DETECON took over TTCL. They took over TTCL by that time making a huge profit CL turnover was 90Billion Tshs. Per annum. The MSI/DETECON agreed to pay 120m/-USD equivalent to 120Billion. Tshs , by that time (1 USD =1000 Tshs 120B/-to acquire 35% shares in TTCL.They first paid half amount at 60B/-Tshs before entering TTCL offices and promised to pay the other half after entering TTCL offices.That was a cheat to the government. Immediately after they grabbed office they just started a dilly dallying of payments. Do you what they last paid? It was only 4.5/- USD equivalent to 4.5 B/-Tshs.That was the end of the story. Instead of paying 120B/-Tshs they ended paying a total of 64.5B/- I am not sure if by that Time the ICC was not there!
After paying the 64.5 Billion T.shillings they assured the Government that all the monie paid for shall be invested in expanding TTCL network i.e TTCL infrastructure to increase the customers Base. In year 2001 the TTCL customer stood at 250,000 for both Data and Voice. The investor promised to increase the same to 805,000. Believe me, by the time MSI/DETECON pulls out of TTCL the CUSTOMER BASE was staggering at 160,000 OR less!!!!
Everybody knows what really happened. These guys were conmen! Instead of expanding TTCL network and Customer base as they agreed as per MOU between Government and MSI/DETECON, they just started a MOBILE company within TTCL going by the name of CELTEL by capitalizing on TTCL resources! Initially they said the same company CELTEL shall be owned by TTCL 100%. But as time goes on it was revealed that CELTEL was owned by MSI/DETECON 100%.It was then baptized with a new name as CELTEL INTERNATIONAL , after few years it was changed to ZAIN and now AIRTEL. It is known that Zain was owned by Government at 40% while the other 60% owned by Celtel International. It is very interesting to note that during the sale of ZAIN share by 100% to AIRTEL at a tune of almost 10Billion USD (NOT MADAFU)theTanzania Government was not involved/informed despite the 40% share they own in Zain. NO BODY QUESTIONED THIS RUBBISH, NEITHER IN OUR MJENGO AT IDODOMYA NOR IN THE ICC COURT!!!!!!!!!REASONS? Best known to JK and his CABINET!!
The TTCL story doesn’t end here,it still continues. From reliable sources it is said that the same CELTEL/ZAIN owners in collaboration with Government officials they put a condition that TTCL NOT BE ALLOWED GO MOBILE as they,TTCL shall paralyze other MOBILE OPERATORS in Tanzania especially ZAIN. You may notice that in ZAIN the following big heads have a good number of shares: SALIM AHMED SALIM, ROSTAM AZIZI, JOSEPH SINDE WARIOBA,MO IBRAHIM,EDWARD LOWASSA and JK !
As that is not enough, The Tanzania government owes TTCL about 7 billion Tshs. BUT the Government is reluctant to settle the debt!!Reasons??The government coffers have no monie!!???But they are ready to pay the Ghost RICHMONDULI alias DOWANS Company a total of 94/= billion Tshs.

The TTCL story still continues……………………

I will come later,by now let me say guten nacht!

Tumekwisha,
 
Tunahitaji complete change ya uongozi. mkwere & his ccm leadership are failures they must step down, otherwise it will be business as usual
 
Hi Great thinkers,

I am back again as I promised.

As I have already said ealier and I say it again,the KILLERS of TTCL is the CCM government under leadership of KIWETE and his henchmen. Most of government leaders are either SHARE HOLDERS or CHAIRMAN/CHAIRPERSON/BOARD MEMBERS in Foreign MOBILE operators.We have live examples:
  1. Pius Msekwa,the former Speaker of Tanzania Parliament was Chairman Board of Directors Vodacom Tanzania.
  2. Salim Ahmed Salim,the former AU Secretary General,PM and Minister is ZAIN/AIRTEL shareholder and Board Member.
  3. Joseph Sinde Warioba,the former PM and Minister is ZAIN/AIRTEL shareholder and Board Member.
  4. Rostam Aziz,the MP for Igunga Constituency is Vodacom shareholder and Board Member.
  5. Basil Pesambil Mramba is Board member and shareholder in Zain/Airtel.
This is just a list of some few Government leaders who are fully engaged in Mobile operators business and therefore making all possible means to make SURE that TTCL is no longer there.
About 2 years ago 2009/10 a secret letter from ZAIN to the Deputy Minister(by then Doctor Maua Daftari) was revealed at the Ministry of Science and Technlogy headquarters STATING A STRATEGIC PLAN TO STOP TTCL FROM OPERATING AND EXPAND THEIR TTCL MOBILE PHONES as it will adversely affect other Mobile operators!

The strategic plan was to make sure that TTCL MOBILE network be controlled and limited! In this plan TCRA wa involved in such a way that TTCL can not expand its Mobile phones without the TCRA authority. TTCL was allowed under special LICENCE to expand its network ONLY by 100,000 customers per year! While other Mobile operators are talking of a Customer base of 4m to 6m like Vodacom TTCL have to expand by 100,000 per year. That means, by just simple arithmetic TTCL can achieve a 1m customer base after 10 years!!!.

This can be proved by poor coverage of TTCL MOBILE. There is only one BTS(a Microwave system which connect mobile customers) in most Regions or Districts to cater for TTCL mobile customers. I know one region where there is ONLY ONE BTS!!!!!! Other companies like Vodacom,Tigo,Zain/Airtel have 30-50 BTS systems approximately in the same region.

The cost of 1 BTS ranges between 200-300m Tshs. which TTCL can afford.

I shall come later on more stories about TTCL.
 
Walisema wakati ule TTC haiwezi regulator na competitor kwenye biashara ya mobile phones, wakaitoa Celtel humo, lakini at the same time wakaanzisha regulatory body!!!!
lakini nasikia sasa tena japo ttcl walikuwa wana njia zote za mawasiliano ya nje, sasa kila mtandao unaruhusiwa kujitegemea??? hii ni njia nyingine ya kupunguza kipato cha TTCL
 
Ndugu Ndibalema,

Ukisoma post zangu huko nyuma nilisema sababu ya TTCL kuingiza CDMA badala ya GSM. Watendaji wazalendo ndani ya TTCL walielewa limitations za CDMA na faida za GSM. Isingewezekana kuingiza GSM kwani board ilikataa TTCL kufanya biashara ya simu za mkononi kwa sababu biashara hiyo hiyo ilikuwa ikifanywa na kampuni dada (wakati huo) Celtel. Kwa hiyo wataalam hao hata hiyo CDMA waliingiza kwa mgongo wa kuingiza Fixed Wireless na si Mobile.

Baada ya board kugundua kuwa kilichoingizwa ni Mobile solution, board ikazuia fedha zaidi kuingizwa huko. Viongozi wapya walipokuja (management contract) kutoka Canada, waliona kuwa solution ya wazalendo ilikuwa inafaa. Wakaitaka board iruhusu uwekezaji kwenye eneo hilo, board na serikali wakazuia fedha. Wa Canada wakaamua kujitoa.

Kwa hiyo Matendo ya Board ya TTCL pamoja na SERIKALI yanazuia kiongozi yeyote anayeendesha kampuni hii kufanikiwa. Hakuna kampuni inayoendeshwa bila uwekezaji. Umeshauliza Tigo, Zain, Vodacom wamewekeza kiasi gani hadi wakafikia hapo walipo? Unafikiri hizo fedha walizowekeza walitoa wapi? Walikopa kwenye mabenki hayo hayo ambayo yalikuwa tayari kuikopesha TTCL iwekeze.

TTCL inazuiwa kuwekeza. Wanaoizuia kuwekeza ni Board yake (imbayo ndo uongozi wa TTCL) na Serikali. Board na serikali wameshindwa kuweka uongozi wa kampuni wa kudumu. Kampuni inaendeshwa na viongozi wa ku-act ambao hawana mamlaka kamili ya kiutendaji. Na hili utawalaumu wafanyakazi??

Be fair
 
Huwa nikiangalia TTCL, Airtle na historia nikiikumbuka huwa nashindwa kumuelewa Mwandoswa hata kidogo, mnakumbuka ule umbea kuwa mwanae alipelewa na kulipiwa Chuo kikuu nchi fulani hivi, sikumbuki ila ilikuwa skendo kwa wakati ule. (sikumbuki kama alikanusha au la)
Inaniuma sana TTCL, masikini.
Kumbe wahujujumu wake hawajaiachia?
mie ningeomba huu utata uwekwe hadharani na magazeti na media nyingine ili ionekane na wengi, itasaidia kupunguza maamuzi machafu.
asanteni kwa kutujuza uozo wa nchi yetu,
Hivi nasikia kuna mtu competent kutoka Vodacom ameajiriwa kama CEO TTCL, ni kweli?

Hakuwahi kukanusha.
Ilisemekana mwane alipelekwa kusomeshwa of all places South Africa, na Mwandosya akakirimiwa kwa kulipiwa safari ya kwenda matembezi huko majuu. (This is how cheap our leaders are)
(Habari hii ni according to magazeti wakati huo. Ni muda mrefu umepita, hivyo facts naweza nikawa nimezisahau zingine au kuzichanganya as they were thenreported).
Halafu huyu ndie some tout as presidential material !! poor tanzania
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom