Why TTCL is not the leading Cellular and internet Operator?

hilo shirika lina matatizo makubwa kwenye uongozi..viongozi wao wengi ni analogy type..upeo mdogo wa uongozi wa biashara wa kisasa,hawana uwezo kustrategize chochote.Na wasipoangalia wataingia kwenye matatizo makubwa hivi karibuni kutokana na kushindwa kujiendesha.bado vilevile kuna politics yaani wafanyakazi wanajiona kama wanastahili nyingi sana ndani ya hilo shirika kwa kutumia hicho kitu kinaitwa tewuta wakati wao ndo chanzo cha hilo shirika kuporomoka kwa kufanya kazi chini ya kiwango.
vilevile hilo shirika lina wafanyakazi wengi makao makuu wakati wangeweza kutumia technology na kupunguza matumizi ya uendeshaji..anatakiwa CEO mwenye upeo wa kimataifa wa uendeshaji wa biashara za IT..bwana Said am afraid ataizamisha hiyo kampuni unless awaambie wafanyakazi ukweli pamoja na Tewuta yao.
Tewuta ndio kitu gani?!
 
TTCL inaongozwa na wazee ambao sio smart, wana akiili finyu balaa, in short wanachofikiria ni kupata salary kila mwisho wa mwezi basi imetoka, wao inciome iliyopo inawatosha, hawakai kufikiria waexpand vipi, wanafikiria watakula nini mwiisho wa mwezi. So stupid
 
yup! Niliambiwa na moja ya staff kuwa hata TTCL mobile ilicheleweshwa kwa makusudi ili kampuni nyingine zisiende mrama maana ingekuwa cheap sana. Je inawezekana uongozi wa juu kuna mapandikizi yaliyopo kwa interest ya kampuni nyingine?
Hata wafanyakazi wa chini hawapo motivated sana! So what should we do ili tuiokoe kampuni yetu?
Na hili ndilo swali la msingi
 
Na hili ndilo swali la msingi

Watu wengi wanasema TTCL imesheleweshwa makusudi ili kampuni zingine ziweze kusonga mbele, lakini ukiangalia sana unagundua hii hoja haina nguvu.

TTCL jinsi inavyoendeshwa, ndio hivyo hivyo kama kampuni au mashirika mengine ya UMMA ya wanavyoendeshwa, mfano mzuri ni Tanesco, hawapo serious hata kidogo, leo Tanesco mtu hana umeme kwake, wanapigiwa simu lakini kufika kwako wanaweza kutumia hata zaidi ya week kuja kutatua tatizo lako na hivyo hivyo TTCL wanafanya kwa wateja wao. Ipo siku itakuja kampuni nyingine serious inafanya kazi kama za Tanesco lakini huduma zake ni bora mara dufu na wateja tutaanza kwenda kwao kwa huduma ya uhakika na mwisho tutakuja kusema Tanesco imechelewesha kuendelea ndio maana kampuni mpya wamekuja kuchukua nafasi yao ya hali ya SOKO.

Cha msingi TTCL wabadilike kwenye huduma zao, huduma zao ni mbaya sana, hawana customer care hata kidogo, wanajibu wateja majibu kama vile wanapata huduma bure. Unapiga simu leo ila wanakuja kuSolve tatizo baada ya wiki, nani ataendelea kuvumilia UTOPOLO kama huo. Kwa hali hiyo jambo la TTCL kufa si jambo la kisiasa, ni jambo la kiungozi kama mashirika mengine ya UMMA.
 
Pole sana mkuu, unapata changamoto ipi unapotumia huduma za TTCL?
 
Mkuu TTCL ilianza kuhujumiwa tangu kuingia kwa Celtel then Zain now Airtel. Watu hawa walitumia (na wanaendelea kutumia) miundo mbinu ya TTCL huenda kwa malipo kidogo sana au bure kabisa. Na inasemekana mojawapo wa viongozi waliotumika kuihujumu TTCL ni Mwandosya (akiwa waziri wa mawasiliano na uchukuzi enzi hizo) na kundi lake (may be Mramba included akiwa waziri wa fedha). Na huenda mpaka sasa wako vigogo wakubwa wenye hisa katika kampuni hiyo wakiendelea kuiwekea mizengwe TTCL isisonge mbele.
Dah yule mzee anavyojifanyaga mzalendo na mstaarabu kumbe matako tu......
 
Huwa nikiangalia TTCL, Airtle na historia nikiikumbuka huwa nashindwa kumuelewa Mwandoswa hata kidogo, mnakumbuka ule umbea kuwa mwanae alipelewa na kulipiwa Chuo kikuu nchi fulani hivi, sikumbuki ila ilikuwa skendo kwa wakati ule. (sikumbuki kama alikanusha au la)
Inaniuma sana TTCL, masikini.
Kumbe wahujujumu wake hawajaiachia?
mie ningeomba huu utata uwekwe hadharani na magazeti na media nyingine ili ionekane na wengi, itasaidia kupunguza maamuzi machafu.
asanteni kwa kutujuza uozo wa nchi yetu,
Hivi nasikia kuna mtu competent kutoka Vodacom ameajiriwa kama CEO TTCL, ni kweli?
Yule mzee ni choko sana yule....
 
Kwa msio jua, ni afadhali msiendelee kujua; ila mambo ni kama hivi,

Wakati Mobitel inaingia TTCL ilikuwa na share mle kama asilimia 40. Baadaye serikali ikazibeba. Walichofanya na hizo hisa hakijulikani, ila leo serikali haina hisa Tigo

Mwaka 1999 TTCL iliamua kuanzisha mradi wake wa simu za Mkononi (kwa fedha zake), wakati huo ilikuwepo Tigo na Tritel peke yake. Serikali kupitia TCRA wakauzuia mradi huo kwa madai kuwa kampuni iko kwenye mchakato wa ubinafsishaji - Mwaka 2000 Vodacom wakaingia.

Mwaka 2001 akaingia Mbia kwa madai ya kununua asilimia 35 kwa Dola million 120. Akaishia kupewa hizo hizo kwa dola million 65.
Mbia huyo akatumia leseni ya biashara za simu za mikononi ya TTCL (mradi ulisimamishwa haukufutwa) kuanzisha celtel Tanzania, TTCL ikawa imenyang'anywa rasmi uwezo wa kufanya biashara za simu za mikononi, si kwa sababu ya uwezo wa watendaji, sababu ya uamzi wa mezani (serikali)

Celtel international (aliyekuwa na hisa ndani ya TTCL) ndo akaanzisha Celtel Tanzania ikiwa kama subsidiary company ya TTCL
Baadaye TTCL ikanyang'anywa Hisa zote ndani ya Celtel, zikahamishiwa hazina, TTCL ikabaki haina hisa na haina biashara ya simu za mkononi na ikazuiwa kuanzisha ya kwake kwa sababu masharti ya leseni hayakuiruhusu kuanzisha

Mwaka 2005, serikali ikaondoa masharti ya leseni, ila mbia mwingine wa serikali; Celtel international (ambaye sasa ni mshindani wa TTCL - lakini akiwa na share ndani ya TTCL) akakataa TTCL isijiingize kwenye biashara ya simu za mikononi.

Wafanyakazi wazalendo ndani ya TTCL wakaamua kuingiza biashara hizo kwa mgongo wa nyuma, ndivyo ilivyoingia TTCL Mobile na Technolojia ya CDMA. Hawa wazalendo waliidanganya bodi kuwa wanaingiza CDMA kufanya fixed wireless (WLL) ila kwa siri wakanunua full mobile solution. Bodi ingejua isingiruhusu asilani.

Hata hivyo baadaye bodi iligundua kuwa kilichoingia ni Mobile si WLL. Ikaamua kuzuia uwekezaji zaidi katika mradi huo, hivyo TTCL mobile ikashindwa kujitanua kama ilivyotarajiwa.

Mwaka 2007, serikali ikaleta menejimenti nyingine ya wazungu, kutoka Canada. Hawa walivyokuja wakaiambia serikali tiba ya TTCL ni kuuendeleza ule mradi wa TTCL mobile ulioanzishwa na wazalendo. Serikali ikakubali, lakini ikishirikiana na Celtel international (wakati huo Zain) wakazuia TTCL kukopa kwa ajili ya kuuendeleza mradi wa TTCL Mobile - Kwa hiyo mradi ukabaki bila kuendelezwa.

Mwaka 2009, baada ya kusuguana sana na serikali kuhusu kuendeleza mradi huo (serikali na Zain wakikataa), wa Canada waliamua kujitoa rasmi wakaondoka mwezi July 2009.

Toka hapo ni dana dana tu. Serikali wanashangaa kwa nini TTCL haifi? Wao wanataka ife, wauze mbao! Menejimenti ya wazalendo na wafanyakazi wao, wanapambana kulinda ajira zao. Ila serikali kwa kushirikiana na Zain (sasa airtel) wanataka hiyo kampuni ife, waipeleke kwa mufilisi ili viongozi wa serikali wajichotee masalia (TTCL inazo mali nyingi sana - Ikiwemo majengo, viwanja katika maeneo muhimu katika miji yote ya Tanzania, n.k.)

Ni dharau kwa watanzania kuwasema vibaya wafanyakazi wa TTCL, ni kampuni ngapi zingeweza kuhimili hujuma kutoka kwa wamiliki wake? Ni wafanyakazi pekee wanojua kuwa wanaohujumiwa pale ni watanzania, si wafanyakazi wa TTCL!! Watanzania ndio wenye mali serikali ni msimamizi tu.

Serikali dhaifu inashirikiana na matapeli wa nje kuhakikisha hii kampuni itakufa. TTCL ikifa, atakayenufaika ni watendaji wa serikali waliokaa mkao wa kula, wakisubiri kujichotea ma properties yatakayotelekezwa. Atakayenufaika ni Makampuni ya nje yatakayojichukulia biashara kubwa ambazo bado TTCL inazo.

TTCL ikifa atakayeumia ni mtanzania atakayekosa kazi. Mapato ya serikali yatashuka kwani TTCL pamoja na hali yake bado ni mlipa kodi mkubwa (waulize TRA watakuambia). TTCL hawafanyi lolote kukwepa kodi. Kodi zote za serikali wanalipa bila matatizo (bado wanalipa kodi kubwa kuliko makampuni mengi ya simu yanayokwepa kulipa kodi). Kushuka kwa mapato ya serikali kutawaumiza watanzania, si wawekezaji kutoka nje.

Ni vizuri tuujue ukweli, kwani ukweli utatuweka huru!
Umemaliza kila kitu.
 
Asante
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom