Wanandugu,
Nashukuru kwa mkubwa hapo juu kwa kutoa ufafanuzi wa undani, mimi nilibahatika kufanya kazi pale kwa muda mfupi,na sasa nipo kwenye upande mwingine wa dunia, niligundua mambo mengi sana.
Kwanza tuwe wakweli, suala la utaalamu upo wa kutosha, na kuna watu wana vichwa vikali huwezi kuamini, na ukitaka kuamini hilo, strategies nyingi zinabuniwa pale, lakini kutokana na uchelewesho wa utekelezaji na ule mwimbo wa ukosefu wa fedha, utashangaa zimeibuka kwa makampuni mengine binafsi (si ajabu kwa sababu kwenye bodi yao Zain wapo ndani).
Kuna miradi ambayo najua ilipangwa pale, kwa ajili ya masuala ya kitaifa, nimeshangaa plan zile zile wamepewa makampuni binafsi (na wanazitekeleza), utajiuliza zimetoka wapi?. sasa hawa tutawaita ma ' Idiot' kweli?. Idiot ataigwa mikakati na ufundi wake?.Sishangai sana kwa sababu ya mchanganyiko wa bodi na utaratibu wa kupeleka 'strategies' wizarani kwa approval...., hapo sasa!.
Hivi hamjiulizi kuwa hao tunaodhani wanaakili (WAZUNGU) waliishapewa TTCL kuiongoza, wakaamua kuingia mitini, wakijua kuwa itakuja kuwafia mbeleni baada ya kukosa ushirikiano toka serikalini?
Suala kubwa kwa TTCL ni uwezeshwaji, haya makampuni tunayoyasifia, jiulize yamepata mikopo mara ngapi toka yameingia kwa ajili ya new investments (mengine yalikuwa yanakufa kabisa, mikopo ikayasaidia) na shughuli za kimasoko. Lakini nilishangaa kuwa TTCL haipewa nafasi hata mara moja ya kupata mkopo, tena hawataki 'fadhira' za bure, ni mkopo lakini tumejiuliza kwanini hawapewi?. kwa kipindi chote hicho wamekuwa wakijiendesha kwa pesa zao wenyewe, bila msaada.
Leo hata ukiwambia TTCL wajitangaze, hawana uwezo wa kutosha kumudu soko bila kuwekeza kuongeza mtandao, kwa kudunduliza billi za kila mwezi hawawezi kwenda popote, na hata ukimpeleka MALAIKA aongoze hapo, bila uwezeshwaji atakimbia tu, kila kitu atakiona cha moto.Kuna fikra potofu kuwa TTCL ipo kila sehemu, si kweli, haijafika sehemu nyingi, na hata kule walipo utakuwa ina uwezo wa kutoa huduma kwa wateja wachache tu. Pia dhana ya kuchanganya kuwa sehemu yeyete waliopo mobile itafanya kazi si kweli, inahitaji uwekezaji mpya kabisa kwani ni technologia ambazo haziingiliani na fixed lines.
Wakati umefika watanzania kuamka na kuacha uvivu wa kufikiri, tujaribu kuyachunguza mambo kwa undani. Makampuni ya umma yenye roho ngumu kama TTCL pengine yanatakiwa YAFE, ndiyo maana hayana support, pengine kama alivyosema mchangiaji hapo juu kuwa "hata kile kidogo walichonacho kinamendewa"
Uzalendo Kwanza,